Nani mbabe England: Mambo muhimu kuhusu Ligi ya Premia 2017

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea walishinda Ligi Kuu England msimu uliopita nao Manchester City wameanza kwa kishindo na kupanua mwanya wa alama 14 kileleni kufikia sasa.
Lakini kwa jumla 2017, nani alikuwa bora zaidi?
Harry Kane ni mchezaji aliyeng'aa sana, lakini alizishinda klabu ngapi, na mameneja kufutwa kulisaidia chochote?
Hizi hapa ni takwimu za kufafanua hayo, pamoja na matukio mengine mengi yaliyovunja rekodi 2017.
Nani anaongoza jedwali ukiangalia mwaka 2017?
Chelsea walishinda ligi msimu uliopita kwa kushinda mechi 30 kati ya 38 na kumaliza alama saba mbele ya Tottenham.
Msimu huu walizembea mwanzoni, na Manchester City ndio wamewika.
City wameshinda mechi 19 kati ya 21 kufikia sasa msimu wa 2017-18.
Ukiongeza mechi 11 walizoshinda nusu ya mwisho ya msimu uliopita, ndio bado wanaongoza 2017.
Licha ya kushinda mechi 18 mtawalia, ya mwisho ikiwa dhidi ya Crystal Palace, City hawajafikia rekodi ya kushinda mechi nyingi msimu mmoja.
Wamepungukiwa na mbili kufikia rekodi ya Chelsea waliyoiweka mwaka 2005 waliposhinda mechi 32.
Chelsea walishinda ligi msimu wa 2004-05 na kuhifadhi tena msimu uliofuata.

Chanzo cha picha, Reece Killworth
Harry Kane ndiye hatari zaidi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Harry Kane bila shaka yupo kwenye timu nyingi bora za mwaka za mashabiki wengi mwaka 2017.
Ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi mwaka mmoja EPL katika historia, na mwaka 2017 ndiye aliyefunga mabao mengi kwa klabu na timu Ulaya.
Kane alifunga mabao 39 ligini 2017, matatu zaidi ya Alan Shearer alipoweka rekodi ya awali ya EPL 1995.
Alikuwa hatari zaidi Mei na Desemba, ambapo alifunga mabao manane kila mwezi.
Kati ya mabao hayo, kuna hat-trick sita za EPL, ambapo anatoshana na wachezaji wengine wafungaji mabao bora msimu huu EPL.
Hiyo inafikisha jumla ya hat-trick zake hadi nane, zaidi ya zilizofungwa na klabu kadha tangu kuanza kwa EPL.
Kane amefunga hat-trick nyingi zaidi kuwashinda Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Edinson Cavani mwaka huu wote kwa pamoja (ambao walifunga jumla ya hat-trick saba).
Kane alifunga mabao mengi kushinda klabu tatu Ligi ya Premia mwaka 2017.

Chanzo cha picha, Getty Images
Alama zaidi na mabao zaidi
Ukiangazia mwezi kwa mwezi, si ajabu kutambua ni kwa nini Manchester City wamezoa alama nyingi kuliko klabu nyingine tangu Oktoba.
La kushangaza hata hivyo ni kwamba Chelsea haikuzoa alama nyingi mwezi wowote nusu ya pili ya msimu uliopita licha ya kushinda ligi.
Na timu iliyofunga mabao mengi zaidi na wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi kila mwezi?
Si kila wakati ambapo imekuwa ni Manchester City na Kane.
Mshambuliaji nyota wa Brighton Glenn Murray ni miongoni mwa waliojitokeza.
Man City wameweka rekodi kwa mabao 102?
Kuna wakati Manchester City walikuwa wanafunga mabao manne au matano katika mechi kila wiki, na wamefunga mabao 102 mwaka wote ligini.
Na tangu kuanza kwa Ligi ya Premia 1993, hakuna klabu nyingine kabla ya City iliyowahi kuzidisha mabao 100.
Mwaka mbaya kuwa meneja?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanzo wa msimu huu mameneja sita walimwaga unga kabla ya Krismasi.
Baada ya kufutwa Paul Clement na Swansea kulikuwa na maana kwamba klabu nne ambazo zinavuta mkia ligini zimewafuta mameneja.
Klabu tano kati ya zote zilizowafuta mameneja zimeanza kuboresha matokeo.
Alan Pardew pekee ndiye hajafanikiwa West Brom.
Na mwanzoni mwa mwaka?
Watano walifutwa kabla ya Juni - Mike Phelan (Hull), Claudio Ranieri (Leicester), Aitor Karanka (Middlesbrough), Walter Mazzarri (Watford) na Claude Puel (Southampton).
Kwa jumla, mameneja 11 wamefutwa mwaka 11 Ligi ya Premia, idadi ya juu zaidi katika mwongo mmoja, idadi sawa na ya 2013.
Unaweza kusoma pia:













