Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Marekani na Uingereza zaanzisha mashambulizi dhidi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen

Mashambulizi mapya ya Uingereza na Marekani dhidi ya wapiganaji wa Houthi nchini Yemen kwa sasa yanaendelea, maafisa wa Marekani waliambia CBS, mshirika wa BBC wa Marekani.

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Wafungwa wa Urusi waliokuwa wakiachiliwa baada ya miezi sita sasa 'kupigana hadi kufa'

    Urusi imekuwa ikiwaachilia wafungwa kupigana nchini Ukraine kwa zaidi ya mwaka mmoja, awali ikiwapa msamaha na uhuru baada ya miezi sita, hata kama wamepatikana na hatia ya uhalifu wa kutumia nguvu.

    Lakini BBC imegundua mpango huu ni kitu cha zamani. Sasa, hawapati tena msamaha, wanakabiliwa na hali ngumu zaidi na badala ya kurudi nyumbani mapema, lazima wapigane hadi mwisho wa vita.

    "Ikiwa utajiandikisha sasa, uwe tayari kufa," anaandika mtu anayeitwa Sergei kwenye chumba cha mazungumzo cha wafungwa wa zamani wa Urusi wanaopigana huko Ukraine.Anasema kuwa tangu Oktoba amekuwa sehemu ya aina mpya ya kitengo cha jeshi kwa jina "Storm V" ambacho wafungwa sasa wanapewa."

    Awali ulikuwa unaweza kupigana kwa miezi sita halafu uanapewa msamaha. Lakini sasa, unalazimika kupigana hadi mwisho wa vita," anaandika.

    Wakati usajili wa wafungwa wengi Urusi ulipoanza katika msimu wa joto wa 2022, uliongozwa na Yevgeny Prigozhin, aliyekuwa mkuu wa kikundi cha kijeshi cha kibinafsi cha Wagner. Wafungwa walipewa rekodi safi, msamaha kamili na kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya miezi sita kwenye uwanja wa vita.

    Kabla ya kufariki katika ajali ya ndege mwezi Agosti, Prigozhin alisema kuwa karibu wafungwa 50,000 wa Urusi walikuwa wametumwa mstari wa mbele chini ya mkataba huu - takwimu kama hizo zimetajwa na wanaharakati wa haki za binadamu.

    Maelfu ya wafungwa hao walikufa, lakini wengine, walimaliza miezi sita na kurudi nyumbani na wengine waliendelea kufanya makosa tena na hata kuua.Jeshi la Urusi lilichukua mpango huo mnamo Februari 2023, hapo awali likitoa motisha sawa na Prigozhin.

    Lakini mpango huo ulimaanisha kuwa wafungwa walioachiliwa kupigana wangeweza kurudi nyumbani baada ya miezi sita na walikuwa katika nafasi ya upendeleo kuliko wanajeshi wa kawaida.

    Jambo hilo liliwakasirisha wanaume ambao walikuwa wamehamasishwa na familia zao.Sasa, masharti mapya kwa wafungwa yanarekebisha usawa huo na ni magumu zaidi.

  2. Marekani yaonya kuhusu hatua zaidi Mashariki ya kati

    Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan amesema kwamba kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani ya Jordan ambayo iliua wanajeshi watatu Jumapili iliyopita.

    Pamoja na mashambulizi ya angani ya pamoja na Uingereza dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen, Marekani imekuwa ikifanya mashambulizi ya angani dhidi ya maeneo yanayoungwa mkono na Iran nchini Syria na Iraq.

    Akizungumza na vyombo vya habari vya Marekani, Sullivan anasema "Kilichotokea Ijumaa kilikuwa mwanzo, sio mwisho, wa majibu yetu, na kutakuwa na hatua zaidi - zingine zimeonekana, zingine hazionekani.

    "Singeielezea kama kampeni ya kijeshi isiyo na mwisho."

    Pia anaongeza kuwa hakuna dalili kwamba Iran imebadili sera yake kuhusu makundi ya wanamgambo, na Marekani itajibu iwapo itaendelea kuona vitisho na mashambulizi.

    Sullivan pia anaongeza kuwa Marekani iko tayari kujibu mashambulizi yake na anaamini kuwa hadi sasa mashambulizi hayo "yalikuwa na matokeo mazuri katika kudhalilisha uwezo wa wanamgambo".

  3. Habari za hivi punde, Rais mpya wa Namibia aapishwa

    Rais Mpya wa Namibia Nangolo Mbumba ameapishwa kuwa rais wa nne wa Namibia baada ya rais Hage Geingob kufariki hospitalini mapema Jumapili.

    Mbumba ambaye aliwahi kuwa makamu wa rais chini ya Geingob alikula kiapo chake cha ofisi katika ikulu ya nchi hiyo.

    Netumbo Nandi_Ndaitwah alikula kiapo cha kuwa makamu wa rais mara moja.

    Katika hali ya utulivu baada ya hafla hiyo, Mbumba alitoa pongezi kwa mtangulizi wake akimtaja kuwa mbunifu mkuu wa katiba na usanifu wa utawala wa Namibia.

    Geingob alikuwa mwanachama mwanzilishi wa nchi ya kisasa baada ya ukoloni. Mbumba ataongoza nchi kwenye uchaguzi utakaofanyika baada ya muda wa miezi 9

  4. Habari za hivi punde, Mwanajeshi wa Israel auawa kusini mwa Gaza

    Jeshi la Israel limetangaza kuuawa kwa mmoja wa wanajeshi wake kusini mwa Gaza hapo jana Jeshi la Israel lilitangaza kuwa mmoja wa wanajeshi wake aliuawa katika mapigano yaliyotokea kusini mwa Ukanda wa Gaza hapo jana.

    Hii inafanya idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini kwenye Ukanda wa Gaza kufikia 225, kulingana na kile ambacho vyombo vya habari vya Israel vinaripoti kuhusu data rasmi.

  5. Video: Tazama mashambulizi ya Marekani dhidi ya mji wa al-Qaim nchini Iraq

  6. Video: Tazama ndege ya kivita ya Uingereza ikielekea kushambulia wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran

  7. Habari za hivi punde, Rais mpya kuapishwa Namibia

    Kaimu Rais Nangolo Mbumba amefichua kuwa Rais mpya ataapishwa saa nane kamili.

    Uamuzi huo ulitolewa kufuatia mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri uliomalizika hivi punde.

    Mbumba, Waziri Mkuu Saara Kuugongelwa-Amadhila, na wajumbe wengine wa baraza la mawaziri walikuwa Ikulu kwa mkutano huo.

    Mkutano wa baraza la mawaziri unafuatia kifo cha Rais Hage Geingob.

  8. Takriban watu 51 wamefariki kutokana na moto wa msituni Chile

    Takriban watu 51 wamefariki kutokana na moto wa msituni katika eneo la Valparaíso nchini Chile, mamlaka za mitaa zimesema.

    Rais Gabriel Boric alitangaza hali ya hatari na kusema atatoa "rasilimali zote muhimu" ili kukabiliana na hali hiyo.Inaaminika kuwa moto mbaya zaidi wa msitu wa Chile kuwahi kurekodiwa.

    Wengi wa walioathiriwa walikuwa wakizuru eneo la pwani wakati wa likizo za majira ya joto.

    Tahadhari ya afya iliwekwa mjini Valparaiso na wizara ya afya.

    Wanafunzi wanaosomea udaktari wanaokaribia kumaliza masomo yao wataajiriwa ili kusaidia kupunguza shinikizo kwa huduma ya afya, wizara ilitangaza katika taarifa hiyo hiyo.

    Huduma za uokoaji zimetatizika kufikia maeneo yaliyoathirika zaidi na Waziri wa Mambo ya Ndani Carolina Tohá alisema idadi ya waliofariki "itafikia idadi kubwa zaidi" katika saa zijazo.

    Serikali ya Chile imewataka watu kutosafiri kwenda katika maeneo yaliyoathiriwa na moto huo.

  9. Kwa Picha: Wapiganaji wa Houthi wakutana kuonyesha umoja wao dhidi ya mashambulizi

    Kwa Picha: Wapiganaji wa Houthi wakutana kuonyesha umoja wao dhidi ya mashambulizi

    Makundi ya waasi wa Houthi yamekuwa yakikusanyika katika kuonyesha umoja wao kufuatia mashambulizi ya hivi punde ya Marekani na Uingereza.

    Mashambulizi hayo, katika malengo 36 ya Wahouthi katika maeneo 13 nchini Yemen, yalitekelezwa baada ya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya meli za kimataifa katika Bahari Shamu.

    Kundi la waasi la Houthi linaloungwa mkono na kufadhiliwa na Iran, limeapa kujibu mashambulizi hayo.

  10. Habari za hivi punde, Wahouthi waapa kujibu mashambulizi ya Marekani na Uingereza

    Waasi wa Houthi wameapa kujibu mashambulizi ya Marekani na Uingereza baada ya mashambulizi kadhaa dhidi ya kundi hilo linaloungwa mkono na Iran kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya meli zinazopitia Bahari Shamu.

    Msemaji wa kundi la waasi alisema katika awamu hii ya tatu ya mashambulio ya pamoja ya Uingereza na Marekani hayatawazuia kutoka kwenye "msimamo wao wa kimaadili, kidini na wa kibinadamu" wa kuunga mkono Wapalestina.

    Wahouthi wamekuwa wakishambulia meli za kibiashara katika Bahari Shamu tangu Novemba. Takriban 15% ya biashara ya kimataifa hupitia Bahari ya Shamu kila mwaka, yenye thamani ya zaidi ya $1tn (£790bn).

    Mashirika mengi ya meli yameanza kuepuka eneo hilo na yanatumia njia ndefu zaidi kuzunguka kusini mwa Afrika badala yake.

    Kulingana na Houthis, mashambulizi 48 yalifanyika katika muda wa saa chache na kulenga mji mkuu Sana'a pamoja na maeneo mengine kote nchini.

    Bado hakuna majeruhi walioripotiwa.Katika taarifa ya pamoja, Marekani, Uingereza na nchi nyingine zinazounga mkono operesheni hiyo zilisema awamu ya tatu ya mashambulizi yaligonga "malengo 36 ya Houthi katika maeneo 13 nchini Yemen".

  11. Shirika la mazingira Kenya lawasimamisha kazi maafisa kuhusu leseni ya kiwanda cha gesi cha Embakasi

    Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira nchini Kenya (NEMA) imewasimamisha kazi maafisa wanne kuhusiana na kupewa leseni kwa mtambo wa kujaza gesi wa Embakasi ambao uliua takriban watu watatu kufuatia mlipuko uliotokea Ijumaa usiku.

    Hatua ya kuwaadhibu maafisa hao inajiri baada ya Rais William Ruto Jumamosi kuagiza Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai(DCI) kumsaka mmiliki wa kiwanda cha gesi cha Embakasi ambacho kilikuwa kimeharibika

    Ruto pia aliagiza maafisa waliotoa leseni kwa mmiliki wa mtambo huo kuanzisha kiwanda cha kujaza gesi katika eneo la makazi waadhibiwe.

    Tukio hilo lililotokea eneo la Mradi, Embakasi Mashariki, lilijeruhi zaidi ya 200 waliolazwa katika hospitali mbalimbali za jiji hilo wakiwa na majeraha ya moto.

    Mwenyekiti wa bodi ya NEMA Emilio Mugo aliwataka maafisa wanne kujiuzulu ili kuruhusu uchunguzi.

  12. Tunachojua kufikia sasa kuhusu mashambulizi ya Marekani dhidi ya Houthi

    Ikiwa unajiunga nasi tu. Kama tumekuwa tukiripoti, vikosi vya Marekani na Uingereza vilianzisha mashambulizi ya angani dhidi ya maeneo 36 ya Houthi katika maeneo 13 nchini Yemen.

    Hebu tuangalie kwa ufupi baadhi ya matukio muhimu katika wiki na miezi ya hivi karibuni ambayo yamesababisha hatua hii.

    • Novemba 2023 - Houthi, ambao ni kundi la waasi wanaoungwa mkono na Iran ambao wanaichukulia Israeli kama adui, wanaanza kushambulia meli katika Bahari Sahamu. Kundi hilo linasema kuwa linalenga meli zenye uhusiano na Israel ili kukabiliana na vita katika Ukanda wa Gaza. Hata hivyo, meli nyingi zilizoshambuliwa hazina uhusiano wowote na nchi hiyo.
    • 11 Januari - Marekani na Uingereza zaanzisha mashambulizi ya pamoja ya angani dhidi ya maeneo ya waasi wa Houthi nchini Yemen, kwa lengo la kudhoofisha uwezo wao wa kushambulia meli za mizigo na kuharibu minyororo ya kimataifa ya usambazaji.
    • 22 Januari - Mashambulizi mapya yanafanywa na Marekani na Uingereza baada ya mashambulizi ya Houthi kuendelea.
    • 28 Januari - Wanajeshi watatu wa Marekani wauawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani kwenye kituo cha Marekani karibu na mpaka wa Jordan na Syria. Rais wa Marekani Biden analaumu "makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali wanaoungwa mkono na Iran" lakini Iran inakanusha kuhusika kwa vyovyote katika shambulio hilo. Kundi la Islamic Resistance in Iraq, kundi linaloaminika kuwa na wanamgambo wengi ambao wamekuwa na silaha, wanafadhiliwa na kupewa mafunzo na kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, hatimaye wanadai kuhusika na mashambulizi hayo
    • Ijumaa Februari 2 - Marekani yazindua wimbi la kwanza la mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Iraq na Syria.
    • Jumamosi tarehe 3 Februari - Marekani na Uingereza zaanzisha mashambulizi yao mapya ya pamoja dhidi ya Houthis nchini Yemen.
  13. Wapiganaji wa Houthi wazimwa na mashambulizi ya Marekani na Uingereza

    Hakuna mashambulio mengine yaliyoripotiwa katika Bahari ya shamu kutoka kwa wapiganaji wa Houthi tangu msururu wa mashambulio ya angani huko Yemen.

    Siku ya Jumamosi, kabla ya mashambulizi hayo kufanyika, wanamgambo hao walitoa picha zinazoonyesha mazoezi yao ya kijeshi.

    Baadhi ya picha zilionyesha silaha zikishambulia shabaha za kejeli zilizokuwa na bendera za Uingereza, Marekani na Israel.

  14. ECOWAS yaelezea wasiwasi wake kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi wa Senegal

    Jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi ECOWAS imeelezea wasiwasi wake kuhusu uamuzi wa mamlaka ya Senegal kuahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 25 Februari 2024.

    Wanasiasa wa upinzani nchini humo wameitaja hatua hiyo kuwa ni mapinduzi ya kikatiba.

    Katika tangazo lililoshangaza nchi, Rais Mackey Sall alisema kuwa sababu ya hatua yake hiyo ni orodha ya wagombea katika chaguzi zilizopangwa. Wengi wa wagombea wamezuiwa kugombea.

    Katika taarifa yake Jumamosi usiku huko Abuja, Makao Makuu ya ECOWAS yalihimiza wanasiasa nchini kutanguliza mazungumzo na ushirikiano kwa ajili ya uchaguzi wa uwazi, jumuishi na wa kuaminika.

    Viongozi wa kambi ya kikanda pia walitoa wito kwa "mamlaka zinazofaa kuharakisha michakato mbalimbali," ili kupanga tarehe mpya ya uchaguzi.

    "Tume ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi imezingatia uamuzi wa mamlaka ya Senegal kuahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 25 Februari 2024," taarifa hiyo ilisema.

    Kambi hiyo imempongeza zaidi Rais wa Senegal, Macky Sall kwa kuendelea na uamuzi wake wa awali wa kutogombea muhula mwingine na kumtaka aendelee kutetea na kulinda mila ya kidemokrasia ya muda mrefu ya nchi hiyo.Tangazo la Rais Sall lilizua hali ya wasiwasi nchini humo.

    Chini ya kanuni za uchaguzi nchini, angalau siku 80 lazima zipite kati ya kuchapishwa kwa amri hiyo na uchaguzi, ambayo ina maana kwamba mapema zaidi inaweza kufanywa ni mwishoni mwa Aprili.Senegal haijawahi kuchelewesha kura ya urais.

  15. Marekani na Uingereza zaanzisha mashambulizi dhidi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen

    Mashambulizi mapya ya Uingereza na Marekani dhidi ya wapiganaji wa Houthi nchini Yemen kwa sasa yanaendelea, maafisa wa Marekani waliambia CBS, mshirika wa BBC wa Marekani.

    Haya ni pamoja na mashambulizi ya "kujilinda" dhidi ya makombora ya cruise ya Houthi ambayo Marekani ilitangaza mapema Jumamosi.

    Mashambulizi hayo ya awali yalilenga makombora sita ya kuzuia meli ambayo yalikuwa yanajiandaa kurushwa kwenye meli katika Bahari ya Shamu, kama tulivyoripoti katika chapisho la awali.

    Hii ni awamu ya tatu ya mashambulizi ya pamoja yanayofanywa na Marekani na Uingereza.

  16. Natumai hujambo