Chini ya theluthi moja ya hospitali za Gaza zinaweza kufanya kazi - WHO

Afisa wa Shirika la Afya Duniani lasema Gaza haiwezi kuendelea kupoteza vituo vingine vya afya.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi, Yusuf Jumah and Asha Juma

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja. Kwaheri!

  2. Mwanamume aliyetembelea wakwe bila mahari ajipata polisi

    Mwanamume mwenye umri wa miaka 60 amejipata polisi baada ya kutembelea wakwe zake kwa sherehe ya utambulisho bila mahari.

    Samuel Maikut kutoka wilaya ya Kween aliwasili katika nyumba ya kina Bibi Harusi Jumamosi mkono mtupu.

    Baba Mkwe, Christopher Ngania, alisema walikuwa na furaha ya kupokea wageni kwa ajili ya shughuli lakini wakashangazwa na kile kilichotokea.

    ‘’Tulikubaliana kuwa mume na timu yake wangekuja na ng’ombe wanne na mbuzi watatu na vitu vingine lakini mwanamume huyo hakuja na chochote,’’ anasema.

    Awali, Ngania alisema hawakutaka kuwapa mzigo mkubwa upande wa mume na kuamua kufanya sherehe ndogo ambayo ilijumuisha kutambulishwa pamoja na harusi, lakini Maikut alikataa.

    Hatimaye, timu ilikubali kufanya sherehe ya utambuzi Jumamosi.

    Bwana Ngania alisema aliandaa sherehe ambayo ilimlazimu kuchinja ng’ombe.

    ‘’Lakini tulisubiri wageni wetu kwa muda mrefu na baadaye tukaruhusu watu wa jamii kula chakula. Watu wawili waliwasili katika eneo kumi na moja jioni na kutufahamisha kuwa Bwana harusi alikuwa anakuja na kuwasili dakika 20 baadaye,’’ aliongeza.

    Bwana Ngania walimuhoji mkwe wao mtarajiwa na kumuita polisi ili wamkamate. ‘’Jamii ilikuwa imekasirishwa naye,’’ alisema.

  3. Rais wa Ankaragucu Faruk Koca akamatwa baada ya kumpiga ngumi mwamuzi

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa klabu ya soka ya Uturuki amekamatwa baada ya kumpiga ngumi mwamuzi kufuatia mchezo wa ligi kuu siku ya Jumatatu.

    Rais wa MKE Ankaragucu, Faruk Koca alikimbia uwanjani na kumpiga afisa wa mechi Halil Umut Meler baada ya timu yake kukubali bao la kusawazisha dakika ya 97 katika sare ya 1-1 na Caykur Rizespor.

    Waziri wa Sheria Yilmaz Tunc alisema Koca na wengine wawili walikamatwa rasmi kwa "kumjeruhi afisa wa umma".

    Soka zote za ligi ya Uturuki zimesimamishwa kufuatia tukio hilo.

    Rais wa Fifa Gianni Infantino alisema tukio hilo "halikubaliki kabisa" na vurugu "hazina nafasi katika mchezo wetu au jamii".

    "Bila wasimamizi wa mechi hakuna soka," alisema. “Waamuzi, wachezaji, mashabiki na wafanyakazi wanatakiwa kuwa salama ili kufurahia mchezo, na nitoe wito kwa mamlaka husika kuhakikisha hili linatekelezwa kikamilifu na kuheshimiwa katika ngazi zote.

    Tunc alisema Koca na wengine wawili walikamatwa baada ya waendesha mashtaka kuchukua taarifa na uamuzi wa udhibiti wa mahakama ukawekwa kwa washukiwa wengine watatu.

    "Uchunguzi unaendelea kwa makini," aliongeza.

    Soma zaidi:

  4. Rais wa Kenya William Ruto aongoza maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru nchini Kenya.

    Rais wa Kenya William Ruto, ameongoza maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru nchini Kenya.

    Sherere hizo ambazo zimeandaliwa katika uwanja wa Uhuru jijini Nairobi zinahusisha hafla muhimu ya kuzindua kikosi cha jeshi la nchi kavu ambalo litafahamika kama 25 Mechanised Infantry Battalion.

    Hiki ni kikosi cha tano katika brigedi ya nane ya jeshi la nchi kavu.

    Ni cha pili kukabidhiwa bendera rasmi na Rais William Ruto ambaye mwaka jana alikipatia kikosi cha 23MIB bendera yao ya kuhudumu. Baada ya kukabidhiwa bendera iliyoombewa na wakuu wa dini ....bendera hiyo ilionyeshwa katika maonyesho rasmi yanayofahamika kama ‘Trooping of the colors’ ambapo wanajeshi walioandaa gwaride maalum wanashiriki katika mipangilio maalum yaani military formations uwanjani.

    Rangi za kikosi kipya ni Maroon ambayo pia itakuwa rangi rasmi ya kikosi hicho cha 25 MIB.

    Bendera hiyo ni muhimu sana na hulindwa vikali kwa maana ndio ishara muhimu ya uhuru wa kazi wa kikosi husika. Na inapopepea ina maana kwamba kikosi kiko kazini na huongozwa na afisa mkuu jeshini.

    Katika miaka ya hivi maajuzi ...jeshi la nchi kavu limekuwa likifanya mabadiliko ya kutumia silaha za kisasa vitani na kubadili vikosi vyake kutoka Kenya Armed Rifles hadi Mechanised Infantry Batallions ambazo zinatumia magari aina ya personel carrier's yaani APC katika shughuli zao za kivita.

    Katika miaka ya hapo awali...jeshi la nchi kavu limebuni brigedi ya nane ambayo ina vikosi yaani battalions za ,23,25 MIB huku Rais wa awali Uhuru Kenyatta akizindua pia vikosi vya 17,19 na 21 Kenya Rifles.

    Hafla ya Trooping of the Color huandaliwa kila mwaka katika sherehe za Jamhuri na ni tamaduni ambayo Kenya imeiga kutoka kwa jeshi la Uingereza ambalo lilikuwa linasimamia taifa hilo wakati wa ukoloni.

    Ni hafla ambayo hufanyika katika uwanja wa kambi za kijeshi ama za kitaifa kama ule wa Uhuru ambapo amiri jeshi mkuu wa majeshi husimamia sherehe hizo.

    Bendera huonyeshwa na kikosi husika ambapo piano wanajeshi hufanya maonyesho rasmi ya kuonyesha bendera hiyo.

  5. Waasi wa Houthi wa Yemen washambulia meli ya mafuta ya Norway kwa kombora

    .

    Chanzo cha picha, J LUDWIG MOWINCKELS REDERI

    Waasi wa Houthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran wameishambulia meli ya mafuta ya Norway kwa takriban kombora moja na kusababisha moto.

    Hakukuwa na majeruhi katika shambulio hilo.

    Msemaji wa Houthi alisema meli MT Strinda ilikuwa ikipeleka mafuta kwa Israel, lakini wamiliki wa meli hiyo walisema ilikuwa inaelekea Italia ikiwa na nyenzo zinazotumika kwa uzalishaji wa mafuta.

    Waasi wa Houthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran wameigonga meli ya mafuta ya Norway kwa angalau kombora moja na kusababisha moto.

    Hakukuwa na majeruhi katika shambulio hilo.

    Msemaji wa Houthi alisema MT Strinda ilikuwa ikipeleka mafuta kwa Israel, lakini wamiliki wa meli hiyo walisema ilikuwa inaelekea Italia ikiwa na malisho ya nishati ya mimea.

    Kundi hilo limeapa kuzuia meli za taifa lolote linaloelekea Israel hadi pale Israel itakapokomesha mashambulizi yake huko Gaza, katika kile ambacho Wahouthi wanasema ni kuonyesha kuwaunga mkono Wapalestina.

    Marekani imesema itazingatia "majibu yanayofaa" kwa mashambulizi yoyote kama hayo, ambayo inaeleza kuwa "yamewezeshwa kikamilifu na Iran".

    Msemaji wa jeshi la Houthi Yahya Saree alisema katika taarifa ya televisheni kwamba meli hiyo ililengwa Jumatatu baada ya wafanyakazi wake kukataa kujibu maonyo.

    Amesema kundi hilo limezuia meli kadhaa kupita katika maji ya Yemen katika siku za hivi karibuni.

    Soma zaidi:

  6. Myanmar yaipiku Afghanistan kwa uzalishaji mkuu wa dawa ya kulevya afyuni (opium)

    .

    Chanzo cha picha, UNODC

    Myanmar sasa ndiyo nchi inayozalisha dawa za kulevya ya opium, ikiipiku Afghanistan, ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema.

    Uzalishaji wake wa opium mwaka huu unakadiriwa kupanda 36% hadi tani 1,080, mbali zaidi ya tani 330 zilizoripotiwa kuzalishwa na Afghanistan.

    Kilimo cha opium nchini Afghanistan kilipungua kwa 95% baada ya marufuku ya dawa za kulevya na chama tawala cha Taliban mwaka jana.

    Wakati huo huo, kilimo kimeongezeka nchini Myanmar, ambapo vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe, vimeifanya kuwa chanzo cha mapato.

    "Matatizo ya kiuchumi, kiusalama na utawala yaliyofuatia utekaji wa kijeshi wa Februari 2021 yanaendelea kuwafanya wakulima katika maeneo ya mbali kulima opium ili kujikimu kimaisha," anasema Jeremy Douglas, mwakilishi wa kikanda wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu (UNODC) ambayo iliandika ripoti hiyo.

    Afyuni, kiungo muhimu kwa heroini, imekuwa ikilimwa nchini Myanmar kwa miongo kadhaa, ambapo imefadhili vikundi vya waasi wanaopambana na serikali.

    Lakini katika mwaka uliopita pekee, wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochochewa na mapinduzi ya 2021 vikiendelea, kilimo kimeongezeka kwa wastani wa 18%, inasema ripoti, ikiwa ni yenye tija zaidi, kwa sababu ya matumizi ya mashamba yaliyopo kwa wingi, mifumo ya umwagiliaji na wakati mwingine mbolea.

    Kupanda kwa bei za zao hilo pia kumevutia watu wengi zaidi kulikuza. Janga hilo na hali mbaya ya uchumi wa Myanmar pia imefanya kilimo cha opium kuwa aina ya ajira ya kuaminika na ya kuvutia zaidi.

  7. Takriban watu 15 wauawa katika maporomoko ya ardhi DR Congo

    Takriban watu 15 wameuawa kwa maporomoko ya ardhi katika mji wa Bukavu katika nchi ya Kidemokrasia ya Kongo, vyanzo vya eneo vimesema.

    Mji mkuu wa Kivu Kusini umekumbwa na mvua kubwa na kusababisha maporomoko ya ardhi na nyumba kadhaa kuzikwa.

    Shirika la Habari la Nation chini Kenya limesema, katika eneo la Ndedere, Chifu wa eneo Albert Migabo Nyagaza, aliambia shirika la AFP, ‘’Baba, watoto wake watano na wajukuu wawili walizikwa na nyumba zao kuharibiwa.

    Aliongeza kuwa maporomoko ya ardhi yalitokea usiku wa manane.

    ‘’Tulisikia mlio mkubwa kama ng’urumo’’, amesema mkaazi wa eneo Medo Igunzi Munene.

    Aliongeza kuwa aliona ukuta wa nyumba ukianguka juu ya mwingine ambapo kulikuwa na watu wanane.’’

    Mwaka huu, Bukavu imekumbwa na mfululizo wa maporomoko ya ardhi na majengo kuporomoka.

  8. Marekani yaonya kuhusu umuhimu wa kulinda maisha ya raia

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani anasema Washington inaisukuma Israel kulinda maisha ya raia huku mapigano makali yakiendelea.

    Nathaniel Tek amesema Marekani inaamini ni "muhimu kwamba Israel inaweka kipaumbele katika ulinzi wa maisha ya binadamu, na kwa uwezo wa mashirika ya misaada kuwafikia raia".

    "Hakika kuna mengi zaidi yanayoweza kufanywa, na maelekezo sahihi zaidi na yaliyo wazi yanaweza kutolewa kwa raia ili kuhakikisha kuwa wako usalama.

    "Tunaamini kwamba wakati dhamira ya Israel ipo kuhakikisha ulinzi wa raia, matokeo pia ni muhimu na tunafanya kazi na kuishinikiza serikali ya Israel kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa maisha ya raia."

    Alisema kuna "pande mbili za mzozo huu" - akiongeza kuwa Hamas pia ina jukumu la kuwalinda raia lakini kundi hilo "halijaonyesha nia yoyote au mwelekeo wa kufanya hivyo".

    Tek alisema Israel inaweza tu kupata ushindi wa kimkakati ikiwa italinda raia na kufanya kazi ikilenga amani ya kudumu.

    "Kwa hivyo kuna mambo mawili katika hili, ya kimaadili na ya kimkakati, ambayo tumekuwa tukijaribu kusukuma."

    Soma zaidi:

  9. Israel- Gaza: Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupiga kura ya kusitisha mapigano mara moja

    Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kupiga kura leo kuhusu usitishaji vita mara moja huko Gaza, siku chache baada ya Marekani kupinga azimio kama hilo lililopendekezwa katika Baraza la Usalama.

    Rasimu ya sasa iliyopendekezwa ilitolewa na kundi la nchi 20 za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu.

    Hakuna nchi iliyo na kura ya turufu katika Mkutano Mkuu wa wanachama 193.

    Walakini, tofauti na Baraza la Usalama, maazimio ya Mkutano Mkuu sio lazima kisheria, ingawa yanaonyesha maoni ya ulimwengu.

    Tangu vita kuanza, Baraza la Usalama limeshindwa mara sita kupitisha azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano kwa sababu ya kutoelewana kati ya wanachama wake 15.

  10. Waasi wa Houthi wadai kuhusika na shambulio dhidi ya meli ya mafuta ya Norway

    Wapiganaji wa Houth nchini Yemen

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wapiganaji wa Houth nchini Yemen

    Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wamedai kuhusika na shambulizi dhidi ya meli ya mafuta ya Norway.

    Kundi hilo lilishambulia meli hiyo kwa roketi baada ya wafanyakazi "kukataa kujibu onyo la", Reuters imeripoti, ikimnukuu msemaji wa jeshi la Houthi Yehia Sareea.

    Pia alidai meli hiyo ilikuwa ikibeba mafuta kuelekea Israel, kwa mujibu wa GLZ Radio, na kusema Wahouthi walizuia njia meli kadhaa katika siku za hivi karibuni.

    Kundi hilo lilisema wiki iliyopita kwamba litashambulia meli zote zinazoelekea kaskazini mwa Israel.

    Pia imezionya kampuni za kimataifa za meli dhidi ya kushughulika na bandari za Israel.

    Wafanyakazi wote 22 waliokuwa kwenye meli ya Strinda hawajajeruhiwa, mmiliki wake Mowinckel Chemical Tankers aliiambia Reuters.

    Meli hiyo sasa inaelekea bandari salama, kampuni hiyo ilisema.

    Pia unaweza kusoma:

    • Houthi: Ni akina nani na harakati zao zilianzaje?
    • Je, kuna vikundi vingapi vyenye silaha huko Gaza na ni nani?
    • Uingereza yatafiti mipango ya kuchora upya ramani ya Gaza
    • Lifahamu kundi la Hezbollah la Lebanon
    • Lebanon: Mstari wa Buluu katikati ya mapambano ya Hezbollah na Israel
  11. Rina Gonoi: Wanajeshi watatu wa zamani wa Japan wapatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mahakama ya Japan imewapata wanajeshi watatu wa zamani na hatia ya kumnyanyasa kingono mwenzao wa kike.

    Uamuzi huo wa kihistoria unakuja baada ya Rina Gonoi, 24, kusababisha kilio cha umma na kuvutia hisia za kimataifa alipoweka hadithi yake kwenye YouTube mnamo 2022.

    Waendesha mashtaka wa Fukushima kisha wakawafungulia mashtaka watu hao watatu mwezi Machi, na kubadili uamuzi wao wa awali.

    Japani ni jamii ya kihafidhina ambapo kuzungumzia unyanyasaji wa kingono bado ni mwiko.

    Shutaro Shibuya, Akito Sekine na Yusuke Kimezawa walipokea hukumu iliyosimamishwa ya miaka miwili katika mahakama ya Fukushima siku ya Jumanne.

    Hii ni hukumu ya kwanza kuu dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia nchini Japan tangu Juni wakati nchi hiyo ilirekebisha sheria zake za uhalifu wa kijinsia, ambayo ni pamoja na kufafanua upya ubakaji na kuongeza umri wa idhini.

    Ilikuwa ni matokeo ya uharakati wa miaka mingi kufuatia msururu wa maamuzi ya mahakama yenye utata ambayo yaliwaachilia watuhumiwa wa shambulizi.

    Wanaharakati wanasema sheria za awali mara nyingi ziliwazuia walionusurika kuzungumza.

  12. Kamera za kijasusi zilizojificha kwenye kifaa cha kushikilia nguo zinauzwa kwenye Amazon

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kamera za kijasusi zilizojificha kwenye kifaa cha kushikilia nguo zinauzwa kwenye Amazon, licha ya kampuni hiyo kushtakiwa kwa vifaa vyake.

    Orodha ya kamera hizo iliyoonekana na BBC ina picha ya kifaa hicho kilichowekwa bafuni.

    Jaji wa Marekani hivi majuzi alitoa uamuzi kwamba mfanyabiashara huyo mkubwa lazima akabiliawe na kesi iliyowasilishwa na mwanamke anayedai kuwa alipigwa picha bafuni kwa kutumia kamera ya kifaa cha chushikilia nguo iliyonunuliwa Amazon.

    Mtaalamu wa masuala ya faragha amesema matumizi mabaya ya vifaa hivyo huenda yakavunja sheria za Uingereza.

    Amazon ilikataa kutoa maoni kuhusaiana na suala hilo.

    Hatua ya kisheria ya Marekani dhidi ya kampuni hiyo ililwasilishwa na mwanafunzi wa fedha za kigeni na mwigizaji mtarajiwa.

  13. Mwanamuziki mashuhuri wa Afrika Kusini Zahara amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 35

    Zahara alikuwa na mashabiki wengi barani Afrika

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Zahara alikuwa na mashabiki wengi barani Afrika

    Mwanamuziki mashuhuri wa Afrika Kusini Zahara, jina halisi Bulelwa Mkutukana, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 35.

    Msanii huyo aliyeshinda tuzo nyingi aliaga dunia katika hospitali ya kibinafsi mjini Johannesburg Jumatatu usiku.

    Taarifa hizo zilithibitishwa na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Zizi Kodwa, ambaye alielezea masikitiko yake makubwa kwenye mitandao ya kijamii.

    "Nimesikitishwa sana na kifo cha @ZaharaSA. Pole zangu za dhati kwa familia ya Mkutukana na tasnia ya muziki ya Afrika Kusini. Serikali imekuwa na familia hiyo kwa muda sasa.

    Zahara na gitaa yake walifanya makubwa na ya kudumu katika muziki nchini Afrika Kusin’ alisema Kodwa kwenye X.

    Kwa mujibu wa habari,Zahara alikuwa amelazwa hospitalini wiki moja kabla, muda mfupi baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Novemba 9.

    Kulazwa huko kulifuatia malipo ya lobola (malipo) na mchumba wake, Mpho Xaba. Taarifa iliyotolewa na familia wiki moja iliyopita ilisema, "Zahara amelazwa hospitalini kufuatia wiki ya malalamiko kuhusu maumivu ya mwili.

    Madaktari wanafanya kazi kwa bidii, na tunasubiri habari zaidi kutoka kwao."

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  14. Cardi B afichua kutengana na mume wake Offset

    Wanandoa hao wamekuwa pamoja tangu 2017

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wanandoa hao wamekuwa pamoja tangu 2017

    Cardi B anatarajia "mwanzo mpya" baada ya kuachana na mume wake Offset, rapa huyo amefichua.

    Akiwahutubia mashabiki kwenye klipu ya moja kwa moja ya Instagram iliyoshirikiwa na akaunti ya pop culture, rapper huyo wa Bongos alikiri: "Nimekuwa single kwa dakika

    Rapa wa Migos Offset bado hajatoa maoni yake hadharani kuhusu kutengana na mkewe.

    Akizungumza na mashabiki wake Jumapili usiku, Cardi B alisema: "Sijui kama nyinyi watu mmekuwa mkipata fununu kutoka kwangu, kutoka kwa maisha yangu au kutoka kwa hadithi zangu ninapoweka muziki fulani au kupata watu wasiofuata ... "Nimekuwa single kwa dakika moja sasa ... sijui jinsi ya kuuambia ulimwengu."

    Rapa huyo wa Bodak Yellow aliongeza: "Nataka kuanza 2024 safi, wazi. Sijui, nina hamu ya maisha mapya, mwanzo mpya.

    Cardi B na Offset, ambao majina yao halisi ni Belcalis na Kiari Cephus, wamekuwa na uhusiano wenye misukosuko tangu walipofunga ndoa mwaka 2017.

    Cardi B na Offset walithibitisha kutengana mnamo Desemba 2018, kabla ya kurudiana tena.

    Baadaye Septemba 2020, iliripotiwa kuwa Cardi B aliwasilisha talaka, kabla ya kuifuta baada ya kurudiana na mume wake.

    Wenzi hao wana watoto wawili Kulture, mwenye umri wa miaka sita, na Wave, mwenye umri wa miaka miwili.

  15. Cristiano Ronaldo afunga bao la 50 la mwaka katika ushindi wa Al-Nassr

    Ronaldo

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 50 mwaka huu wakati Al-Nassr ilipowafunga wapinzani wao Al-Shabab 5-2 na kutinga nusu fainali ya Kombe la Mfalme wa Saudia.

    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United aliifungia timu yake bao la nne katika kipindi cha pili.

    Hilo lilimfanya kufikisha mabao 26 msimu huu, huku 16 kati ya mabao hayo akifunga katika mechi 15 za Saudia Pro League.

    Siku tatu zilizopita, Ronaldo alicheza mechi ya 1,200 katika taaluma yake katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Al-Riyadh.

    Alifunga bao moja na kuchangia kufunga jingine katika mchuano huo

  16. Ligi ya Uturuki yasitishwa baada ya rais wa klabu kumpiga ngumi refa

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Viongozi wa mchezo wa kandanda nchini Uturuki wamesimamisha ligi zote baada ya refa kupigwa ngumi na rais wa klabu kufuatia mchezo wa ligi kuu siku ya Jumatatu.

    Halil Umut Meler alipigwa na rais wa MKE Ankaragucu, Faruk Koca, ambaye alikimbia uwanjani baada ya timu yake kufungwa bao la kusawazisha dakika ya 97 katika sare ya 1-1 ya Super Lig na Caykur Rizespor.

    "Mechi katika ligi zote zimeahirishwa kwa muda usiojulikana," mwenyekiti wa FA [TFF] wa Uturuki Mehmet Buyukeksi alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

    "Shambulio hili ni aibu kwa soka la Uturuki," aliongeza.

    Meler alipokea vipigo kadhaa kutoka kwa wengine alipokuwa amelala kwenye nyasi na kupata majeraha ikiwa ni pamoja na kuvunjika kidogo.

    Tukio hilo lilizua taharuki iliyohusisha wachezaji na viongozi wa klabu.

    Koca alihitaji matibabu hospitalini lakini "taratibu za kuwekwa kizuizini zitatekelezwa baada ya matibabu", alisema waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki, Ali Yerlikaya.

    Yerlikaya aliongeza wengine wamekamatwa kwa mchango wao katika tukio hilo, ambalo "alililaani vikali".

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Baada yya matukio hayo ya kushangaza Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema: "Ninalaani shambulizi dhidi ya refa Halil Umut Meler baada ya mechi ya MKE Ankaragucu-Çaykur Rizespor iliyochezwa jioni ya leo, na ninamtakia ahueni ya haraka," alisema.

    "Michezo ina maana ya amani na udugu. Michezo haiendani na vurugu. Hatutaruhusu vurugu kutokea katika michezo ya Uturuki."

    Klabu ya MKE Ankaragucu ilijutia hatua ya rais wao, ikisema katika taarifa yake: "Tunasikitishwa na kitendo kilichotokea jioni ya leo.

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

  17. Mateka wa Israel 'walipewa dawa za kulevya na kunyanyaswa kingono'

    xx

    Chanzo cha picha, EPA

    Raia wa Israel ambao walitekwa nyara na Hamas na kupelekwa Gaza walipewa madawa za kulevya ili kuwafanya wawe watulivu na wengine kudhulumiwa kingono, kulingana na daktari anayewatibu baadhi ya wale ambao wameachiliwa.

    Renana Eitan, mkurugenzi wa kitengo cha magonjwa ya akili katika Kituo cha Matibabu cha Tel Aviv Sourasky-Ichilov, alisema "unyanyasaji wa kimwili, kingono, kiakili, na kisaikolojia wa mateka hawa walioachiwa huru ni mbaya sana".

    "Sijawahi kuona kitu kama hicho" katika miaka 20 ya kuwahudumia waathiriwa wa kiwewe, alisema. "

    Mmoja wa wasichana alipewa ketamine kwa wiki chache," aliongeza. "

    Watoto walitenganishwa na familia zao, na mgonjwa mmoja alimwambia Eitan kwamba mateka kadhaa walikuwa wamezuiliwa kwenye giza kwa zaidi ya siku nne.

    "Walikuwa na akili, walikuwa na ndoto," Eitan aliongeza.

    Maelezo zaidi:

  18. Israel haina nia ya kukaa muda mrefu Gaza - Waziri wa ulinzi

    Wanajeshi wa Israel wakiwa katika picha ya kufanya kazi katika wilaya ya Shajaiya ya Gaza siku ya Jumapili

    Chanzo cha picha, Reuters

    Waziri wa ulinzi wa Israel amesema nchi yake haina nia ya kukaa muda mrefu katika ukanda wa Gaza.

    Yoav Gallant amesema wako tayari kufanya mazungumzo kuhusu nani atadhibiti Gaza ilimradi sio kundi linalochukuliwa hasimu na Israel.

    Gallant pia alisema mamia ya wanamgambo wa Hamas mjini Gaza wamejisalimisha au wamekamatwa katika siku za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na watu walioshiriki katika mashambulizi ya Oktoba 7.

    "Tumezingira ngome za mwisho za Hamas katika miji ya Jabaliya na Shejaiya, katika vita ambavyo vilionekana kuwa haviwezi kushindwa, ambavyo vilitayarishwa kwa miaka mingi kupigana nasi,vinaelekea kusambaratishwa," Gazeti la Times la Israel lilimnukuu akisema.

    “Wale ambao watajisalimisha watashughulikiwa kivyao, na wale ambao hawatasalimu amri pia watashughulikiwa kwa njia nyingine,” aliongeza.

    Pia unaweza kusoma:

    • Je, kuna vikundi vingapi vyenye silaha huko Gaza na ni nani?
    • Uingereza yatafiti mipango ya kuchora upya ramani ya Gaza
    • Lifahamu kundi la Hezbollah la Lebanon
    • Lebanon: Mstari wa Buluu katikati ya mapambano ya Hezbollah na Israel
  19. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumanne 12.12.2023

    • Mapigano makali yameendelea kuripotiwa kaskazini mwa Gaza ambako wanamgambo wa Hamas wanajaribu kuzuia vifaru vya jeshi la Israel kuendelea kusonga mbele kuelekea eneo ambalo Israel inasema wakipafikia operesheni yao itakuwa imefanikiwa pakubwa.
    • Israel imewataka makamanda wa Hamas kusalimu amri la sivyo waangamizwe. Zaidi ya wapalestina 18,000 wameuawa tangu mwezi Oktoba.
    • Majadiliano yameendelea karibu usiku kucha katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi COP28 unaokamilika leo huko Dubai.
    • Mahakama ya juu ya Marekani imesema itathmini ombi lililowasilisha kuangalia madai ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump kuwa hapaswi kushitakiwa kwa mashitaka ya kihalifu kwani ana kinga kisheria.
    • Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewakosoa vikali wabunge wa Republican nchini Marekani kwa kuzuia kutolewa kwa misaada zaidi ya kijeshi kwa nchi yake. Leo Bwana Zelensky anayetarajiwa kufanya mkutano na Rais Joe Biden mjini Washington
    • Na Shirikisho la wanariadha duniani limemtaja Noah Lyles,kuwa mwanariadha bora zaidi mwaka 2023.