Kwaheri!
Tukomee hapo kwa leo.
Asante sana kwa kujiunga nasi kuanzia alfajiri kwa matiukio haya ya moja kwa moja.Tukutane tena kesho panapo majaaliwa.Alamsiki!
Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
’Miili kadhaa ikiwemo ya Watoto imetapakaa kwenye sakafu ya lori.Kando dimbwi la damu linatoa taswira ya ukatili uliotokea hapa’
Yusuf Jumah
Tukomee hapo kwa leo.
Asante sana kwa kujiunga nasi kuanzia alfajiri kwa matiukio haya ya moja kwa moja.Tukutane tena kesho panapo majaaliwa.Alamsiki!
Ikiwa unajiunga nasi, hapa kuna muhtasari wa matukio ya hivi punde nchini Israel na Gaza.
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alishiriki video kwenye X, ikimuonyesha akiwatembelea na kuzungumza na askari wa jeshi la Israel.
Katika chapisho hilo anaandika: "Pamoja na wanajeshi kwenye mstari wa mbele na Gaza. Sote tuko tayari."
Taarifa tofauti ya ofisi yake ilisema Netanyahu aliwaambia askari wa miguu wa Israel nje ya Ukanda wa Gaza: "Je, mko tayari kwa hatua inayofuata? Hatua inayofuata inakuja."
Lebanon kuwasilisha malalamiko rasmi kwa UN kwa mauaji ya mwandishi wa habari
Lebanon inawasilisha malalamiko rasmi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kile inachosema ni "mauaji ya kimakusudi ya Israel" ya mwandishi wa habari wa Reuters, Issam Abdallah, ambaye pia ni raia wa Lebanon.
Abdallah aliuawa kusini mwa Lebanon siku ya Ijumaa wakati makombora yaliyorushwa kutoka upande wa Israel yalipopiga kundi la waandishi wa habari, mashahidi katika eneo la tukio wamesema, kulingana na ripoti iliyochapishwa na Reuters.
Abdallah alikuwa akifanya kazi karibu na mpaka wa Lebanon na Israel, ambapo mapigano kati ya wanamgambo na wanajeshi wa Israel yamezidi.
Wanahabari wengine sita, wakiwemo kutoka Reuters, Al Jazeera na Agency France-Presse, walijeruhiwa.
Msemaji wa jeshi la Israel baadaye alisema kuwa jeshi "linajutia sana tukio hilo" na kwamba "linalichunguza kikamilifu".
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Baadhi ya wanaoripoti sasa kutoka kwenye kivuko cha Rafah ambacho, kama tulivyokuwa tukieleza, ndicho kinachozingatiwa na baadhi ya raia wa Magharibi wanaojaribu kuondoka Gaza.
Mtayarishaji wa maudhui wa Palestina, Mohamed Aborjelaa, amekuwa katika kivuko cha Rahaf siku nzima kwenye kati ya Misri na Gaza.
Anasema karibu watu 500 wanaoshikilia pasipoti za kigeni wamekuwa wakijaribu kutoka, bila mafanikio.
“Kuvuka mpaka wenyewe si salama, kuna mashambulizi ya mabomu na hakuna pa kujikinga.Watu walipata jumbe za kuwaambia wawe hapo kuanzia saa 12 hadi 3 jioni kwa saa za hapa nchini lakini hakuna wakati wowote katika dirisha hilo ambapo kivuko kilikuwa wazi,” aliambia BBC.
Raia katika mpaka huo ni pamoja na Wamarekani, Waingereza, Wafaransa, Wachina, Waswizi na wenye hati za kusafiria za Uswidi.Wengi wao walikuwa raia wa nchi mbili pia waliokuwa na hati ya kusafiria ya Palestina.
“Baadhi yao wanawasiliana na balozi zao, ambao waliwaambia warudi majumbani mwao.Lakini baadhi yao hawana nyumba za kurudi.Haiwezekani”.
Katika ukurasa wake wa Instagram, alichapisha mahojiano na msichana mdogo aliyekuwa na pasipoti ya Uingereza.
“Naogopa kufa.Hakuna maji, umeme, mtandao,” anasema.“Kuna milipuko ya mabomu kila mahali, na sijui niende wapi.Niende wapi?”
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Serikali ya Marekani inawahimiza raia wake huko Gaza kuelekea kusini ili kuingia kivuko cha Rafah na Misri.
Njia pekee ya kuingia na kutoka Gaza ambayo haidhibitiwi na Israeli imefungwa kwa sababu ya mashambulio ya Israeli upande wa lango la Gaza
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema kuwa raia wake wanapaswa kuwa tayari katika kivuko hicho kwa uwezekano wa kufunguliwa tena huku kukiwa na mzozo wa kibinadamu, hasa baada ya Israel kuamuru kuhamishwa kwa raia kutoka sehemu ya kaskazini ya Ukanda huo.
"Tumewafahamisha raia wa Marekani walioko Gaza ambao tunawasiliana nao kwamba ikiwa wataitathmini kuwa iko salama, wanaweza kutaka kusogea karibu na kivuko cha mpaka cha Rafah," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alisema.
"Kunaweza kuwa na ilani ndogo sana ikiwa kivuko kitafunguliwa na kinaweza kufunguliwa kwa muda mfupi."
Biden anasema Marekani inafanya kazi kupunguza mateso ya kibinadamu
Rais wa Marekani Joe Biden anasema nchi yake inashirikiana na Israel, Misri, Jordan na Umoja wa Mataifa kutoa usaidizi wa kibinadamu kwa Gaza huku jeshi la Israel likiendelea kushambulia kile inachosema kuwa ni shabaha zinazohusishwa na wanamgambo wa Hamas.
Bila kutoa maelezo zaidi, Biden aliandika kwenye X kwamba Marekani ilikuwa ikifanya kazi "kuunda hali zinazohitajika ili kuanza tena mtiririko wa usaidizi na kutetea kuzingatiwa kwa sheria ya vita".
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
Kiongozi wa zamani wa Hamas amesema walichokifanya wanamgambo hao Jumamosi iliyopita ni "jaribio la kumaliza uvamizi wa Israel" na kwamba "anajivunia" waliotekeleza shambulio hilo
Akizungumza na Haberturk TV ya Uturuki, mkuu wa masuala ya kigeni wa Hamas Khalid Meshal aliongeza mzozo huo haukuanza wiki iliyopita, bali mwaka 1948.
"Israel imekuwa ikisema kuwa jeshi lao lilikuwa na nguvu zaidi na lisiloweza kushindwa. Tulipoona kwamba wameshindwa kwa saa chache, tulishangaa pia," alisema.
Alipoulizwa kuhusu mashambulizi ya wanamgambo wa Hamas dhidi ya raia, watoto na wazee, alisema: "Tuliendelea kuwaambia wasifanye hivyo. Lakini nyakati za vita, matukio haya yanaweza kutokea. Je, si ndivyo Israel inavyosema kila mara, kwamba wao hawakufanya hivyo [kuwaua raia] kwa makusudi?"
Alipoulizwa kama Hamas imefanya sawa na inavyoishutumu Israeli kufanya, Meshal alisema kulikuwa na "tofauti kubwa":
"Sisi ndio wamiliki wa ardhi hii. Adui anapotoka nje, ama askari au raia, wote ni maadui. Yeyote anayekuja katika ardhi yangu [kuikalia] ni adui, na ana hatia."
Marekani na China zazungumza kuhusu Israel-Gaza kwa njia ya simu
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametumia simu na mwenzake wa China Wang Yi kuomba msaada wa Bejing katika kuhakikisha mzozo wa Israel na Hamas hauenei katika nchi nyingine za Mashariki ya Kati.
Kwa upande wake, Wang alisema Washington inapaswa "kuchukua jukumu la kujenga na kuwajibika":
"Wakati wa kushughulika na masuala ya kimataifa, nchi kubwa lazima zifuate usawa , kudumisha utulivu na kujizuia, na kuongoza katika kutii sheria za kimataifa," alisema Wang.
Waziri wa mambo ya nje wa China pia ameongeza kuwa Beijing imetoa wito wa "mkutano wa kimataifa wa amani" haraka iwezekanavyo.
Taarifa rasmi za China kuhusu mzozo huo hazijawataja haswa Hamas katika kulaani ghasia, badala yake zimehimiza kusitishwa mara moja kwa mapigano, kulaani "matumizi ya nguvu kiholela", na kutaka kukomeshwa kwa "adhabu ya pamoja ya watu huko Gaza".
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Onyo: Chapisho hili lina maelezo ambayo baadhi ya watu wanaweza kupata kuwa ya kuhuzunisha.
Watu wengi wamekufa - takribani 12 - katika shambulio dhidi ya msafara wa raia wanaokimbia kaskazini mwa Gaza kwenye moja ya njia za kuwahamisha.
Kama tulivyoripoti awali, tumethibitisha video kutoka kwa matokeo ya shambulio - lakini hapa kuna maelezo zaidi kuhusu kile kinachoonyeshwa.
Video hii ni taswira ya karibu mauaji yasiyofikirika, na cha kusikitisha, ni ya hivi punde kati ya mengi yaliyoletwa na mzozo huu.
Inaonyesha kundi la wanaume wakikimbia kuelekea kwenye lori.Wengine wanapanda juu ihuku wengine wakirekodi tukio hilo.
Wanapiga kelele sala na maombolezo kwa ajili ya waathiriwa katika hewa iliyojaa moshi, sauti zao mara kwa mara zilizimwa na mlio wa honi za gari.
Kamera inapokaribia lori, hofu kamili yashambulio hilo inabainika
Miili kadhaa, iliyojeruhiwa na nguvu ya mlipuko huo, imetapakaa kwenye sakafu ya lori.Madimbwi ya damu yanatapakaa kote
Mtazamo unapoelekea upande wa pili wa lori, mwili wa mtoto mdogo - waziwazi asiye na umri wa zaidi ya miaka minne - unaonekana.
Kanda zingine zilizochukuliwa kabla ya shambulio hilo zilionyesha kuwa lori sawa na hizi zilikuwa na watu wengi kama 30 waliokuwa wakisafiri kuelekea kusini, kutafuta usalama.Wengine watakuwa wametupwa kutoka kwenye gari, wengine wanaweza kuwa wamenusurika na kuondoka eneo hilo.
Kamera inaposogea mbele ya lori tunaona magari mengine mawili yaliyoshambuliwa na kuungua - huenda yakiwa na waathiriwa bado ndani.
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Lita moja ya mafuta ya petroli nchini Kenya imeongezeka kwa Sh5.72 , Dizeli kwa Sh4.48 lita na Mafuta ya Taa kwa Sh2.45 lita katika bei mpya za mwezi huu zilizotolewa na mdhibiti wa nishati Epra.
Hii inamaanisha kuwa lita moja ya petroli itauzwa kwa Sh217.36 jijini Nairobi, dizeli kwa Sh205.47 huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa Sh205.06.
Bei hizo ni pamoja na asilimia 16 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Fedha ya 2023, Sheria ya Kodi (Iliyorekebishwa) ya Sheria ya 2020 na viwango vilivyorekebishwa vya Ushuru wa Bidhaa kwa mfumuko wa bei kwa mujibu wa Notisi ya Kisheria Na. 194 ya 2020.
Serikali imewapunguzia watumiaji gharama kutokana na ongezeko hilo lililotarajiwa kupitia utaratibu wa uimarishaji utakaofadhiliwa na Ushuru wa Hazina ya ustawi wa Petroli (PDL) .
Bila ruzuku hiyo, lita ya super Petrol ilipaswa kuongezeka kwa Sh8.79, dizeli kwa Sh16.12 na Mafuta ya Taa kwa Sh12.05.
Kwa mujibu wa EPRA, hali ingekuwa mbaya zaidi bila ruzuku hiyo.
Maandamano ya wafuasi wa Palestina yanafanyika Glasgow na miji kadhaa ya Uingereza ili kukabiliana na mzozo wa Israel na Gaza.
Waandishi wa habari wa BBC mjini Manchester. wanasema takriban watu 2,000 wanahudhuria maandamano hayo, ingawa wengi walitarajiwa kujumuika njiani.Huku kukiwa na msururu mkubwa wa polisi, kelele za "Palestina itakuwa huru" zilisikika wakati wanaharakati walipofika Platt Fields Park, ambako maandamano yalianza.
Wakati huo huo, polisi wanasema maandamano yaliyoandaliwa na Muungano wa Stop the War hukoCambridgeyamevutia takriban watu 300.Wale waliokuwa wakiandamana walionekana wakiwa na mabango yaliyokuwa yakisema: "Komesha Mauaji ya Kimbari" na "Haki za Kibinadamu?"
Mamia zaidi wamejitokeza kwa maandamano hukoLiverpool, na kuungana na 100 hukoExeterna karibu 60 hukoPlymouth
Pia kulikuwa na maandamano ya wafuasi wa Palestina hukoGlasgow, yaliyohudhuriwa na maelfu kwa mujibu wa waandishi wa BBC.Wazungumzaji walitoa wito wa Palestina huru na kukosoa vyombo vya habari - ikiwa ni pamoja na BBC - kwa uandishi wake wa mgogoro huo.Mwanamke mmoja alisema matukio hayo yalimwacha moyo wake ukiwa na huzuni.
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Qatar na Saudi Arabia zote zinasema kuwa zinakataa kabisa kuhamishwa kwa nguvu kwa Wapalestina ndani ya Gaza, baada ya Israeli kutoa wito kwa Wagaza kuondoka kaskazini mwa eneo hilo na kuelekea kusini.
Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Qatar inasema inataka "kuondolewa kwa mzingiro wa Ukanda wa Gaza, na kutoa ulinzi kamili kwa raia wa Palestina kulingana na sheria za kimataifa na za kibinadamu".
Maoni kama hayo yalichapishwa kwenye Xna wizara ya mambo ya nje ya Saudia usiku kucha.
Pia ilitoa wito wa kutolewa kwa misaada na vifaa vya matibabu kwa wakazi wa Gaza, "kwa sababu kuwanyima mahitaji haya ya kimsingi ili kuishi kwa utu ni sawa na ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu".
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Ripoti ziliibuka kwa mara ya kwanza jana jioni za shambulizi la msafara wa magari yanayoelekea kusini mwa Gaza.Video zinazoonyesha mauaji katika eneo la tukio ziliibuka muda mfupi baadaye.
BBC Verify imethibitisha shambulio hilo lililotokea katika mtaa wa Salah-al-Din;moja ya njia mbili za uokoaji kutoka kaskazini mwa Gaza kuelekea kusini.
Barabara hiyo ilijaa msongamano wa magari siku nzima jana huku wakazi wa Gaza walioko kaskazini wakizingatia maonyo ya Israel ya kutaka kuondoka eneo hilo.
Takriban maiti 12 zinaonekana kwenye picha, wengi wao wakiwa wanawake na watoto - ambao baadhi yao wanaonekana kuwa na umri wa miaka miwili hadi mitano.Mpangilio wa vivuli kwenye video unapendekeza kuwa ilirekodiwa karibu 17:30 saa za ndani.
Wengi wanaonekana wamelala nyuma ya lori - wengine wametawanyika kuzunguka barabara.Magari mengine yaliyoharibika pia yametapakaa eneo hilo.
Wizara ya Afya ya Palestina inasema watu 70 waliuawa katika eneo la tukio, na inalaumu Israel kwa shambulio hilo.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema kuwa linachunguza lakini likasema maadui wake wanajaribu kuzuia raia kuondoka kaskazini.
Msafara wa Wapalestina waliokuwa wakikimbia ulishambuliwa kwenye njia maalum ya kuwahamisha
Shambulio la msafara wa raia huko Gaza ambao tumekuwa tukikuambia unakuja wakati Wagaza wanaambiwa na Israeli waelekee kusini kwa njia maalum.
shambulio hilo lilifanyika kwenye mojawapo ya njia hizo mbili.
Zaidi ya Wapalestina milioni moja waliambiwa siku ya Ijumaa kuhama kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa ya Israel.Na leo, Israel imesema inawapa raia hao wa kaskazini mwa Gaza masaa mengine machache kuondoka.
Eneo la uokoaji linajumuisha eneo lote la Gaza City na kambi mbili kuu za wakimbizi, Jabalia na Beach Camp.
Kwa pamoja, hii inawakilisha mojawapo ya sehemu yenye watu wengi zaidi ya Ukanda wa Gaza - unaweza kuona ramani ya eneo hilo hapa chini.
Mashirika ya haki za binadamu yamesema kwamba kundi kubwa kama hilo la watu litaonekana kuwa lenye machafuko na hatari sana - Umoja wa Mataifa uliita vuguvugu hili la watu wengi katika muda mfupi
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Urusi inasema naibu waziri wake wa mambo ya nje anatarajia kukutana na wawakilishi wa Hamas katika nchi ya Ghuba ya Qatar wiki ijayo kujadili kuachiliwa kwa mateka wa Israel, kwa mujibu wa shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Urusi Ria-Novosti.
Moscow imekuwa ikijitokeza kama nchi inayoweza kuleta amani,mhariri wa BBC Russia Steve Rosenberg anasema katika muhtasari wake wa hivi punde.Anataja pia kwamba Urusi ina uhusiano na Hamas na Iran - ambayo inaaminika kuhusika katika kufadhili wanamgambo hao.
Mikhail Bogdanov aliiambia Ria-Novosti "hakufutilia mbali uwezekano " kukutana na wawakilishi wa Hamas wakati wa safari yake, na kuongeza: "Ikiwa wako tayari, sisi daima tunapendelea kuwasiliana.
"Hasa katika hali hii [mkutano] ungekuwa na manufaa kwa kutatua masuala ya vitendo, ikiwa ni pamoja na kuwaachilia mateka."
Kamanda aliyekufa wa Hamas aliachiliwa huru mnamo 2011 katika makubaliano ya kubadilishana wafungwa
Mengi Zaidi yanajitokeza kuhusu kifo cha Ali Qadhi, kamanda wa Hamas ambaye aliongoza mashambulizi ya wanamgambo hao kusini mwa Israel wiki moja iliyopita.
Jeshi la Israel lilisema kwamba "ndege zilimuua Ali Qadi, kamanda wa kikosi cha makomando wa Hamas 'Nukhba'.
Kwa mujibu wa Jeshi la Ulinzi la Israel, kijana huyo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa mmoja wa wafungwa 1,000 wa Kipalestina walioachiliwa huru mwaka 2011 badala ya Gilad Shalit, mwanajeshi wa Israel ambaye alitekwa na Hamas.
Mnamo 2005, Qadi alikamatwa kwa utekaji nyara na mauaji ya mwanamume wa Israeli ambaye aliripotiwa kufanya kazi na jasusi wa Shin Bet.
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Kamanda mkuu wa Hamas ameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) amesema.
Katika chapisho kwenye X, iliyoandikwa kwa Kiarabu, Avichay Adraee alisema Murad Abu Murad alihusika pakubwa katika shambulio la Israel Jumamosi iliyopita, ambalo liliua zaidi ya watu 1,300.
Hamas haijathibitisha kifo hicho.
Israel na Misri zasema raia wa Marekani huenda wakaondoka Gaza
Raia wa Marekani wataweza kuondoka Gaza kupitia mpaka wa Rafah kuelekea Misri, afisa wa Marekani anasema.
Kivuko hicho kitafunguliwa kuanzia saa 12:00 hadi 17:00 kwa saa za huko leo, kufuatia makubaliano kati ya serikali ya Israel na Misri.
Bado haijabainika iwapo Hamas, ambayo inadhibiti Gaza, itawaruhusu raia wa Marekani kuondoka katika eneo hilo.
Zaidi ya 2,200 waliuawa na 8,700 kujeruhiwa huko Gaza - wizara
Takriban watu 2,215 wameuawa na 8,714 wamejeruhiwa huko Gaza, Wizara ya Afya ya Palestina imesema.
Katika Ukingo wa Magharibi, watu 54 waliuawa na 1,100 walijeruhiwa.
Darroch: Uingereza lazima iitake Israel kuongeza muda wa uokoaji
Lord Kim Darroch, balozi wa zamani wa Uingereza nchini Marekani na mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Uingereza, anasema ni lazima muda zaidi utolewe kwa Wagaza kuondoka kaskazini mwa eneo hilo ili kuepuka "janga la kibinadamu".
Akizungumza na kipindi cha Today Radio 4, Lord Darroch alisema anafikiri mashambulizi ya ardhini ya Israel yenye lengo la kuwaondoa Hamas yatashindwa, wakati kizazi kijacho cha wapiganaji wa Kipalestina "tayari kimekuwa na itikadi kali".
Bwana Darroch pia alisema ataishauri serikali ya Uingereza - ambayo imesisitiza uungaji mkono wake kwa Israel na imelaani mashambulizi yaliyoanzishwa na Hamas - kuhimiza kupunguza kasi ya dirisha la saa 24 kwa watu kuondoka kaskazini mwa Gaza.
Alisema pia atawataka mawaziri kuwaambia Israel "ifikirie kwa makini kuhusu operesheni hiyo".
"Lakini mimi ni mgeni sasa," anaongeza.
Israel 'yaomba radhi ' kwa kifo cha mwandishi wa habari wa Reuters
Jeshi la Israel lilisema Jumamosi kuwa "linasikitika sana" kwa kifo cha mwandishi wa habari wa Reuters aliyeuawa jana wakati wa mashambulizi ya kuvuka mpaka kwenye mpaka na Lebanon, shirika la habari la AFP liliripoti.
Hata hivyo, jeshi la Israel halikukiri kuhusika.
"Tunaichunguza," msemaji wa jeshi Richard Hecht alisema kuhusu tukio hilo ambapo wanahabari wengine sita, wakiwemo wawili kutoka AFP, pia walijeruhiwa.
Jeshi la Israel limekanusha kuchukua miili kutoka Gaza
Jeshi la Ulinzi la Israel leo asubuhi limekanusha taarifa zinazosema kuwa huenda lilipata miili ya baadhi ya mateka wakati wa msako mkali uliofanyika jana huko Gaza.
Msemaji Lt Kanali Richard Hecht asubuhi ya leo alisema: "Madai haya si sahihi.Hatuna habari kuhusu suala hili."
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) amesema kutakuwa na mbinu ya "kutovumilia kwa vyovyote" hatari viwanjani ili kuhakikisha viwanja viko salama kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 itakayoanza Januari.
Akiongea kwenye droo ya mchujo wa mwaka ujao nchini Ivory Coast, Patrice Motsepe alikiri makosa "yanayoweza kuepukika" yalifanywa wakati wa mashindano ya 2021 nchini Cameroon, ambayo yalishuhudia maafa wakati takriban watu wanane waliuawa kwenye mvutano nje ya uwanja wa Olembe wa Yaounde.
"Kuna kiwango kikubwa cha umakini kwa sababu usalama wa mashabiki wetu ni muhimu," Motsepe aliiambia BBC Sport Africa.
"Familia wanapokuja kutazama mechi ya mpira wa miguu, wanapaswa kuhakikishiwa kabisa kwamba, kwa mtazamo wa Caf na washirika wetu, tumefanya kila linalowezekana kulingana na njia bora za kimataifa ili kuhakikisha kuwa vifaa na miundombinu ni salama.
Mkanyagano wa Olembe - 'makosa yalifanyika'
Janga hilo mnamo Januari 2022 lilitokea baada ya lango la kuingia Uwanja wa Olembe mjini Yaounde kufunguliwa kutokana na mkusanyiko mkubwa wa mashabiki wakati wa mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa kati ya wenyeji Cameroon na Comoro.
Uwanja uliwekwa kama uwanja wa fainali, licha ya tukio hilo baya.
“Baadhi ya makosa yalifanyika, na baadhi ya makosa hayo yaliweza kuepukika,” alisema Motsepe, akipongeza “kujitolea kabisa” kwa wahusika wakuu waliohusika.
"Tuko wazi kwamba ubora wa miundombinu ya kuandaa shindano la juu la Afrika lazima uwe wa kiwango cha kimataifa.
Shambulio la juma lililopita la Hamas dhidi ya Israel lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,300.
Shirika la habari la AFP limeandaa orodha ya zaidi ya wageni 100 ambao wamethibitishwa kufariki, kutoweka, au kuchukuliwa mateka, kulingana na taarifa kutoka kwa mamlaka za kitaifa.Wengine wengi hawajulikanaji walipo
Mzozo wa Israel-Gaza:Mengi zaidi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan amesema hatua yoyote ya Israel ya kuwalazimisha Wapalestina kuyahama makazi yao italitumbukiza eneo hilo kwenye "dimbwi" la mzozo mkubwa zaidi.
Katika taarifa, Ayman Safadi pia anasema kuzuia kwa Israel misaada ya kibinadamu kwa Gaza na agizo lake kwa raia wa kaskazini mwa eneo hilo kuhama ni "ukiukaji wa wazi" wa sheria za kimataifa.
Ndege ya Umoja wa Mataifa yenye vifaa vya matibabu kwa Gaza yatua Misri
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani la Umoja wa Mataifa (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema katika chapisho kwenye X kwamba ndege yenye vifaa vya matibabu ili kusaidia mahitaji ya dharura ya afya imetua katika mji wa Arish nchini Misri, takriban maili 28 (45km) kutoka mpaka na Gaza.
Anasema vifaa viko tayari kutumwa Gaza mara tu ufikiaji wa kibinadamu kupitia kivuko utakapoanzishwa.
Inafuatia mkutano aliofanya na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi siku ya Jumatatu, ambapo walijadili kuhusu usambazaji msaada huko Gaza.
Zaidi ya majengo elfu moja yameharibiwa huko Gaza - UN
Zaidi ya majengo 1,300 katika Ukanda wa Gaza yameharibiwa wakati wa mashambulizi ya karibu ya wiki moja ya Israel, Umoja wa Mataifa unasema.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu OCHA lilisema "nyumba 5,540" katika majengo hayo ziliharibiwa na karibu nyumba 3,750 zaidi ziliharibiwa vibaya na haziwezi kukaliwa.
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Jeshi la Israel linasema limewaua " magaidi kadhaa" baada ya kujaribu kuvuka kutoka Lebanon na kuingia katika ardhi ya Israel.
Kwa mujibu wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF), "seli ya kigaidi" ilitambuliwa muda mfupi uliopita.
Jeshi la anga la Israel lilifanya shambulio hilo kwa kutumia ndege isiyo na rubani, inaongeza.Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu idadi ya waliouawa wala kundi walilokuwamo.
BBC haijathibitisha madai hayo.
Mzozo wa Israel-Gaza:Mengi zaidi
Mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa kufanyika Gaza yanatawala kurasa za mbele za Jumamosi.
Gazeti la Daily Telegraph linamnukuu msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel akisema mashambulizi yaliyofanywa siku ya Ijumaa kabla ya shambulizi hilo yalilenga kuwatafuta mateka wa Israel na "kusafisha eneo dhidi magaidi na silaha".
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amenukuliwa na Daily Mail akisema operesheni hiyo itakuwa "mwanzo tu" na kuapa kwamba "tutamaliza vita hivi kwa nguvu zaidi kuliko hapo awali".
The i inaripoti kwamba Umoja wa Mataifa umeonya kwamba Gaza inageuka katika "shimo la kuzimu" na iko kwenye "kingo za kuporomoka", wakati Financial Times linasema shirika hilo linakadiria kuwa zaidi ya watu 423,000 katika eneo hilo tayari wamekimbia makazi yao.
"Wape wasio na hatia nafasi ya kuishi," kinasema kichwa cha habari katika Daily Express.Jarida hilo limebeba ombi kwa Israeli kutoka kwa Askofu Mkuu wa Canterbury kwamba "dhambi za Hamas hazibebwi na raia wa Gaza".
Gazeti la Daily Mirror linasema kuwa hapa Uingereza Polisi wa Met wako katika hali ya tahadhari na wanajiandaa kwa shambulio la kigaidi kabla ya maandamano ya wafuasi wa Palestina yanayopangwa kufanyika London siku ya Jumamosi.Naibu kamishna msaidizi Laurence Taylor amenukuliwa akisema "operesheni muhimu sana ya polisi" iko.
Waisraeli wanasema Wagaza wanapaswa kuelekea kusini kati ya 10am na 4pm kwa saa za ndani
Raia wanaoishi kaskazini mwa Gaza wameambiwa na jeshi la Israel kutumia barabara mbili kuelekea kusini leo, kwa mujibu wa msemaji.
Katika taarifa iliyotumwa kwa Kiarabu kwenye X, zamani Twitter, Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Avichay Adraee alisema njia mbili zinaweza kutumika kati ya saa 10 asubuhi na 4pm kwa saa za ndani (saa 7 asubuhi hadi 1pm GMT) "bila madhara yoyote".
Wale wanaoishi katika mji wa Gaza wameshauriwa kuhamia kusini kutoka Beit Hanoun hadi Khan Yunis, kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayoweza kufanywa na jeshi la Israel.
Watu wanaoishi karibu na ufuo wa bahari na magharibi mwa Olive pia wataruhusiwa kuhama kwenye Barabara za Daldul na Al-Sana kuelekea Salah Al-Din na Al-Bahr, Adraee anaongeza.
Mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza milioni 1.1 'haiwezekani kabisa kutekelezwa'
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba amri ya Israel ya kuwahamisha watu kaskazini mwa Gaza "haiwezekani kabisa kutekelezwa".
Makumi kwa maelfu ya raia walianza kukimbilia kusini mwa Gaza jana baada ya Israel kuwaambia watu kuondoka katika eneo hilo kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa.
"Kufikiria kuwa unaweza kuhamisha watu milioni moja katika masaa 24 katika hali kama Gaza inaweza kuwa shida ya kibinadamu," Borrell alisema, katika siku ya mwisho ya ziara ya siku tatu ya kidiplomasia nchini China.
Licha ya EU kujieleza kuunga mkono Israel, pia alionya kuwa pia inawajibika kufuata sheria za kimataifa za kibinadamu katika mchakato wa kujilinda.
"Msimamo uko wazi," Borrell alisema."Lakini, kama haki yoyote, ina kikomo. Na kikomo hiki ni sheria ya kimataifa."
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Zaidi ya Wapalestina milioni moja katika nusu ya kaskazini ya Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na makataa ya Israel hii leo kuhama kuelekea kusini.Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa makumi ya maelfu wamehama.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alionya kwamba mashambulizi makubwa zaidi ya nchi yake kuwahi kutokea Gaza katika siku za hivi karibuni ni "mwanzo tu".
Takriban watu 1,900 huko Gaza wameuawa katika mashambulizi yaliyotekelezwa kulipiza kisasi mauaji ya Waisraeli 1,300 katika mashambulizi ya kushtukiza yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la Hamas wiki moja iliyopita.
Kumekuwa na hofu katika sehemu ya kaskazini ya Ukanda wa Gaza wenye wakazi wengi tangu Israel ilipotupa vipeperushi vilivyowaagiza wakaazi kuondoka.Ingawa mistari mirefu ya watu na magari ilionekana kwenye njia za kusini, wengi walisema watakaidi agizo hilo au bado hawajahama.
Umoja wa Mataifa na mashirika mengine yameonya juu ya maafa ikiwa Wapalestina wengi watalazimika kukimbia, na kuitaka Israel iondoe mzingiro wake wa Gaza ili kuruhusu misaada ya kibinadamu.
Wiki moja baada ya Israel kukumbwa na mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa siku moja, inaendelea na mashambulizi yake makubwa ya mabomu huko Gaza ikisema inalenga kulitokomeza kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas ambalo linatawala eneo hilo.Hamas imeapa kupigana hadi tone la mwisho la damu.
Huku kukiwa na maandalizi ya uvamizi wa ardhini, jeshi la Israel linasema kuwa vikosi vyake tayari vimefanya mashambulizi machache ndani ya Gaza yakiwalenga Wapalestina wanaorusha makombora na kukusanya taarifa kuhusu makumi ya mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas.
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina