Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mapigano makali yazuka nchini Mali baada ya waasi wa Tuareg kuua 'zaidi ya wanajeshi 80'

Waasi wa Tuareg washambulia mji wa kaskazini wakati ujumbe wa Umoja wa Mataifa ukiendelea kuondoka nchini Mali.

Moja kwa moja

  1. Tunakomea hapo kwa leo. Hadi kesho kwaheri.

  2. Mzozo wa Mali: Mapigano makali yazuka baada ya waasi wa Tuareg kuua 'zaidi ya wanajeshi 80'

    Mapigano makali yamezuka kaskazini mwa Mali huku waasi wa Tuareg wakisema wameudhibiti mji wa Bamba kutoka kwa jeshi.

    Haya yanajiri baada ya wapiganaji hao wanaotaka kujitenga kusema wamewaua zaidi ya wanajeshi 80 katikati mwa nchi

    Serikali ilithibitisha kuwa kambi ya jeshi katika eneo la Mopti ilikuwa ikilengwa siku ya Alhamisi, lakini haikutoa maelezo.

    Kuongezeka kwa ghasia kunakuja wakati walinda amani wa Umoja wa Mataifa, waliotumwa Mali mwaka 2013, wakijiondoa kwa amri ya jeshi.

    Shambulio la Alhamisi dhidi ya mji wa Dioura ni la hivi punde zaidi tangu waasi wa Tuareg kuanzisha upya uhasama mwezi Agosti baada ya kuvunjika kwa mkataba wa amani wa 2015.

    Hii imeambatana na kuongezeka kwa ghasia kutoka kwa vikundi vya wanamgambo wa Kiislamu, licha ya kutumwa mnamo Desemba 2021 kwa mamluki wa Kikundi cha Wagner cha Urusi.

    Jeshi tayari lilikuwa likilengwa huko Bamba mapema mwezi Septemba na wanajihadi wenye uhusiano na al-Qaeda.

    Katika chapisho la mtandao wa kijamii, jeshi lilisema mapigano huko Bamba siku ya Jumapili yalianza saa 06:00, na kuyaelezea kuwa "makali".

    Haikuwataja wapiganaji waliohusika, iliwataja tu kama "magaidi".

    Muungano wa vikundi vya Tuareg, ikiwa ni pamoja na Co-ordination of Azawad Movements (CMA), ulisema katika taarifa kwamba sasa umedhibiti eneo karibu na Bamba, mji ulioko kwenye ukingo wa kushoto wa Mto Niger kati ya miji ya Timbuktu na. Gao.

    Waasi wa Tuareg, ambao wanataka uhuru wa kaskazini mwa Mali, wanapinga jeshi kuchukua udhibiti wa kambi zilizoachwa na maelfu ya wanajeshi wanaoondoka wa Umoja wa Mataifa.

    Pia unaweza kusoma:

  3. Mechi ya Uholanzi yasimamishwa baada ya kipa kupoteza fahamu

    Mechi ya vinara wa Uholanzi kati ya RKC Waalwijk na Ajax iliachwa baada ya kipa wa Etienne Vaessen kupoteza fahamu.

    Mchezo huo ulisimamishwa katika dakika ya 84 baada ya Mholanzi huyo, 28, kugongana na mshambuliaji wa Ajax, Brian Brobbey.

    Wachezaji walitaka usaidizi kwa hamaki na walikuwa wakibubujikwa na machozi wakati Vaessen aliyekuwa kimya akipatiwa matibabu uwanjani, na skrini iliyowekwa ikionyesha kinachojiri.

    Klabu yake ilisema alipata fahamu wakati akitolewa kwenye machela. RKC alisema: “Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina wa kimatibabu amesafirishwa hadi hospitali kwa uchunguzi zaidi.

    Ajax walikuwa wakiongoza mchezo wa Jumamosi wa Eredivisie kwa mabao 3-2 kabla ya mechi kusimamishwa.

  4. Uturuki: Maafisa wawili wajeruhiwa katika mlipuko nje ya wizara ya mambo ya ndani

    Mlipuko nje ya wizara ya mambo ya ndani ya Uturuki katika mji mkuu, Ankara, ulikuwa "shambulio la kigaidi", waziri wa mambo ya ndani amesema.

    Washambuliaji wawili walifika kwa gari la kibiashara mwendo wa 09:30 (06:30 GMT) na kufanya shambulio hilo na kuwajeruhi maafisa wawili, Ali Yerlikaya alisema.

    Bw Yerlikaya alisema mshambuliaji alijilipua mbele ya jengo la wizara na mwingine "hakuhusika".

    Mlipuko huo ulitokea saa chache kabla ya bunge kuanza tena.

    Haijabainika washambuliaji hao walikuwa ni akina nani. Hakuna aliyedai shambulio hilo.

    Afisa mkuu wa Uturuki aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba washambuliaji waliteka nyara gari hilo na kumuua dereva wake huko Kayseri, mji ulioko kilomita 260 kusini-mashariki mwa Ankara.

  5. Uhispania: Moto wa klabu ya usiku waua watu 11 huko Murcia

    Takriban watu 11 wamefariki katika ajali ya moto iliyotokea katika klabu moja ya burudani katika mji wa kusini-mashariki wa Murcia, mamlaka ya Uhispania inasema.

    Moto huo ulizuka katika klabu maarufu ya usiku ya Teatre, iliyoko katika eneo la Atalayas, mwendo wa saa 06:00 kwa saa za huko (04:00 GMT).

    Mamlaka inasema idadi ya vifo inaweza kuongezeka. Huduma za dharura zinatafuta watu ambao wamepotea na walikuwa kwenye majengo wakati huo.

    "Idadi ya vifo ndani ya kilabu cha usiku cha Atalayas imeongezeka hadi saba," Meya wa Murcia Jose Ballesta aliandika kwenye X.

    "Tumehuzunishwa," alisema kwenye kituo cha TV cha Uhispania 24h, akiongeza waokoaji walikuwa bado wakiwatafuta watu kadhaa walioripotiwa kupotea.

    Huduma za dharura zilisema wazima moto walifanikiwa kuingia mwendo wa 08:00 na kupata miili minne, kisha mingine miwili dakika 40 baadaye.

  6. Waasi wadai kuwaua askari 98 nchini Mali

    Makundi ya watu wanaotaka kujitenga yenye wafuasi wengi wa Tuareg nchini Mali, yamedai kuwaua takriban wanajeshi mia moja katika shambulio lililotokea katikati mwa nchi hiyo inayokumbwa na mzozo.

    Taarifa kutoka kwa Mfumo Maalum unaongozwa na Uratibu wa Harakati za Azawad (CMA), muungano wa vikundi vilivyojitenga vya Tuareg ulisema kuwa wamelisababishia hasara kubwa jeshi - ikiwa ni pamoja na kujeruhi makumi ya askari, kuchukuliwa wafungwa watano, huku wakipoteza. saba kati ya wapiganaji wao wenyewe.

    Madai yaliyotolewa na waasi hayakuweza kuthibitishwa kikamilifu. Maeneo ya matukio ni ya mbali na ni vigumu kupata vyanzo huru.

    Operesheni hiyo inasemekana ilianza kwa shambulio la kujitoa mhanga, ambapo mhusika aliuawa, na kufuatiwa na shambulio la silaha nzito na nyepesi, inasema GSIM.

    Kundi hilo pia lilidai kuua askari wengi na kudhibiti wadhifa huo na kuuchoma moto na kukamata magari sita na silaha na risasi nyingi.

    Kaskazini mwa Mali kumeshuhudia kuongezeka kwa uhasama na CMA, ongezeko ambalo limendana na kujiondoa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, unalazimishwa kuondoka nchini na utawala wa kijeshi uliongia madarakani tangu 2020.

    Tayari utawala wa kijeshi umewaamuru wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa wakikabiliana na makundi ya jihadi kuondoka nchini humo tangu mwaka 2022.

    Pia unaweza kusoma:

  7. Bajeti ya Serikali ya Marekani chupuchupu kukwama - yapata idhini ya matumizi ya wiki sita tu

    Bajeti ya Serikali ya Marekani imeponea kukwama baada ya Bunge na Seneti kukubaliana juu ya mpango wa ufadhili wa muda mfupi.

    Mswada unaohakikisha ufadhili hadi tarehe 17 Novemba ulipata uungwaji mkono mkubwa, na hatimaye kutiwa saini na Rais Joe Biden kuwa sheria dakika chache kabla ya tarehe ya mwisho.

    Lakini, mpango huo haujajumuisja msaada wowote mpya kwa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi - mahitaji muhimu ya Democrat.

    Spika wa Bunge la Republican Kevin McCarthy aliwasilisha mswada huo kinyume na viongozi wenye msimamo mkali katika chama chake.

    Ufungaji wa serikali, ambao ungeathiri maelfu ya wafanyikazi wa umma na kusitisha huduma mbali mbali za serikali, ulipangwa kuanza saa 00:01 ET (04:01 GMT) siku ya Jumapili.

    Lakini katika mabadiliko makubwa Jumamosi alasiri, Bw McCarthy aliamua kupiga kura hatua ya ufadhili wa muda ambao ingeweka serikali ambayo ina kabiliwa na changamoto ya ufadhili wa majanga ya asili lakini haitilii maanani mabadiliko makubwa juu ya viwango vya matumizi - hitaji kuu la Republican kudhibiti hali ya chini.

    Soma:

  8. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja leo Jumapili 01.10.2023.