Charles III atawazwa rasmi kuwa Mfalme wa Uingereza
Mfalme Charlse ameahidi kuzingatia sheria wakati wa utawala wake, katika hafla iliyohudhuriwa na watu mashuhuri 2,200.
Moja kwa moja
Mwana Mfalme Harry hajaalikwa katika kasri la Buckingham kujumuika na familia

Chanzo cha picha, Getty Images
Duke wa Sussex amehudhuria kutawazwa kwa baba yake, aliketi safu mbili nyuma ya kaka yake, Mwana Mfalme wa Wales huko Westminster Abbey.
Harry alifika peke yake bila mkewe Meghan, ambaye amesalia Marekani, na aliondoka mara moja baadaye.
BBC inaelewa kuwa hakualikwa kwenye Jumba la Buckingham ili kusalimiana na umati kufuatia sherehe hiyo. Inadhaniwa kuwa ameelekea katika uwanja wa ndege wa Heathrow.
Ni mara ya kwanza kwa Mwana Mfalme huyo kuonekana kwenye hafla ya hadhara akiwa na familia yake tangu riwaya yake yenye utata, Spare, kuchapishwa.
Harry aliingia kwenye gari peke yake muda mfupi baada ya ibada kukamilika. Saa chache baadaye, kwenye baraza la Jumba la Buckingham, Mfalme na Malkia walijumuika na washiriki wengine wanaofanya kazi wa Familia ya Kifalme, wakiwemo Mwana Mfalme na Binti wa Wales, na watoto wao.
Mke wa Mwana Mfalme Harry, Duchess wa Sussex, alibaki Los Angeles na watoto wao, ambapo mtoto wao Archie anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimika miaka minne.
Uhusiano kati ya Harry na washiriki wengine wa familia umekuwa mbaya tangu kitabu chake kilipochapishwa.
Kitabu hicho kilifichua kwa uwazi mizozo na kutoelewana na watu wa ukoo, na tangu wakati huo amesema kujisikia "tofauti" na familia yake yote.
Uamuzi wa Meghan kukataa mwaliko huo ulionekana sana kama sehemu ya mivutano hii ya kifamilia inayoendelea, ambayo haijatatuliwa.
Messi aomba radhi kwa kusafari Saudi Arabia bila idhini

Chanzo cha picha, Getty Images
Lionel Messi amewaomba radhi wachezaji wenzake wa klabu ya Paris St-Germain na kusema kuwa atasubiri klabu hiyo kuamua hatua itakayochukua dhidi yake baada ya kufanya safari bila kibali nchini Saudi Arabia.
Nahodha huyo wa Argentina alisimamishwa na klabu hiyo kwa wiki mbili kwa ajili ya safari hiyo.
Ilifuatia PSG kushindwa nyumbani na Lorient siku ya Jumapili - la tatu katika mechi sita - wakati Messi alicheza dakika 90.
"Naomba radhi kwa nilichofanya na nasubiri kuona klabu itaamua nini," Messi alisema kwenye video iliyowekwa kwenye mtandao wa Instagram.
"Kwa kweli nilifikiri tungekuwa na siku ya mapumziko baada ya mechi kama ilivyokuwa wiki zilizopita.
"Nilikuwa nimepanga safari hii kwenda Saudi Arabia baada ya kuighairi hapo awali. Wakati huu sikuweza kuighairi."
Messi anakaribia kuondoka PSG mkataba wake utakapomalizika majira ya joto.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye pia amepigwa faini na klabu hiyo, ana jukumu la kuwa balozi wa utalii wa Saudi Arabia.
Meneja wa PSG Christophe Galtier anasema "hakuwa na uhusiano wowote na" kusimamishwa kwa Messi, huku pia akilaani maandamano ya mashabiki nje ya nyumba za wachezaji.
Baada ya Kutawazwa kwa Mfalme: Ni nini kinachofuata?
Mfalme na Malkia aliyetawazwa muda mfupi uliopita wanaondoka Westminster Abbey na kwa sasa wnashiriki katika gwaride la pili - kubwa zaidi kuliko lile la kwanza - linalojumuisha washiriki wengine wa familia ya kifalme.
Msafara wa kutawazwa unarejea kwenye Jumba la Buckingham kupitia njia ile ile ya maili 1.4 (km 2.3) iliyotumiwa asubuhi ya leo.
Endelea kuwa nasi kwa matukio ya hivi punde ya sherehe hii ya kihistoria

Mkuu wa kundi linalopinga utawala wa kifalme akamatwa katika maandamano ya kutawazwa kwa Mfalme Charles

Chanzo cha picha, PA Media
Mkuu wa kikundi cha kampeni dhidi ya ufalme cha Republic amekamatwa katika maandamano katika eneo la Trafalgar kabla ya shughuli ya kutawaza kwa Mfalme Charles. Kanda za video zinaonyesha waandamanaji waliovalia fulana za "Not My King" wakizuiliwa, akiwemo Mkurugenzi Mkuu Mtendaji kikundi hicho Graham Smith.
Waandamanaji sita, akiwemo Bw Smith, walikamatwa na polisi walipokuwa wakipakua mabango karibu na njia ya msafara wa kutawazwa kundi hilo lilisema.

Chanzo cha picha, Reuters
Republic ilichapisha picha za maafisa wakichukua maelezo kutoka kwao kwenye ukurasa wao wa Twitter.
"Sana kwa haki ya kuandamana kwa amani," kikundi hicho kilisema, na kuongeza maafisa hao hawatatoa sababu za kukamatwa kwao na kuthibitisha Mkurugenzi Mtendaji wao alikuwa miongoni mwao.
Matt Turnbull, mmoja wa waliokamatwa, alisema kamba zilizokuwa na mabango "zimeeleweka vibaya" kama kitu ambacho kinaweza kutumika kwa kufunga. "Kusema kweli hatukuwahi kuruhusiwa kuwa nguvu inayoonekana hapa - walijua tunakuja, na wangetafuta njia ya kukomesha hili," aliiambia BBC.
Baadaye BBC ilimwona Bw Turnbull akitolewa akiwa amefungwa pingu.
Polisi hawajathibitisha idadi kamili ya watu waliozuiliwa, lakini walisema watu kadhaa walikamatwa karibu na njia ya gwaride la kutawazwa.
Maandamano ya kupinga ufalme yalipangwa karibu na Trafalgar Square katikati mwa London, huku umati wa watu wakiimba nyimbo za "Not my King" na "Free Graham Smith".
Maelfu ya watu wamekusanyika kutazama msafara wa kutawazwa kutoka kasri la Buckingham hadi Westminster Abbey kabla ya sherehe.
Katika Picha: Malkia Camilla akitawazwa
Askofu Mkuu wa Canterbury pia ameongoza sala nyingine na baraka. Hizi hapa ni baadhi ya picha za Camilla, Mke wa Mfalme Malkia akivishwa Taji la Malkia Mary.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Taji ya Malkia Mary na Taji ya St Edward kando kando kwenye madhabahu Charles III atawazwa rasmi kuwa Mfalme wa Uingereza
Askofu mkuu anaweka Taji la St Edward juu ya kichwa cha Mfalme.
Ni wakati pekee Charles atalivaa katika maisha yake.

Chanzo cha picha, PA Media

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Unaweza kuliona Taji la St Edward hapa kwa ukaribu zaidi, baada ya kuvishwa kwenye kichwa cha Mfalme. Taji hilo liliyotengenezwa kwa dhahabu dhabiti ya karati 22,limedumu kwa miaka 360 na ina urefu wa zaidi ya 30cm (futi moja) na, ina uzani wa takriban kilo 2.23. 
Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Baada ya Mfalme Charles kutawazwa, mwanawe Mwana Mfalme William alimbusu kwenye shavu Katika Picha: Familia ya kifalme ikifuatilia kutawazwa kwa Mfalme
Picha hizi za hivi punde ni za Mwana Mfalme na Binti Mfalme wa Wales, watoto wao na washiriki wengine wa familia ya kifalme wakifuatilia sherehe hiyo.

Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Binti Mfalme wa Wales ameketii kando ya Mtawala wa Edinburgh 
Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Mtawala wa Wales, Binti Mfalme Charlotte, Mwana Mfalme Louis, Binti Mfalme wa Wales na Mtawala wa wa Edinburgh 
Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Binti Mfalme Charlotte na Mwana Mfalme Louis walipigwa picha wakizungumza Mfalme ala Kiapo cha Kutawazwa

Chanzo cha picha, PA Media
Askofu Mkuu wa Canterbury ametambua imani tofauti zinazozingatiwa nchini Uingereza kwa kusema Kanisa la Uingereza "litajizatiti kukuza mazingira ambayo watu wa imani zote wanaweza kuishi kwa uhuru".
Welby kisha akaongoza Kiapo cha Kutawazwa - hitaji la kisheria.
Alimuomba Mfalme Charles athibitishe kwamba atadumisha sheria na Kanisa la Uingereza wakati wa utawala wake.
Mfalme kisha akaweka mkono wake juu ya Injili Takatifu na kuahidi “kutekeleza na kutimiza” ahadi hizo.
Pia alikula kiapo cha pili - Kiapo cha Azimio la Kuingia - akisema kwamba yeye ni "Mprotestanti mwaminifu".
Maeleza zaidi:
Kwa picha: Watu mbalimbali walivyowasili katika sherehe ya kutawazwa kwa Mfalme Charles III

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby aliwakaribisha wageni Zaidi ya watu 8,000 walihudhuria kutawazwa kwa Malkia Elizabeth II mwaka wa 1953. Orodha ya wageni wa Mfalme Charles’ ni ndogo zaidi, na takriban watu 2,000 wamealikwa. Miongoni mwa walioalikwa ni washiriki wa Familia ya Kifalme, waziri mkuu, wawakilishi kutoka Mabunge, wakuu wa nchi, na washiriki wengine wa familia ya kifalme kutoka kote ulimwenguni. Mialiko pia imeenda kwa wawakilishi 850 wa jumuiya kwa kutambua michango yao ya hisani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mke wa Rais wa Marekani Jill Biden alipowasili 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mke wa rais wa Ukraine, Bi Olena Zeleska 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Waziri mkuu wa Uingereza Rish Sukan alipowasili 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mwanamuziki Katty Perry atatumbuiza katika sherehe hizo 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wanamuziki wakitumbuiza katika ukumbi wa Westminster Abbey wageni walipofika wakaketi kabla ya sherehe hiyo ya kihistoria Vita vya Ukraine: Urusi yatuhumiwa kutumia mabomu ya phosphorus mjini Bakhmut

Chanzo cha picha, Wizara ya ulinzi ya Ukraine
Ukraine imeishutumu Urusi kwa kushambulia mji wa Bakhmut uliozingirwa kwa mabomu ya phosphorus.
Katika picha za ndege zisizo na rubani zilizotolewa na jeshi la Ukraine, Bakhmut inaweza kuonekana akiwaka moto huku kile kinachoonekana kuwa mvua ya phosphorus nyeupe inanyesha kwenye mji huo.
Silaha za phosphorus nyeupe hazijapigwa marufuku, lakini matumizi yake katika maeneo ya kiraia inachukuliwa kuwa uhalifu wa kivita.
Urusi imeshutumiwa kwa kuzitumia hapo awali. Urusi imekuwa ikijaribu kuuteka mji wa Bakhmut kwa miezi kadhaa, licha ya thamani yake ya kimkakati ya kutiliwa shaka.
Maafisa wa nchi za Magharibi wamekadiria kuwa maelfu ya wanajeshi wa Moscow wamekufa katika shambulio hilo.
Ikiandika kwenye Twitter, wizara ya ulinzi ya Ukraine ilisema shambulio hilo la phosphorus lililenga "maeneo ambayo hayajatekwa ya Bakhmut".
Kamandi ya vikosi maalum vya Kyiv iliongeza kuwa vikosi vya Moscow viliendelea "kuharibu mji".
Unaweza kusoma:
Iran yamnyonga raia wa Uswidi na Iran kwa madai ya ugaidi

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Chaab alipatikana na hatia ya "ufisadi duniani" - adhabu yake ni kifo Iran imemnyonga mwanamume raia wa Uswidi mwenye asili ya Iran anayetuhumiwa kuhusika na shambulio baya la 2018 kwenye gwaride la kijeshi.
Habib Chaab alikuwa mwanzilishi wa kundi linalopigania uhuru wa Waarabu katika jimbo la Khuzestan kusini-magharibi mwa Iran.
Alikuwa akiishi uhamishoni nchini Uswidi kwa muongo mmoja alipotekwa nyara na maajenti wa Iran nchini Uturuki mwaka 2020.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uswidi Tobias Billstrom alisema serikali yake imeitaka Iran kutomnyonga Chaab.
"Hukumu ya kifo ni adhabu ya kinyama na isiyofaa na Sweden, mataifa mengine ya EU, yanalaani utekelezaji wake kwa hali zote," alisema.
Mahakama ya Iran ilimshutumu Chaab kwa kuongoza Harakat al-Nidal, au Vuguvugu la Mapambano ya Ukombozi wa Waarabu wa Ahvaz, ambalo Iran inasema ni kundi la kigaidi lililoendesha mashambulizi kusini-magharibi mwa nchi hiyo.
Jimbo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta lina Waarabu walio wachache ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia kutengwa na kubaguliwa, jambo ambalo Tehran inakanusha.
Shambulio la 2018 kwenye gwaride la kijeshi katika mji wa Ahvaz lilishuhudia watu wenye silaha wakiwafyatulia risasi wanajeshi wa Walinzi wa Mapinduzi, na kuua watu 25 wakiwemo wanajeshi na raia waliokuwa wakitazama gwaride hilo.
Chaab aliripotiwa kuhadaiwa na kuletwa hadi Istanbul kukutana na mwanamke kabla ya kutekwa nyara na kusafirishwa hadi Iran katika operesheni inayosemekana kuratibiwa na kiongozi maarufu wa uhalifu wa Iran anayeishi Uturuki.
Maafisa wa Iran hawajatoa maelezo kuhusu jinsi Chaab alivyokamatwa.
Pia unaweza kusoma:
- Hukumu ya kifo: Ni nchi ngapi ambazo bado zinatekeleza hukumu ya kifo?
- Adhabu ya kifo Tanzania: 'Nilihukumiwa kunyongwa bila kosa'
Katika Picha: Wageni wanawasili Westminster Abbey
Watu wanamiminika Westminister Abbey muda huu kuajiandaa kwa sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Charlse III wa Uingereza.

Chanzo cha picha, PA Media

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, PA Media

Chanzo cha picha, PA Media

Chanzo cha picha, Getty Images
Pande zinazozozana Sudan zajiandaa kwa mazungumzo Saudi Arabia

Chanzo cha picha, Reuters
Saudi Arabia itaandaa mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana siku ya Jumamosi kati ya majeshi yanayopigana nchini Sudan, baada ya usitishaji mapigano mara kadhaa kutibuka.
Taarifa ya pamoja ya Marekani na Saudia imekaribisha kuanza kwa "majadiliano ya kabla ya mazungumzo" huko Jeddah kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Dharura(RSF).
Siku ya Ijumaa ripoti zilisema mapigano yanaendelea huko Khartoum.
Jeshi la Sudan linasema kuwa mazungumzo hayo yanalenga kushughulikia masuala ya kibinadamu.
RSF haijatoa kauli rasmi kuhusiana namazungumzo hayo.
Jeshi lilithibitisha kuwa limetuma wajumbe huko Jeddah kushiriki katika mazungumzo hayo, ambayo Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada yamekuwa yakishinikiza, yakikabiliwa na mzozo mbaya wa kibinadamu nchini Sudan.
Wiki tatu za mapigano makali yamesababisha vifo vya mamia ya watu na kuwafanya raia 450,000 kuyahama makazi yao.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji linasema, zaidi ya watu 115,000 wametafuta hifadhi katika nchi jirani.
Kamanda wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan - rais halisi wa Sudan - yuko katika mzozo mkali wa madaraka na kiongozi wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, kwa jina maarufu Hemedti.
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Sudan:Mahasimu wa Sudan wakubaliana 'kimsingi' kusitisha mapigano kwa wiki moja
- Mzozo wa Sudan: Mgogoro wa Sudan unaweza kuisha kwa njia hizi tatu
- Mzozo wa Sudan: Jeshi na RSF zalaumiana kwa kutoheshimu makubaliano ya kusistisha vita
Hujambo na karibu.
