Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mapigano Sudan: wanadiplomasia wa Uingereza waokolewa kutoka Sudan

Wanadiplomasia wa Uingereza na familia zao wameokolewa kutoka Sudani katika operesheni "ngumu na ya haraka’’ Waziri mkuu Rishi Sunak amethibitisha.

Moja kwa moja

  1. Thabo Bester: Mwili uliotumiwa na mbakaji sugu wa Afrika Kusini kutoroka gerezani watambuliwa

    Thabo Bester aliweza kujificha kwa mwaka mmoja kabla ya kukamatwa nchini Tanzania mapema mwezi huu

    Baba wa mwanaume ambaye mwili wake ulitumiwa na mbakaji sugu wa Afrika kusini kutoroka gerezani amedai kufahamu jinsi mwanaye alivyofariki

    Thabo Bester aliweza kutoroka gerezani mwaka jana baada ya kudanganya kuhusu kifo chake mwenyewe kwa kuwasha moto kwenye mahabusu yake.

    Mwili ulipatikana kando, ambao awali uliaminiwa kuwa ni wa Bester lakini sasa imefahamika kuwaulikuwa ni mwili wa Katlego Bereng.

    Baba yake, Batho Mpholo, anasema anahitaji kujua " anataka kufahamu ukweli halisi".

    Anasema kwamba polisi walimwambia kwamba mwanaye alikuwa ameanguka katika mji wa Bloemfontein na baadaye akafariki hospitalini, kabla ya kupelekwa katika hifadhi ya maiti.

    "Ni vipi Thabo Bester aliupata mwili wa mwanangu kama alikuwa katika hifadhi ya maiti ya serikali’’, aliuliza katika mahojiano na kituo cha habari cha ENCA news channel.

    Wakati mwili ulipopatikana katika mahabusu ulipimwa tena mwezi machi mwaka huu baada ya mashaka yaliyoibuliwa na vyombo vya habari nchini Afrika kusini, ilibainika kwamba mtu aliyepatikana alikuwa amefariki kutokana na majeraha ya kuungua kwa moto kwenye kichwa chake.

    Bw Mpholo anasema haamini maelezo ya polisi kuhusu kile kilichotokea kwa mwanaye, ambaye alikuwa na umri wa miaka 31, wakati alipotoweka mwezi Aprili, 2022.

    Polisi ya Afrika Kusini imekataa kuzungumzia kuhusu kauli iliyotolewa ni Bw Mpholo, licha ya kusema kuwa wameridhidhwa na kwamba kesi imeisha kwa familia.

    Unaweza pia kusoma:

    • Thabo Bester: Mbakaji wa Afrika Kusini ambaye alidanganya kifo chake ili kutoroka jela
  2. Habari za hivi punde, Mapigano Sudan: wanadiplomasia wa Uingereza waokolewa kutoka Sudan

    Wanadiplomasia wa Uingereza na familia zao wameokolewa kutoka Sudani katika operesheni "ngumu na ya haraka’’ Waziri mkuu Rishi Sunak amethibitisha.

    Bw Sunak alisema kuwa kazi ilikuwa ikiendelea kuhakikisha usalama unakuwepo kwa raia wa Uingereza wanaobakia nchini Sudan.

    Waliookolewa walichukuliwa katika uwanja wa ndege uliopo nje ya Khartoum usiku, Waziri wa ulinzi Ben Wellace ameiambia BBC.

    Ghasia kubwa ziliibuka wiki iliyopita katika mji mkuu Khartoum baina ya makundi mawili ya kijeshi yanayohasimiana.

  3. Je kampeni ya ‘’kuwa mwanaume ‘’ iliyoanzishwa Urusi ni nini?

    "Wewe ni mwanaume. Kuwa mwanaume," linasema tangazo la kibiashara la Wizara ya ulinzi likiwataka Warusi kujiunga na jeshi

    Matangazo mengi ya kibiashara yanaonekana kuanzishwa nchini Urusi kuwataka raia wajiunge na jeshi.

    Hii inakuja huku vikosi vya Urusi vikiripotiwa kupoteza vibayana kuhangaika kusonga mbele kuelekea Ukrainezaidi yam waka mmoja tangu vianze uvamizi.

    Wizara ya ulinzi mjini Moscow ilioa video ikiwaomba Warusi kuacha kazi zao za kiraiaili kufanya mikataba ya kazi na jeshi.

    Video hiyo ilimuonyesha mlinzi wa maduka ya jumla (supermarket ), mwalimu wa mazoezi ya mwili na dereva wa teksi – wote pamoja wakionekana kutofurahishwa na maisha ya uraia baada ya kuridhika baada ya kujiunga na jeshi.

    Video hiyo inaahidi kutoa mshahara watakriban robo 204,000 ($2,500; £2,000), mara nne zaidi ya wastani wa mshahara wa Urusi.

    Wanapropaganda wa Ukraine walikuwa tayari kupinga tangazo hilo, wakitoa tangazo laolililoharirirwa huku wakibadilisha maneno. Walioonekana kwenye video hiyo wanaelezea kupinga mauajiya watoto na ukataji wa vichwa vya watu, na ‘’hatutaki kuwajibishwa kwa ajili ya mauaji ya uhalifu wa kivita wa [Rais Vladimir]".

    Huku lile la Urusi likisema ‘’kuwa mwanaume ", video ya Ukraine "kuwa mtu" - kwa maneno mengine, usitekeleze maasi.

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  4. NYT: Jack Teixeira amekuwa akituma nyaraka za siri za pentagon tangu mwanzoni mwa vita vya Ukraine

    Mwanajeshi wa Massachusetts National Guard, nchini Marekani Private Jack Teixeira, anayeshutumiwa kufichua mamia ya nyaraka za siri za Pentagon, alianza kutuma taarifa hizo kutoka siku za mwanzoni za vita vya Ukraine, na katika kikundi cha wazi cyenye washiriki mamia kadhaa, limebaini gazeti la New York Times.

    Gazeti hilo liligundua kuwa awali jumbe ambazo hazikutambulika kutoka kwa akaunti ya Teixeira kutoka katika sava vyingine ya kikundi katika mtandao wa siri, zilikuwa ni maarufu miongoni mwa wachezaji wa michezo ya kompyuta, baada ya kutumwa na Teixeira.

    taarifa hizo za siri zilianza kuonekana mwishoni mwa mwezi wa Februari 2022, saa 48 kabla ya kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine, na kusitishwa Machi 19 mwaka huu, wakati Teixeira alipoandika: "Nimeamua kuacha kutuma taarifa hizi."

    Teixeira alikamatwa na FBI tarehe 13 Aprili, baada ya waandishi wa habari kufahamu kuhusu uvujaji wa nyaraka hizo.

  5. Shilingi bilioni 2 za Uganda ziliibiwa kwenye ATM kwa siku 14

    Kikosi maalum cha polisi nchini Uganda -Flying Squad, kinachunguza wizi wa kushangaza uliofanyika kwenye machine za kutoa na kuweka pesa (ATMs), katika vitongoji vinne vya jiji la Kampala na matokeo, yake shilingi bilioni 2 za Uganda zikapotea katika kipindi cha wiki mbili, limeripoti gazeti la Sunday Monitor.

    Mtandao wa wezi 15 ulikamatwa siku chache zilizopita baada ya timu ya walinzi wa kampuni ya ulinzi ya SGA Security Group kutumwa kuongeza pesa kwenye mashine yaATM f iliyopo kwenye benki yya kitongoji cha Nansana ambapo pesa zilipotea.

    Maafisa wanaojaza pesa kwenye ATM , walikuwa wamepewa pesa, nywira (passwords) na alama za siri ili kuweza kuchukua pesa katika ATM ya Nansana. Walikuwa welindwa na walinzi.

    Maafisa wa kuweka pesa na walinzi wao kwa pamoja walitoweka, jambo lililoifanyaSGA Security Group kufanya uchunguzi ambao ulifichua kuwa shilingi bilioni 2 ziliibiwa – huenda na wafanyakazi wake.

    SGA Security Group husimamia shughuli zamachine za ATM kwa niaba ya taasisi kadha za kifedha zikiwembo benki nchini Uganda.

    Timu ya maafisa wa usalama wa kampuni ya SGA Security Group ilisambaa katika eneo la Nansana kwa ajili ya kile kilichodhaniwa kuwa ni shuguli ya kawaida ya kuongeza pesa kwenye ATM ikiwa na wahudumu watano.

    Jumapili gazeti la Sunday Monitor limefahamu kua wote walipotea na kiasi cha fedha ambacho hakijafahamika.

    Hii ni mara ya pili pesa zinapotea kwenye benki yaNansana katika hali ya kutatanisha kwenye mashina ya ATM.

    Wafanyakazi kumi wa SGA Security Group kwa sasa wanashikiliwa polisi baada ya machine za ATM za Kawaala, Namirembe Road, Kasubi na Nansana kuwekwa kiasi kidogo sana cha pesa ikilinganishwa , na shilingi bilioni 2 zilizopaswa kujazwa kwenye ATM.

  6. Burundi: Waziri mkuu wa zamani wa zamani Alain Bunyonyi anashikiliwa na ngazi za usalama

    Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Burundi, CNIDH, limesema kuwa lilimtembelea aliyekuwa Waziri mkuu wa Burundi , Alain-Guillaume Bunyoni, lakini halikutaja yuko wapi.

    Hii inakuja baada ya taarifa zilizotolewa na waziri wa ulinzi , usalama na maendeleo wa Burundi Martin Niteretse, ambaye alikiri kuwa Jenerali Bonyonyi anasakwa ili afikishwe mahakamani.

    CNIDH halisemi lilimpata wapi wala alisimamishwa kazi na nani, lakini limesema kuwa “Hali yake ni nzuri. Hakuteswa hata mara moja au kufanyiwa jambo lolote baya tangu aliposimamishwa kazi ”.

    Alipoulizwa na BBC, ni wapi amefungiwa, mkuu wa CNIDH alisema kuwa sio jukumu lake kusema ni wapi alipo Jenerali Bunyonyi.

    Wakati huo huo, baada ya maelezo ya CNIDH, chanzo cha idara ya upepelelezi ya taifa, SNR, kiliiambia BBC kuwa yuko mikononi mwake.

    Jenerali Bunyoni alikuwa waziri mkuu wa Burundi tangu alipoingia madarakani Rais Evariste Ndayishimiye baada ya kushinda uchaguzi mwaka 2020.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mfahamu Alain-Guillaume Bunyoni, Waziri Mkuu mpya wa Burundi
  7. Kenya: Miili 18 zaidi yafufuliwa katika uchunguzi unaohusisha kanisa lililowaagiza watu kufunga hadi kufa

    Polisi wa Kenya wamefukua miili 47 karibu na mji wa pwani wa Malindi, huku wakimchunguza mhubiri anayesemekana kuwaambia wafuasi wake kufa kwa njaa.

    Miili ya watoto ilikuwa miongoni mwa waliofariki.Polisi walisema uchimbaji wa makaburi mengine ili kutafuta miili zaidi unaendelea.

    Makaburi hayo yenye kina kifupi yako katika msitu wa Shakahola, ambapo waumini 15 wa Kanisa la Good News International waliokolewa wiki iliyopita.

    Kiongozi wa kanisa hilo, Paul Makenzie Nthenge yuko rumande, akisubiri kufikishwa mahakamani.

    Shirika la utangazaji la KBC lilimtaja kama "kiongozi wa ibada", na liliripoti kuwa hadi sasa makaburi 58 yametambuliwa.

    Moja ya makaburi hayo inaaminika kuwa na miili ya watu watano wa familia moja - watoto watatu na wazazi wao.

    Bw Nthenge amekana kutenda makosa, lakini amenyimwa dhamana.Anasisitiza kwamba alifunga kanisa lake mnamo 2019.

    Inadaiwa aliwaambia wafuasi wajinyime kwa njaa ili "kukutana na Yesu".

    Gazeti la kila siku la Kenya, The Standard, lilisema wataalamu wa magonjwa watachukua sampuli za DNA na kufanya vipimo ili kubaini iwapo waathiriwa walikufa kwa njaa.

    Polisi walimkamata Bw Nthenge kufunga hadi kufa.

    Victor Kaudo wa Kituo cha Haki za Kijamii cha Malindi aliambia Citizen TV "tunapokuwa kwenye msitu huu na kufika katika eneo ambalo tunaona msalaba mkubwa na mrefu, tunajua hiyo inamaanisha zaidi ya watu watano wamezikwa humo".

    Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya, Kithure Kindiki, alisema ekari zote 800 za msitu huo zimefungiwa na kutangazwa kuwa eneo la uhalifu.

    Bw Nthenge alidaiwa kuvipa majina vijiji vitatu vya Nazareti, Bethlehemu na Yudea na kuwabatiza wafuasi kwenye madimbwi kabla ya kuwaambia wafunge, gazeti la The Standard linaripoti.

    Kenya ni nchi ya kidini na kumekuwa na visa vya hapo awali vya watu kuvutiwa katika makanisa hatari, yasiyodhibitiwa au madhehebu.

  8. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara ya leo Jumapili tarehe 23.04.2023