Thabo Bester: Mwili uliotumiwa na mbakaji sugu wa Afrika Kusini kutoroka gerezani watambuliwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Thabo Bester aliweza kujificha kwa mwaka mmoja kabla ya kukamatwa nchini Tanzania mapema mwezi huu
Baba wa mwanaume ambaye mwili wake ulitumiwa na mbakaji sugu wa Afrika kusini kutoroka gerezani amedai kufahamu jinsi mwanaye alivyofariki
Thabo Bester aliweza kutoroka gerezani mwaka jana baada ya kudanganya kuhusu kifo chake mwenyewe kwa kuwasha moto kwenye mahabusu yake.
Mwili ulipatikana kando, ambao awali uliaminiwa kuwa ni wa Bester lakini sasa imefahamika kuwaulikuwa ni mwili wa Katlego Bereng.
Baba yake, Batho Mpholo, anasema anahitaji kujua " anataka kufahamu ukweli halisi".
Anasema kwamba polisi walimwambia kwamba mwanaye alikuwa ameanguka katika mji wa Bloemfontein na baadaye akafariki hospitalini, kabla ya kupelekwa katika hifadhi ya maiti.
"Ni vipi Thabo Bester aliupata mwili wa mwanangu kama alikuwa katika hifadhi ya maiti ya serikali’’, aliuliza katika mahojiano na kituo cha habari cha ENCA news channel.
Wakati mwili ulipopatikana katika mahabusu ulipimwa tena mwezi machi mwaka huu baada ya mashaka yaliyoibuliwa na vyombo vya habari nchini Afrika kusini, ilibainika kwamba mtu aliyepatikana alikuwa amefariki kutokana na majeraha ya kuungua kwa moto kwenye kichwa chake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Bw Mpholo anasema haamini maelezo ya polisi kuhusu kile kilichotokea kwa mwanaye, ambaye alikuwa na umri wa miaka 31, wakati alipotoweka mwezi Aprili, 2022.
Polisi ya Afrika Kusini imekataa kuzungumzia kuhusu kauli iliyotolewa ni Bw Mpholo, licha ya kusema kuwa wameridhidhwa na kwamba kesi imeisha kwa familia.
Unaweza pia kusoma:
- Thabo Bester: Mbakaji wa Afrika Kusini ambaye alidanganya kifo chake ili kutoroka jela





