Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mpango wa wahamiaji wa Rwanda: Mahakama yaruhusu ndege ya kwanza kuelekea Rwanda

Ndege ya kwanza ya serikali ya Uingereza inayowapeleka wa waombaji wa uhamiaji hadi Rwanda inaweza kufanya safari hiyo Jumanne, Majaji wa mahakama ya rufaa wamesema.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Mpango wa wahamiaji wa Rwanda: Mahakama yaruhusu ndege ya kwanza kuelekea Rwanda

    Ndege ya kwanza ya serikali ya Uingereza inayowapeleka wa waombaji wa uhamiaji hadi Rwanda inaweza kufanya safari hiyo Jumanne, Majaji wa mahakama ya rufaa wamesema.

    Mahakama hiyo imeunga mkono uamuazi uliotolewa awali na Mahakama ya juu nchini humo kwambani katika "maslahi ya umma" kwa serikali kutekeleza sera zake.

    Chini ya mpango huo, baadhi ya wale wanaoingia nchini Uingereza kinyume cha sheria watasafirishwa kwa ndege hadi Rwanda ambako wataweza kutuma maombi ya uhamiaji wakiwa huko.

    Wanaharakati walikuwa wakijaribu kuzuwia ndege kusafiri kabla ya kesi kamili kusikilizwa juu ya iwapo sera hiyo ni ya kisheria mwezi ujao.

    Mapemamahakama iliambiwa kuwa watu 11 walitarajiwa kuondoka katika ndege ya Jumanne.

    Hatahivyo, shirika la misaada la Care4Calais, ambalo lilikuwa ni miongoni mwa wale waliokata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya juu, lilisema kuwa watu wanane tu ndio wanaojiandaa kusafirishwa kwa ndege hadi Rwanda.

    Idadi imepungua kwa kiwango kikubwa baada ya sera hiyo kupingwa kisheria ikihusishwa na utumwa wa kisasa na madai ya haki za binadamu, Chanzo cha wizara ya mambo ya ndani kimeiambia BBC.

    Serikali inatumaini kuwa mpango huo utawakatisha tamaa wanaoomba uhamiaji ya kuvuka njia za kuingia Uingereza na hivyo kuzuwia magenge ya wafanyabiashara haramu ya watu.

    Lakini Care4Calais limeuelezea mpango huo kama " ukatili ", na mfumo huo umekosolewa na mashirika mengine, viongozi wa kidini navyama vya upinzani.

    Sera hiyo itawasaidia watu hao kupata makazi na usaidizi nchini Rwanda huku maombi yao yakiangaliwa na serikali ya Rwanda.

    Iwapo yatafanikiwa, wanaweza kuendelea kubakia nchini Rwanda kwa hadi miaka mitano, wakiwa na uwezo kupata elimu na usaidizi mwingine.

    Wale ambao maombi yao ya uhamiaji yatakataliwa nchini Rwanda watapewa fursa ya kuomba kwa kutumia njia nyingine za uhamiaji, lakini wanaweza kukabiliwa nahatua ya kurejeshwa walikotoka.

    Unaweza pia kusoma:

    • 'Mpango wa Uingereza wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda 'ni kinyume cha Mungu' - Welby
    • Mkataba wa wahamiaji wa Uingereza: Je, Rwanda ni nchi ya usalama au hofu?
  3. Ghadhab ya Waislam wa India yaendelea baada ya kauli za kumtusi Mtume Mohammad

    Waislamu nchini India wanaendelea kuonyesha hasira yao kuhusu matamshi ya Msemaji wa chama tawala cha India cha BJP, ya matusi dhidi ya Mtume Mohammad (SAS).

    Chama cha BJP kilimsimamisha kazi Bi Nupur Sharma , ambaye amelaumiwa kwa kumtusi Mtume Mohammad mwezi uliopia.

    Hatahivyo Waislamu nchini India wamekuwa wakiendelea na maandamano kulaani kitendo hiyo.

    Kuharibiwa kwa nyumba za baadhi ya Waislamu katika Uttar Pradesh pia kumechochea maandamano na polisi inasema walihusika katika ghasia.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mtume Muhammad: Mfahamu mwanamke wa India aliyemtusi Mtume Muhammad
    • Nabii Muhammad: Putin atuma ujumbe kwa India baada ya kumtusi Mtume Mohammad
  4. Pitso Mosimane: Kocha wa Al Ahly aachana na wababe wa Misri

    Pitso Mosimane ameachana na miamba ya Misri Al Ahly kwa makubaliano, miezi mitatu baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kama kocha mkuu.

    Raia huyo wa Afrika Kusini aliiongoza klabu hiyo ya Cairo kunyakua mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kujiunga nayo mwaka 2020, lakini timu yake ilipoteza fainali ya msimu huu kwa Wydad Casablanca.

    Mosimane mwenye umri wa miaka 57 pia alifanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu mfululizo katika Kombe la Dunia la Klabu, ikiwa ni pamoja na michuano ya 2021 iliyochezwa Februari.

    Uamuzi wa kuachana nao ulifikiwa kufuatia kikao kilichofanywa na rais wa Al Ahly Mahmoud El Khatib, mwenyekiti Yassin Mansour, mjumbe wa bodi Hossam Ghaly na wajumbe wengine wa kamati ya mipango ya klabu hiyo.

    Taarifa ilisema kuwa klabu hiyo inatamani Mosimane aendelee na Ahly, lakini kocha huyo wa zamani wa Afrika Kusini na Mamelodi Sundowns aliomba kuondoka katika klabu hiyo.

    "Wakati wa mkutano huo, wote waliamua kwamba aendelee na ariri aliyokuwa nayo Al Ahly kutokana na mafanikio aliyoweza kuyatimiza," taarifa ya Al Ahly ilisema.

    "Lakini, wakati wa mkutano ambao ulifanyika hapo awali, Mosimane aliomba kuondoka. "Uamuzi wa Mosimane ulijadiliwa na ikaamuliwa kuidhinisha ombi lake la kuachana na klabu."

    Mosimane alikuwa amekubali kusaini mkataba mpya mwezi Machi, ambao ungemwezesha kusalia Ahly hadi 2024.

    Samy Komsan amepewa nafasi ya kuongoza kwa muda kwa michezo ijayo ya kikosi cha kwanza katika Ligi Kuu ya Misri na Kombe la Misri.

  5. Erling Haaland: Manchester City wakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Norway kutoka Borussia Dortmund

    Erling Haaland anasema yuko "mahali pazuri kutimiza ndoto yake" baada ya kukamilisha uhamisho wa £51.2m kwenda Manchester City kutoka Borussia Dortmund.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifunga mabao 86 katika miche 89 aliyoichezea Dortmund na kufika kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu kama mmoja wa washambuliaji wanaotamaniwa sana katika soka duniani.

    Amesaini mkataba wa miaka mitano hadi 2027 na atajiunga na City Julai tarehe moja.

    Makubaliano ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway yalifikiwamwezi Mei baada ya City kuamilisha kipengele cha kuachiliwa kwake.

    "Hii ni siku ya kujivunia kwangu na kwa familia yangu," alisema Haaland, mtoto wa nahodha wa zamani wa City Alf-Inge, ambaye aliichezea klabu hiyo kati ya 2000 na 2003.

    "Siku zote nimekuwa nikiitazama City na nimejipata nikifanya hivyo katika misimu ya hivi karibuni.

    Huwezi kujizuia kufurahia aina yao ya uchezaji - inasisimua na wanatengeneza nafasi nyingi, ambazo ni sawa kwa mchezaji kama mimi," aliongeza.

    "Kuna wachezaji wengi wa kiwango cha kimataifa kwenye kikosi hiki na Pep [Guardiola] ni mmoja wa makocha wakubwa wa muda wote, hivyo ninaamini niko mahali pazuri kutimiza matamanio yangu.

    "Nataka kufunga mabao, kushinda mataji, na kuimarika kama mwanasoka na nina imani naweza kufanya hivyo hapa.

    Hii ni hatua nzuri kwangu, nakamia sanakuanza kwa msimu mpya."

    Maelezo zaidi:

  6. Waasi wadai kuuteka mji wa mpakani wa DR Congo

    Waasi wa M23 mashariki mwa DR Congo wanadai kuuteka mji wa mpakani wa Bunagana karibu na Uganda, kwa mujibu wa msemaji wao.

    "Tunadhibiti mji mzima sasa," Willy Ngoma, msemaji wa M23 aliiambia BBC Maziwa Makuu.

    Madai hayo yanafuatia mapigano makali kati ya jeshi na waasi ambayo siku ya Jumatatu yalishuhudia baadhi ya wanajeshi wa serikali wakivuka hadi Uganda, ripoti ya Radio Okapi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ikinukuu vyanzo.

    Mamlaka ya DR Congo bado haijatoa maoni yoyote kuhusu madai ya M23.

    Msemaji wa jeshi Lt Kanali Guillaume Ndjike Kaiko alisema atatoa maoni yake "baadaye", lakini taarifa ya Jumapili usiku ilisema walikomesha shambulio la waasi huko Bunagana.

    Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 30,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano ya hivi punde.

    Mji wa Bunagana ni wa kimkakati katika biashara ya kuvuka mpaka na unapatikana baadhi ya kilomita 70 (maili 43) kaskazini-mashariki mwa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

    Mji huo ulitumika kama kituo cha M23 walipoiteka Goma mnamo Novemba 2012 kabla ya kushindwa vita na kukimbilia Uganda.

    Maelezo zaidi:

    • DR Congo: FARDC yaishtumu Rwanda kwa kuisaidia M23
    • Mzozo wa DRC na Rwanda : M23, majirani na bahati mbaya ya DRC
  7. Kenya: Asilimia 6 ya watoto wameshirikisha picha au video zao za utupu

    Upatikanaji wa mtandao kwa urahisi umefanya watoto kuwa katika hatari ya kukabiliwa watu wanaotaka kuwatumia vibaya.

    Hilo limedhihirika katika ripoti iliyopewa jina la ‘Disrupting Harm in Kenya’ iliyotolewa na Wizara ya Utumishi wa Umma, Jinsia, Masuala ya Wazee na Mipango Maalum nchini Kenya.

    Upatikanaji huu wa mtandao kwa urahisi kwa watoto kumesababisha idadi kubwa ya watoto kuwa na uwezo wa kuangalia picha za ponografia, kutumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya na hata makundi ya kidhehebu wakati wakiwa mtandaoni kulingana na ripoti ya Wizara ya Utumishi wa Umma, Jinsia, Masuala ya Wazee na Mipango Maalum nchini Kenya.

    ‘’Katika ulimwengu unaozidi kuathiriwa na mageuzi ya haraka na kupitishwa kwa teknolojia ya dijitali, mtandao ni nyenzo ya watoto kujihusisha kwa njia inayowawezesha sana, lakini pia ni upanga wenye makali kuwili hivyo mkakati unahitajika kwa matumizi sahihi. mtandao kwa manufaa na wakati huo huo fahamu hatari zinazotokana na mtandao,’’ Waziri wa wizara hiyo Margaret Kobia alisema wakati akitoa maoni yake kuhusu matokeo ya ropoti hiyo.

    Ripoti hiyo inasema kuwa 14% ya watoto walikutana na mtu ana kwa ana baada ya kukutana naye mtandaoni mwaka uliopita.

    Pia (watoto 60) walikuwa wameshirikisha picha au video zao wakiwa uchi na watumiaji wengine wa mtandao katika mwaka uliopita.

    Watoto wengi wamenaswa na watu hao wenye nia mbaya ambao huwatumia video za ngono huku wengine wakitumbikia kwenye mikono ya walaghai wanaowauliza maelezo ya kibinafsi.

  8. DRC: Zaidi ya 30,000 wakimbia mapigano ya Jumapili huko Bunagana

    Zaidi ya watu 30,000 waliokimbia makazi yao walikimbia mapigano ya Jumapili kati ya vikosi vya serikali, FARDC, na waasi wa M23 huko Bunagana na viunga vyake katika eneo la Rutshuru katika jimbo la Kivu Kaskazini, kulingana na UN.

    Baada ya mapigano hayo, mji wa Bunagana uko chini ya udhibiti wa vikosi vya serikali, kulingana na taarifa.

    Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 5,000 wametoroka eneo la Bunangana na viunga vyake hadi Uganda, kulingana na Umoja wa Mataifa.

    Shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda linasema kuwa kuna haja ya msaada zaidi kwa wakimbizi wa Jumapili.

    Zaidi ya wengine 25,000 pia walikimbia makwao siku ya Jumapili hadi shule na makanisa huko Rwanguba, Kabindi na Kinoni kwenye barabara ya Rutshuru, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi, OCHA.

    Jumapili usiku, msemaji wa M23 aliambia BBC kwamba wanajeshi wengi wa FARDC waliuawa katika mapigano hayo na wengine walikimbia na silaha zao.

    Alipoulizwa iwapo walikuwa wanasimamia mji wa Bunagana, Willy Ngoma alisema: FARDC inadai kuwa imerudi nyuma na kuwasaka wapiganaji wa M23 ambao walivamia Bunagana na ‘’kuacha maiti kadhaa’’.

    Taarifa iliyotolewa na FARDC ilisema wakati wa mapigano ya Jumapili, walisaidiwa na ndege za kivita za MONUSCO.

    FARCD pia iliishutumu Rwanda kwa kuwasaidia M23 katika jaribio la kuiteka Bunagana, jambo ambalo serikali ya Rwanda imekuwa ikikanusha mara kwa mara.

    Inadaiwa kuwa mshambuliaji huyo alilipua eneo la kituo cha polisi cha Bunagana muda mfupi baadaye.

  9. Urusi yadai kuharibu silaha za Magharibi mashariki mwa Ukraine

    Wizara ya ulinzi ya Urusi inasema kuwa imeharibu silaha nyingi na zana za kijeshi katika eneo la Donetsk, zikiwemo baadhi zilizotumwa kutoka Marekani na Ulaya.

    Ilisema makombora ya anga ya juu yalipiga karibu na kituo cha reli cha Udachne, na kugonga vifaa ambavyo viliwasilishwa kwa vikosi vya Ukraine.

    BBC haiwezi kuthibitisha madai hayo, lakini ikiwa ni kweli, itakuwa pigo kubwa kwa Ukraine, ambayo inakabiliwa na hasara kubwa katika eneo la mashariki la Donbas, ambako Urusi ina silaha nyingi.

    Soma zaidi:

  10. Ukraine yatoa wito wa ulinzi wa anga na msaada wa silaha

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito wa kuwekewa kwa mifumo ya kisasa ya ulinzi wa makombora kwa nchi yake akisema kuwa zaidi ya makombora 2,600 yametua nchini mwake tangu kuanza kwa uvamizi huo.

    Mifumo ya Iron Dome wa Israeli na American Patriot batteries ndio aina ya mifumo ambayo Zelensky anasema nchi yake inahitaji.

    Makombora ya umbali mrefu ya Urusi yamekuwa wakirushwa kuelekea Ukraine tangu kuanza kwa vita hivi, wakati mengi yamedunguliwa, mengi zaidi yamefanikiwa kutua nchini humo.

    Lakini ulinzi wa anga sio jambo pekee ambalo Waukraine wanataka.

    Wanasema wanahitaji sana mifumo zaidi ya silaha, huku mapigano katika eneo la mashariki la Donbas yakiendelea.

    Mapigano ya Severodonetsk yamegeuka kuwa vita vya umwagaji damu mitaani, na hasara kubwa zimeripotiwa pande zote mbili.

    Miongoni mwao ni mwanajeshi wa zamani wa Uingereza, aliyeuawa Ijumaa iliyopita.

    Mshauri wa Rais Zelensky alitoa pongezi kwa Jordan Gatley, akisema “alikuwa shujaa wa kweli.” Mykhailo Podolyak alisema: “Siku zote tutakumbuka mchango wake katika ulinzi wa Ukraine na ulimwengu huru.”

    Soma zaidi:

  11. 'Pigania kila hatua ya ardhi yako' Severodonetsk – Zelensky

    Katika hotuba yake ya kitamaduni ya video usiku wa manane, Rais Zelensky wa Ukraine alisema Urusi ilikuwa inapeleka "makurutu walio na mafunzo duni na wale waliokusanywa kwa uhamasishaji wa siri" katika eneo la mashariki la Donbas.

    Kulingana na yeye, Urusi inapeleka vikosi vya akiba huko Donbas kusaidia shambulio lake kwenye jiji la Severodonetsk, "ambapo mapigano makali sana yanaendelea kwa kila mita", pamoja na Lysychansk, Bakhmut na maeneo mengine.

    "Urusi inaweza kupita wanajeshi wake 40,000 waliopoteza maisha tayari kufikia mwezi Juni. Katika vita vingine katika miongo mingi wamepoteza sana," alisema, akiwashutumu majenerali wa Kirusi kwa kuona watu wao kama "wakifyekwa-fyekwa na mizinga".

    Kwa mara nyingine tena alitoa wito kwa viongozi wa dunia kuipatia Ukraine mifumo ya kisasa ya kujikinga na makombora, akitaja majeruhi wa shambulio la hivi punde la kombora magharibi mwa Ukraine.

  12. Habari za hivi punde, Urusi inataka kulinyakua eneo la Severodonetsk - gavana

    Kama ambavyo tumekuwa tukiripoti , vita vinaendelea katika eneo la Severodonetsk , ambapo hali inaendelea kuwa ngumu , baada ya jeshi la Urusi kuharibu daraja la pili kuingia katika mji huo na imekuwa ikishambulia daraja la mwisho kulingana na gavana wa jimbo hilo Serhiy Haidai.

    Uharibifu wa daraja la pili ukivuka mto na kuingia Lysychansk unamaanisha Urusi imejizatiti kuukata na kuuteka mji wa Severodonetsk, anasema.

    ‘’Tayari haupitiki , na kwasasa wanaendelea kushambulia daraja la mwisho la tatu. Kama ninavyoelewa , wanataka kuukata mji huo ili kutowezesha uokozi wa watu kufanyika , ama kuleta usaidizi’’ , alisea siku ya Jumapili.

    "Pengine leo au kesho, watatumia kila njia ili kujaribu kuuteka mji huo. Au pengine maeneo mengine ili kuweza kuukata na hatimaye kuidhibiti barabara ya Lysychansk-Bakhmut," alisema.

  13. Rufaa ya kupinga usafirishaji wa waomba hifadhi hadi Rwanda kusikilizwa

    Mahakama ya Rufaa inatazamiwa kuamua baadaye ikiwa itaruhusu ndege ya kwanza ya Ofisi ya Mambo ya Ndani kwenda Rwanda ikiwa na watu wanaotafuta hifadhi.

    Wanaharakati na wahamiaji wiki jana walishindwa kushinda zuio dhidi ya sera ya serikali katika Mahakama Kuu.

    Lakini inadhaniwa idadi inayokabiliwa na kuondolewa hadi mji mkuu wa Rwanda Kigali siku ya Jumanne imepungua sana.

    Uingereza inasema kuwatuma baadhi ya waomba hifadhi wanaofika kinyume cha sheria hadi nchini Rwanda kutadhoofisha magenge ya magendo yanayojihusisha na usafirishaji haramu wa binadamu.

    Rufaa hiyo imeletwa na Muungano wa Huduma za Umma na Biashara, ambao unawakilisha 80% ya wafanyakazi wa Kikosi cha Mipaka, pamoja na mashirika ya misaada Care4Calais na Detention Action.

    Kesi tofauti pia inatazamiwa kusikilizwa katika Mahakama Kuu siku ya Jumatatu, baada ya shirika lingine la kutoa misaada kwa wakimbizi, Asylum Aid, kutuma maombi ya zuio la dharura la muda dhidi ya safari za ndege kuelekea taifa hilo la Afrika mashariki.

    Chanzo cha Wizara ya Mambo ya Ndani kimeiambia BBC kwamba kati ya watu 37 waliopangwa kusafiri hadi Rwanda siku ya Jumanne, changamoto za kisheria zinazohusiana na utumwa wa kisasa na madai ya haki za binadamu zimepunguza idadi hiyo hadi chini ya 10.

    Mhariri wa BBC Mark Easton anasema inatarajiwa kwamba inaweza ‘’kupunguzwa hadi sifuri’’ kabla ya ndege hiyo kusafiri.

    Sera ya Rwanda imekosolewa na mashirika ya misaada, viongozi wa kidini, vyama vya upinzani - na kuripotiwa na Prince of Wales ambaye inaeleweka kuwa binafsi aliielezea kama ‘’ya kutisha’’.

    Soma zaidi:

  14. Fahamu matukio muhimu ya Ukraine kwa leo

    Fahamu matukio muhimu ya Ukraine kwa leo:

    • Makombora ambayo yanalaumiwa vikosi vya Urusi yamesababisha moto mkubwa katika kiwanda cha kemikali cha Azot katika mji muhimu wa mashariki wa Severodonetsk ambapo hadi raia 800 wanaripotiwa kupata makazi.
    • Maafisa wanasema vikosi vya Ukraine vinasalia kudhibiti kinu cha Azot na vikosi vya Urusi na washirika wao wanaotaka kujitenga huko Luhansk wamesema hawana mpango wa kuvamia kiwanda hicho kikubwa cha kemikali.
    • Mwanajeshi wa zamani wa Uingereza ameuawa akipigania jeshi la Ukraine huko Severodonetsk, familia yake imesema.
    • Ukraine imetoa wito kwa nchi za Magharibi kuwasilisha haraka silaha nzito ili kukabiliana na mashambulizi ya vikosi vya Urusi mashariki mwa nchi hiyo.
    • Jeshi la Urusi limeharibu daraja la pili linalounganisha miji jirani ya Severodonetsk na Lysychansk na wanashambulia wa tatu, Serhiy Haidai, gavana wa eneo la Luhansk, anasema.
    • Migahawa ya kwanza ya McDonald imefunguliwa huko Moscow leo chini ya umiliki mpya na jina jipya linaloitwa "Vkusno i tochka", ambalo hutafsiriwa "Kitamu na ndivyo hivyo".

    Soma zaidi:

  15. Kwa Picha: Wanajeshi wa Ukraine wakiwashambulia wanajeshi wa Urusi Donetsk

  16. Kiwanda cha kemikali chashambuliwa huku mapigano yakiendelea mashariki mwa Ukraine

    Vikosi vya Urusi na washirika wao wanaotaka kujitenga mjini Luhansk hawana mpango wa kushambulia kiwanda cha kemikalikatika mji wa Severodonetsk , ambapo vikosi vya Ukraine vimekita kambi , amesema mmoja ya maafisa hao wanaotaka kujitenga.

    Afisa huyo ambaye amekataa jina lake litajwe aliambia kitengo cha habari cha Urusi cha Interfax kwamba majadiliano na vikosi vya Ukraine katika eneo hilo yamefeli .

    Hakuna mpango wa kushambulia kiwanda cha Azot . Kiwanda hicho kimezingirwa . Wanajeshi wa Ukraine waliopo katika kiwanda hicho watalazimika kusalimu amri, afisa huyo alisema.

    Alipinga hatua ya kuwaachilia huru waondoke ili kujiunga na jeshi kuu la Ukraine – kitu walichodai walitaka.

    Mapema gavana wa Ukraine mjini Luhansk , Serhiy Haidai alisema kwamba takriban raia 800 ikiwemo Watoto walikuwa wakijificha katika mahandaki katika kiwanda hicho cha Azot . Alisema kwamba mashambulio ya Urusi yalisababisha moto mkubwa katika kiwanda hicho lakini hakuripotiwa majeruhi wowote wa Ukraine.

  17. Natumai hujambo