Ukraine na Urusi: 'Hatutakubali mupeleke silaha Ukraine’, Urusi yaiambia Marekani
Urusi imeionya Marekani dhidi ya kutuma silaha zaidi Ukraine , balozi wa urusi nchini Marekani ameambia runinga ya Urusi.
Moja kwa moja
Habari za hivi punde, Uingereza kupeleka magari haya ya kivita UKraine ili kulinda anga yao

Chanzo cha picha, Mike Weston/MOD
Maelezo ya picha, Gari la Kivita aina ya stormer Uingereza inaipatia Ukraine idadi ndogo ya magari ya kivita yalio na uwezo wa kushambulia ndege ili kuimarisha ulinzi wa angani wa taifa hilo.
Waziri wa Ulinzi Ben Wallace aliambia bunge la Uingereza kwamba magari hayo ya kivita yatalipatia taifa hilo uwezo wa kukabiliana na ndege za adui mchana na usiku.
Alisema kwamba silaha ya StarStreak tayari ilikuwa imetumika nchini Ukraine kwa takriban wiki tatu.
Wallace alisema kwamba robo ya vikosi vya Urusi nchini Ukraine vilikuwa vimepunguzwa makali huku akiipongeza Ukraine kwa makabiliano makali.
Urusi yadai kukishambulia kiwanda cha kusafisha mafuta na maeneo ya kijeshi

Chanzo cha picha, Reuters
Vikosi vya Urusi vimedai kuteketeza vituo vya kusafishia mafuta huko Kremenchuk, mji ulioko katikati ya Ukraine kaskazini-magharibi mwa Dnipro, wizara ya ulinzi ilisema hayo Jumatatu.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov amesema katika taarifa za hivi karibuni kuhusu "operesheni maalum ya kijeshi" ya Urusi nchini Ukraine ni kuwa wamefanya shambulizi katika maeneo kadhaa ya kijeshi.
Akionekana kwenye kituo cha habari cha serikali Rossiya 24, Konashenkov alisema: "Vikosi vya kijeshi vya Urusi vinaendelea na operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine.
Silaha za masafa marefu zinazoongozwa kikamilifu zimeharibu vifaa katika kiwanda cha kusafisha mafuta katika maeneo ya kaskazini mwa mji wa Kremenchuk, pamoja na vifaa vya kuhifadhi bidhaa za petroli vinavyotoa vifaa vya kijeshi kwa kikundi cha askari wa Ukraine.
" Aliongeza kuwa vikosi vya Urusi "vimeshambulia vituo 56 vya kijeshi vya Ukraine". BBC haijaweza kuthibitisha madai haya.
Akaunti ya Youtube ya Diamond platnumz wafungwa kwa kukiuka muongozo

Chanzo cha picha, Diamond/Instagram
Akaunti ya You Tube ya mwanamuziki maarufu kutoka Afrika Mashariki Diamond Platinumz imefungwa kwa kukiuka utaratibu na masharti ya mtandao huo.
Akaunti hiyo rilikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 6 na video ambazo zimetazamwa na mamilioni ya watu.
Video yake maarufu aliyofanya na msanii kutoka Congo Dr Inno’s B ilikua na zaidi ya watazamaji milioni 100.
Kwa ujumla video zake zimetazamwa na watazamaji mara bilioni 1.
Sababu za kufungwa kwa mtandao zimeanishwa kuwa kukiuka masharti na sheria za mtandao.
Hatahivyo kwa mjibu wa meneja wa Diamond Hamisi Shaban Tale Tale amesema akaunt ya mnsanii huyo imechukuliwa na wadukuzi na hii ni mara ya pili kufanywa hivyo.
Diamond platnumz amekua ni msanii mwenye watazamaji wengi katika mtandao wa Youtube katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.
- Diamond Platnumz analinganishwaje na nyota wengine wa Afrika katika mtandao wa YouTube?
- Msanii nyota wa Tanzania Diamond Platnumz afikisha mashabiki milioni 5 youtube
Habari za hivi punde, ‘’Hatutakubali mupeleke silaha Ukraine’’, Urusi yaiambia Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Antonov Anatoly Urusi imeionya Marekani dhidi ya kutuma silaha zaidi Ukraine , balozi wa urusi nchini Marekani ameambia runinga ya Urusi.
‘’Tunasisitiza kwamba hatua ya Marekani kupeleka silaha Ukraine haikubaliki , na tunataka isitishwe mara moja’’, Anatoly Antoniv alinukuliwa na Reuters akisema katika mahojiano na chombo cha runinga cha Rossiya 24 .
Antonov alisema kwamba barua rasmi ya kidiplomasia imetumwa Washington ili kuonesha wasiwasi wa Urusi iliongezea.
Kama tunavyoripoti mapema leo alfajiri, Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani na waziri wa ulinzi Marekani alikutana na rais Zelensky mjini Kyiv jioni siku ya Jumapili, akiahidi msaada zaidi wa kijeshi utakaogharimu dola za Marekani milioni 700.
Mashambulizi ya anga yapiga vituo vya treni vya Ukraine
Kama tulivyoripoti hapo awali, mashambulizi ya Urusi yamepiga vituo kadhaa katikati na magharibi mwa Ukraine.
Mojawapo ya vituo walivyopiga ilikuwa Krasne, mashariki mwa Lviv. Maksym Kozytskyi, mkuu wa eneo la Lviv, amechapisha kwenye chaneli yake ya Telegram kwamba kombora liligonga kituo kidogo cha umeme hapo majira ya saa 08:30 za nchini humo (06:30 BST).
"Bado hakuna habari kuhusu majeruhi," aliandika.
Huduma za dharura ziko kwenye eneo la tukio na zinafanya kazi kuzima moto.
Picha zilizochapishwa mtandaoni zinaonesha moshi mwingi mweusi ukitoka kwenye tovuti.
Tunaelekea kituoni na kupiga king'ora kingine cha mashambulizi ya anga huko Lviv. Taarifa zaidi zitatolewa.
Watu kadhaa wauawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya vituo, mamlaka yanasema

Mamlaka ya hapo imetangaza idadi kadhaa ya makombora ya Urusi kwenye vituo vya magharibi na kati ya Ukraine.
Mkuu wa mkoa wa kati wa Vinnytsia ametangaza kwenye Telegraph kwamba kuna waliokufa na waliojeruhiwa , baada ya kuepo kwa mashambulizi hayo kwenye vituo vya Zhmerynka na Kozyatyn.
Serhiy Borzov hakusema ni wangapi waliojeruhiwa lakini alisema Warusi walikuwa wakijaribu kuharibu "miundombinu muhimu".
Shirika la reli la Ukraine limesitisha au kuelekeza treni upande wa magharibi na katikati baada ya mashambulizi hayo.
Jaji wa Uganda anusurika jaribio la kuua

Chanzo cha picha, Mahakama ya Uganda
Jaji wa Uganda amenusurika katika shambulio la silaha baada ya msafara wake kupigwa risasi Jumamosi usiku, mamlaka imesema.
Katika taarifa yake siku ya Jumapili, mahakama ilisema Jaji Flavian Zeija na timu yake hawakujeruhiwa wakati wa ufyatulianaji wa risasi uliotokea mwendo wa saa 19:00 majira ya Uganda.
Msemaji wa mahakama Jameson Karemani alitaja tukio hilo kuwa la kushtusha na kusema kuwa wahusika watafikishwa mahakamani.
Mamlaka imeanza uchunguzi kuhusu shambulio hilo.
Idadi ya watu wenye hadhi ya juu nchini Uganda wamewahi kulengwa na mashamulizi katika miaka ya hivi karibuni. Kesi nyingi bado hazijatatuliwa.
Mwezi Juni mwaka jana, waziri mmoja alinusurika jaribio la mauaji lililofanywa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki katika kitongoji cha Kampala. Binti yake na mlinzi wake waliuawa.
Wengine ambao wameuawa kwa kupigwa risasi katika hali kama hiyo ni pamoja na afisa mkuu wa polisi, mwendesha mashtaka mkuu na mbunge.
- Muhoozi Kainerugaba: Je, tunajua nini kuhusu tangazo la kustaafu la mtoto huyu wa Rais Museveni?
- Judith Nakitu : Mwanamke wa Uganda aliyepoteza figo yake bila kujua Saudia afidiwa
Mwili wa aliyekuwa rais wa Kenya, Mwai Kibaki wawasili Ikulu
Rais Uhuru Kenyatta na Mkewe Margaret Kenyatta, wameongoza nchi kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais Emilio Mwai Kibaki ambao umelazwa katika Bunge jijini Nairobi.
Mwili wa Rais Mwai Kibaki utalala Bungeni kwa siku tatu, kuanzia leo Jumatatu, Aprili 25 hadi Jumatano, Aprili 27, 2022, ili kuwapa Wakenya muda wa kutosha wa kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Mkuu wa Nchi.

Chanzo cha picha, Ikulu Kenya

Chanzo cha picha, Ikulu Kenya

Chanzo cha picha, Ikulu Kenya

Chanzo cha picha, Ikulu Kenya

Chanzo cha picha, Ikulu Kenya

Chanzo cha picha, Ikulu Kenya
- Mwai Kibaki: Ratiba ya mazishi ya aliyekuwa rais wa kwanza wa upinzani Kenya
- Mwai Kibaki: Fahamu mambo matano usiyoyajua kuhusu Mwai Kibaki
Bodi ya Twitter kukutana na Musk kujadili kuhusu zabuni

Chanzo cha picha, Getty Images
Bodi ya Twitter inaripotiwa kukutana na Elon Musk mwishoni mwa juma kujadiliana juu ofa yake ya dola bilioni 43 (£33.6bn) kuuchukua mtandao wa kijamii wa Twitter.
Baada ya bosi wa Tesla kubainisha ombi lake kwa mara ya kwanza, Uongozi wa Twitter ulitangaza mkakati unaojulikana kama "kidonge cha sumu" ili kuzuia uwezekano wa ununuzi mbaya.
Bw Musk anapanga kufadhili zabuni zake kwa kuungwa mkono na mkopeshaji wa Marekani Morgan Stanley na taasisi nyingine za kifedha.
Msemaji wa Twitter alikataa kutoa maoni yake kuhusu ripoti hizo.
Maelezo ya jinsi Bw Musk alivyokuwa na nia ya kufadhili ofa yake, ambayo yalifichuliwa kwa mamlaka ya Marekani siku ya Alhamisi, yaliifanya bodi ya Twitter yenye wanachama 11 kuzingatia kwa uzito mkubwa mpango unaowezekana, kwa mujibu wa Reuters, New York Times na Bloomberg - wakinukuu vyanzo vya habari ambavyo havikutajwa.
Bw Musk, ambaye ana miliki zaidi ya asilimia 9 ya hisa kwenye Twitter, amepanga kufadhili sehemu yenye thamani ya dola bilioni 46.5 za zabuni zake, kwa mujibu wa jalada la udhibiti.
Ufadhili huo utatoka kwa mchanganyiko wa mali yake mwenyewe na kuungwa mkono na kampuni kubwa ya benki ya Wall Street Morgan Stanley na makampuni mengine.
Inasemekana kuwa wanahisa kadhaa wa Twitter waliwasiliana na kampuni hiyo baada ya Bw Musk kutangaza mpango wa ufadhili na kuitaka isikose fursa ya kufikia makubalino.
- Elon Musk: Mmiliki wa kampuni ya Tesla atangazwa kuwa mwenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 185
- Elon Musk: Fahamu siri sita za ufanisi wa kibiashara kutoka kwa mtu tajiri zaidi duniani
Habari za hivi punde, Waziri wa ulinzi nchini Marekani anataka ‘kuona Urusi imedhoofishwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Lloyd Austin Afisa mkuu wa idara ya Pentagon nchini Marekani Lloyd Austin amesema siku ya Jumamosi kwamba Marekani inataka kuona Urusi imeedhofishwakwa kiwango cha kutoweze tena kutekeleza uvamizi kama ule ilioifanyia Ukraine .
Waziri huyo pia amesema kwamba anaamini kwamba Ukraine inaweza kushinda vita hivyo ikiwa itapata usaidizi wa kutosha . ".
Matamshi yake yanajiri kufuatia ziara yake ya Kyiv siku ya Jumapili pamoja na waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Antony Blinken, ambapo wote walikutana na Rais Zelensky.
Wakati wa ziara hiyo , walitangaza kwamba wanadiplomasia wa Marekani wataanza kurudi polepole ncini Ukraine na kwamba Marekani imeipatia msaada mwengine wa $700m wa silaha za kijeshi
Urusi inaonesha dalili za ujinga au kukata tamaa - mchambuzi

Chanzo cha picha, EPA
Imepita wiki moja tangu kuanza kwa harakati za Urusi zote kuanza kuteka na kukalia mashariki mwa Ukraine - kwa hivyo je, vikosi vya Kremlin viko karibu na mafanikio?
Profesa Phillips O'Brien, profesa wa masomo ya kimkakati katika Chuo Kikuu cha St Andrews, aliambia kipindi cha Today cha Radio 4 cha BBC kwamba jeshi la Urusi sivyo ambavyo wengi waliamini lingekuwa – likiishinda Ukraine kivita .
"Kwa kweli haijasonga mbele hata kidogo," anasema. "Wamepata hasara nyingi katika kampeni ya Kyiv na nyinginezo... na haipigani hasa kwa akili kadri tunavyoweza kusema." Pia anasisitiza kwamba wanadamu "sio tu mashine zinazoweza kupangwa".
"Wanajeshi hawa ambao walitolewa nje ya Kyiv walikuwa askari walioshindwa - waliona na wamefanya uhalifu wa kivita, waliona watu wakifa, walikuwa wamechoka, vifaa vyao vimepotea."
Ukweli ni kwamba Warusi hawawaruhusu wanajeshi wake kupumzika, anaendelea, "ni ishara ya ujinga au kukata tamaa".
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Ebola yaibuka tena DR Congo

Chanzo cha picha, AFP
Mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola umeenea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hii ni kwa mjibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Ingawa hadi sasa ni mtu mmoja pekee ambaye amethibitishwa kukutwa na Ebola, kuna wasiwasi kwamba mlipuko huo unaweza kusambaa, kwani mgonjwa huyo hakugunduliwa mapema na mara moja alikumbwa na hali ya kutojitambua kukosa fahamu.
Mwanamume huyo alikuwa mgonjwa kwa zaidi ya wiki moja kabla ya kutibiwa, na alifariki siku ambayo alilazwa hospitalini.
Tayari watu 100 walikutana na mgonjwa mmoja mwenye ebola wametambuliwa na WHO Watu hao sasa wanafuatiliwa kwa makini na mchakato wa chanjo utaanza.
Ugonjwa wa Ebola uliikumba Afrika Magharibi kati ya mwaka 2013 na 2016, na kuua takriban watu 11,000.
Ugonjwa huu unaua hadi 50% ya wagonjwa. Mlipuko huu mpya wa Ebola ulianza katika mji wa Mbandaka zaidi ya kilomita 500 kutoka mji mkuu Kinshasa katika jimbo la kaskazini-magharibi mwa Ecuador nchini DR Congo.
Jiji hilo lina watu wengi na linajumuisha barabara zinazounganisha Kinshasa, pamoja na usafiri wa anga kati ya miji hiyo miwili.
- Coronavirus: Je dunia imepata funzo gani kutokana na mlipuko wa Ebola DRC?
- WHO yaidhinisha chanjo ya kwanza dhidi ya Ebola ambayo ni ya kwanza kutumika duniani
Kagame wa Rwanda akutana na Museveni katika mahusiano yanayoendelea kupamba moto

Chanzo cha picha, Yoweri Museveni Twitter
Maelezo ya picha, Rais wa Rwanda Paul Kagame akutana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika ziara yake ya kwanza katika nchi jirani ya kaskazini baada ya mvutano wa mwaka 2019 na kusababisha kufungwa kwa mpaka wanchi hizo mbili kwa miaka mitatu.
Taarifa kutoka Ikulu ya Entebbe imesema viongozi hao wawili walikubaliana kutoa kipaumbele kwa amani na utulivu katika eneo hilo kwa kushughulikia mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ilisema wawili hao walifanya mazungumzo siku ya Jumapili.
Bw Museveni aliutaka umoja wa kikanda kushughulikia ukosefu wa usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kabla ya mzozo huo kuongezeka.
Bw Kagame alisema ni muhimu pande zote katika mzozo huo zishirikishwe ili kutatua mgogoro huo mara moja.
Wiki iliyopita, Kenya, Burundi, Uganda, DR Congo na Rwanda zilikubaliana kupeleka kikosi cha kikanda kupambana na makundi ya waasi katika eneo hilo lenye matatizo.
Rais Kagame alikuwa katika ziara ya faragha nchini humo kuhudhuria dhifa ya mtoto wa Bw Museveni ambaye pia ni kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha Uganda Lt Jenerali Muhoozi Kainerugaba, aliyesherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 48 mwishoni mwa juma.
Bw Museveni baadaye alituma picha za chakula cha jioni kwenye mtandao wa Twitter na kumshukuru Rais Kagame kwa kuheshimu mwaliko huo ‘’baada ya miaka mingi ya kutokuja hapa.’’
Soma zaidi kuhusu mtoto wa Museveni:
Ukraine inaweza kushinda vita ikiwa itapewa vifaa sahihi - Mkuu wa Pentagon Marekani

Chanzo cha picha, Reuters
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin pia amekuwa akizungumza - akirejea kutoka safari ya ujumbe wa Marekani mjini Kyiv jana.
Anasema kuwa njiani kuelekea mji mkuu ilionekana kana kwamba mambo yameanza kurejea katika hali yake ya kawaida.
Austin anasema asili ya mapigano nchini Ukraine imebadilika kwa hivyo inahitaji silaha za masafa marefu, na imeelezea hitaji la vifaru.
Anasema ni vigumu kwa Marekani kufuatilia nini kinatokea kwa silaha zilizohamishiwa Ukraine, kwani hakuna vikosi vya Marekani vilivyoko ardhini.
Lakini alizungumza na Waukraine ili kuhakikisha kuwa silaha zinafuatiliwa vizuri iwezekanavyo.
“Hatua ya kwanza ya kushinda ni kuamini kuwa unaweza kushinda... Tunaamini kwamba tunaweza kushinda, wanaweza kushinda wakiwa na vifaa vinavyofaa, msaada sahihi,” anasema.
Mkuu wa Pentagon anaongeza kuwa Zelensky alishukuru kwa kila kitu ambacho Marekani inafanya, lakini anazingatia kile anachohitaji baadaye ili kufanikiwa.
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Mwili wa rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki kuagwa bungeni,

Chanzo cha picha, Ikulu ya Rais Kenya
Mwili wa Rais Emilio Mwai Kibaki umewasili katika majengo ya Bunge kwa ajili ya kuagwa. Hii leo mwili huo utaagwa na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Rais William Ruto, mawaziri, mabalozi, wakuu wa jeshi na viongozi wengine wakuu wa serikali.

Chanzo cha picha, Ikulu ya Rais Kenya
Kesho Jumanne na Jumatano itakuwa zamu ya wananchi wa kawaida kuutazama mwili wa Hayati Kibaki ndani ya majengo ya bunge la taifa.

Chanzo cha picha, Ikulu ya Rais Kenya
Misa ya kitaifa ya kumuaga Hayati Kibaki itafanywa siku ya Ijumaa tarehe 29, halafu rais huyo watatu wa Kenya atazikwa Jumamosi Aprili 30 nyumbani kwake huko Othaya Nyeri.
Taliban yapiga marufuku mtandao wa video wa TikTok

Chanzo cha picha, Getty Images
Kundi la Taliban limepiga marufuku mtandao wa video wa TikTok na mchezo wa mtandaoni wa PUBG, wakisisitiza kuwa progamu hizo zinawaongoza vijana wa Afghanistan "kupotea".
Kundi hilo la wanamgambo lilisema pia litapiga marufuku vituo vya televisheni kurusha hewani kile walichokiona kuwa "vitu visivyo vya maadili".
Hii inakuja baada ya kupigwa marufuku hivi majuzi kwa muziki, sinema na michezo ya kuigiza ya televisheni.Kundi la Taliban liliahidi uhuru ilipochukua mamlaka mwaka jana, lakini limezidi kukandamiza uhuru huo hasa kwa wanawake.
Waandamanaji wanawataka Taliban kufungua tena shule za wasichana.Taliban wanazuia pia BBC kwenye ratiba za runinga za Afghanistan.Msemaji wa Taliban Inamullah Samangani alisema marufuku ya hivi punde ni muhimu ili "kuzuia kizazi kipya kupotoshwa".
Lakini haijulikani ni lini marufuku hiyo itaanza kutumika, na kwa muda gani.Hii ni mara ya kwanza kwa kikundi hicho kupiga marufuku programu tangu waingie mamlakani.
TikTok na PUBG zimekuwa zinafaa zaidi kwa vijana wa Afghanistan katika miezi ya hivi karibuni kwa sababu aina nyingi za burudani zimepigwa marufuku, anasema mhariri wa BBC wa Huduma ya Afghanistan Hameed Shuja.
TikTok haswa imekuwa maarufu kwa vijana wanaofurahia kupiga video klipu fupi za ucheshi na kuziweka kwenye jukwaa, anasema mwenzetu.
PUBG, ambayo ni kifupi cha Uwanja wa Vita wa PlayerUnknown, ni mchezo wa upigaji risasi mtandaoni ulioundwa na msanidi programu wa Korea Kusini ambao pia umekuwa maarufu sana. Jaribio la hapo awali la serikali ya zamani kupiga marufuku PUBG halikufaulu.
Idadi ya watumiaji wa mtandao nchini Afghanistan imeongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni pamoja na idadi ya vijana, na takriban watumiaji milioni tisa hivi sasa.
- Afghanistan: Je, Iran inaelekea kukubali utawala wa Taliban?
- Wanawake wa Afghanstan wapigwa marufuku kwenda safari ndefu wenyewe bila wanaume
Mamia ya walinda amani kutoka Tigray,wakataa kurejea Ethiopia wakihofia usalama wao

Chanzo cha picha, MINUSMA/MARCO DORMINO
Mamia ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka eneo la Tigray nchini Ethiopia wamekataa kurejea nyumbani kutoka Sudan kwa kuhofia usalama wao.
Walikuwa wametumwa Abyei - eneo la mpaka linalozozaniwa kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Wanajeshi hao wa Ethiopia waliotumwa katika maeneo mengine ya bara hilo hapo awali walikataa kurejea nyumbani wakisema wanahofia kudhulumiwa na serikali mjini Addis Ababa kufuatia kuzuka kwa vita katika eneo la Tigray mnamo Novemba 2020.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Ethiopia vilivyodumu kwa miezi kumi na saba nchini humo vimesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na mamilioni kuhitaji msaada.
Makubaliano ya kibinadamu kati ya serikali na waasi wa Tigray yametajwa kuwa ni hatua muhimu ya kupata suluhu.
- Mzozo wa Ethiopia: Ndani ya mji wa Makelle uliotengwa na ulimwengu
- Zaidi ya Urusi na Ukraine: Mizozo 6 ya kivita ambayo inatokea ulimwenguni
Rais Kagame ahudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mtoto wa Museveni
Rais wa Rwanda Paul Kagame amesafiri hadi nchi jirani ya Uganda kushiriki sherehe ya kuzaliwa ya mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba.
Safari hii nchini Uganda, ya kwanza kwa Bw Kagame katika kipindi cha miaka minne, inaonekana kama ishara ya kupunguza hali ya wasiwasi kati ya nchi hizo mbili.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Shirika la utangazaji la taifa la Rwanda lilisema kuwa Bw Kagame pia ataketi na mwenzake wa Uganda.Luteni Jenerali Kainerugaba, ambaye anasimamia vikosi vya nchi kavu vya Uganda, ameonekana kuwa na mchango mkubwa katika kurahisisha uhusiano kati ya Rwanda na Uganda.
Kuingilia kati kwake kuliaminika kuwa sababu kuu katika kufunguliwa tena kwa mpaka wa pamoja wa nchi hizo mapema mwaka huu. Mipaka hiyo ilikuwa imefungwa tangu 2019.
Nchi zote mbili zilikuwa zinashutumiana kuingilia mambo ya kila mmoja.Katika ukurasa wake wa Twitter mapema wiki hii, Jenerali Kainerugaba alimtaja rais wa Rwanda kama mjomba wake
- Jenerali Muhoozi Kainerugaba wa Uganda ni nani?
- Muhoozi Kainerugaba: Je, tunajua nini kuhusu tangazo la kustaafu la mtoto huyu wa Rais Museveni?
- Zijue siasa nyuma ya ziara ya Muhoozi Kainerugaba nchini Rwanda
Urusi inapanga kura ya maoni huko Kherson-Uingereza

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Vifaru vya urusi Urusi inapanga "kura ya maoni" katika mji wa kusini wa Kherson kwa lengo la kuhalalisha kuuteka mji huo , kulingana na ripoti ya hivi punde ya Wizara ya Ulinzi ya Uingereza.
Inasema kuwa jiji hilo ni muhimu kwa lengo la Urusi la kuanzisha daraja la ardhini kuelekea peninsula ya Crimea - ambayo ilitwaliwa na Urusi mwaka 2014 - na kutawala kusini mwa Ukraine.
Inaongeza kuwa Urusi ilitumia mbinu hii ili kuhalalisha unyakuzi wake wa Crimea.
Kherson ndio mji mkuu pekee ambao Urusi imeweza kuuteka tangu ilipovamiaUkraine mwishonimwa mwezi Februari. Lakini baadhi ya maeneo jirani yamechukuliwa tena na wanajeshi wa Ukraine, na mapigano katika eneo hilo yanaendelea.
- Vita vya Ukraine: Je, madai ya Putin kuhusu Ukraine yana ukweli au hayana msingi kiasi gani?
- Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
