Waziri mkuu wa Uingereza awasili Kyiv kuonyesha ushirikiano na Waukraine

Ofisi ya waziri mkuu wa nchini Uingereza, Downing Street imethibitisha kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson anakutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika mji mkuu Kyiv.

Moja kwa moja

  1. Na hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu mubasha kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Hali ya wasi wasi yatanda katika mji Siolo Kenya baada ya shambulio la mauaji

    Kuna hali ya wasi wasi katika mji wa kaskazini mashariki wa Isiolo baada ya watu tisa kuuawa na watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi.

    Waliouawa walitekwa na washambuliaji walipokuwa kwenye ufugaji wa ngamia na mifugo wengine Ijumaa jionii. Saba walikufa mara moja na wengine walifariki kutokana na majeraha mapema Jumaomosi. Wengine watatu wamelazwa hospitalini huku wakiwa katika hali mahututi.

    Biashara zimefungwa katika mji huo wenye shuguli nyingi baada ya wakazi kufanya maandamano katika kati ya mji, huku wakifunga barabara na kuwasha mioto kupinga mauaji mauaji hayo.

    Usalama umeimarishwa katika eneo hilo baada ya kikosi maalum cha polisi kupelekwa kuwasaka washambuliaji ambao walitoroka na mifugo baada ya shambulio.

  3. Habari za hivi punde, Waziri mkuu wa Uingereza awasili Kyiv kuonyesha ushirikiano na Waukraine

    Ofisi ya waziri mkuu wa nchini Uingereza, Downing Street imethibitisha kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson anakutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika mji mkuu Kyiv.

    Msemaji wa ofisi ya Waziri mkuu amesema : “Waziri mkuu amesafiri kwenda Ukraine kukutana na Rais Zelensky binafsi ili kuonyesha ushirikiano na watu watu wa Ukraine.

    "Watajadili uungaji mkono wa Uingereza wa muda mrefu kuisaidia Ukraine na waziri mkuu atatenga fedha usaidizi mpya wa kifedha na kijeshi.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Waukraine waambiwa watoroke kutoka mashariki mwa nchi haraka iwezekanavyo

    reuters

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mfanyakazi wa shrika la msalaba mwekundu akipeleka misaada ya kiutu kwa watu wa Luhansk

    Watu wamekuwa wakiambiwa waondoke haraka iwezekanavyo kutoka katika jimbo la Luhansk mashariki mwa Ukraine huku makombora yakiendelea kuongezeka na Pamoja na kuwasili kwa vikosi zaidi vya Urusi, anasema gavana wake.

    Serhiy Gaidai ameiambia televisheni ya kibinafsi kwamba 30% ya wakazi bado wamebaikia katika miji na vijiji katika maneo mbali mbali ya jimbo hilo, limeripoti shirika la habari la Reuters.

    Hii inakuja huku kukiwa na tahadhari kwamba Urusi inapanga kuimarisha mashambulio yake katika jimbo la mashariki mwa Ukraine la Donbas , ambalo linajumuisha Luhansk, huku likitaka kubuni ardhi inayoiunganisha na jimbo la Crimea lililolitwaa awali.

    Ramani inayoonyesha umbali uliofikiwa na vikosi vya Urusi katika Ukraine

    BBC
  5. Jinsi mama alivyoshuhudia binti na mumewe wakiuawa na jeshi la Urusi

    BBC

    Siku tisa ndani ya vita nchini Ukraine, huku mapigano nyakiendelea, Viktoria na mume wake Petro walikuwa wameamua hatimaye kuukimbia kutoka mji wao wa Chernihiv, uiopo kaskazini mwa nchi. Walitaka kuwaweka Watoto wao katika hali ya usalama. Veronika mwenye umri wa miaka kumi na miwili alikuwa mtoto wa Viktoria aliyempata katika ndoa yake ya kwanza . Binti yake mwingine Varvara, ana umri wa mwaka mmoja tu.

    Walichukua walichokihitaji, na kuondoka kwa gari kwenda mbali na nyumba yao ya familia. Wakati walioondoka viungani mwa mji, wakielekea kusini karibu na kijiji cha Yahidne, waliona mawe yaliyoziba njia yao. Petro aliyavuta, akapanda nje na kuanza kuyaondoa akiyaweka kando ya njia.

    Sekunde kadhaa baadaye, gari lao lilimiminiwa risasi.

    Unaweza kusoma taarifa hii zaidi lakini tahadhari ina maelezo ambayo baadhi ya wasomaji wanaweza kuhisi ni ya kuogofya ...Urusi na Ukraine: Jinsi mama alivyoshuhudia binti na mumewe wakiuawa na jeshi la Urusi.

    Taarifa zaidi kuhusu vita vya Ukraine:

  6. Habari za hivi punde zaidi kuhusu vita vya Ukraine

    Askari akiwa amesimama katikati ya majengo yaliyoharibiwa katika Mykolaiv - karibu na Odesa mji ambao umeweka amri ya kutotoka nje wikendi

    Chanzo cha picha, REUTERS/Ueslei Marcelino

    Maelezo ya picha, Askari akiwa amesimama katikati ya majengo yaliyoharibiwa katika Mykolaiv - karibu na Odesa mji ambao umeweka amri ya kutotoka nje wikendi

    Iwapo ndio kwanza unajiunga nasi huu ni muhtasari wa yale yaliyojiri leo kuhusu vita vya Ukraine

    • Maafisa wa Ukraine wanasema – njia kumi za misaada ya kibinadamu kwa ajili ya kuwaokoa watu kutoka kwenye majimbo ambayo yamekumbwa na mashambulio ya vikosi vya Urusi zimeafikiwa kwa leo
    • Watu zaidi wanahitaji kuokolewa kutoka jimbo laLuhansk lililoko mashariki mwa Ukraine ambako kuna mashambulizi ya makombora na na kuwasili kwa vikosi vya Urusi , amesema gavana wa jimbo hilo
    • ·Amri ya kutotoka nje imewekwa katika mji wa kusini mwa Ukraine wa mwambao wa Odesahuku kukiwa na hofu ya mashambulio ya Urusi
    • Miili 132 ya wafu imegundulika katika Makariv, kilomita zipatazo 50 (au maili 30 ) kutoka Kyiv, kulingana na wavuti wa Ukrainska Pravda
    • Shambulio la kombora la ndege la Ijumaa kwenye kituo cha leri limeelezewa kama ‘’uhalifu mwingine wa kivita wa Urusi’’ na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
    • Ukraine inasema takriban watu 50 walikufa, wakiwemo Watoto, na makumi kadhaa walijeruhiwa
    • Maafisa wa Magharibi wanasema Jenerali Mrusi mwenye uzoefu mkubwa katika Syria amepewa jukumu la kuongoza operesheni za kivita katika Ukraine
    • Urusi inaaminiwa kupanga upya uongozi wake wa kijeshi katika Ukraine, huku Jenerali Alexander Dvornikov akipewa jukumu lote la kuongoza vita
    • Mhandisi katika mtambo wa nyuklia katika Chernobyl ameiambia BBC kuhusu juhudi zake za kuzuwia janga la nyuklia wakati mtambo huo ulipokuwa umetwaliwa na na vikosi vya Urusi

    Unaweza pia kusoma

  7. Urusi imembadilisha kamanda wake wa vita, afisa wa Magharibi athibitisha

    Gen Alexander Dvornikov

    Chanzo cha picha, Klemlin

    Maelezo ya picha, Gen Alexander Dvornikov

    Afisa wa magharibi amethibitisha kuwa Urusi imepanga upya uongozi wa operesheni zake za kivita katika Ukraine, na kumteua Jenerali mpya mwenye uzoefu wa mapambono ya kivita katika Syria kusimamia vita vya Ukraine.

    Akizungumza mwandishi wa BBC Gordon Corera kwa sharti kwamba asitajwe jina lake, chanzo cha taarifa hii kilisema kuwa kamanda wa wilaya ya kijeshi ya kusini mwa Urusi, Jenerali Alexander Dvornikov, sasa ndiye anayeoongoza uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

    “Kamanda huyo ana uzoefu mkubwa wa operesheni za Urusi nchini Syria. Kwahiyo tunamtarajiauongozi na udhibiti utaboreka ,” kilisema chanzo hicho.

    Uteuzi mpya ulifanyika katika jaribio la kuimarisha uratibu baina ya vikosi mbali mbali , kwani makundi ya Urusi yamekuwa yakipangwa na kuongozwa na wakuu tofauti, alisema afisa.

    Urusi hadi sasa inahangaika kufikia malengo yake ya kivita, ikishindwa kuichukua miji muhimu kama vile Kyiv kabla ya hatimaye kuelekeza macho yake katika jimbo la Donbas mashariki.

    Afisa huyo alisema kuwa mbinu za Urusi zimekuwa zikiwafanya warudishwe nyuma na vikosi vyenye askari wachache wa Ukraine wanaopigana kwa akili zaidi na kwa kushitukiza-licha ya Urusi kufikiriwakuwaina kikosi "kikubwa" chenye bataliani 100 zenye wanajeshi wenye ujuzi.

    “Bila kubadili mbinu zake ni vigumu sana kwa Urusi kufanikiwa kwa malengo yao waliyojiwekea wenyewe ," alisema afisa huyo.

    Unaweza pia kusoma

  8. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara leo Jumamosi tarehe 09.04.2022