Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Zelensky ahutubia ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Rais wa Ukraine amelihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa nija ya mtandao kwa mara ya kwanza tangu Urusi ilipoanza uvamizi dhidi ya nchi yake.

Moja kwa moja

  1. Tunakomea hapo kwa leo. Hadi kesho Kwaheri.

  2. Picha ya satelaiti kutoka Bucha inakinzana na madai ya Urusi

    Onyo:Habari hii ina picha zinaweza kuogofya.

    Mwakilishi wa Urusi amekuwa akikanusha ukatili ulifanyika huko Bucha, akidai miili iliyopigwa picha na kurekodiwa na waandishi wa habari haikuwepo kabla ya vikosi vya Urusi kuondoka.

    Lakini uchambuzi wa picha za satelaiti zilizotolewa na kampuni ya Marekani Maxar - na kuthibitishwa na BBC - inaonyesha kulikuwa na miili kwenye barabara moja huko Bucha mnamo 19 Machi.

    Vikosi vya Urusi viliondoka mwishoni mwa Machi. Soma zaidi hapa.

  3. Zelensky azungumza na UN kwa niaba ya waathiriwa wa Urusi

    Baada ya matatizo kadhaa ya kiufundi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoka tu kuonesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kamda ya video ya kutoka Ukraine.

    Kanda hiyo iliyodumu kwa takriban dakika moja na ilionyesha picha mojabaada ya nyingine ya watu wa Ukraine waliokufa - ikiwa ni pamoja na baadhi ya miili iliyochomwa na kuharibika.

    BBC haijathibitisha video hiyo. Dame Barbara Woodward - mwakilishi wa Uingereza katika baraza hilo, ambaye anahudumu kama rais wa baraza hilo - alimshukuru Zelensky kwa kushiriki video hiyo.

    Picha hizo "zinatisha", anasema. "Nikizungumza katika nafasi yangu ya kitaifa, tumeshangazwa na kile tulichoona na kusisitiza mshikamano wetu na Ukraine," anaongeza.

    Huku hayo yakijiri Rais Zelensky anaendelea kuitaka Urusi "kuwajibishwa", akisema inapaswa kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa sawa na ile iliyofanyika Nuremberg baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

    "Mauaji" huko Bucha ni mfano mmoja tu wa mengi ya yale ambayo Urusi imekuwa ikifanya katika siku 41 zilizopita, Zelensky amesema.

    Bw. Zelensky pia anahoji jukumu la Urusi ndani ya Umoja wa Mataifa, akisema uvamizi huo "unadhoofisha" usalama wa kimataifa.

    Anatoa wito kwa baraza hilo kuiondoa Urusi kama mwanachama wake.

  4. Mnigeria asiyeamini kuna Mungu afungwa jela kwa kukufuru Uislamu

    Raia wa Nigeria asiyeamini kuna Mungu amehukumiwa kifungo cha miaka 24 jela na mahakama kuu katika jimbo la kaskazini la Kano baada ya kupatikana na hatia ya kukufuru Uislamu.

    Mubarak Bala, rais wa chama cha Humanist cha Nigeria mwenye umri wa miaka 37, alikiri mashtaka yote 18 na kuomba ahurumiwe.

    Amekuwa kizuizini tangu 2020. Kundi lmoja la Kislamu liliwasilisha ombi kwa mamlaka likimtuhumu Bala kwa kuchapisha ujumbe wa kejeli kuhusu Uislamu kwenye mitandao ya kijamii.

    Kano ina idadi kubwa ya Waislamu. Ni mojawapo ya majimbo 12 kaskazini mwa Nigeria ambapo sheria ya Kiislamu inatekelezwa pamoja na sheria za nchi.

    Bala angekabiliwa na hukumu ya kifo ikiwa angeshitakiwa katika mahakama ya Kiislamu.

    Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yamelaani kuzuiliwa kwake na kutaka aachiliwe.

    Bala alikana imani yake ya Kiislamu mwaka wa 2014. Kisha aliripotiwa kupelekwa katika hospitali ya magonjwa ya akili kabla ya kuruhusiwa.

    Alikamatwa mwaka wa 2020 katika jimbo jirani la Kaduna, na kuhamishiwa Kano, jimbo lake la nyumbani.

  5. Habari za hivi punde, Mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu Ukraine waanza

    Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndio umeanza.

    Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky atahutubia kupitia mtandaoni katika muda wa dakika 30 hivi.

    Itakuwa mara yake ya kwanza kuhutubia baraza hilo tangu Urusi ilipovamia nchi yake mwishoni mwa Februari.

    Kabla ya hapo tutasikia kutoka kwa watu watatu muhimu:

    • Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
    • Martin Griffiths, Naibu Katibu Mkuu wa idara ya masuala ya kibinadamu
    • Rosemary DiCarlo, Naibu Katibu Mkuu wa idara ya masuala ya kisiasa
  6. Zelensky kuhutubia ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

    Rais wa Ukraine anatarajiwa kulihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa nja ya mtandao mwendo wa saa 14:00 GMT (15.00 BST) – mkutano wake wa kwanza tangu Urusi ilipoanza uvamizi dhidi ya nchi yake

    Volodymyr Zelensky anatarajiwa kutoa wito kwa nchi kuiwekea Moscow vikwazo vikali zaidi, kufuatia ziara yake ya jana huko Bucha - eneo la mauaji ya raia yanayodaiwa kufanywa na wanajeshi wa Urusi.

    Amemshutumu adui yake kwa mauaji ya halaiki, na kuonya kuwa kunaweza kuwa na uvumbuzi mbaya zaidi ambao haujakuja baada ya wanajeshi wavamizi kuondoka katika maeneo karibu na mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv.

    Nchi za Magharibi zikiwemo Marekani, Uingereza na Ufaransa pia zinatarajiwa kuilaumu Moscow kwa kutekeleza uhalifu wa kivita.

    Lakini Urusi inakanusha kuwalenga raia huko Bucha na maeneo ya kaskazini mwa Ukraine, na kuahidi kuwasilisha ushahidi kwa Umoja wa Mataifa kwamba vikosi vyake havikuhusika.

    Unaweza pia kusoma

  7. Ukraine inasema watoto 165 wameuawa tangu Urusi ilipoivamia

    Watoto hadi 165 wamekwishauawa nchini Ukraine tangu mwanzoni mwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, limeripoti shirika la habari la Interfax-Ukraine, likinukuu ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa nchi hiyo (PGO).

    Pia limesema kuwa Watoto 266 wamejeruhiwa.

    Unaweza pia kusoma

  8. Kenya yatenga mamilioni ya dola kukabiliana mfumuko wa bei ya mafuta

    Serikali ya Kenya imetenga dola milioni 295 kwa ajili ya mpango wa kuimarisha sekta ya mafuta nchini humoili kuwaepusha wenye magari na gharama ya juu ya mafuta.

    Fedha hizo zimetolewa kutoka kwenye mfuko wa dharura wa bajeti ambao ulikuwa moja ya miswada ya bunge iliyosainiwa na Rais Uhuru Kenyatta Jumanne jioni.

    Taarifa hii ni ahueni kwa wenye magari na pikipiki ambao wamekuwa wakipanga misururu kwenye vituo vya mafuta ambavyo vimekuwa vikiishiwa na bidhaa hiyo muhimu.

    Vyanzo vilivyo karibu na makampuni ya usambazaji wa mafuta vinasema wamekuwa hawatoi mafuta kwenye vituo vya uuzajikutokana na ruzuku yao ambayo hawakupewa na serikali.

    Mzozo wa uhaba wa mafuta umesababisha athari mbaya kwa biashara licha ya kwamba serikali inasisitiza kwamba kuna mafuta ya kutosha nchini.

    Wenye magari wamekuwa wakipanga misururu kwa saa kadhaa katika vituo vya mafuta na kufanya safari ndefu kutafuta mafuta.

    Wataalamu wanasema hali huenda ikarejea kuwa ya kawaida katika kipindi cha wiki moja kwani makampuni ya wauzaji wa mafuta wataanza kuyasambaza kwenye vituo vya uuzaji.,

    Unaweza pia kutazama:

    Unaweza pia kusoma:

    • Uchaguzi Kenya 2022: Je ni masuala gani muhimu yanayotawala uchaguzi wa 2022 nchini Kenya?
    • Wazijua bidhaa tatu zilizopanda bei Tanzania, Kenya na Uganda?
    • Vita vya Ukraine: Fahamu ongezeko la bei ya bidhaa linavyoathiri Ramadhani
  9. Kila euro unayopokea kutoka Urusi... ni damu ya watu wa Ukraine - meya wa Kyiv

    Meya wa mji mku wa Ukraine Kyiv, Vitali Klitschko, amewataka wanasiasa wa Ulaya kukata uhusiano wa kibiashara na Moscow, akisema kuwa malipo yoyote ya Urusi yamejaa "damu" na yanasaidia kufadhili jeshi lake.

    “Kila euro, kila senti unayopokea kutoka au kutumwa kwa Urusi ina damu, ni pesa ya damu na damu ya pesa hii ni damu ya Waukraine. Damu ya watu wa Ukraine.”

    Klitschko pia ameelezea kuhusu “mauaji ya kimbari ya Waukraine” kufuatia ziara katika miji ya setilaiti yaKyiv kama vile Bucha wiki hii.

    Anasema aliwaona wafu raia, wakiwemo wanawake wakongwe, na gari lenye bendera nyeupe na barua "watoto" nje ambao walikuwa wamepigwa risasi na lilikuwa na damu ndani yake.

    Klitschko alikuwa akizungumza kwa njia ya video katika mkutano wa video na mameya mjini Geneva.

    Unaweza pia kusoma

  10. Korea Kaskazini yaionya Korea Kusini juu ya ​​"shambulio la nyuklia"

    Korea Kaskazini imeonya kwamba "Korea Kusini ikiwashambulia, wataishambulia kwa makombora ya nyuklia ."

    Taarifa hii imetolewa na dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, huku hali ya wasi wasi ikiendelea kuongezeka baina ya nchi mbili.

    Siku chache zilizopita, Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini alisema jeshi lake lina uwezo wa kushambulia eneo lolote ndani ya Korea Kaskazini.

    Dada yake Kim Jong Un, Bi Yo-Jong alisema, "Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini amefanya ’’kosa kubwa’’ kwa kusema kuwa ataishambulia Korea Kaskazini. ''Iwapo atafanya hivyo, Korea Kaskazini itajibu kwa shambulio la nyuklia. ", amesema.

    Hatahivyo, amseeleza bayana kuwa Korea kaskazini haitaki vita. Kwahivyo haitakuwa ya kwanza kushambulia kabla haijashambulia.

    Unaweza pia kusoma:

    • Kim Yo-jong: Dada yake Kim Jong-un aitaka Marekani isilete 'mtafaruku'
    • Kim Yo-jong: Mwanamke mwenye uwezo mkubwa anayeonekana kuwa mrithi wa Kim Jong-un Korea Kaskazini
    • Kim Jong-un: Ni nani anayeweza kuiongoza Korea Kaskazini bila Kim?
  11. Polisi ya Afrika Kusini inamsaka mwendesha troli ya dukani

    Polisi katika mji mkuu wa Afrika Kusini wanamsaka mwendesha troli ya dukani ambaye alichukuliwa video akiwa ndani ya troli hilo huku akiwa ameshikilia lori la mafuta ambalo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi katika moja ya barabara kuu mjini humo.

    Tukio hilo lilitokea Jumapili baada ya mvua kubwa kunyesha, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari. Mwanaume huyo alionekana akitabasamu na kuwapungia mkono watu waliokuwa ndani ya magari.

    Picha ya tukio hilo imekuwa ikisambazwa sana miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo.

    “Wapelelezi wanaofuatilia tukio hilo sasa wanasema mwanaume huyo atafikishwa mbele ya sheria hivi karibuni,” Msemaji wa kikosi cha usalam barabarani wa eneo Sello Maremane alinukuliwa akisema.

    Aliwataka watu "kutumia usafiri wa umma kama njia mbadala kuliko kuhatarisha Maisha yao na ule wa watumiaji wengine wa barabara."

  12. Shirika la ujasusi laonya juu ya njama ya kuwashambulia viongozi wa Somalia

    Shirika la ujasusi la Somalia limeonya kuhusu madai ya njama ya wanamgambo washirika wa al-Qaeda- al-Shabab ya kumshambulia rais na waziri mkuu.

    Shirika la ujasusi na usalama nchini Somalia (Nisa) limesema katika ujumbe wake wa Twitter kwamba limewafahamisha viongozi hao wa taifa kuhusu "njama ambayo inapangwa na mafia wa al-Shabab".

    Shirika hilo halikutoa maelezo zaidi, lakini lilisema kwamba linamsaka yeyote anayehusika na njama hiyo.

    Onyo hili linakuja huku kukiwa na mzozo wa kisiasa nchini humo kutokana na kucheleweshwa sana kwa uchaguzi usio wa moja kwa moja.

    Al-Shabab pia imeimarisha mashambulizi yake kote nchini Somalia.

    Kikundi hicho hivi karibuni kilishambulia eneo lenye ulinzi mkali la uwanja wa ndege ambako kuna ofisi za Umoja wa Mataifa, na balozi za kigeni katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

    Pia lilifanya mashambulio ya mabomu ya kujitoa muhanga katika mji wa kati wa Beledweyne, na kuwauwa watu wapatao 48, akiwemo mbunge mwanamke wa bunge la shirikisho.

    Unaweza pia kusoma:

    • Je wapiganaji wa al-Shabab kutoka Somalia wana malengo gani?
    • Wanamgambo wa al-Shabab hukusanya mapato makubwa kuliko serikali ya Somalia
    • al-Shabab Somalia: Kwanini wanamgambo huzilenga hoteli katika mashambulio ya kigaidi?
  13. Wanyarwanda waliokimbilia Msumbiji waanza kurejea nyumbani

    Baadhi ya Wanyarwanda wakimbizi ambao wamekuwa wakiishi nchini Msumbiji wameanza kurejea nyumbani baada ya miongo mitatu tangu walipotoroka mauji ya kimbari ya mwaka 1994.

    Kati ya miezi ya Aprili na Juni, 1994, Wanyarwanda wanaokadiriwa kuwa 800,000 waliuawa katika kipindi cha siku 100. Mamilioni kadhaa wengine walikimbilia katika nchi jirani.

    Mamlaka nchini Msumbiji zinakadiria kuwa kuna Wanyarwanda wakimbizi wapatao 3,000 wanaoishi nchini humo.

    Wengi wao kwa sasa wanaamini kuwa hali iliyowafanya waitoroke nchi yao imebadilika.

    Serikali ya Rwanda inawasaidia wakimbizi kurejea katika maisha ya kawaida. Kurejea ni kwa hiari na wakimbizi wapatao 19 wataondoka wiki hii kwa ndege kuelekea nyumbani.

    Mmoja wa wakimbizi, Miyonsenoa Domoties, alisema kuwa anaamini kuna amani nchini Rwanda na anarejea nyumbani baada ya kuishi Msumbiji kwa miaka minane.

    “Tulichagua kukimbilia Msumbuji. Lakini baada ya muda fulani, taarifa nzuri zilitufikia zikiashiria kwamba kuna amani nchini Rwanda, kwahiyo tumeamua kwenda nyumbani, alisema.

    Mauaji ya kimbari yalitokea kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana, wakati ndege yake ilipodunguliwa karibu na uwanja wa ndege wa Kigali tarehe 6 Aprili 1994.

  14. Rais wa Afrika kusini atangaza mwisho wa sheria za Covid

    Afrika Kusini imetangaza ukomo wa sheria za kukabiliana na Covid, miaka miwili baada ya sheria hizo kuwekwa kote nchini humo.

    Katika hotuba yake iliyotangazwa kwa televisheni, rais Cyril Ramaphosa alisema kuwa hali ya janga ya taifa itamalizika usiku saa sita siku ya Jumatatu.

    Barakoa hata hivyo zitaendelea kuvaliwa katika kumbi zenye mikusanyiko ya watu kwa kipindi cha mwezi mwingine mmoja.

    Alisema ingawa janga bado halijaisha, anaamini kwamba kuna siku njema zijazo mbeleni.

    Bw Ramaphosa alisema ni muhimu kuinua uchumi na kubuni ajira

    Afrika kusini imerekodi visa zaidi vya virusi vya corona kuliko nchi nyingine yoyote ile ya Afrika, ikiwa na takriban robo tatu ya maambukizi yote barani Afrika.

    Ilirekodi vifo rasmi 100,000 vilivyotokana na corona.

    unaweza pia kusoma:

    • Afrika Kusini imesema 'imeadhibiwa' kwa kugundua virusi vipya vya corona aina ya Omicron
    • Kirusi Kipya cha Covid-19: Abiria13 kutoka Afrika Kusini wakutwa na maambukizi Uholanzi
  15. Mzozo wa Darfur Sudan: ICC kuendesha kesi dhidi ya mshukiwa wa uhalifu wa kivita

    Kesi ya kwanza kwa jili ya maafa yaliyofanyika katika jimbo la Darfur inakaribia kuanza katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) , karibu miaka 20 baada ya ghasia kulikumba jimbo hilo ya Sudan.

    Mshukiwa ambaye alikuwa ni kiongozi wa wanamgambo waliokuwa wanaunga mkono wakifahamika kama Janjaweed ameshitakiwa makosa 31 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

    Ali Muhammad Ali Abd-al-Rahman anakana mashitaka yote dhidi yake.

    Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Sudan wameelezea kesi hiyo kama ya kihistoria.

    "[Jumanne] ni siku muhimu kwa waathiriwa na manusura katika Darfur ambao hawakukoma kupambana kuona mzunguko wa kutaka haki ya kisheria itendekea unavunjika," wakili wa Sudan wa haki za binadamuMossaad Mohamed Ali alisema.

    "Tuna matumaini kuwa kesi dhidi ya Abd-al-Rahman itatoa mwanagza juu ya jukumu lake katika uhalifu , hususan uhalifu wa kingono, uliotekelezwa nay eye binafsi na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali wa Janjaweed chini ya uongozi wake," aliongeza.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mzozo wa Sudan: Ni mamluki gani katili wanaiongoza Sudan sasa?
    • Mzozo wa Sudan: Ni mamluki gani katili wanaiongoza Sudan sasa?
  16. Nchi za Magharibi zatahadharisha kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi

    Katika saa za hivi karibuni Marekani na washirika wake wa Magharibi wameonya kuwa wataiadhibu Urusi kwa hatua zake katika Bucha.

    Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema Jumatatu kwamba Rais wa UrusiVladimir Putin na wafuasi wake ‘’watahisi athari’’ na kwamba washirika wa magharibi wataimasha vikwazo dhidi ya Moscow.

    Wakati huo huo mshauri wa masuala ya kiusalama wa Marekani Jake Sullivan alisema kuwa marekani inafanya inashirikiana ‘’kwa juhudi na washirika wake wa Ulaya kwa ajili ya kuweka vikwazo zaidi ili kuimarisha shinikizo na kuongeza garama kwa Putin na kwa Urusi ".

    Ufaransa na Ujerumani pia zimesema kuwa zinaweza kuwafukuza mabalozi wa Urusi katika nchi zao.

    Katika ujibu hayo, Urusi ilisema itajibu na" kwa kufunga milango ya balozi za Magharibi ", Shirika la habari la Reuters iliripoti kuwa rais wa zamaniwa Urusi na naibu mkuu wa baraza la usalama Dmitry Medvedev alisem"

    Itakuwa rahisi kwa kila mmoja. Na halafu tutaishia kutoangaliana kwa njia nyingine ila kwa njia ya mtutu wa bunduki," alionya.

    Unaweza pia kusoma

  17. Biden atoa wito kwa Putin kushtakiwa kwa uhalifu wa kivita baada ya mauaji ya Bucha

    Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi ya rais wa Urusi Vladimir Putin kwa uhalifu wa kivita huku ushahidi ukiibuka wa ukatili unaodaiwa kufanywa na majeshi ya Urusi nchini Ukraine.

    Kumekuwa na hasira ya kimataifa juu ya madai ya mauaji ya raia huko Bucha, mji ulio karibu na mji mkuu wa Kyiv.

    "Mtu huyu ni mkatili," Bw Biden alisema kuhusu kiongozi huyo wa Urusi, na kuongeza kwamba anaamini Bw Putin "ni mhalifu wa vita".

    Bila ushahidi, Urusi ilisema picha za ukatili zimeonyeshwa na Ukraine.

    Maafisa wa Marekani wanasema wanaunga mkono timu ya waendesha mashtaka wa kimataifa wanaoelekea Bucha kukusanya ushahidi.

    Serikali ya Ukraine imeanza uchunguzi wa uhalifu wa kivita baada ya kusema miili ya raia 410 imepatikana katika maeneo karibu na Kyiv. Mingine iligunduliwa kwenye makaburi ya halaiki huku wengine wakiwa wamefungwa mikono na inaonekana walikuwa wamepigwa risasi kwa karibu.

    Maafisa wa Kyiv pia walishutumu vikosi vya Urusi kwa kumuua mkuu wa kijiji, mumewe na mwanawe katika kijiji cha Motoyzhyn kwa kusaidia wanajeshi wa Ukraine katika eneo hilo.

    Unaweza pia kusoma

  18. Watoto wachanga wa Ukraine wapewa majina ya makombora

    Watoto wawili waliozaliwa nchini Ukraine katika siku za hivi karibuni wamepewa majina ya makombora ya kutoka ardhini hadi angani ya Uingereza, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Ukraine.

    Watoto hao walikuwa mvulana anayeitwa Yan Javelin na msichana aliyeitwa Javelina.

    Majina hayo yasiyo ya kawaida yalisajiliwa katika Jimbo la Vinnytsia, kulingana na mke wa rais wa zamani wa Ukraine Kateryna Yushchenko, ambaye alisema ni ishara ya shukrani kwa silaha za Magharibi ambazo zimetumwa Ukraine.

    • Mzozo Ukraine: 'Mtoto wangu anaficha mikate, akihofia chakula kukosekana'
    • Mzozo Ukraine: 'Tunajaribu kuwaambia ukweli' - malezi wakati wa vita
  19. Urusi inajaribu kuficha uhalifu wa kivita - Zelensky

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu Urusi kwa kujaribu kuficha ushahidi wa uhalifu wa kivita uliofanywa na wanajeshi wake katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

    Zelensky, ambaye atahutubia mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, aliushutumu utawala wa Vladimir Putin kwa kuanzisha operesheni ya "propaganda" ili kutilia shaka ripoti kwamba raia wa Ukraine wameuawa na vikosi vyake.

    "Lazima pia tufahamu kwamba baada ya kufichuliwa kwa mauaji makubwa ya raia katika eneo la Kyiv, wavamizi wanaweza kuwa na mtazamo tofauti na uhalifu wao katika sehemu nyingine ya nchi yetu walikofika," kiongozi huyo wa Ukraine alisema.

    "Tayari wanaanzisha kampeni ya uwongo kuficha hatia yao katika mauaji makubwa ya raia huko Mariupol. Watafanya mahojiano kadhaa jukwaani, kurekodiwa upya, na wataua watu haswa ili ionekane kama waliuawa na mtu mwingine. ."

    "Walitumia mbinu zilezile wakati wavamizi walipoiangusha ndege ya Malaysia Boeing juu ya Donbas. Waliilaumu Ukraine. Hata walikuja na nadharia mbalimbali za njama. Walifikia hata kudai kuwa maiti "zilitupwa" ndani ya ndege hiyo hapo awali’ .Aliongeza.

    Alitoa wito kwa viongozi wa Magharibi kuweka vikwazo zaidi kwa utawala wa Vladimir Putin, akisema kwamba adhabu "lazima hatimaye ziwe na nguvu".

    • Ukraine na Urusi: Ukraine inaweza 'kushinda' vita?
    • Mzozo wa Ukraine na Afrika: Athari kwa mafuta,wanafunzi na mkate
  20. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Jumanne tarehe 6 Aprili 2022