Urusi 'kupunguza mashambulizi karibu na Kyiv na Chernihiv'

Alexander Fomin alisema uamuzi wa "kupunguza kwa kiasi kikubwa" shughuli za kijeshi za Urusi katika miji hiyo miwili ulichukuliwa ili "kuongeza uaminifu wa pande zote"

Moja kwa moja

  1. Na hadi kufikia hapo tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja hivi leo.Hadi hapo kesho panapo majaaliwa

  2. Hakuna msaada uliowasili Tigray licha ya kusitishwa kwa mapigano, waasi wasema

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waasi katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray wanasema hakuna msaada wa chakula umefika katika eneo hilo licha ya serikali kutangaza makubaliano ya upande mmoja wiki iliyopita ili kuruhusu msaada wa kibinadamu kwa mamilioni wanaokabiliwa na njaa.

    Wanasema msafara wa lori zinazobeba chakula na dawa bado zinangojea kibali hadi Tigray, ambayo haijapokea usafirishaji tangu katikati ya Desemba.

    Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia amezitaka mamlaka kurejesha huduma za umma mjini Tigray, zikiwemo benki, umeme na mawasiliano ambayo yamekatika tangu mzozo huo uanze Novemba 2020.

    Mashirika ya kibinadamu yanakabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta na pesa ili kutekeleza kazi yao.

    Serikali imeshutumiwa kwa kuweka kizuizi, jambo ambalo imekanusha.

    Waasi pia wamekabiliwa na madai ya kuzuia usafirishaji kwa sababu ya mapigano yanayoendelea katika eneo la Afar - njia rahisi zaidi ya ardhini kuelekea Tigray.

  3. Botswana kutengeneza chanjo ya Corbevax ya Covid

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Botswana ndiyo nchi ya hivi punde zaidi kuidhinisha matumizi ya chanjo ya Corbevax coronavirus - na pia inapanga kuizalisha nchini humo ifikapo 2026.

    Haya ni kwa mujibu wa bilionea wa kibayoteki mzaliwa wa Afrika Kusini Patrick Soon-Shiong, ambaye alitoa tangazo hilo akiwa ziarani nchini Botswana siku ya Jumatatu.

    Kampuni yake ya NantWorks imeshirikiana na serikali ya Botswana kuanzisha kiwanda cha kutengeneza chanjo - na alikuwa katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kuashiria kuanza kwa mradi huo.

    Wakati wa safari yake, Dk Soon-Shiong alisema amepanga Botswana kupata mara moja dozi milioni 100 za chanjo ya Corbevax inayozalishwa mahali pengine.

    Alisema chanjo inayotegemea protini imetangazwa kuwa salama, imefanyiwa kazi dhidi ya kila aina na dozi milioni 10 tayari zimetolewa, haswa nchini India na Bangladesh.

    Chanjo hiyo isiyo na hati miliki , iliyotengenezwa na watafiti wa Marekani, kwa sasa inazalishwa nchini India na hakuna sharti la Corbevax kuhifadhiwa katika halijoto ya chini sana.

    Hivi sasa, ni 1% tu ya chanjo zinazotumiwa barani Afrika zinazozalishwa katika bara hilo - na takwimu za hivi punde zinaonyesha kuwa ni 15% tu ya Waafrika walio na chanjo kamili dhidi ya Covid-19.

  4. Kuna tofauti kati ya kile Russia inasema na kufanya, Blinken asema

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Marekani haijaona "dalili za umakini wa kweli" kutoka kwa Urusi kuhusu kutafuta amani tangu ilipoivamia Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amesema.

    Blinken alitoa maoni hayo baada ya Urusi na Ukraine kufanya mazungumzo ya amani mapema leo na Moscow kutangaza "itapunguza kwa kiasi kikubwa" operesheni za mapigano huko Kyiv na Chernihiv ili "kuongeza kuaminiana".

    Uturuki imesema mazungumzo hayo yamewakilisha maendeleo makubwa zaidi katika majadiliano kati ya pande zote mbili.

    Lakini Blinken alisema kulikuwa na tofauti kati ya kile Russia inachosema na kile inachofanya na Marekani ilizingatia mwisho.

    Aliongeza kuwa Urusi inapaswa kukomesha uchokozi wake sasa na kurudisha majeshi yake nyuma.

    Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  5. Nigeria yasitisha utumiaji wa mkondo wa reli wa Abuja-Kaduna baada ya mauaji ya abiria katika treni

    TH

    Chanzo cha picha, NRC

    Serikali ya Jimbo la Kaduna imethibitisha kuwa baadhi ya abiria waliokuwa kwenye treni iliyokuwa ikielekea Kaduna iliyoshambuliwa Jumatatu usiku waliuawa. Vyanzo vya habari katika hospitali ya kijeshi 44 huko Kaduna vimeiambia BBC kwamba miili 7 ilipatikana huku majeruhi 22 wakitibiwa.

    Shirika la Reli la Nigeria sasa limesitisha operesheni kwenye njia ya Abuja-Kaduna baada ya shambulio hilo.

    Taarifa ya kamishna wa usalama wa ndani wa Jimbo la Kaduna, Samuel Aruwan, ilisema kuwa uondoaji wa abiria waliokwama umekamilika lakini shughuli za kuwatafuta na kuwaokoa zinaendelea.

    Alisema kuwa serikali inawasiliana na Shirika la Reli ili kufahamu orodha hiyo kutoka kwenye majina ya abiria kwa ufuatiliaji wa ufanisi ili kupata hesabu sahihi ya abiria wote na hali zao halisi. Magenge yenye silaha yalilipua njia na kulazimisha treni kuacha mkondo wake .

    Washambuliaji waliingia kwa nguvu kwenye treni hiyo, na kuwapiga risasi baadhi ya abiria waliokuwa karibu na kuteka nyara idadi isiyojulikana ya watu. Kulikuwa na takriban abiria 1,000 kwenye treni hiyo wakati wa tukio.

    Kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara na utekaji nyara katika barabara kuu kati ya Abuja na Kaduna, wasafiri wengi sasa wanapendelea kusafiri kwa treni, lakini hii ni mara ya pili kwa reli hiyo kushambuliwa katika miezi sita iliyopita.

  6. Watu saba wauawa katika shambulizi dhidi ya ofisi ya serikali katika mji wa Mykolaiv nchini Ukraine

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Shambulizi la Urusi katika jengo la serikali katika mji wa Mykolaiv nchini Ukraine limesababisha vifo vya watu saba na kujeruhi wengine zaidi ya 20, rais Volodmyr Zelensky amesema.

    Roketi ilitoboa tundu kwenye jengo la orofa tisa muda mfupi kabla ya saa 9:00 za hapa (06:00 GMT) Jumanne asubuhi.

    Mamlaka bado inatafuta watu zaidi walionusurika kwenye vifusi.

    Shambulio hilo liliharibu ofisi ya gavana wa eneo hilo Vitaliy Kim ambaye hakuwepo wakati huo.

    Jengo hilo pia lina ofisi za serikali ya mkoa wa Mykolaiv.

    Huduma za dharura zinasema watu 22 pia walijeruhiwa.

    Katika hotuba yake ya video kwa Bunge la Denmark, Bw Zelensky alilaani shambulizi hilo:

    "Hakukuwa na shabaha za kijeshi huko Mykolaiv. Watu wa Mykolaiv hawakuwa tishio kwa Urusi’.

    Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  7. Wakimbizi zaidi watoroka mashambulizi ya M23 nchini DRC karibu na mpaka wa Uganda.

    th

    Chanzo cha picha, AFP

    Kumekuwa na mapigano mapya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, karibu na mpaka wa Uganda, na kusababisha wakimbizi wengi zaidi kukimbilia nchi jirani. Siku ya Jumapili usiku, waasi wa M23 walishambulia maeneo ya jeshi na vijiji katika eneo la Rutshuru nchini DRC na kusababisha mmiminiko wa wakimbizi hadi taifa jirani la Uganda .

    Umati wa watu umekuwa ukimiminika katika mji wa mpakani wa Bunagana, wakikimbia mapigano.

    Hapo awali, mashirika ya misaada ya kibinadamu na viongozi wa eneo hilo walikuwa wameiambia BBC kwamba takriban wakimbizi 5000 walikuwa wamevuka mpaka siku ya Jumatatu.

    Lakini wengi wanaokimbia wanakaa karibu na eneo la mpaka, kwa matumaini kwamba wanaweza kurudi nyumbani ikiwa mambo yatatulia.

    th

    Jeshi la Uganda pia limekanusha ripoti za awali kwamba limetuma majeshi DRC, kupambana na waasi wa M23.

    Msemaji wa Jeshi Brigedia Felix Kulayigye aliambia BBC kwamba M23 walishambulia kituo cha jeshi la DRC kilicho umbali wa nusu kilomita kutoka mpaka wa Uganda, na jeshi la Uganda liliweka uinzi upande wake wa mpaka wa pamoja ili kuhakikisha mapigano hayavuki.

    Serikali ya DRC imeishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi, madai ambayo Rwanda imetupilia mbali.Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2013 ilizishutumu Rwanda na Uganda kwa kuunga mkono kundi la M23, kundi la waasi linaloundwa na watu wengi wa mashariki mwa Kongo.

  8. Urusi 'kupunguza mashambulizi karibu na Kyiv na Chernihiv'

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Naibu waziri wa ulinzi wa Urusi Alexander Fomin anasema Urusi "itapunguza kwa kiasi kikubwa" shughuli za kijeshi nje ya Kyiv na Chernihiv - hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Tass.

    Vikosi vya Urusi vinaonekana kukwama katika eneo hili - hapo awali wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema kwamba vikosi vya Ukraine vilifanikiwa kuwarudisha nyuma Warusi kutoka nafasi kadhaa.

    Ilisema Urusi ilisalia kuwa tishio kubwa kwa Kyiv kutokana na uwezo wake wa kushambulia.

    Mji wa kaskazini uliozingirwa wa Chernihiv umesalia chini ya mashambulizi ya Urusi leo, kulingana na maafisa wa Ukraine.

    Meya wa jiji hilo anakadiria kuwa wakaazi 400 wameuawa hapo tangu vita kuanza.

    Alexander Fomin alisema uamuzi wa "kupunguza kwa kiasi kikubwa" shughuli za kijeshi za Urusi katika miji hiyo miwili ulichukuliwa ili "kuongeza uaminifu wa pande zote" na kusaidia kusababisha mazungumzo zaidi na kufikia "lengo la mwisho" la makubaliano yaliyotiwa saini kati ya pande hizo mbili. maoni yaliyoripotiwa na shirika la habari la Urusi Ria Novosti.

    th

    Ukraine yasema haitagemea upande wowote ili kurudisha dhamana ya usalama

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Zaidi sasa kutoka kwa mazungumzo ya amani kati ya Ukraine na Urusi ambayo yamekuwa yakifanyika Istanbul leo.

    Ukraine imesema itapitisha msimamo wake kutoegemea upande wowote - moja ya matakwa muhimu ya Urusi - ili kurudisha dhamana ya usalama, wapatanishi wake wamesema.

    Hali ya kutoegemea upande wowote itamaanisha kwamba Ukraine haitajiunga na mashirikiano yoyote ya kijeshi, kama vile Nato, au kambi za jeshi.

    Poland, Israel, Uturuki na Kanada zinaweza kuwa miongoni mwa wadhamini wa usalama wa Ukraine.

    Mapendekezo hayo pia yatajumuisha muda wa miaka 15 wa mashauriano kuhusu hali ya Crimea iliyotwaliwa na yataanza kutumika iwapo tu kutakuwa na usitishaji vita kamili, Ukraine ilisema.

    Wapatanishi wake walisema kuna nyenzo za kutosha katika mapendekezo ya sasa ya Ukraine ya kutaka kufanyika kwa mkutano kati ya Zelensky na Rais wa Urusi Vladimir Putin, na kuongeza kuwa wanasubiri majibu ya Urusi.

    Hapo awali Ukraine ilipewa njia ya kujiunga na Nato, jambo ambalo Urusi inapinga vikali.

    Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  9. Ripoti ya kumuwekea sumu Abramovich ni sehemu ya vita vya habari - Kremlin

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Tukio linaloshukiwa la kutiliwa sumu kwa bilionea wa Urusi Roman Abramovich katika mazungumzo ya amani mapema mwezi huu halina uhusiano wowote na ukweli, Kremlin inasema, kulingana na shirika la habari la Reuters.

    Wanasema kisa hicho ni sehemu ya "vita vya habari".

    Kremlin pia inasema Abramovich si mwanachama rasmi wa ujumbe wa Urusi nchini Uturuki - ingawa amepigwa picha kwenye mazungumzo na Ukraine.

    Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  10. Wafanyabiashara wa Rwanda wafurahia DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki

    Mpaka wa Petite Bariere

    Mpaka wa Rubavu nchini Rwanda na Goma-DRC ni moja wapo wa mipaka yenye shughuli nyingi na muingiliano mkubwa wa watu.

    Kwa mujibu wa makadirio ya idara husika watu wasiopungua elfu 50 hupitia kwenye mpaka huo kila siku.

    DRC ndiyo soko kubwa la bidhaa za Rwanda hasa chakula kwa wakati huu kupitia kituo hicho cha mpaka.

    Leo DRC inatarajiwa kujiunga rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kukiwa na suala la wachuuzi wadogo-wadogo kutoka Rwanda ambao kwa sasa wanaombwa kuingia nchini humo kwa masharti ya kulipia visa kinyume na ilivyokuwa awali.

    Kwenye mpaka wa Petite Bariere baina ya mji wa Rubavu upande wa Rwanda na mji wa Goma (DRC) wanaovuka mpaka wakati huu siyo wengi kama ilivyokuwa kawaida.

    Kwa mujibu wa wafanyabiashara kutoka Rwanda,hii ni kutokana na vikwazo vilivyowekwa na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya nchi mbili kukubali kufungua mipaka yake mwaka jana ,baada ya mipaka kufungwa mwaka 2020 kutokana na janga la Covid-19.

    Bwana Baringana Teresphore ni fundi umeme mjini Rubavu lakini pia anafanyia kazi mjini Goma,anasema sasa hivi kuingia mjini Goma siyo rahisi :

    ‘’Tunaombwa kuwa karatasi inayoitwa ‘permis de sejour’ ni kibali cha kuonyesha kwamba wewe unaishi Congo au unafanyia kazi nchini Congo.’’

    Kibali hicho kukipata unalipa 40$ na franga 3000 za Congo. Kama unafanya biashara ndogo ndogo ambazo hata mtaji wako siyo kiwango hicho huwezi kumudu gharama ya kibali hicho’’ ameongeza kusema.

    Kabla ya mlipuko wa Covid mambo yalikuwa shwari kiasi kwamba ID au kitambulisho cha kawaida kilitosha kwa wakazi kuvuka na kuruhusu biashara ndogo ndogo.

    th

    DRC ni soko kubwa na muhimu kwa Rwanda hususan chakula lakini pia Rwanda ni njia ya mkato kupitishia bidhaa kutoka nchi nyingine wanachama zikienda DRC –maeneo yake ya mashariki.

    Matarajio ya wananchi wengi kwenye mpaka wa Rwanda na DRC kukubaliwa rasmi kuwa mwanachama wa jumuia afrika mashariki ni kwamba masharti na vikwazo wanavyowekewa watu wa Rwanda yanaondolewa.

    Bi Uwamahoro Alphonsine mjasiriamali kutoka Rwanda anasema huenda kuingizwa kwa DRC ndani ya jumuiya ya EAC ni faraja :

    ‘’Kuna unayanyasaji mwingi tunaopata tukiingia DRC ukiwemo rushwa na pia maswala ya ushuru kwani tunatozwa ushuru mwingi na ambao bila shaka Congo ikiingia ndani ya EAC mambo yatalainika zaidi’’

    Kulingana na wizara ya biashara na viwanda nchini Rwanda mwaka 2020 biashara ya kuvuka mpaka wa DRC ziliingiza pesa milioni 340$ huku mwaka jana biashara baina ya nchi mbili ikiingiza milioni 600$ na kwamba nchi mbili zinafanya kila njia kutafuta mwafaka wa masuala yaliyopo.

  11. Usile au kunywa chochote katika mazungumzo ya Urusi - waziri wa Ukraine

    th

    Kabla ya mazungumzo ya leo mjini Istanbul kuanza, waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alishauri mtu yeyote anayekwenda kwenye mazungumzo na Urusi "asile au kunywa chochote, na ikiwezekana kuepuka kugusa sehemu yoyote".

    Alikuwa akizungumza wakati wa mahojiano na kituo cha habari cha Ukraine Ukrayina 24.

    Onyo hilo lilitolewa baada ya kushukiwa kuwekewa sumu bilionea wa Urusi Roman Abramovich na wapatanishi wa Ukraine mapema mwezi huu katika mazungumzo ya amani kwenye mpaka wa Ukraine na Belarus.

    Kuna tashwishi kuhusu madai hayo ya sumu na afisa mmoja wa Marekani ambaye jina lake halikutajwa alinukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema kuwa taarifa za kijasusi zilidokeza kuwa dalili za wanaume hao zilitokana na sababu za "mazingira", sio sumu.

    Kama tumekuwa tukiripoti, Abramovich ameonekana kwenye mazungumzo, katika picha zinazotangazwa na vyombo vya habari vya Uturuki.

    Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  12. Cadbury yapunguza mraba wa chokoleti ya Dairy Milk

    Chokoleti ya Dairy Milk

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Chokoleti ya Dairy Milk

    Cadbury imepunguza ukubwa wa mraba wake wa chokoleti ya Maziwa yaani Dairy Milk kwa 10%, lakini haitapunguza bei kwa wateja.

    Kampuni mama ya Mondelez imehusisha hatua hiyo na utengenezaji wa chokoleti yake, kwani ilipunguza saizi ya mraba kutoka 200g hadi 180g.

    Bado zinauzwa kwa £2 licha ya kupunguzwa.

    Kampuni ya Marekani ya Mondelez ilisema hatua hiyo ilikuwa ya kwanza ya kupunguzwa kwa ukubwa wa mraba wa chokoleti ya Maziwa ya Dairy Milk katika kipindi cha muongo mmoja.

    Mnamo mwaka 2020, kampuni hiyo ilishutumiwa kwa kupunguza saizi ya bidhaa hiyo huku bei ikiendelea ile ile ili kuongeza faida.

    Kupanda kwa gharama

    Hatua ya hivi punde inawadia wakati gharama ya chakula inaongezeka, na kuweka shinikizo zaidi kwa kaya za Uingereza wakati wa mgogoro wa kupanda kwa maisha.

    Wiki iliyopita, kasi ya mfumuko wa bei (ambayo hufuatilia jinsi gharama ya maisha inavyobadilika kadri muda unavyopita) ilifikia kiwango cha juu cha miaka 30 cha 6.2% kwa mwaka hadi Februari.

    Msemaji wa kampuni ya Mondelez alisema: " Tunakabiliwa na changamoto zilezile ambazo kampuni nyingi za chakula tayari zimeripoti linapokuja suala la kuongezeka kwa gharama za uzalishaji - ikiwa ni viungo, nishati au ufungaji - na kuongezeka kwa mfumuko wa bei.

  13. Roman Abramovich anaonekana kuwa kwenye mazungumzo ya Istanbul

    Roman Abramovich anaonekana kwenye mazungumzo ya Istanbul

    Chanzo cha picha, TRT

    Maelezo ya picha, Roman Abramovich anaonekana kwenye mazungumzo ya Istanbul

    Bilionea wa Urusi Roman Abramovich - mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea - ameonekana kwenye meza ya mazungumzo huko Istanbul.

    Katika picha zinazooneshwa na vyombo vya habari vya Uturuki, anaonekana akiwa ameketi kwenye meza pamoja na Ibrahim Kalin - msemaji wa Rais Erdogan, na amevaa vipokea sauti vya kutafsiri sauti.

    Hayuko kwenye meza kuu ya wajumbe wa Urusi na Ukraine.

    Kalin ameripotiwa kusaidia kuratibu mikutano kati ya viongozi wafanyabiashara matajiri wa Urusi na mjumbe wa Ukraine katika hoteli za Istanbul.

    Uwepo wa Abramovich unaonyesha bado anahusika katika kiwango fulani kwenye majaribio ya upatanishi.

    Jana ripoti ziliibuka kwamba alipata dalili za tuhuma za sumu katika mazungumzo ya amani kwenye mpaka wa Ukraine na Belarus mapema mwezi huu.

    Soma zaidi:

  14. Truss anamshutumu Putin kwa kitendo cha kuchukiza cha 'utekaji nyara'

    Rais wa Urusi Vladmir Putin

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais wa Urusi Vladmir Putin

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Liz Truss amemshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kutumia "mbinu ya kuchukiza" ya kuwateka nyara raia wa Ukraine.

    Katika ujumbe wa Twitter, Truss alisema kwamba Putin aliamua "kuchukua hatua za kukata tamaa".

    Maoni yake yalikuja baada ya shirika la kutetea haki za binadamu la Ukraine, Zmina, kusema kuwa limewatambua watu kadhaa ambao walikuwa wamechukuliwa mateka.

    Kundi hilo pia linadai kuwa "maelfu" ya raia wa Ukraine wamepelekwa Urusi kinyume na matakwa yao.

    Soma zaidi:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  15. Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lawahusisha wanajeshi wa Rwanda na waasi

    Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linasema kuwa wanajeshi wa Rwanda waliwasaidia waasi wa M23 wakati wa shambulio la Jumatatu karibu na mpaka wake na Rwanda na Uganda.

    Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema limewakamata wanajeshi wawili wa Rwanda waliohusika na shambulizi hilo na kuwawasilisha katika mkutano na waandishi wa habari.

    Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa msemaji wa serikali ya Rwanda, msemaji wa jeshi na mwanasheria mkuu hawakujibu maombi ya kutoa maoni yao.

    Katika taarifa, jeshi la Congo limesema waasi walishambulia maeneo yao huko Tshanzu na Runyonyi.

    Ilisema "hatua zote zimechukuliwa ili kurejesha mamlaka haraka" katika mikoa hiyo miwili.

    Umoja wa Mataifa umekuwa ukishutumu Rwanda na Uganda kwa kuunga mkono M23 ingawa serikali zote mbili zinakanusha madai hayo.

    Kundi hilo la waasi, linaloundwa na waasi wa jeshi ambao wengi wao ni wa kabila la watutsi, lilipewa jina baada ya mkataba wa amani wa Machi 23, 2009 uliotiwa saini na serikali na wanamgambo wa zamani.

  16. Watu wenye silaha washambulia treni ya Nigeria yenye takriban watu 1,000

    Wasafiri wengi wanapendelea kusafiri kwa treni kwa sababu ya kuongezeka kwa mashambulizi ya barabarani

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Wasafiri wengi wanapendelea kusafiri kwa treni kwa sababu ya kuongezeka kwa mashambulizi ya barabarani

    Watu wenye silaha nchini Nigeria wameripotiwa kuwateka nyara idadi isiyojulikana ya abiria kutoka kwa treni katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa nchi hiyo.

    Genge hilo lilichimba njia kati ya mji mkuu Abuja na mji wa Kaduna na kulazimisha treni ya jioni kusimama. Baadhi ya abiria 1000 waliokuwa ndani ya treni hiyo walijificha huku risasi zikifyatuliwa.

    Mwanamume mmoja anaripotiwa kuuawa baada ya watu wenye silaha kupanda treni.

    Vikosi vya usalama sasa vimeingilia kati na kuwapeleka majeruhi hospitalini.

    Kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi na utekaji nyara kwenye barabara kuu kati ya Abuja na Kaduna, wasafiri wengi sasa wanapendelea kusafiri kwa treni.

    Hii ni mara ya pili kwa reli hiyo kushambuliwa katika muda wa miezi sita iliyopita.

    Utekaji nyara wa kuitisha kikombozi umekuwa jambo la kawaida kaskazini mwa Nigeria na majambazi, kama wanavyojulikana nchini humo, wanazidi kuwa wajasiri.

    Siku ya Jumamosi walishambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kaduna.

  17. Mzozo wa Ukraine: Habari za hivi punde

    Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi haya ndio matukio ya hivi punde:

    • Wajumbe wa Urusi na Ukraine wamewasili Istanbul kwa mazungumzo ya kwanza baada ya wiki kadhaa. Ukraine inasema kipaumbele chake ni kufanya mazungumzo ya kusitisha mapigano, lakini Marekani na Ukraine pia zimeonyesha mashaka kuhusu nia ya Urusi.
    • Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliomba mara moja mataifa yenye nguvu duniani kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya mafuta.
    • Ving'ora vya mashambulizi ya anga vilisikika kabla ya mapambazuko siku ya Jumanne, huku maafisa wakisema njia za kutoka katika baadhi ya miji zimezibwa na mashambulizi ya Urusi.
    • Vyanzo vya karibu na bilionea wa Urusi Roman Abramovich vinasema alipata dalili za tuhuma za kuwekewa sumu kwenye mazungumzo ya amani mapema mwezi huu. Sasa amepata nafuu. Wapatanishi wawili wa amani wa Ukraine pia walisemekana kuathirika.
    • Rais wa Marekani Joe Biden amesema "hatageuza" maoni yake yenye utata kwamba Vladimir Putin "hawezi kubaki madarakani". Biden alisema alikuwa akielezea "ghadhabu ya kimaadili ninayohisi", badala ya "kueleza mabadiliko ya sera"
    • Wizara ya Ulinzi ya Uingereza inaamini kwamba mamluki kutoka kundi la Wagner la Urusi wametumwa mashariki mwa Ukraine, na takriban wafanyakazi 1,000 wakiwa njiani.
    • Afisa mkuu wa ulinzi wa Marekani alithibitisha kuwa Ukraine imefanikiwa kuuteka tena mji wa Trostyanets karibu na Sumy na kwamba kusonga mbele kwa Urusi kuelekea Kyiv kumekwama huku kukiwa na mwelekeo kuelekea eneo la mashariki la Donbas.
  18. Ujumbe wa Ukraine wawasili Uturuki kwa mazungumzo

    Wajumbe wa Ukraine wametua Istanbul kwa mazungumzo

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wajumbe wa Ukraine wametua Istanbul kwa mazungumzo

    Ujumbe wa Ukraine umewasili mjini Istanbul, Uturuki kwa mazungumzo ya amani na wenzao wa Urusi.

    Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Oleksii Reznikov, pamoja na = Mikhail Podolyak, kiongozi wa ofisi ya Rais.

    Kundi hilo linasema kipaumbele chake ni kusitisha vita ijapokuwa kuna mashaka ikiwa hilo litafanyika.

    Mazungumzo haya ya ana kwa ana, ambayo ni ya kwanza ndani ya zaidi ya wiki mbili, yataongozwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

    Mkutano huo umepangiwa kuanza leo saa nne (07:00 GMT).

    Miongoni mwa matakwa ya Urusi ni Ukraine kuachana na mpango wowote wa kujiunga na Nato – suala ambalo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kuafikiana.

    Masuala mengine msumari moto yanayotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na hatima ya maeneo yanayodhibitiwa na watu wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine, pamoja na hali ya Crimea, ambayo ilichukuliwa rasmi na Urusi mwaka 2014.

    Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  19. Will Smith amuomba radhi Chris Rock baada ya kumzaba kofi

    Will Smith akimzaba kibao Chris Rock

    Chanzo cha picha, Reuters

    Will Smith amemuomba msamaha Chris Rock baada ya kumzaba kibao katika jukwaa la Oscars, akisema tabia yake "haikubaliki na haina udhuru".

    "Ningependa kukuomba msamaha hadharani, Chris," alisema katika taarifa yake. "Nilivuka mpaka na nilikosea."

    Haya yanajiri baada ya Chuo cha filamu cha Oscars kilimlaani Smith juu ya tukio hilo na kutangaza kwamba inatathmini marekebisho rasmi

    Nyota huyo alimpiga kibao Rock jukwaani baada ya mcheshi huyo kufanya utani kuhusu mke wa mwigizaji huyo, Jada Pinkett Smith.

    Rock alimtaniaPinkett Smith kwa kunyoa nywele, baaada ya kuzipoteza kutokana na hali inayofahamika kama alopecia.

    Muda mfupi baadaye Smith alishinda tuzo yake ya kwanza ya Oscar kutokana na uigizaji wake wa baba ya wachezaji nyota wa tennis Venus na Serena Williams katika filamu ya King Richard.

    "Vurugu njia zote ni sumu na uharibifu," Smith alisema katika taarifa hiyo, ambayo ilitumwa kwenye mtandao wa Instagram.

    "Mwenendo wangu wa jana usiku katika Tuzo za Academy hazikubaliki na hazina udhuru. Utani ni sehemu ya kazi, lakini mzaha kuhusu hali ya kiafya ya Jada ulikuwa mzito sana kwangu na niliitikia kihisia."

    Smith alimuomb msahamaha Rock moja kwa moja, akisema " alivuka mpaka". Pia aliomba msamaha kwa Chuo na familia ya Williams.

    "Ninajuta sana kwamba tabia yangu imetia doa safari ambayo imekuwa ya kupendeza kwetu sote," aliandika.

    Ruka Instagram ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe

    Kabla ya msamaha wa Smith, shirika lililo nyuma ya Oscars lilisema katika taarifa kwamba "linalaani vitendo" vya Smith.

    "Tumeanza rasmi ukaguzi kuhusu tukio hilo na tutachunguza hatua na matokeo zaidi kwa mujibu wa Sheria zetu, Viwango vya Maadili na sheria za California," ilisema.

    Soma zaidi:

    • Will Smith amzaba kibao mchekeshaji Rock jukwaani kwenye tuzo za Oscars
  20. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumanne 29.03.2022.