Tunapoingia
siku ya 13 ya uvamizi wa Warusi nchini Ukraine, haya hapa ni baadhi ya matukio
makuu kutoka saa 24 zilizopita:
•
Ukraine inasema mashambulizi ya Urusi yanawazuia raia kuondoka kwa usalama
katika miji yao iliyozingirwa
• Makumi
ya maelfu ya watu kote Ukraine hawana kawi na, katika mji wa bandari wa
Mariupol, wanakosa chakula na maji.
• Duru
ya tatu ya mazungumzo ya amani kati ya Russia na Ukraine yamalizika kwa
makubaliano madogo. Raundi ya nne itafanyika Jumanne
•
Marekani, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zimeapa kuendelea kupandisha gharama
kwa Urusi kwa uvamizi wake wa "bila sababu" dhidi ya Ukraine.
• Urusi
ilitishia kupunguza uagizaji wake wa gesi asilia Ulaya kama kulipiza kisasi kwa
vikwazo vya Magharibi
• Katika
hotuba yake ya hivi punde ya video, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema
atakaa Kyiv "ilimradi tu kushinda vita hivi"
•
Coca-Cola na McDonalds ni miongoni mwa makampuni yanayokabiliwa na uwezekano wa
kususia wateja kwa kushindwa kwao kujiondoa nchini Urusi.
•
Ukraine inasema imemuua kamanda mkuu wa jeshi la Urusi katika vita karibu na
Kharkiv - madai hayo hayajathibitishwa na BBC
Kiongozi
wa kijeshi wa Urusi auawa vitani, yasema Ukraine
Kamanda
wa ngazi za juu katika jeshi la Urusi ameuawa wakati wa mapigano karibu na
Kharkiv, kulingana na wizara ya ulinzi ya ujasusi ya Ukraine.
BBC
haiwezi kuthibitisha dai hilo kwa uhuru; Maafisa wa Urusi hawajatoa maoni
yoyote.
Kulingana
na taarifa kutoka wizara ya ulinzi ya Ukraine, Vitaly Gerasimov alikuwa
jenerali mkuu, na naibu kamanda wa kwanza wa Jeshi la 41 la Wilaya ya Kati ya
Kijeshi ya Urusi.
Idadi ya
maafisa wakuu wa jeshi la Urusi pia waliuawa na kujeruhiwa, inasema.
Ujasusi
wa Ukraine unasema Gerasimov alishiriki katika vita vya pili vya Chechnya na
operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Syria. Alipokea medali "kwa kuirejesha
Crimea".
Maafisa
wa Ukraine walituma picha ya mtu waliyesema kuwa ni Gerasimov kwenye ukurasa wa
Twitter, yenye neno "Amefutwa" kwa herufi nyekundu chini kabisa.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine