Ukraine na Urusi: Marekani na Uingereza zatangaza marufuku ya mafuta kutoka Urusi
Serikali ya Uingereza itaanza kupiga maraufuku mafuta ya Urusi na bidhaa zake kuanzia mwisho wa 2022. Tayari Rais Joe Biden amethibitisha marufuku hiyo kuhusu mafuta ya Urusi , gesi na mkaa unaoingia nchini mwake.
Moja kwa moja
Rais Zelensky: Tutapigana na Urusi, fukweni, msituni na ardhini
Chanzo cha picha, Getty Images
Zelensky amemuiga kiongozi wa wakati wa vita Uingereza
Winston Churchill huku akiapa Ukraine "itapigana hadi mwisho".
Akirejelea hotuba ya Churchill maarufu ya 1940
"tutapigana kwenye fukwe," Zelensky anasema: "Hatutaacha na
hatutapoteza.
"Tutapigana hadi mwisho baharini, angani, tutaendelea
kupigania ardhi yetu, kwa gharama yoyote. Tutapigana misituni, mashambani,
ufukweni, mitaani."
Habari za hivi punde, Mzozo wa Ukraine: Marekani na Uingereza kusitisha ununuzi wa mafuta kutoka Urusi
Rais Joe Biden amethibitisha kwamba taifa lake limepiga
marufuku ununuzi wa mafuta, gesi na mkaa kutoka Urusi .
Anasema kwamba hatua hiyo inamaanisha kwamba , raia wa Marekani
watauathiri kwa mara nyengine uongozi wa rais Putin.
Hatua hiyo inajiri baada ya Serikali ya Uingereza kutagaza
kwamba itaanza kupiga marufuku ununuzi wa mafuta hayo Pamoja na bidhaa zake
mwisho wa mwaka 2022.
Imesema kuwa wakati huo utapatia soko , biashara na wasambazaji
wa bidha hiyo muda zaidi kutafuta njia mbadala .
Wanajeshi wa Urusi kati ya 2,000 na 4,000 wameuawa Ukraine, Marekani yasema
Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi imekumbwa na vifo vingi vya wanajeshi wake kati ya 2,000 na 4,000 nchini Ukraine, mkuu wa idara ya ujasusi ya Marekani ameliambia bunge la Marekani.
"Walikuwa na mpango mbaya," Scott Berrier alisema, wakati akikadiria, kwa ujasiri mdogo, vifo kulingana na taarifa za usalama na vyanzo vingine.
Maelezo hayo yanafuatia ripoti za awali, kutoka wizara ya ulinzi ya Ukrania, kwamba kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Urusi aliuawa katika mapigano makali katika mji wa mashariki wa Ukraine wa Kharkiv.
Urusi kufunga bomba kuu la gesi Ulaya kama marufuku ya ununuzi wa mafuta ya Urusi itaendelea
Chanzo cha picha, AFP
Urusi imesema imetishia kulifunga bomba lake kuu la gesi inayosafirishwa kuelekea Ujerumani iwapo mataifa ya magharibi yataendelea na msimamo wa kuzuia mafuta ya Urusi.
Naibu Waziri Mkuu Alexander Novak alisema "kuzuiwa kwa mafuta ya Urusi kutasababisha athari mbaya kwa soko la dunia", na kusababisha bei kuwa zaidi ya mara mbili hadi $ 300 kwa pipa.
Marekani imekuwa ikichunguza uwezekano wa kupigwa marufuku na washirika wake kama njia ya kuiadhibu Urusi kwa uvamizi wake nchini Ukraine. Lakini Ujerumani na Uholanzi ziliukataa mpango huo siku ya Jumatatu.
Umoja wa Ulaya (EU) inapata karibu 40% ya gesi yake na 30% ya mafuta yake kutoka Urusi, na haina mbadala rahisi ikiwa Urusi itafunga ama kuharibu mifumo na mabomba ya kusafirisha gasi na mafuta.
Uingereza inatarajiwa kutangaza marufuku ya uagizaji wa mafuta ya Urusi. Waziri Mkuu Boris Johnson anatarajiwa kutoa tangazo muda wowote, kuuungana na Marekani kupiga marufuku juu ya uagizaji wa mafuta na gesi ya Urusi.
Hasira zaongezeka Kenya baada ya mwanamke kuvuliwa mchana kweupe
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameiagiza mamlaka kuwasajili tena waendesha boda boda wote kufuatia hasira ya umma juu ya shambulio dhdi ya mwanamke aliyekuwa ndani ya gari lake katika mji mkuu wa Nairobi.
Kanda ya video ilimuonesha mwanamke huyo - kutoka Zimbabwe - akinyang'anywa nguo zake na kushambuliwa huku akipiga mayowe kuomba msaada.
Inaaminika gari la mwanamke huyo lilihusika kwenye ajali ya bodaboda na madereva hao wa bodaboda walimshambulia na kumtisha kwa kisasi.
Tukio hilo lilitokea siku ya Ijumaa katika barabara ya Wangari Maathai, iliyopewa jina la mwanamitindo maarufu wa na mwanamitindo wa Kenya na mwanamke wa kwanza mwafrika kushinda tuzo ya amani ya Nobel.
Polisi wanasema wamewakamata waendesha bodaboda waliohusika, ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani. Angalau pikipiki 100 pia zinashikiliwa.
Mapema leo Jumanne , kulikuwa na maandamano ya wanawake katika jiji la Nairobi kulaani tukio hilo.
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang'i alisema ameshangazwa na kukadhabishwa na tukio hilo.
Eritrea walilia huduma za Intanet, wamtaka Bilionea Musk kuwasaidia
Bilionea mzaliwa wa Afrika Kusini Elon Musk ameombwa kutoa huduma yake ya intaneti nchini Eritrea baada ya hivi karibuni kuisaidia Ukraine.
Mwanzilishi wa SpaceX ametoa msaada wa dishi za mtandao za Starlink kwa Ukraine kwa hofu kwamba upatikanaji wa intaneti ungeweza kukatizwa kufuatia uvamizi wa Urusi.
Kupitia mtandao wa twitter na hashtag ya #Starlink4Eritrea, raia wengi wa Eritrea wanaoishi nje ya nchi wamekuwa wakisema kuwa Eritrea imetengwa na dunia kwa miongo miwili kwa sababu ya ukosefu wake wa intaneti.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 2
Eritrea ina moja ya viwango vya chini kabisa vya huduma za intaneti barani Afrika - ripoti ya Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano iliiweka nchi hiyo kwenye kiwango cha chini ya asilimia 1.
EriTel inayomilikiwa na serikali ni mtoa huduma pekee wa huduma za mawasiliano ya simu nchini humo.
Ili kuingia kupata mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter, watu hutumia VPN) ili kuzuia udhibiti wa serikali.
Tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993, Eritrea imekuwa nchi ya chama kimoja kinachoongozwa na Rais Isaias Afwerki. Nchi hiyo haijawahi kuwa na uchaguzi na Wiki iliyopita, ilikuwa moja ya nchi tano tu duniani ambazo zilipiga kura kupinga azimio la kubatilisha uvamizi wa Urusi kwa Ukraine katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Wanafunzi 11 wa Kitanzania waliokwama Sumy wafika Moscow
Wanafunzi wa Kitanzania waliokwama huko Sumy, kaskazini-mashariki mwa Ukraine, wametakiwa kuelekea Sudja mara moja ambapo wanajeshi wa Urusi watawaruhusu kuondoka nchini humo salama.
Wanafunzi hao, wanaosoma karibu na mpaka na Urusi, hawakuweza kuondoka nchini kutokana na uvamizi wa Urusi.
Wiki iliyopita, Tanzania ilisema inafanya kila iwezalo kuhakikisha raia wake wanahamishwa wakiwa salama huku wanafunzi wengine walioweza kuondoka salama Ukraine walisema wanawasiliana na waliokwama nchini humo.
The Citizen limeripoti kuwa wanafunzi wanne waliokimbia vita walifika nyumbani Tanzania Jumatano iliyopita.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumamosi, Balozi wa Tanzania mjini Moscow aliwaambia wanafunzi hao waondoke mara moja kuelekea Sudja ambako watapokelewa na wanajeshi wa Urusi na kusafirishwa hadi kwenye ubalozi huko Belgorod.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Takribani watu 400 wapoteza maisha, 801 wajeruhiwa Ukraine - UN
Chanzo cha picha, Reuters
Kulingana na takwimu za hivi punde za Umoja wa Mataifa, watu 1,207 wamepata madhara tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kuanza tarehe 24 Februari.
Idadi hiyo inajumuisha watu 406 waliouawa na 801 kujeruhiwa - lakini takwimu "zina uwezekano mkubwa kuwa idadi zaidi ya hiyo" anasema Liz Throssell, msemaji wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu.
Majeraha mengi ni matokeo ya "mashambulio ya anga na silaha za milipuko", unasema Umoja wa Mataifa, na "mamia ya majengo ya makazi" yameharibiwa katika miji kote Ukraine.
Mwanahabari mmoja anaripotiwa kuuawa. Umoja wa Mataifa pia umeelezea wasiwasi wake kuhusu "kukamatwa kiholela" kwa wafuasi wanaounga mkono Ukraine katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa kijeshi wa Urusi - pamoja na ghasia dhidi ya wale wanaochukuliwa kuwa wanaounga mkono Urusi katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali ya Ukraine.
Takwimu za hivi punde za Umoja wa Mataifa zinaonesha takriban watu 12,700 wamekamatwa nchini Urusi kwa kufanya maandamano ya amani ya kupinga vita.
Shirika hilo lilikosoa "sheria kandamizi" zilizowekwa na Urusi hivi karibuni ambazo zinaweka kifungo cha hadi miaka 15 jela kwa wale wanaoshtakiwa kwa kueneza habari iliyoitwa ya "uongo" kuhusu uvamizi huo, au kudharau vikosi vya jeshi la Urusi.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Watu milioni mbili wameondoka Ukraine-UN
Chanzo cha picha, Getty Images
Idadi ya wakimbizi wanaokimbia vita nchini Ukraine imepita milioni mbili.Umoja wa Mataifa umeambia BBC.
Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi, hapo awali alitaja kuhama kwa watu wengi kutoka nchi hiyo kuwa mzozo wa wakimbizi unaokua kwa kasi zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Watu milioni1.2 kutoka Ukraine wakimbialia Poland
Chanzo cha picha, EPA
Kwa mujibu wa shirika la ulinzi wa Mipaka wa Poland, watu milioni 1.2 wamekimbia kutoka Ukraine hadi Poland tangu vita kuanza.
Siku ya Jumatatu pekee, watu 141,500 walivuka mpaka, shirika hilo liliandika kwenye ukurasa wa Twitter - chini ya rekodi ya kila siku ya Jumapili ya 142,300.
Takriban 90% ya watu wanaokimbia ni raia wa Ukraine, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Inakadiriwa kuwa takriban 40% ya wakimbizi tayari wameondoka Poland na kwenda nchi nyingine.
Poland ilikuwa tayari nyumbani kwa Waukraine wengi - makadirio yanatofautiana kati ya watu milioni moja na mbili - na wengi wamekuja kukaa na familia au marafiki hapa.
Maelfu ya Wapoland wanawahifadhi wakimbizi katika makazi yao pia, na leo bunge la Poland litajadili sheria ya dharura ili kuwafidia wale wanaowahifadhi kwa gharama zao za ziada.
Sheria hiyo pia itawaruhusu Waukraine kuishi na kufanya kazi nchini Poland kwa muda wa miezi 18 na kupokea huduma za afya na masomo bila malipo.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Moderna kujenga kituo cha kutengeneza chanjo nchini Kenya
Chanzo cha picha, Moderna
Kenya imetia saini mkataba na kampuni ya teknolojia ya kibayoteknolojia ya Marekani, Moderna Inc, kujenga kituo cha kutengeneza chanjo nchini.
Kituo hicho ikiwa kinatarajiwa kutoa hadi dozi milioni 500 za chanjo kila mwaka.
Mpango huo umesifiwa kuwa utasaidia kutatua upatikanaji wa chanjo katika janga la sasa la virusi vya corona na katika milipuko ya siku zijazo. Moderna inatarajia kuwekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 500 katika kituo hicho.
Benin yamwachilia huru kiongozi wa kundi linalotaka kujitenga na Nigeria Sunday Igboho
Chanzo cha picha, SAIF
Mamlaka
nchini Benin imemwachilia huru kiongozi wa Nigeria anayetaka kujitenga, Sunday
"Igboho" Adeyemo, kulingana na msemaji wake.
Bw
Igboho alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Benin Julai 2021 pamoja na mkewe
kwa ombi la Nigeria, ingawa mkewe aliachiliwa siku chache baadaye. Wanandoa hao
walisemekana kuelekea Ujerumani ambako mkewe ni raia.
Alishtakiwa
kwa kuingia Benin kinyume cha sheria na kupanga kuleta fujo lakini alikanusha
mashtaka. Mamlaka ya Nigeria haikuwahi kutoa ombi rasmi la kurejeshwa kwake
nchini mwake.
Katika
taarifa yake siku ya Jumatatu, msemaji wake alisema Bw Igboho aliachiliwa kwa
kiongozi wa shirika mwamvuli la Makundi ya Kujitawala ya Yoruba, Banji
Akintoye.
Maelezo
juu ya kuachiliwa kwake bado hajayatolewa
Nigeria
inamtuhumu Bw Igboho kwa kuhifadhi silaha, akitaka nchi hiyo isambaratike na
kuchochea mauaji ya kikabila.
Bw
Igboho anasifiwa kama shujaa na wafuasi wake baada ya kutoa wito kwa taifa la
Yoruba kusini-magharibi mwa nchi hiyo.
Alitoroka
nchini baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na polisi wa siri wa Nigeria mnamo
Julai 2021 ambapo washirika wake wawili waliuawa.
Watoto waripotiwa kuuawa katika shambulio kwenye kitongoji cha Sumy
Chanzo cha picha, Reuters
Hapo awali tuliripoti kwamba watoto ni miongoni mwa waathiriwa wa mashambulizi ya anga kwenye mji wa Sumy na vitongoji vyake mwishoni mwa Jumatatu, kwa mujibu wa afisa wa jeshi la Kiukreni.
Dmytro Zhyvytsky, anayeongoza Utawala wa Kijeshi wa Mkoa wa Sumy, alisema katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook kwamba baada ya 23:00 saa za ndani ndege za kivita za Urusi zilifanya mashambulizi kwenye jiji la kaskazini-mashariki.
"Kwa bahati mbaya, watoto ni miongoni mwa waliouawa." Zhyvytsky alisema, na kuongeza kuwa zaidi ya watu 10 waliuawa.
BBC haikuweza kuthibitisha madai hayo . "Watoto wanauawa," aliandika kwenye chapisho la Facebook, akichapisha video ya shambulio lililoripotiwa. "Hatutasamehe kamwe!" aliongeza.
Moscow iko tayari kupisha raia waliokwama Ukraine kuondoka
Urusi iko tayari kutoa nafasi kwa raia kutoka nchini Ukraine saa 10:00 saa za Moscow (07:00 GMT), zilisema ripoti za vyombo vya habari vya serikali ya Urusi.
Wamenukuu maafisa wa wizara ya ulinzi ya Urusi wakisema hili litafanywa ili kuwahamisha raia kutoka miji ya Kyiv, Chernihiv, Sumy, Kharkiv na Mariupol.
Njia nyingi za uokoaji zinazotolewa na Moscow ni kwenda Urusi - hali ambayo hapo awali ilielezewa kuwa isiyokubalika na serikali ya Kyiv.
Ukraine haijasema chochote kuhusu mpango huo mpya wa Urusi.Majaribio kadhaa ya hapo awali ya kuwahamisha hayakufaulu, huku pande zinazozozana zikilaumiana.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Vita nchini Ukraine: Urusi yaonya inaweza kukata usambazaji wa gesi ikiwa marufuku ya mafuta itaendelea
Chanzo cha picha, AFP
Urusi
imesema huenda ikafunga bomba lake kuu la gesi hadi Ujerumani ikiwa nchi za
Magharibi zitaendelea na kupiga marufuku mafuta ya Urusi.
Naibu
Waziri Mkuu Alexander Novak alisema "kukataliwa kwa mafuta ya Urusi
kutasababisha matokeo mabaya kwa soko la kimataifa", na kusababisha bei
kuwa zaidi ya mara mbili hadi $300 kwa pipa.
Marekani
imekuwa ikichunguza uwezekano wa kupiga marufuku pamoja na washirika wake kama njia ya kuiadhibu Urusi kwa uvamizi
wake nchini Ukraine.
Lakini
Ujerumani na Uholanzi zilikataa mpango huo siku ya Jumatatu.
EU
inapata takriban 40% ya gesi yake na 30% ya mafuta yake kutoka Urusi, na haina
mbadala rahisi ikiwa usambazaji utakatizwa.
Katika
hotuba yake kwenye runinga ya serikali ya Urusi, Bw Novak alisema
"haitawezekana kupata haraka mbadala wa mafuta ya Urusi kwenye soko la
Ulaya".
"Itachukua
miaka, na bado itakuwa ghali zaidi kwa watumiaji wa Ulaya. Hatimaye, wataumizwa
zaidi na matokeo haya," alisema.
Akiashiria
uamuzi wa Ujerumani mwezi uliopita wa kufungia uidhinishaji wa Nord Stream 2,
bomba jipya la gesi linalounganisha nchi hizo mbili, aliongeza kuwa vikwazo vya
mafuta vinaweza kusababisha hatua za kulipiza
kisasi.
"Tuna
kila haki ya kuchukua uamuzi unaolingana na kuweka zuio la kusukuma gesi
kupitia bomba [lililopo] la Nord Stream 1," alisema.
Urusi
ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa uzalishaji wa gesi asilia na ya pili kwa mafuta
yasiyosafishwa, na hatua yoyote ya kuiwekea vikwazo sekta yake ya nishati
itaharibu vibaya uchumi wake yenyewe.
Ukraine
imezisihi nchi za Magharibi kupitisha marufuku hiyo, lakini kuna wasiwasi
kwamba ingepelekea bei kupanda. Hofu ya wawekezaji ya kuwekewa vikwazo
ilipelekea mafuta ghafi ya Brent kufikia $139 kwa pipa kwa wakati mmoja
Jumatatu - kiwango chake cha juu zaidi kwa karibu miaka 14.
Bei ya
wastani ya petroli ya Uingereza pia ilifikia rekodi mpya ya 155p kwa lita.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Maandamano dhidi ya shambulizi dhidi ya dereva wa kike Kenya huku 200 wakikamatwa
Chanzo cha picha, Getty Images
Polisi nchini Kenya wamewakamata zaidi ya waendeshaji 200 wa boda boda katikati mwa jiji la Nairobi huku msako mkali dhidi ya sekta hiyo ukizidi kufuatia unyanyasaji wa kingono wa dereva wa kike kwenye barabara ya Wangari Maathai.
Inspekta Mkuu wa polisi Hillary Mutyambai alitangaza hayo Jumanne. Idadi hiyo iliongezeka kutoka 32. Zaidi ya pikipiki 12 zimezuiliwa.
Hapo awali, polisi walisema ni watu 16 pekee waliotambuliwa na kuhusishwa na shambulio dhidi ya mwanamke huyo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 1
Video ya
dereva huyo wa kike mwenye
umri wa 32, akinyanyaswa kimwili na kingono na genge la waendesha bodaboda
iliibuka mtandaoni Jumatatu, na kuzua taharuki kwa umma.
Shambulio
hilo lilitokea Ijumaa iliyopita saa kumi na moja jioni wakati dereva huyo alipomgonga mwendesha mmoja wa boda boda
.
Alisimama
mita chache kutoka eneo la tukio, lakini alifukuzwa na kundi la waendesha boda
boda , ambao baadhi yao walijaribu kumwibia.
Walimfuata
kwa kilomita chache na kulizuia gari lake.
Kisha
wakafungua mlango wa gari lake kwa nguvu na mwanamke huyo akapiga mayowe kuomba
msaada. Mmoja wa washambuliaji wake, wakati huu wote, alikuwa akirekodi matukio.
Alipoteza
pesa na vitu vingine vya thamani kwenye zogo hilo. Aliokolewa na polisi wa
trafiki ambao walitahadharishwa na madereva wengine waliokuwa wameshuhudia kisa
hicho.
Waziri
wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i
alisema "alishtushwa na kuchukizwa" na klipu hiyo ya video.Watu wengi
mtandaoni wamelaani kitendo hicho na kuwataka polisi kuwachukulia hatua kali
waliohusika
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 2
Jaji mkuu wa Kenya Martha Koome akilaani kitendo hicho amesema kuna haja ya kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya visa kama hivyo vya unyanyasaji ili wajihisi salama katika nchi yao .
Koome alisema ni jambo la kusikitisha kwa shambulio hilo kufanyika katika mkesha wa siku ya Kimataifa ya Wanawake.
Amesema mashirika na idara za serikali zinafaa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba visa kama hivyo havitokei .
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 3
Leo maandamano yamefanyika jijini Nairobi kulalamikia tukio hilo .Mamia ya watu walijitokeza wakiwa na mabango kutaka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya waendesha boda boda waliomshambulia mwanamke huyon
Ukraine yadai kumuua kamanda mkuu wa kijeshi wa Urusi
Chanzo cha picha, Ukrainian ministry of defence
Tunapoingia
siku ya 13 ya uvamizi wa Warusi nchini Ukraine, haya hapa ni baadhi ya matukio
makuu kutoka saa 24 zilizopita:
•
Ukraine inasema mashambulizi ya Urusi yanawazuia raia kuondoka kwa usalama
katika miji yao iliyozingirwa
• Makumi
ya maelfu ya watu kote Ukraine hawana kawi na, katika mji wa bandari wa
Mariupol, wanakosa chakula na maji.
• Duru
ya tatu ya mazungumzo ya amani kati ya Russia na Ukraine yamalizika kwa
makubaliano madogo. Raundi ya nne itafanyika Jumanne
•
Marekani, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zimeapa kuendelea kupandisha gharama
kwa Urusi kwa uvamizi wake wa "bila sababu" dhidi ya Ukraine.
• Urusi
ilitishia kupunguza uagizaji wake wa gesi asilia Ulaya kama kulipiza kisasi kwa
vikwazo vya Magharibi
• Katika
hotuba yake ya hivi punde ya video, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema
atakaa Kyiv "ilimradi tu kushinda vita hivi"
•
Coca-Cola na McDonalds ni miongoni mwa makampuni yanayokabiliwa na uwezekano wa
kususia wateja kwa kushindwa kwao kujiondoa nchini Urusi.
•
Ukraine inasema imemuua kamanda mkuu wa jeshi la Urusi katika vita karibu na
Kharkiv - madai hayo hayajathibitishwa na BBC
Kiongozi
wa kijeshi wa Urusi auawa vitani, yasema Ukraine
Kamanda
wa ngazi za juu katika jeshi la Urusi ameuawa wakati wa mapigano karibu na
Kharkiv, kulingana na wizara ya ulinzi ya ujasusi ya Ukraine.
BBC
haiwezi kuthibitisha dai hilo kwa uhuru; Maafisa wa Urusi hawajatoa maoni
yoyote.
Kulingana
na taarifa kutoka wizara ya ulinzi ya Ukraine, Vitaly Gerasimov alikuwa
jenerali mkuu, na naibu kamanda wa kwanza wa Jeshi la 41 la Wilaya ya Kati ya
Kijeshi ya Urusi.
Idadi ya
maafisa wakuu wa jeshi la Urusi pia waliuawa na kujeruhiwa, inasema.
Ujasusi
wa Ukraine unasema Gerasimov alishiriki katika vita vya pili vya Chechnya na
operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Syria. Alipokea medali "kwa kuirejesha
Crimea".
Maafisa
wa Ukraine walituma picha ya mtu waliyesema kuwa ni Gerasimov kwenye ukurasa wa
Twitter, yenye neno "Amefutwa" kwa herufi nyekundu chini kabisa.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo tarehe Jumanne tarehe 8 Machi 2022