Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Shambulio la Urusi katika mtambo wa nishati wa Ukraine lasababisha moto mkubwa

Kinu kikubwa cha umeme kinachotumia nguvu za kinyuklia nchini Ukraine kimeshika moto kufuatia shambulio la Urusi lakini maafisa wanasema vifaa muhimu vinafanya kazi.

Moja kwa moja

  1. tumefika tamati ya taarifa zetu za moja kwa moja..uwe na mapumziko mema ya mwishoni mwa juma

  2. ‘Wamerushiwa mabomu kwa siku tatu bila kukoma’

    Ana Morari, kutoka Leicestershire, ana familia huko Izyum, kaskazini-mashariki mwa Ukrainia, ambao wamekuwa wwakimuarifu jinsi mambo yalivyo.Binamu yake ana mtoto wa miaka mitatu na amehamia Petrovs'kyi kutafuta usalama.

    Wakati huo huo, mama yake, baba na kaka bado wako Izyum.

    "Binamu yangu amehamia mahali penye usalama, lakini familia yake yote haikutaka kuondoka Isyum."

    "Shangazi yangu ni mfamasia. Amekuwa akifanya kazi muda wote, lakini hawezi kwenda kwenye maduka.

    "Wamenaswa kabisa na vita. Wamerushiwa mabomu kwa siku tatu bila kukoma. Wako kwenye makazi.

    "Habari za Kirusi zinasema Izyum ni hatua ya kimkakati ya kijeshi. Labda ilikuwa miaka 100 iliyopita. Ilikuwa na kiwanda kimoja cha kutengeneza silaha ambacho kilifungwa miaka 30 iliyopita. Walakini, Warusi wanasema hii ndiyo inahitaji kusawazishwa.

    "Sasa wanafyatua risasi kwenye vyumba vya orofa, majumbani, shuleni. Ghala moja limepigwa makombora. Hawana chochote pale.

    "Tunaangalia jinsi tunavyoweza kusaidia angalau wapate kitu. Waliomba nepi na vinginevyo kwa ajili ya watoto. Pia mjomba wangu ni mgonjwa sana.

    ‘’Wengi hawataki kuondoka kwa sababu kuna majambazi tayari kuvamia maghorofa na nyumba zao. Sasa wamekwama. Hawawezi hata kutoka nje.’’

    Soma zaidi:

  3. Urusi yaridhia kusaidia kuwaondoa wanafunzi wa Kitanzania Ukraine

    Ubalozi wa Tanzania mjini Stockholm Sweden pamoja na Ubalozi wa Tanzania ulio nchini Urusi zimesema kwamba kupitia njia za kidiplomasia, serikali ya Urusi imeridhia wanafunzi wa Kitanzania walioko Chuo Kikuu Sumy State kutoka nchini Ukraine kwa kupitia mpaka wa Urusi.

    Taarifa ya Ubalozi wa Tanzania mjini Stockholm na Ubalozi wa Tanzania mjini Moscow inasema zoezi la kutoa wanafunzi kutoka Sumy hadi kwenye mpaka wa Urusi linaratibiwa na serikali ya Urusi na tayari mipango ya utekelezaji imeanza.

    ''Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi utawapokea kwa taratibu nyingine za kurejea nyumbani'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

  4. Habari za hivi punde, Urusi inatumia mabomu mtawanyiko nchini Ukraine - Nato

    Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg anasema kuna ushahidi kwamba Urusi inatumia mabomu ya mtawanyiko (cluster) katika uvamizi wake.

    Katika mkutano na waandishi wa habari, aliwaambia waandishi wa habari: "Tumeona matumizi ya mabomu ya mtawanyiko na tumeona ripoti za matumizi ya aina nyingine za silaha ambazo zitakuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

    Pia anasema muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi hautaweka marufuku ya kuruka ndege juu ya anga ya Ukraine wala kutuma wanajeshi wake huko lakini anaahidi msaada mwingine kwa Kyiv na kumtaka Rais Vladimir Putin kukomesha uvamizi huo mara moja.

  5. Viongozi mbalimbali walaani shambulio dhidi ya kituo cha nyuklia

    Kumekuwa na kilio cha kimataifa kuhusu shambulio lililotokea usiku la Urusi kushambulia kituo kikubwa zaidi cha nishati ya nyuklia barani Ulaya, huko Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine.

    Shambulio hilo lilisababisha jengo la utawala kushika moto, lakini mtambo wenyewe uko salama - ingawa chini ya udhibiti wa Urusi.

    "Vitendo vya hatari vya Rais Putin sasa vinaweza kutishia moja kwa moja usalama wa Ulaya yote," Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema.

    "Sio tu hatari kwa Ukraine na Warusi, ni hatari kwa Ulaya na inacheza na moto ambao kwa kweli hauna umuhimu au ulazima wowote," Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace ameongeza.

    Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema "mashambulizi ya kutisha" kutoka Urusi "lazima yasitishwe mara moja", huku Rais wa Marekani Joe Biden ameitaka Moscow kusitisha shughuli zake za kijeshi katika eneo hilo.

    Jens Stoltenberg, mkuu wa Nato, anasema shambulio hilo linaonesha "kutojali kwa vita hivi na umuhimu wa kuvimaliza".

    Taarifa ya Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi inalaani "shambulio hilo baya" kama "shambulio dhidi ya usalama wa kila mtu" na kutoa wito kwa EU "kuendelea kuitikia kwa umoja na azma kubwa" kuiunga mkono Ukraine.

    Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store pia ameolaani vikali kwa shambulio hilo. "Aina hii ya shambulio ni wazimu," amesema.

    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu kura ya turufu ya Urusi katika azimio la Umoja wa Mataifa, je ina maana gani?
    • Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
  6. Putin: Msituwekee vikwazo zaidi

    Rais Putin ametoa onyo kwa wale wanaopinga hatua ya Urusi nchini Ukraine "kutozidisha tatizo kuwa baya zaidi" kwa kuiwekea nchi yake vikwazo zaidi.

    Rais wa Urusi alikuwa akizungumza katika mkutano wa serikali uliotangazwa kwenye kituo cha habari cha Rossiya 24 kinachomilikiwa na serikali.

    "Hatuna nia mbaya dhidi ya majirani zetu," Putin amedai.

    Na anasema serikali yake haioni " haja" kwa majirani zake kuchukua hatua zaidi ambazo "zitafanya uhusiano wao kuwa mbaya zaidi".

    "Nadhani kila mtu lazima afikirie jinsi ya kurekebisha uhusiano, kushirikiana kawaida na kukuza uhusiano kama kawaida," ameongeza.

    Haya yanajiri wakati mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi za Magharibi wakikusanyika mjini Brussels kutafakari jinsi ya kuishinikiza Urusi kusitisha vita.

    Putin pia anarudia madai yake ya awali kwamba hatua zote zilizochukuliwa na jeshi la Urusi hadi sasa zimefanywa "pekee katika kukabiliana na baadhi ya hatua zisizo za kirafiki dhidi ya Urusi".

    • Mzozo wa Ukraine: Ni vikwazo gani vilivyowekwa dhidi ya Urusi?
    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia kimya
  7. DW yapigwa marufuku Urusi

    Awali tuliripoti juu ya kuzuiwa kwa matangazo ya shirika la utangazaji la Uingereza BBC News nchini Urusi.

    Lakini sasa shirika la utangazaji la Ujerumani Deutsche Welle (DW) nalo limepigwa marufuku nchini Urusi.

    Mamlaka ya Urusi imeizuia mtandao wa DW.

    Urusi ilikuwa tayari imepiga marufuku huduma ya DW ya Urusi kutangaza na kuondoa kibali kutoka kwa wanahabari wake mwezi uliopita, kabla ya uvamizi wa Ukraine.

  8. Urusi yakidhibiti kituo cha nyuklia cha Ukraine

    Urusi imekidhibiti kituo cha nishati cha nyuklia nchini Ukraine baada ya kukishambulia kwa makombora.

    Moto ulizuka katika kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia - kikubwa zaidi barani Ulaya - na Ukraine imesema kuwa kilishambuliwa na wanajeshi wa Urusi.

    Mamlaka imesema kituo hicho sasa kiko salama na viwango vya mionzi ni vya kawaida.

    Viongozi wa dunia wameishutumu Urusi kwa kuhatarisha usalama wa bara zima, na rais wa Ukraine aliishutumu Urusi kwa "ugaidi wa kinyuklia".

    Rais wa Marekani Joe Biden aliitaka Moscow kusitisha shughuli zake za kijeshi katika eneo hilo, huku Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akisema "mashambulizi ya kutisha" kutoka Urusi lazima yasitishwe mara moja.

    Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema shambulio hilo "la kizembe" linaweza "kuhatarisha moja kwa moja usalama wa Ulaya yote".

    Viongozi wote watatu walizungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa njia ya simu.

    Bw Zelensky, wakati huohuo, alisema Urusi inataka kurudiwa kwa Chernobyl, eneo lililo shuhudia maafa mabaya zaidi ya nyuklia duniani mwaka 1986.

    "Ikiwa kuna mlipuko, ni mwisho wa kila kitu. Mwisho wa Ulaya,"

    Wizara ya ulinzi ya Urusi ililaumu shambulio hilo dhidi ya wavamizi wa Ukraine, ikilitaja kuwa "uchochezi mbaya" bila kutoa ushahidi.

    Video kutoka kwa kiwanda cha nyuklia ulionyesha milipuko angani nyakati za usiku na kutoa moshi mwingi.

    Soma zaidi:

    • Mzozo wa Ukraine: Ilikuwa mguu niponye kwa mtangazaji huyu baada mlipuko kutokea nyuma yake
    • Urusi na Ukraine: Je bomu la Cluster lenye milipuko ya kutapakaa ni silaha ya aina gani na Je Urusi inalitumia
  9. Urusi yaweka sheria mpya dhidi ya vyombo vya habari

    Sheria mpya nchini Urusi imewekwa adhabu ya miaka 15 kwa wale watakaotoa taarifa "feki".

    Siku ya Alhamisi, chombo huru kimoja cha habari cha Urusi, TV Rain kilikuwa cha mwisho kusitisha matangazo baada ya kushinikizwa kutangaza uvamizi huo.

    Kituo hicho, ambacho pia kinajulikana kama Dozhd, kilimaliza kurusha matangazo yake ya mwisho kwa kuonesha wafanyakazi wakitoka ofisini.

    Mdhibiti wa mawasiliano wa Urusi aliishutumu kituo hicho kwa "kuchochea itikadi kali, kuwatusi raia wa Urusi, na kusababisha usumbufu mkubwa wa utulivu na usalama wa umma, na kuhimiza maandamano".

    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu kura ya turufu ya Urusi katika azimio la Umoja wa Mataifa, je ina maana gani?
    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia kimya
  10. Rais wa Uganda akutana na balozi wa Urusi

    Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni alikutana na balozi wa Urusi Vladlen Semivolos siku ya Alhamisi kujadili "masuala yenye maslahi kwa pande zote mbili".

    Hakutoa maelezo zaidi, lakini ilikuja siku moja baada ya Uganda kujizuia kupiga kura kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

    Nchi nyingine 16 za Afrika zikiwemo Afrika Kusini, Angola, Algeria na Mali hazikupiga kura.

    Mtoto wa kiume wa Rais Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Jumatatu alieleza kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine katika ujumbe wa Twitter.

  11. BBC: Tutaendeleza juhudi zetu za kupatikana nchini Urusi

    Vyombo vya habari huru vinakabiliwa na shinikizo nchini Urusi wakati huu wa uvamizi.

    BBC imesema sasa kuwa inajaribu kuweka huduma yake ya habari kuendelea kupatikana nchini Urusi, kufuatia ripoti kwamba imefungiwa.

    "Upatikanaji wa habari sahihi na huru ni haki ya msingi ya binadamu ambayo haipaswi kunyimwa watu wa Urusi, ambao mamilioni yao hutegemea BBC News kila wiki," msemaji alisema.

    "Tutaendeleza juhudi zetu za kufanya BBC News ipatikane nchini Urusi, na duniani kote."

    Tovuti ya BBC ya habari za lugha kwa Kirusi imekuwa na idadi ya watazamaji rekodi tangu Urusi ilipovamia Ukraine.

    Waliotembelea tovuti ya bbc.com ya lugha ya Kiingereza kutoka Urusi pia waliongezeka kwa zaidi ya 250% wiki iliyopita.

    Televisheni ya Urusi hadi sasa imeonesha vita kwa njia tofauti kabisa na ulimwengu wote.

  12. Kundi la kwanza la Wanaigeria kutoka Ukraine lawasili nyumbani

    Kundi la kwanza la raia wa Nigeria walioondolewa kwenye mzozo wa Ukraine wamewasili mji mkuu, Abuja majira ya asubuhi.

    Kundi hilo lina wanafunzi 451 kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Nigeria kuhusu masuala ya kigeni, bwana Yusuf Buba, ambaye aliandamana nao kutoka mji mkuu wa Romania, Bucharest.

    Nigeria inatarajiwa kuwahamisha raia 5,000 wanaokimbia vita nchini Ukraine.

    Wengi wamevuka hadi nchi jirani ya Romania, Poland na Hungary.

    Zoezi la kuwarejesha kwao lilikusudiwa kuanza Jumatano lakini lilicheleweshwa kwa sababu ya changamoto za usafirishaji.

    Tume ya Wanigeria waliopo nje imetuma picha za kuwasili kwa wanafunzi hao katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikwe.

    • Mzozo wa Ukraine: Simulizi ya mwanafunzi mjamzito wa Nigeria aliyebaguliwa kwa kuwa mweusi, licha ya kuwa kudanganya kuwa mjamzito
    • Mzozo wa Ukraine: 'Tulitendewa kama wanyama' – Waafrika wanaokimbia Ukraine
  13. Idadi ya vifo vinavyotokana na mashambulizi ya anga ya Urusi yaongezeka

    Watu 47 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Urusi kwenye makazi ya mji wa Chernihiv siku ya Alhamisi, mamlaka ya kikanda imesema.

    Kazi ya uokoaji ilibidi kusitishwa siku ya Alhamisi kwa sababu ya mizinga mikubwa, kulingana na huduma za dharura za eneo hilo.

    Jumla ya watu 148, wengi wao wakiwa raia, wamefariki tangu kuanza kwa mapigano katika eneo hilo, mamlaka imeeleza.

    Jiji la watu 300,000 liko kaskazini mwa nchi, karibu na mipaka ya Urusi na Belarusi.

    • Urusi na Ukraine: Je bomu la Cluster lenye milipuko ya kutapakaa ni silaha ya aina gani na Je Urusi inalitumia
    • Mzozo wa Ukraine: Mkakati wa jeshi la Urusi na kile ilijifunza baada ya kuanguka kwa USSR
    • Urusi na Ukraine: Hawa ndio Majenerali na maafisa wa karibu zaidi na Rais Putin wanaomsaidia katika vita ya Ukraine
  14. Shangwe za wanachama wa Chadema baada ya Mbowe kuachiwa huru

    Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi, katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, hatua ambayo imepelekea Mbowe na wenzake watatu kuachiliwa huru mara moja.

    Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ilikuwa imemshikilia Mbowe na wenzake watatu kwa kesi ya kujibu kuhusiana na tuhuma mbalimbali zikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi.

    Taarifa ya kuondoa mashtaka iliwasilishwa na wakili wa serikali.

    • Freeman Mbowe: Haya ni matukio muhimu kuhusu kesi Freeman Mbowe
    • Tanzania:Mkutano wa Rais Samia na Lissu umepokelewa vipi?
    • Freeman Mbowe: Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema aachiwa huru
  15. Meli ya mizigo yazama kwenye pwani ya Ukraine baada ya mlipuko

    Wamiliki wa meli ya mizigo za Estonia wanasema kuwa imezama katika pwani ya Ukraine baada ya mlipuko.

    Wanasema wafanyakazi wawili walipatikana kwenye viokozi baharini na wengine wanne hawakupatikana - wote sita baadaye walichukuliwa na huduma ya uokoaji ya Ukraine.

    Meli hiyo yenye bendera ya Panama inamilikiwa na kampuni ya Vista Shipping Agency yenye makao yake huko Estonia. Jimbo la Baltic Estonia ni mwanachama wa Nato na ina mpaka na Urusi.

    Meli hiyo ilikuwa imetia nanga katika pwani ya Ukraine baada ya kuondoka katika bandari ya kusini ya Chornomorsk karibu na Odesa siku kadhaa zilizopita.

    Haijabainika ni nini kilisababisha mlipuko huo.

    Jeshi la Ukraine linasema kuwa Urusi inatuma meli za kutua ili kukamata Odesa, jiji la watu milioni moja na bandari kuu, wakati inaendelea kusonga mbele kusini mwa Ukraine.

    • Urusi na Ukraine: Je bomu la Cluster lenye milipuko ya kutapakaa ni silaha ya aina gani na Je Urusi inalitumia
    • Mzozo wa Ukraine: Mkakati wa jeshi la Urusi na kile ilijifunza baada ya kuanguka kwa USSR
  16. Marekani kuweka katika tahadhari timu ya nyuklia

    Marekani itaweka katika tahadhari kikosi cha usaidizi cha nyuklia (NEST). Uamuzi huu ulifanywa na Waziri wa nishatiJ ennifer Granholm baada ya mazungumzo ya dharura na Ukraine.

    NEST kikundi cha wanasayansi, mafundi na wahandisi ambao kazi yao ni kujibu haraka iwezekanavyo aina yoyote ya tisho la nyuklia kokote duniani.

    "Operesheni ya jeshi la Urusi katika eneo la nyuklia ni uzembe kabisa na lazima usitishwe ," alisema, na kuongeza kuwa mitambo ya nyuklia imelindwa na mifumo imara na inafungwa kwa usalama.

    " Hatuoni viwango vya hali ya juu vya mionzi ya nyuklia karibu na eneo ," Granholm alisema.

    • Urusi na Ukraine: Hujui kinachokuja - Joe Biden amwambia Putin
    • Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • Mzozo wa Ukraine: Mambo matano ambayo hukujua kuhusu uvamizi wa Urusi huko Ukraine
  17. Rais wa Ukraine atoa wito wa kufanya mazungumzo na Putin

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema njia ya ya kumaliza vita mara moja nchini Ukraine ni kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Vladimir Putin.

    "Hatutaki kuishambulia Urusi na hatupangi kushambulia. Mnataka nini kutoka kwetu? Tokeni kwenye ardhi yetu, ”alisema rais wa Ukraine.

    Aliongeza kuwa, akielezea umuhimu wa kufanya mazungumzo mwezi uliopia:

    "Njoni tuketi Pamoja. Msiketi umbali wa mita 30, kama alivyofanya wakati rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipokutana na Putin."

    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
  18. Mzozo wa Ukraine: Picha zinazoonyesha uharibifu wa Urusi

    Mashambulio ya makombora ya Urusi yameiharibu miji na vijiji kote nchini Ukraine. Hizi ni picha za baadhi ya maangamizi yaliyofanyika katika makazi ya raia tangu Ulipoanza uvamizi wa Urusi wiki iliyopita.

    Jengo hili chini la gorofa la makazi ya raia lilipigwa na kombora la Urusi katika masaa ya asubuhi Jumamosi iliyopita

    Mji mdogo wa Irpin unapatikana kilomita 20 tu (maili 12) kaskazini mwa Kyiv na umejipata katika vita baina ya vikosi vya Urusi na Ukraine kwa kipindi cha wiki iliyopita.

    Mashambulio ya anga na ardhini yamesababisha uharibifu mkubwa katika eneo hili, huku shambulio moja likiacha eneo la makazi ya watu katika picha hii chini karibu likiangamia kabisa.

    Maafisa wa Ukrainewanasema eneo la makazi la mji wa Kharkiv, ambao ni wa pili kwa ukubwanchini Ukraine na maeneo mengine "vimekuwa vikipigwa usiku mzima" Jumatano na makombora ya anga ya Urusi, ambayo Waendesha mashitaka wa Urmoja wa Mataifa wanayachunguza 9kama uwezekano wa uhalifu wa kivita.

  19. Moto kwenye kiwanda cha nyuklia umezimwa: Huduma za Dharura

    Huduma za dharura za Ukraine zinasema kuwa zimefaulu kuuzima moto kwenye kinu cha umeme kinachotumia nguvu za nyuklia.

    "Saa 06:20 (04:20 GMT) moto katika jengo la mazoezi la Zaporizhzhya NPP huko Energodar ulizimwa.

    Hakuna waathiriwa," Huduma ya Dharura ya Serikali iliandika kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

    • Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • Urusi na Ukraine: Kati ya Urusi na Ukraine nani ana jeshi lililo na nguvu zaidi?
  20. Wazima moto wanajaribu kila njia kuuzima moto katika mtambo wa nishati Ukraine

    Kundi la wazima moto hatimaye wamefanikiwa kuingia katika mtambo wa nishati unaotumia nguvu za kinyuklia katika eneo la Zaporizhzhya ambapo moto mkubwa uliwaka katika jumba la kufanyia mazoezi baada ya jeshi la Urushi kutekeleza mashambulizi katika eneo hilo, kimesema kitengo cha huduma za dharura cha taifa la Ukraine.

    Huduma ya dharura ya Ukraine ilithibitisha katika ukurasa wao wa facebook kwamba wazima moto hao walifanikiwa kufika katika eneo hilo mwendo wa saa kumi na moja saa za Ukraine .

    Moto huo ulianza kuwaka katika saa moja iliopita huku wazima moto wakijaribu kufika katika jumba hilo.

    Awali kitengo hicho cha dharura kiliripoti kwamba wanajeshi wa Urusi walikuwa wanawazuia kuuzima moto huo.

    • Mzozo wa Ukraine: Ilikuwa mguu niponye kwa mtangazaji huyu baada mlipuko kutokea nyuma yake
    • Mzozo wa Ukraine: Mkakati wa jeshi la Urusi na kile ilijifunza baada ya kuanguka kwa USSR