Urusi yaanzisha mashambulizi makali ya kila upande dhidi ya Ukraine
Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Ukraine Sergiy Kyslytsya anasema mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Urusi amethibitisha kwamba rais wake ametangaza "vita dhidi ya nchi yangu", linaripoti shirika la habari la Reuters.
Moja kwa moja
Sauti za uvamizi wa anga katika Kyiv

Chanzo cha picha, AFP
Waandishi wetu waliokokatika mji mkuu wa Ukraine Kyiv wanaripoti milio ya sauti za ndege za uvamizi wa anga katika mwa mji mkuu, huku hofu ya uwezekano wa kuongezeka kwa mashambulio ya anga ikiendelea kuongezeka.
Watu wameshauriwa kutafuta hifadhi na kama ambavyo tumekuwa tukiripoti-wengi wametafuta maficho katika vituo vya treni zinazosafiri chini ya ardhi.
"Niliamshwa na sauti za mabomu. Nikapanga vitu vyangu ndani ya begi na kujaribu kutoroka ," Maria Kashkoska aliliambia shirika la habari la AFP mapema leo , wakati alipokuwa amejificha katika kituo cha treni.
Awali, wakati walipokuwa wakiripoti moja kwa moja , mwandishi wa BBC Lyse Doucet na Clive Myrie walikuwa wamevalia fulana ya kujikinga risasi huku milio ndege za uvamizi ikisikika.

Fahamu kwa nini kiongozi huyu wa Urusi anapendwa na kuchukiwa
Rais Vladimir Putin anatarajiwa kuwa kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi duniani katika historia ya Urusi. Fahamu kwa nini anapendwa na kuchukiwa na wengi.
Maelezo ya video, Valdmir Putin: Fahamu kwa nini kiongozi huyu wa Urusi anapendwa na kuchukiwa Taarifa zaidi kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine:
- Mzozo wa Ukraine: Tunayofahamu mpaka sasa kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
- Urusi na Ukraine: Kati ya Urusi na Ukraine nani ana jeshi lililo na nguvu zaidi?
- Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- Mzozo wa Ukraine:Putin atangaza operesheni ya kijeshi nchini Ukraine
Moshi waonekana ukipaa angani kutoka uwanja wa ndege mashariki mwa Ukraine

Wakati mashambulio ya Urusi nchini Ukraine yakiendelea, waandishi wa habari waliomo ndani ya Ukraine wanatoa ripoti za mashuhuda kutoka maeneo mbali mbali yan chi hiyo.
Video na picha zinaonyesha moshi ukipata juu angani kutoka kwenye uwanja wa ndege karibu na Chuguev katika jimbo la Kharkiv mashariki mwa Ukraine. Picha hizo zimethibitishwa, lakini chanzo chake hakijulikani.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Wakati hayo yakijiri rai awa Ukraine walioko katika mataifa ya Ulaya wamekuwa waelezea hisia zao za kupinga uvamizi wa Urusi dhidi yan chi yao.
Mjini London, rai awa Ukraine wameandamana nje ya ofisi ya Waziri mkuu wa Uingereza Downing Street.
Umati wa watuulitembea kimya huku wimbo wa taifa hilo ukichezwa kabla ya kupiga makofi na kuanza paza sauti kwa Pamoja wakisema "mzuwie Putin. Acha vita."

Chanzo cha picha, PA media

Chanzo cha picha, PA media

Chanzo cha picha, PA media
Soma zaidi kuhusu hali inavyoendelea Ukraine:
- Saa za giza zakumba Ulaya tangu vita ya pili ya dunia
- Rais wa Ukraine kumpatia silaha mtu yeyote anayetaka
Mashirika ya ndege yanaepuka anga ya Ukraine kufuatia shambulio la Urusi

Chanzo cha picha, Flightrader
Maelezo ya picha, Mashirika ya ndege yanavyobadilisha mkondo wa safari zake kuepuka Ukraine Picha hii inaonyesha hatua ya Urusi kuvamia Ukraine ilivyoathiri usafiri wa angani barani Ulaya huku mashirika ya ndege yakiepuka anga ya Ukraine wakati mzozo wake na Urusi ukizidi kufukuta.
Ukraine ilifunga anga yake kwa safari za ndege za kiraia saa za mapema baada ya Urusi kuanza mashambulizi yake.
Waziri wa Uchukuzi wa Uingereza Grant Shapps ameagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga kuhakikisha mashirika ya ndege yanaepuka anga ya Ukraine "kufuatia matukio ya kutisha usiku mmoja".
Soma zaidi kuhusu hali inavyoendelea Ukraine
TCRA kusaidia Watanzania kufuatilia matumizi ya data ya simu,

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Baadhi ya watanzania wamekuwa wakilalamikia matumizi ya data Mamlaka ya kudhibiti mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) inaunda programu tumishi itakayowasaidia watumiaji wa mtandao wa intaneti kupitia simu zao kufuatilia utumiaji wa data zao.
Hatua hiyo inafuatia malalamishi kutoka kwa Watanzania ambao wamekuwa wakilalamika kuwa vifurushi vya data zao zinaisha ndani ya muda mfupi.
App hiyo inayoundwa na Mamlaka ya kudhibiti mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) itakuwa tayari kufikia mwisho wa mwezi Machi, alisema Emmanuel Manase, Mkurugenzi wa TCRA wa masuala ya viwanda.
Pia aliagiza waendeshaji wote wa simu kuunda zana zao za programu ili kuwasaidia wateja kufuatilia matumizi ya data - kama njia ya kupunguza malalamiko ya umma.
Pia unaweza kusoma:
Habari za hivi punde, Saa za giza zakumba Ulaya tangu vita ya pili ya dunia

Chanzo cha picha, getty images
Maelezo ya picha, Mwanamke akiomba mjini Kiev Ukraine Kiini cha lawama kinazidi kuongezeka huku ulimwengu ukiamka kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
"Hizi ni miongoni mwa saa za giza kuu kwa Ulaya tangu vita ya pili vya dunia" - hayo yalikuwa maneno ya mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell.
Anasema nguvu kubwa ya nyuklia inayoshambulia nchi jirani na kutishia kulipiza kisasi taifa lolote litakaloweza kuinusuru ni "ukiukaji mkubwa zaidi wa sheria za kimataifa" na "ukiukaji wa kanuni za msingi za kuishi pamoja kwa binadamu".
‘EU itaweka vikwazo vikali zaidi kuwahi kuwekwa’, anasema.
Rais wa Ukraine kumpatia silaha mtu yeyote anayetaka

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa atampatia silaha mtu yeyote anayetaka, kulingana na shirika la habari la kitaifa.
Picha kadhaa ziliwahi kuibuka mitandaoni zikionesha raia wa Ukraine wakipewa mafunzo ya msingi ya kijeshikatika wiki za hivi karibuni hali ya taharuki ilipopanda katika mzozo wake na Urusi.
Wakati huo huo, Ukraine imekatiza rasmi uhusiano wake wa kidiplomasia na Urusi baada ya nchi hiyo kuvamia ardhi yake.
Rais Volodymyr Zelensky amesema hayo katika taarifa kwa vyombo vya habari.
Soma zaidi:
'Nimehesabu roketi saba' - Mwanahabari wa Ukraine

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ndege ya kivita Mwanahabari wa Ukraine Lyubov Velychko anaishi karibu na kambi ya jeshi iliyopo karibu na mji mkuu Kyiv.
Anasema aliamka saa kumi unusu alfajiri na “kusikia milio mikubwa alipotoka nje kuangalia aliona “kitu kilichoonekana kama moto”.
Velychko anasema majirani zake walishutuka na baadhi yao walianza kulia, akiongeza “ilipofika saa kumi na moja asubuhi tulikua tunawaficha watoto wetu katika vyumba vya chini ya ardhi”.
Baadaye alienda katika kambi ya jeshi ambako anasema alikuta “imelipuliwa kwa makombora ya angani” na watu wawili walikuwa wamefariki.
“Nilihesabu maroketi saba,” anasema.
Kwa sasa anaondoka mjini humo na familia yake na anasema “anahisi hayupo salama” kwa sababu amesikia vifaru vya Urusi viko karibu na mpaka wa Belarus, ambao uko kilomita 80 kutoka nyumbani kwake.
Soma zaidi
Tunachojua hadi sasa kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

Chanzo cha picha, reu
Maelezo ya picha, Raia wakijaribu kutoroka mji wa Kyiv Ikiwa ndio unajiunga nasi wakati huu. Bado tunaendelea kuangazia taarifa za uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Na hivi ndivyo mambo yalivyo kufikia sasa:
Katika hotuba ya televisheni saa 05:55 saa za Moscow (02:55 GMT), Vladimir Putin wa Urusi alitangaza "operesheni ya kijeshi" katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine. Putin alisema Urusi ilikuwa ikijilinda.
Aliwataka wanajeshi wa Ukraine kuweka chini silaha zao.
Uingiliaji wowote wa mataifa ya nje dhidi ya Urusi kutapata jibu la "papo hapo", alisema
Urusi imeshambulia miundombinu ya Ukraine kwa makombora, Ukraine inasema. Pia inasema imedungua ndege za Urusi - jambo ambalo Moscow inakanusha.
Misafara ya wanajeshi na vifaru imeingia Ukraine kutoka pande zote. Msafara mmoja umevuka kutoka Belarus kuelekea kaskazini mwa mji mkuu wa Kyiv. Mwingine umeingia kutoka Crimea kusini, ambayo Urusi ilitwaa kutoka Ukraine mnamo 2014
Takriban watu wanane wanaripotiwa kuuawa...soma taarifa hii kwa kina zaidi kwenye mtandao wetu bbcswahili.com
Taarifa zaidi kuhusu uvamizi wa Urusi ndani ya Ukraine:
- Urusi na Ukraine: Kati ya Urusi na Ukraine nani ana jeshi lililo na nguvu zaidi?
- Mzozo wa Ukraine:Putin atangaza operesheni ya kijeshi nchini Ukraine
- "Vita dhidi ya nchi yangu"
Uuzaji wa maziwa ya fomula kwa watoto 'usio wa kimaadili' unaodhuru Waafrika - utafiti

Chanzo cha picha, Getty Images
Takriban nusu ya akina mama wachanga nchini Nigeria, wawili kati ya akina mama watano kutoka Morocco na zaidi ya theluthi moja ya akina mama wa Afrika Kusini wameshauriwa na mtaalamu wa afya kuwalisha watoto wao bidhaa ya maziwa, utafiti wa pamoja wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) limegundua.
"Ripoti hii inaonyesha kwa uwazi kwamba uuzaji wa maziwa ya fomula bado unaenea kwa njia isiyokubalika, ya kupotosha na ya fujo," alisema Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO.
Wataalamu wa afya nchini Nigeria na Morocco wameripoti kuwa mawasiliano na makampuni ya kutengeneza maziwa ya watoto yalikuwa ya kawaida sana katika mazingira ya huduma za afya ya umma na ya kibinafsi.
Ripoti hiyo ilichunguza wazazi na wanawake wajawazito 8,500, na wahudumu wa afya 300 katika miji kote ulimwenguni ikiwa ni pamoja na Bangladesh, Uchina, Mexico, Morocco, Nigeria, Afrika Kusini, Uingereza na Vietnam.
"Tunahitaji sera madhubuti, sheria na uwekezaji katika unyonyeshaji ili kuhakikisha kuwa wanawake wanalindwa dhidi ya mazoea yasiyo ya kimaadili ya uuzaji -- na kupata taarifa na usaidizi wanaohitaji kulea familia zao." Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Unicef Catherine Russell.
Maziwa ya mama ni chakula bora kwa watoto wachanga. Ni salama, ni safi na ina kingamwili ambazo husaidia kulinda dhidi ya magonjwa mengi ya kawaida ya utotoni.
Soma zaidi:
Habari za hivi punde, Mzozo wa Ukraine: Watu saba wafariki baada ya shambulio la bomu la Urusi

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Polisi wa Ukraine wakikagua mabaki ya kombora lililoanguka mtaani mjini Kyiv Watu saba wanaaminiwa kufariki katika shambulio la bomu llililofanywa na vikosi vya Urusi, Polisi wa Ukraine wanasema.
Maafisa wanasema shambulio dhidi ya kambi ya jeshi ya Podilsk, nje ya mji wa Odessa liliwaua watu sita na kuwajeruhi wengine saba. watu 19 hawajulikani waliko huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki katika Mariupol, waliongeza kusema.
Huku hayo yakijiri Wizara ya Ulinzi ya Urusi imenukuliwa na shirika la habari la Urusi -Interfax ikisema kuwa "Ulinzi wa anga wa vikosi vya jeshi la Ukraine umekandamizwa".
Wizara inaongeza kuwa "vikosi vya mpaka vya Ukraine havikupinga vitengo vya Urusi".
Hakujawa na uthibitisho huru wa madai haya.
‘ Dunia haimpi Mwanamke au Msichana fursa ya kuwa anachotaka kuwa’- Jesca Mshama
Maelezo ya video, Jesca Mshama:Dunia haimpi mwanamke au msichana fursa ya kuwa anachotaka kuwa Katika mfululizo wa makala kuhusu vijana walio chini ya miaka 30 leo tunae Jesca Mshama, msanii wa muziki nchini Tanzania, balozi kijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mjasiriamali na msimamizi wa shule ya msingi ya kidigitali jijini Dar es salaam akiwa na umri wa miaka 26.
Lengo lake ni kusimamia makuzi na malezi bora ya watoto pamoja na ustawi wa vijana na wanawake katika jamii.
Mwandishi wa BBC @frankmavura amefanya mazungumzo na @jessicamshama
Kwa picha: Hali ilivyo mjini Kyiv
Zaidi ya saa mbili zilizopita, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza hatua ya kijeshi.
Watu wengi katika mji mkuu wa Kyiv nchini Ukraine wamekimbilia kwenye vituo vya treni vya chini ya ardhi kupata makazi. Wengine wamepanda mabasi kuondoka jijini, na kuna misururu ya magari yanayojaribu kutoka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Umati wa watu katika kituo cha treni unaonekana mjini Kyiv huku ving'ora vya mashambulizi ya anga vikilia katika jiji lote. Watu wengi wamebeba mifuko na masanduku 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Baba akimtuliza mwanawe wakati familia yake inakimbilia kwenye kituo cha treni 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wasichana kwenye simu zao, wakijificha ndani ya kituo cha chini ya ardhi 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Watu walionekana wakiwa na hofu wanaonekana mitaani 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Baadhi ya wakazi wanaonekana wakikumbatiana mitaani wakiwa njiani kuelekea katika vituo vya treni Mzozo wa Ukraine: Wakazi wakimbia mji mkuu wa Kyiv

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Magari yanapanga foleni kuondoka Kyiv asubuhi na mapema ya Alhamisi Vladimir Putin alitangaza oparesheni ya kijeshi nchini Ukraine saa 5.55 asubuhi majira ya Moscow - na dakikaka chache baadaye makombora ya kwanza yalirushwa Ukraine, kulingana na ripoti.
Katika mji mkuu wa Kyiv, king'ora cha dharura kililia, na picha zinaonyesha msururu wa magari yakifunga barabara ya mwendokasi huku watu wakiukimbia mji huo.
Watu katika mitandao ya kijamii wanangazia kuongezeka kwa hali ya hofu, huku baadhi yao wakisema wanakimbizwa kwenye makazi ya mabomu na kwenye vyumba vya chini ya ardhi. Kanda za televisheni zimeonyesha watu wakisali barabarani, wakiwa wamekusanyika kwa vikundi.
Mwandishi wa habari wa Guardian Luke Harding huko Kyiv anasema kwenye kwenye Twitter kwamba kuna watu wachache mitaani, na watu wanapanga foleni kwenye mashine za kutoa pesa.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Jeshi la anga Ukraine lazuia shambulio la anga la Urusi
Wanajeshi wa Ukraine wamechapisha taarifa wakisema kwamba jeshi la Urusi lilianza "kushambulia kwa makombora" vitengo vyake mashariki mwa nchi.
Urusi pia ilirusha makombora katika uwanja wa ndege wa Boryspil karibu na Kyiv na viwanja vingine kadhaa vya ndege, ilisema taarifa hiyo.
Ilisema jeshi la anga la Ukraine linapambana na mashambulizi ya anga ya Urusi.
Taarifa hiyo hata hivyo imenusha ripoti kuhusu uwepo wa wanajeshi wa Urusi wa kuruka kwa miavuli katika mji wa bandari wa Odesa kusini mwa nchi hiyo.
Tunisia yazuia filamu iliyoigizwa na Gal Gadot juu ya mzozo wa Israel

Chanzo cha picha, AFP
Tunisia imeiondoa katika kumbi za sinema filamu mpya iliyoigizwa na mwigizaji wa Israel Gal Gadot.
Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia maandamano ya wanaharakati wanaosema Gadot alihudumu katika jeshi la Israel na anaunga mkono uvamizi wa Israel katika maeneo ya Wapalestina, Wizara ya Utamaduni ilisema.
Filamu hiyo, ambayo ni muundo mpya kitabu cha Death on the Nile cha mwandishi wa Uingereza Agatha Christie, tayari imepigwa marufuku nchini Kuwait na Lebanon.
Tunisia, ambayo huandaa tamasha kubwa za kusherehekea filamu za Kiarabu na kimataifa, pia ilipiga marufuku filamu ya 2017 ya Wonder Woman, ambayo ilimshirikisha Gal Gadot kama mhusika mkuu.
Habari za hivi punde, Ukraine: Wanajeshi wanaingia kutoka Belarus
Ripoti nyingi sasa zinawanukuu maafisa wa Ukraine wakisema wanajeshi nchini Belarus wanajiunga na shambulio la Urusi, kumaanisha kuwa mashambulizi hayo sasa yanatoka kaskazini mwa Ukraine.
Belarus, ambayo iko kwenye mpaka wa kaskazini wa Ukraine, kwa muda mrefu imekuwa ikishirikiana na Urusi. Wachambuzi wanaelezea nchi hiyo ndogo kama "taifa mteja" kwa Urusi.
Shambulio hilo kutoka kaskazini linaongeza mashambulizi ya Urusi mashariki mwa Ukraine, na harakati za wanajeshi wa Urusi kwenye Odessa kusini.
Biden anasema Marekani na washirika wataweka vikwazo vikali
Rais wa Marekani Joe Biden anasema amezungumza na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na kumweleza kuhusu hatua anazochukua "kuleta shutuma za kimataifa".
Katika taarifa yake, Biden anasema alilaani shambulizi hilo kama "lisilochochewa na lisilo na msingi".
Zelensky "aliniomba nitoe wito kwa viongozi wa dunia kusema waziwazi dhidi ya uchokozi wa wazi wa Rais Putin, na kusimama na watu wa Ukraine", Biden anaongeza.
Rais wa Marekani anasema atakutana na viongozi wa G7 siku ya Alhamisi, na Marekani na washirika "watakuwa wakiiwekea Urusi vikwazo vikali".
"Tutaendelea kutoa msaada na usaidizi kwa Ukraine na watu wa Ukraine," anasema.
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Ukraine:Putin atangaza operesheni ya kijeshi nchini Ukraine
- Ukraine yawaambia raia wake waondoke Urusi
- Ujerumani yasimamisha bomba huku mataifa yakiiwekea vikwazo Urusi
- Hatua 5 zinazoweza kuzuia vita Ukraine
‘Makombora yanarushwa,wanajeshi wa Urusi wanatokea kila upande Ukraine’

Chanzo cha picha, Getty Images
Wizara ya ulinzi ya Urusi imekanusha kushambulia miji ya Ukraine - ikisema kuwa inalenga miundombinu ya kijeshi, ulinzi wa anga na vikosi vya anga kwa "silaha za usahihi wa hali ya juu", shirika la habari la serikali ya nchi hiyo RIA liliinukuu wizara hiyo kusema.
Urusi ilianzisha mashambulizi ya makombora
Rais wa Ukraine Zelensky amethibitisha ripoti za mashambulizi ya makombora nchini humo, kwa mujibu wa ripoti ya Reuters.
Anasema Urusi imefanya mashambulizi ya makombora kwenye miundombinu ya Ukraine na walinzi wa mpakani.
Mwandishi wa BBC Kyiv James Waterhouse anasema afisa wa serikali ya Ukraine ametoa dalili ya upana wa hatua za kijeshi za Urusi kufikia sasa.
Afisa huyo anasema kumekuwa na mashambulizi ya makombora yaliyozinduliwa leo asubuhi huko Kyiv, pamoja na harakati za askari huko Odessa kusini mwa nchi hiyo.
Wanajeshi pia wamekuwa wakivuka mpaka wa Kharkiv, takriban maili 25 kutoka mpaka wa Urusi, afisa huyo anasema.
Dalili za mapema kulingana na mashahidi na maafisa wa serikali ni kwamba hili ni jambo kubwa kabisa, Waterhouse inasema.
Pia kuna ripoti nyingi kutoka kwa vyombo vya habari vya ndani vinavyonukuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine ambayo inasema baadhi ya mashambulizi ya makombora yameshambulia vituo vya makombora ya kijeshi ya Ukraine na makao makuu ya kijeshi huko Kyiv.
Wizara ya ulinzi ya Urusi imekanusha kushambulia miji ya Ukraine - ikisema inalenga miundombinu ya kijeshi, ulinzi wa anga na vikosi vya anga kwa "silaha za usahihi wa hali ya juu".
Bei ya mafuta yapanda hadi zaidi ya $100 kwa pipa huku mvutano ukiongezeka

Chanzo cha picha, Getty Images
Bei ya mafuta imepanda hadi zaidi ya $100 kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka saba huku Rais Putin akitangaza "operesheni ya kijeshi" mashariki mwa Ukraine.
Habari hizo pia zilisababisha masoko ya hisa ya Asia kufanya biashara ya chini kwa asimilia 2 hadi 3. Masoko yamekuwa yakidorora katika siku chache zilizopita huku hali ya wasiwasi ikiongezeka - bei iligonga $98 siku chache zilizopita wakati Bw Putin alipovunja makubaliano ya amani na kuamuru wanajeshi katika majimbo mawili ya mashariki yanayodhibitiwa na waasi.
Mwandishi wa BBC Mariko Oi anasema wawekezaji wamekuwa wakikimbilia kile wanachokiona kama mali salama. Bei za dhahabu ziko katika kiwango cha juu zaidi kwa zaidi ya mwaka mmoja huku dola ya Marekani na Yen ya Japan pia zikiimarika.
Rais wa Ukraine atoa wito kwa sheria ya kijeshi
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatoa wito kwa baraza lake la usalama na ulinzi kutangaza sheria ya kijeshi.
Baraza hilo linatarajiwa kufanya mkutano wa dharura kuamua suala hilo.
Biden,Trump,Nato watoa maoni kuhusu uvamizi wa Ukraine

Chanzo cha picha, EPA
Mashambulizi ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa, anasema Katibu Mkuu wa Nato
Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg amelaani "shambulio la kizembe" la Urusi dhidi ya Ukraine.
Katika chapisho kwenye Twitter, anasema "inaweka maisha ya raia wengi hatarini". "Huu ni uvunjaji mkubwa wa sheria za kimataifa na tishio kubwa kwa usalama wa Euro-Atlantic," anaongeza.
Anasema washirika wa Nato watakutana kushughulikia "uchokozi mpya" wa Urusi.
Trump: Putin aliona 'udhaifu' wa Marekani
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alienda hewani kwenye runinga ya Fox News huku mashambulizi ya Urusi yakianza Jumatano usiku saa za Marekani kwa hoja kwamba "haingefanyika" wakati wa utawala wake.
Trump alipiga simu na kusema hakuamini kwamba Putin "alitaka kufanya hivi mwanzoni".
"Nadhani alitaka kufanya jambo na kujadiliana, na hali ikawa mbaya zaidi, na ndipo akaona udhaifu," Trump alisema.
Zaidi ya hayo, Trump alisema kwamba anaamini uvamizi wa Urusi ulichochewa kwa sehemu na "udhaifu" wa kujiondoa kwa Amerika kutoka Afghanistan.
Biden: Ulimwengu utaiwajibisha Urusi
Rais wa Marekani Joe Biden amejibu kile anachokiita "shambulio lisilo na msingi la vikosi vya jeshi la Urusi".
Anasema "sala za dunia nzima ziko pamoja na watu wa Ukraine".
"Rais Putin amechagua vita vya kutayarishwa ambavyo vitaleta maafa makubwa ya kupoteza maisha na mateso ya wanadamu," anasema.
"Urusi pekee ndiyo inayohusika na vifo na uharibifu utakaoletwa na shambulio hili, na Marekani na washirika wake watajibu kwa umoja na njia madhubuti. Ulimwengu utaiwajibisha Urusi."
Biden anasema atahutubia Wamarekani siku ya Alhamisi kuhusu matokeo ambayo Urusi itakumbana nayo.
Anasema atafuatilia hali hiyo kutoka Ikulu ya Marekani na atakutana na viongozi wa G7 asubuhi kabla ya kutangaza "matokeo zaidi" kwa Urusi.
Uingereza na washirika watajibu ‘vikali’, asema Boris Johnson
Waziri Mkuu wa uingereza Boris Johnson anasema "amechukizwa na matukio ya kutisha nchini Ukraine" na kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin "amechagua njia ya umwagaji damu na uharibifu kwa kuanzisha shambulio hili lisilochochewa".
Anaongeza kuwa amezungumza na rais wa Ukraine kujadili jinsi ya kujibu na kuahidi hatua madhubuti za Uingereza na washirika.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe


