Serikali ya Tanzania yabadili kanuni za miundombinu ya utangazaji kidigitali

Maelezo ya sauti, Serikali ya Tanzania imebadili kanuni za miundombinu ya utangazaji kidigitali

Serikali ya Tanzania imebadili kanuni za miundombinu ya utangazaji kidigitali ambapo sasa chaneli zote za ndani ya nchi zitapatikana kwenye visimbusi vyote.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema tangu kuondolewa kwa chaneli hizo kwenye visimbusi vya kulipia kumekuwa na kilio kikubwa kwa wananchi, na hata wadau wengine.

Kuhusu hayo na mengine kuhusu kanuni mbalimbali amezungumza na Scolar Kisanga.