Kiswahili kuadhimishwa duniani kila tarehe 7 mwezi Julai-UNESCO
Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO limeitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.
Moja kwa moja
Lizzy Masinga
Ubalozi wa Marekani nchini Ethiopia watoa tahadhari ya ugaidi

Chanzo cha picha, Getty Images
Ubalozi wa Marekani nchini Ethiopia umetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi katika mji mkuu Addis Ababa na maeneo mengine ya nchi.
Ubalozi huo maeneo ambayo yanakabiliwa na uwezekano wa kushambuliwa kuwa "majengo ya kidiplomasia, maeneo ya watalii, vituo vya usafiri, masoko/maduka makubwa, biashara za kimataifa migahawa, hoteli, vituo vya serikali za mitaa na maeneo mengine ya umma".
uliwataka Wamarekani kuwa waangalifu na kuepuka maeneo yenye watu wengi na maeneo yanayotembelewa na wageni.
Tahadhari hiyo ya ugaidi huenda ikaikasirisha mamlaka ya Ethiopia, ambayo hivi majuzi iliwahakikishia wanadiplomasia wa kigeni kwamba Addis Ababa iko "salama".
Serikali ya Ethiopia ilitangaza hali ya hatari mapema mwezi huu huku waasi kutoka eneo la kaskazini la Tigray wakichukua udhibiti wa maeneo zaidi huku wapiganaji wake wakielekea kusini, karibu na mji mkuu.
Soma zaidi:
- Mzozo wa Tigray, Ethiopia: Kwa nini ulimwengu mzima una wasiwasi na mzozo huu?
- Mgogoro wa Ethiopia wa Tigray: Jinsi TPLF ilivyolizidi maarifa jeshi la Ethiopia
- Mzozo wa Tigray Ethiopia: Ripoti yasema uhalifu wa kivita huenda ulifanyika
Mabegi yaliyotelekezwa Kampala yatolewa baada ya kuibua hofu ya mabomu

Chanzo cha picha, AFP
Polisi nchini Uganda wameondoa mabegi yametelekezwa mtaani katika mji mkuu wa Kampala baada ya kusababisha hofu ya mabomu mjini humo. Tovuti ya habari ya eneo hilo imechapisha picha za operesheni ya polisi.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Wakazi wamekuwa katika hali ya tahadhari tangu mashambulio ya wiki iliyopita ya kujitoa muhanga yaliyoua watu wanne.
Grammy 2022: Wizkid, Rocky Dawumi, Femi Kuti, Angelique Kidjo wawania tuzo ya albamu bora

Chanzo cha picha, OTHERS
Onesho la Tuzo za Grammy za 2022, zinazojulikana rasmi kama Tuzo za 64 za Grammy, zimekaribia.
Tuzo hizo zimefanya uteuzi katika vipengele 86. Tuzo za 64 za Grammy zinatambua rekodi zilizotolewa kati ya Septemba 1, 2020 - Septemba 30, 2021.
Miongoni mwa wanaowania ni mwanamuziki wa Nigeria, Wizkid na Femi Kuti katika kipengele cha albamu bora ya dunia miongoni mwa wanamuziki wengine kama Rocky Dawuni, Angelique Kidjo, and Daniel Ho & Friends.
Washindi wa Albamu bora ya mwaka ya dunia katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ni;
2020: Burna Boy win wit im 'Twice As Tall''
2019: Angelique Kidjo 'Celia'
2018: Soweto Gospel Choir 'Freedom'
2017: Ladysmith Black Mambazo 'Shaka Zulu Revisited: 30th Anniversary Celebration'
2016: Yo-Yo Ma & The Silk Road Ensemble 'Sing Me Home'
2015: Angelique Kidjo 'Sings'
2014: Angelique Kidjo 'Eve'
2013: Mwaka huu kulikuwa na washindi wawili Gipsy Kings Savor Flamenco plus Ladysmith Black Mambazo 'Singing For Peace Around The World.'
2012; Ravi Shankar 'The Living Room Sessions Part 1'
2011: Tinariwen 'Tassili'
Manchester United yawasiliana na kocha wa zamani wa Barcelona

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ernesto Valverde Manchester United wamewasiliana na meneja wa zamani wa Barcelona Ernesto Valverde kuhusu kuchukua jukumu la kuwa kocha wa muda mfupi.
Valverde, 57, ni miongoni mwa makocha wachache wanaopatiwa fursa ya kuifunza timu hiyo kwa muda hadi pale itakapopata mkufunzi wa muda mrefu.
United inamtafuta mkufunzi wa muda mrefu atakayechukua kazi ilioachwa na Ole Gunnar Solskjaer.
Wanahisi sio rahisi kumuajiri mkufunzi wa PSG Mauricio Pochettino mara moja kama ilivyotarajiwa .
Meneja huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham alisema siku ya Jumanne kwamba anafurahi kuwa PSG na kwamba hatovurugwa akili na kuhusishwa kwake na kazi hiyo ya United.
Valverde ni kiolezo cha kocha mwenye uzoefu ambaye hatarajii kupata kazi hiyo kwa kandarasi ya kudumu bali kama meneja wa muda.
Jukumu la mwisho la kocha huyo wa Uhispania lilikuwa ni Barcelona, ambayo aliiongoza kutwaa mataji mfululizo ya La Liga na Copa del Rey 2018 kabla ya kutimuliwa Januari 2020.
Karim Benzema: Mchezaji mpira wa Ufaransa apatikana na hatia ya ulaghai kupitia kanda ya ngono

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa timu ya taifa ya Ufaransa na Real Madrid, Karim Benzema amepatikana na hatia ya kula njama ya kumtusi mwanasoka mwenzake wa Ufaransa kutumia kanda ya ngono.
Jaji alimpa Benzema kifungo cha mwaka mmoja jela na kuamuru alipe faini ya €75,000 (£63,000; $84,000).
Benzema alikuwa mmoja wa watu watano walioshtakiwa mwezi uliopita kwa jaribio la kumpunja fedha Mfaransa Mathieu Valbuena kutumia kanda hiyo.
Kashfa hiyo imeshangaza jamii ya soka nchini Ufaransa na wachezaji wote wawili kupoteza nafasi katika timu yao ya taifa.
Kesi hiyo ilianza Juni 2015, wakati wanasoka hao wawili walikuwa kwenye kambi ya mazoezi ya Ufaransa.
Katika kambi hiyo, Benzema aliweka shinikizo kwa Valbuena kuwalipa watu waliodai kuwa na kanda hiyo, ambao alikuwa amefanya nao njama ya kuwa mpatanishi, waendesha mashtaka walisema.
Benzema amekuwa akikanusha madai hayo na kusisitiza kuwa alikuwa akijaribu tu kumsaidia Valbuena kujiondoa kutoka kashfa ya video hiyo iliyomtia hatarini
Watoto wanatumika katika vita Afrika Magharibi-UN
Umoja wa Mataifa unasema watoto wengi wanaingizwa katika vita huko Afrika Magharibi na Kati kuliko mahali pengine popote duniani.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, Unicef, liligundua zaidi ya watoto 20,000 wamejiunga na makundi yenye silaha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Iinasema watoto wanatumika kama wapiganaji pamoja na wajumbe, wapelelezi, wapishi, wasafishaji, walinzi na wapagazi kutoka Mali hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Afrika Magharibi na Kati pia ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya watoto waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia ulimwenguni na idadi kubwa ya pili ya utekaji nyara.
Ukanda hiyo una mizozo kadhaa ya kivita inayoendelea ikiwa ni pamoja na waasi wa Kiislamu na vita vya kujitenga.
Unicef inatoa wito wa kuongezwa uungwaji mkono kwa juhudi za kuzuia na kukabiliana na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto.
Sudan yachunguza ukiukaji wa haki dhidi ya waandamanaji

Chanzo cha picha, AFP
Sudan imeanzisha uchunguzi kuhusu ukiukaji wa haki dhidi ya waandamanaji tangu mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 25, Waziri Mkuu aliyerejeshwa madarakani Abdalla Hamdok amesema.
Bw Hamdok alisema hayo Jumanne baada ya kukutana na wanachama wa Forces of Freedom and Change (FFC), muungano wa zamani wa kiraia unaotawala ambao umekuwa ukipinga utawala wa kijeshi.
Shirika la Habari la Sudan (Suna) linalomilikiwa na serikali liliripoti kwamba muungano huo sasa unaunga mkono mpango wa Bw Hamdok na wanajeshi baada ya mazungumzo ya mjini Khartoum.
Muungano huo hapo awali ulikuwa umesema hautambui makubaliano yoyote ya kisiasa na uongozi wa kijeshi kufuatia kurejeshwa kwa Bw Hamdok.
Siku ya Jumanne, Waziri Mkuu na kundi hilo walitaka wafungwa wa kisiasa waachiliwe na jeshi liheshimu haki za kufanya maandamano ya amani.
Udhibiti wa jeshi mwezi uliopita ulisababisha maandamano, na zaidi ya watu 40 wameripotiwa kuuawa wakati wa maandamano.
Kiswahili kuadhimishwa duniani kila tarehe 7 mwezi Julai-UNESCO

Chanzo cha picha, UNESCO
Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO limeitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.
Taarifa hiyo imetangazwa makao makuu ya UNESCO mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO azimio maalum la kuitangaza siku hiyo limepitishwa na wanachama wote bila kupungwa, tovuti ya taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza
Hatua hiyo inakifanya Kiswahili kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kuwa na siku maalum ya kuadhimishwa.Kiswahili hadi sasa tayari kinatambulika kama miongoni mwa lugha rasmi Umoja wa Afrika, na kinatumika kama lugha rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na bunge la Afrika na ni moja ya lugha za Afrika zinazozungumzwa na watu wengi duniani.
Malikah Shabbaz: Mwana wa kike wa Malcom X afariki

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Malikah alikuwa hajazaliwa wakati babake alipouawa Malikah Shabazz, mwana wa mwanaharakati wa haki za kibinadamu aliyeuawa Malcom Xalipatikana amefariki siku ya Jumatatu nyumbani kwake Brooklyn, mjini New York, kwa mujibu wa polisi.
Shabbaz mwenye urmi wa miaka 56 , alikuwa kitinda mimba wa wasichana sita wa mwanaharakati huyo maarufuambaye miaka 1960 alipigania kuwezeshwa kwa Wamarekani weusi.
Shabbaz alipatikana akiwa amepoteza fahamumwendo wa 4.40 jioni Alitangazwa kufariki muda mfupi baadaye.
Habari hizo zinajiri siku chache tu baada ya wanaume wawili waliopatikana na hatia ya kumuua Malcolm X, Muhammad Aziz na Khalili Islam kuondolewa makosayamuaji yake na mahakama ya mjini New York.
Mapema mwaka huu , Watoto wa kike wa shujaa huyo waliomba kwamba uchunguzi ufunguliwe upya , wakidai kwamba kuna Ushahidi mpya.
Malawi yamuomba Tyson kuwa balozi wake wa bangi

Chanzo cha picha, Getty Images
Wizara ya kilimo ya Malawi imemwandikia barua bingwa wa zamani wa ndondi duniani Mike Tyson ikimuomba kuwa balozi wa bangi nchini humo.
Waziri Lobin Lowe alisema kuhalalishwa kwa bangi mnamo 2020 kumeunda fursa kimataifa.
Wizara hiyo ilisema Jumuiya ya Bangi ya Marekani ilikuwa kuwezesha mpango huo na Tyson.
"Malawi inaweza isijiendeshe peke yake kwani tasnia hii ni ngumu inayohitaji ushirikiano. Kwa hivyo ningependa kukuteua, Bw Mike Tyson, kuwa balozi wa Tawi la Bangi la Malawi," Bw Lowe aliandika.

Chanzo cha picha, Malawi's Agriculture Ministry
Tyson pia ni mjasiriamali na amewekeza katika kilimo cha bangi.
Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba Tyson alitarajiwa nchini Malawi wiki iliyopita lakini ziara yake iliahirishwa.
Matokeo ya mechi za Klabu bingwa Ulaya

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Man United yailaza Vilareal ugenini Meneja wa mpito wa Manchester United Michael Carrick alitoa ushindi dhdi ya Villarreal kwa meneja wa zamani Ole Gunnar Solskjaer huku United wakichukua nafasi yao katika Chambioni Ligi mwisho 16.
Magoli kutoka kwa Cristiano Ronaldo ana Jadon Sancho yalimpa ushindi Carrick katika mechi yake yaka kwanza katika usimamizi wam uda siku mbili naada ya kufutwa kazi kwa Solskjaer.
Mautmaini ya Barcelona ya kufikia katika ngazi ya mchujo katika Championi Ligi hayajulikani baada ya kutoka sare katika Nou Camp by Benfica.
Robert Lewandowski alishinda mechi tisa za mafanikio za Championi Ligi huku Bayern Munich wakiendela kushikilia rekodi ya ushindi wa 100% kwa ushini wa 2-1 katika kundi E dhidi ya Dynamo Kyiv.
Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel alisema kuwa klabu ilipata " mafanikio mazuri" huku klabu hiyo ikisonga hadi katika kuwa miongoni mwa timu 16 za mwisho za Championi Ligi kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Juventus katika Stamford Bridge.
Mwanariadha Haile Gebrsellasie kujiunga katika vita Ethiopia

Chanzo cha picha, afp
Maelezo ya picha, Mwanariadha wa zamani nchini Ethiopia Gebrsellasie Bingwa wa mbio za Olimpiki na mwanariadha wa zamani nchini Ethiopia Haile Gebrselassie ametangaza mipango ya kujiunga na jeshi la taifa lake siku moja tu baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kutangaza kwamba anajiunga katika vita dhidi ya waasi kutoka jimbo la kaskazini la Tigray.
Pia miongoni mwa watakaojiunga katika vita hivyo ni mwanaraidha wa mbio ndefu Feyisa Lelisa ambaye alikuwa maarufu kwa pingamizi yake katika michezo ya olimpiki ya Rio alipoinua mikono juu ya kichwa chake – ishara iliotumika wakati huo na raia wa Ethiopia kupinga hatua ya serikali dhidi ya raia wa kabila la Oromo.
Baadhi ya watu maarufu nchini Ethiopia wametoa tangazo kama hilo huku vita vikiendelea huku waasi wakitangaza kufanikiwa kuteka baadhi ya maeneo na sasa wanakaribia mjii mkuu wa Addis Ababa.
Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na picha ya waziri mkuu Abiy Ahmed aliyeonekana akielekea katika vita hivyo akiwa amevalia magwanda ya kijeshi katika gari lililozungukwa na vikosi maalum.
Hatahivyo sio wazi kwamba Abiy amejiunga katika vita hivyo kwasababu BBC haikuweza kuthibitisha picha hizo.
Mazungumzo ya upatanishi yanayoongozwa na mjumbe wa Muungano wa AU , Olesegun Obasanjo bado hayajafua dafu.
Kufuatia ziara yake nchini Ethiopia wiki hii , mjumbe maalum kutoka Marekani katika eneo la upembe wa Afrika Jeffrey Feltman alisema kwamba wote waziri mkuu Abiy Ahmed na chama cha wapiganaji wa TPLF waliamini kwamba walikuwa
Natumai hujambo ni siku nyengine ambapo tunaendelea kukupasha habari kutoka maeneo tofauti duniani
