Watoto takribani 7000 waugua ugonjwa usiojulikana DRC
Afisa wa afya katika Jimbo la Kwilu, takriban kilomita 680, mashariki mwa Mji Mkuu wa DRC, Kinshasa alimeviambia vyombo vya habari kuwa karibu watoto 7,000 waliambukizwa na kwa sasa wanatibiwa.
Moja kwa moja
Lizzy Masinga
De Klerk alikuwa mhalifu - Watetezi wa haki
Rais wa mwisho mweupe wa Afrika Kusini FW de Klerk, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 85, ameshutumiwa kama "mhalifu wa ubaguzi wa rangi" na taasisi inayopigania haki kwa watu, ikiwa ni pamoja na watoto, waliouawa na utawala wa zamani wa wazungu wachache.
Katika taarifa yake, Wakfu wa Fort Calata ulisema kwamba De Klerk aliamuru uvamizi wa usalama katika mji wa Mthatha mwaka 1993, ambao ulisababisha watoto watano, miongoni mwao mapacha, kuuawa wakiwa usingizini.
Pia aliketi kwenye mikutano ya Baraza la Usalama la Taifa la utawala wa kibaguzi, ambalo lilijadili "hatma" ya wanaharakati mashuhuri wa kupinga ubaguzi wa rangi Fort Calata na Methhew Goniwe katika miaka ya 1980, ilisema taarifa hiyo.
Wawili hao waliuawa mwaka 1985 na vikosi vya usalama, na kusababisha hasira kubwa miongoni mwa watu weusi nchini Afrika Kusini.
Hata hivyo katika ujumbe wake wa mwisho wa video uliotolewa na Taasisi yake, FW de Klerk aliomba msamaha kwa "maumivu na aibu ambayo ubaguzi wa rangi umeleta kwa watu wa rangi nchini Afrika Kusini.
"wengi waliniamini, lakini wengine hawakuniamini. "Kwa hiyo, hebu leo, katika ujumbe wa mwisho nirudie: Mimi, bila sifa, naomba msamaha kwa maumivu na kuumizwa, na kudharauliwa, na uharibifu, kwa weus na Wahindi nchini Afrika Kusini," anasema katika ujumbe huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Matthew Goniwe (kulia) na Fort Calata (wa pili kutoka kulia) waliuawa mwaka 1985 na vikosi vya ulinzi vya taifa hilo. 'Ujumbe wa mwisho' wa Rais FW de Klerk

Chanzo cha picha, Getty Images
Kipande cha video chenye 'ujumbe wa mwisho' wa FW de Klerk kwa raia wa Afrika Kusini, kimeachiwa na taasisi yake.
De Klerk akionekana dhaifu anasema kwamba mara nyingi aliomba msamaha kwa "maumivu na aibu ambayo ubaguzi wa rangi umeleta kwa watu wa rangi nchini Afrika Kusini.
"wengi waliniamini, lakini wengine hawakuniamini. "Kwa hiyo, hebu leo, katika ujumbe wa mwisho nirudie: Mimi, bila sifa, naomba msamaha kwa maumivu na kuumizwa, na kudharauliwa, na uharibifu, kwa weus na Wahindi nchini Afrika Kusini," anasema.
Jumuiya ya Kiislamu ya Indonesia yakataza matumizi ya sarafu ya digitali

Chanzo cha picha, Getty Images
Baraza la Maulamaa la Indonesia (MUI), limesema kuwa kutumia sarafu za kidigitali kama njia ya malipo ni kinyume cha sheria katika Uislamu, lakini biashara ya mali ya kidigitali inaweza kuruhusiwa, mmoja wa viongozi wake alisema Alhamisi,Reuters limeripoti.
Indonesia, nchi kubwa zaidi ya Waislamu duniani, inapiga marufuku matumizi ya sarafu za digitali kama sarafu za kawaida, lakini uwekezaji katika na kufanya biashara ya tokeni za kidigitali unaruhusiwa katika soko la bidhaa
Thamani ya jumla ya biashara ya sarafu ya digitali imefikia rupiah trilioni 370 (dola bilioni 25.96) mwaka huu hadi Mei, kulingana na wizara ya biashara.
Kama njia ya malipo, sarafu za digitali zimekatazwa kwa mujibu wa Shariah kwa sababu zinabeba vipengele vya kutokuwa na uhakika na madhara, na zinakiuka sheria za serikali, Asrorun Niam Sholeh, mkuu wa kanuni za kidini wa MUI, aliiambia Reuters.
Uuzaji wa sarafu za digitali kama bidhaa pia ni haramu, huku MUI ikifananisha na kamari, kwa sababu haikidhi kanuni za Kiislamu.
Jinsi Mandela alivyowaleta pamoja De Klerk na Fidel Castro

Chanzo cha picha, Mandela inauguration ceremony
Rais wa mwisho mweupe wa Afrika Kusini FW de Klerk alikuwa mpinzani mkali wa ukomunisti. Alijaribu sana kumlazimisha Nelson Mandela - ambaye alikuja kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini - kusitisha ushirikiano wake wa kisiasa na Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini (SACP).
Bw Mandela alikataa, na kusifu jukumu la wakomunisti - nchini Afrika Kusini na nje ya nchi - katika kupiga vita ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Fidel Castro wa Cuba alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Mandela kama rais mwaka wa 1994 - na huku nguli huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi akitazama, yeye na Bw De Klerk walisalimiana kwa mikono ishara ya mabadiliko ya kisiasa yaliyokuwa yakienea duniani kote wakati huo.
Somo tunalopata kutoka kwa Mandela na De Klerk

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakfu wa Nelson Mandela umetukumbusha hotuba ambayo rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini aliitoa katika sherehe za miaka 73 ya kuzaliwa kwa mtangulizi wake, FW de Klerk.
Bwana Mandela alisema: "Ikiwa sisi wawili wazee, tuna somo lolote kwa nchi yetu na kwa ulimwengu, ni kwamba suluhu za mizozo zinaweza kupatikana tu ikiwa wapinzani wamejitayarisha kimsingi kukubali uadilifu wa kila mmoja."
Mandela alifariki mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 95.
De Klerk amefariki leo akiwa na umri wa miaka 85. Wawili hao walipataTuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1993 kwa jukumu lao katika kukomesha mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini mwaka 1994.
Mageuzi katika Shirikisho la Soka la Kenya laitia katika hatari ya kupigwa marufuku na Fifa

Chanzo cha picha, Getty Images
Kenya iko katika hatari ya kufungiwa kutoka shirikisho la soka duniani Fifa baada ya Waziri wake wa Michezo kuagiza kamati ya muda kusimamia shirikisho la soka nchini humo.
Waziri wa Michezo Amina Mohamed ameunda kamati ya muda ya watu 27 kusimamia Shirikisho la Soka la Kenya (FKF).
Fifa inapinga kuingiliwa kwa serikali katika uendeshaji wa mashirikisho wanachama na imepiga marufuku nchi kutoka kwa aina zote za kandanda kama matokeo hapo awali.
"Ili kuhifadhi mchezo wa kandanda, nimeamua kuteua kamati ya walezi ya FKF kwa muda wa miezi sita," Mohamed alisema kwenye taarifa.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Wizara ya Michezo, Utamaduni na Urithi itawezesha utendaji kazi wa kamati ya muda."
Mojawapo ya malengo yaliyotajwa ya kamati hiyo ni "kukabidhi FKF kwa maafisa wapya watakaochaguliwa baada ya uchaguzi ".
Taarifa ya Mohamed ilisema kuwa FKF "katika miaka michache iliyopita ... imekabiliwa na masuala kadhaa ya utawala ambayo yamekuwa yakisumbua sana Wizara".
"FKF imeshindwa kuwajibikia pesa zote ilizotengewa na serikali," aliandika.
Ripoti ya hivi majuzi iliyoidhinishwa na Wizara ilipendekeza kwamba mamlaka za Kenya zifanye uchunguzi zaidi ili kubaini "kiasi ambacho ufujaji wa fedha katika FKF unaweza kuwa ulitokea, kwa lengo la kuwashtaki wale ambao wanaweza kupatikana na hatia".
Chuo kikuu cha Oxford chaanza majaribio mapya ya chanjo ya Ebola

Chanzo cha picha, AFP
Majaribio yameanza ya chanjo mpya ya Ebola iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford.
Chanjo imeundwa kukabiliana na aina ya Ebola ya Zaire na Sudan, ambayo kwa pamoja imesababisha karibu milipuko yote ya Ebola na vifo ulimwenguni kote.
Chuo Kikuu cha Oxford kimezindua awamu ya kwanza ya majaribio yake, kuijaribu chanjo kwa watu wanaojitolea.
Chanjo za Ebola zipo kwa spishi za Zaire lakini watafiti wa Oxford wanatumai kuwa chanjo mpya itakuwa na ufikiaji mpana zaidi.
Teresa Lambe, mchunguzi mkuu wa kisayansi katika Chuo Kikuu cha Oxford, alisema: "Milipuko ya mara kwa mara ya virusi vya Ebola bado inatokea katika nchi zilizoathirika, na kuweka maisha ya watu binafsi, hasa wahudumu wa afya walio mstari wa mbele katika hatari.
Tunahitaji chanjo zaidi kukabiliana na ugonjwa huu mbaya." Kuna aina nne za virusi vya Ebola ambazo zimejulikana kusababisha magonjwa kwa wanadamu.
Kati ya hizi, Zaire ndio hatari zaidi, na kusababisha kifo katika 70% hadi 90% ya kesi ikiwa haitatibiwa.
Chanjo mpya iliyotengenezwa na wanasayansi wa Oxford inatokana na toleo dhaifu la virusi vya homa ya kawaida ambayo imebadilishwa vinasaba ili isiwezekane kwa wanadamu.
Njia hii tayari imetumika kwa mafanikio katika chanjo ya Oxford-AstraZeneca Covid-19.
Awamu ya kwanza ya majaribio itashuhudia watu 26 wenye umri wa miaka 18 hadi 55 wakipokea dozi moja ya chanjo ya ChAdOx1 biEBOV Ebola katika chuo kikuu.
Kisha zitafuatiliwa kwa muda wa miezi sita, na matokeo yanatarajiwa katika robo ya pili ya mwaka 2022.
Ndugu wanne waliotekwa nyara waokolewa nchini Afrika Kusini
Ndugu wanne wa Afrika Kusini ambao walitekwa nyara wakielekea shuleni wiki tatu zilizopita wameokolewa, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti.
Wanaojiita ndugu wa Moti, wenye umri wa kati ya miaka sita na 15, walikuwa wametekwa nyara baada ya watu wenye silaha kufunga barabara kuu na kuwalazimisha kutoka kwenye gari.
Watoto hao hawajajulikana waliko tangu kutekwa nyara hadi sasa.
Polisi walisema walipokea simu Jumatano usiku kutoka kwa mkazi wa Vuwane huko Limpopo, ambaye alisema wavulana hao walikuwa wameshushwa kutoka kwenye eneo la barabara iliyo karibu.
Walisema daktari alithibitisha kwamba walikuwa na afya njema - na walikuwa wameunganishwa tena na familia yao.
Familia hiyo pia ilishirikisha habari kwenye ukurasa wake wa biashara kwenye Facebook:
Hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa na sababu ya utekaji nyara huo.
Haijabainika pia ikiwa fidia ililipwa kwa kuachiliwa kwao. Polisi bado wanachunguza suala hilo na wameomba kwa yeyote mwenye taarifa zaidi kuwasiliana nao.
Mlipuko waua mtu mmoja katikati mwa Uganda
Mlipuko umesababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine wawili katika wilaya ya Nakaseke katikati mwa Uganda.
Tukio hilo lilitokea katika mji mdogo wa Kapeeka, yapata saa mbili kutoka mji mkuu Kampala. Walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa kifaa hicho kilikuwa kwenye rundo la vyuma chakavu, na mlipuko huo ulimuua mfanyabiashara wa vyuma chakavu aliyekuwa akipasha moto ili kuviyeyusha.
Polisi wamezingira eneo la tukio na kuanza uchunguzi kuhusu chanzo cha kilipuzi hicho.
Msemaji wa polisi aliambia BBC kwamba wanaamini kuwa kifaa hicho kinaweza kuwa kilipuzi cha kale.
Nakaseke ni sehemu ya Pembetatu ya Luweero, ambako vita vilivyomuingiza Rais Yoweri Museveni madarakani miaka ya 1980 vilipiganwa.
Na huko nyuma, mabaki ya vilipuzi yameua au kuwajeruhi watu katika eneo hilo.
Habari za hivi punde, Steven Gerrard: Aston Villa imemteua kocha wa Rangers kama meneja mpya

Chanzo cha picha, SNS GROUP
Aston Villa wamemteua Steven Gerrard kama meneja kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu, na hivyo kuhitimisha uongozi wake wa miaka mitatu katika klabu ya Rangers.
Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool, 41, anawaacha mabingwa hao wa Scotland akiwa amewaongoza kutwaa taji la kwanza la ligi katika kipindi cha miaka 10 msimu uliopita.
Gerrard anachukua nafasi ya Dean Smith, ambaye alitimuliwa Jumapili baada ya kushindwa mara tano mfululizo.
Villa wako katika nafasi ya 16 kwenye Premier League, pointi mbili juu ya eneo la kushushwa daraja.
"Aston Villa ni klabu yenye historia na utamaduni mzuri katika soka ya Uingereza na ninajivunia kuwa kocha mkuu mpya," alisema Gerrard.
"Katika mazungumzo yangu na Nassef [Sawiris], Wes [Edens] na wengine wa bodi, ilionekana wazi jinsi mipango yao ilivyo kabambe kwa klabu na ninatazamia kuwasaidia kufikia malengo yao."
Gerrard alichukua hatua zake za kwanza katika uongozi wa juu akiwa na klabu ya Rangers ya Scotland mwaka wa 2018, na kuondoka nao pointi nne mbele ya wapinzani wao Celtic kileleni mwa jedwali.
Aliichezea Liverpool mara 710, akishinda mataji tisa, na alitumia msimu mmoja katika klabu ya MLS ya LA Galaxy mwaka wa 2015 kabla ya kustaafu kama mchezaji mwaka uliofuata.
Watoto takribani 7000 waugua ugonjwa usiojulikana DRC

Chanzo cha picha, Getty Images
Afisa wa afya katika Jimbo la Kwilu, takriban kilomita 680, mashariki mwa Mji Mkuu wa DRC, Kinshasa alimeviambia vyombo vya habari kuwa karibu watoto 7,000 waliambukizwa na kwa sasa wanatibiwa.
Dalili ni pamoja na homa kali na kuhara. Mlipuko huo ulianza Agosti mwaka huu. Novemba 7 mwaka jana, sampuli zilifika katika Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Biolojia, mjini Kinshasa ili kubaini chanzo cha ugonjwa huo.
Mgomo wa wafanyakazi wa matibabu katika Mkoa wa Kwilu ulicheleweshwa tahadhari ya mapema
Watoto 286 wenye umri wa kati ya mwaka 0 na 5 walifariki katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na ugonjwa ambao haukujulikana asili yake,
Mkuu wa kitengo cha afya cha jimbo la Kwilu Jean Pierre Baseke alithibitisha haya kwenye redio ya umoja wa mataifa katika jahmuri ya kidemokrasia ya Congo maarufu radio okapi.
Alibainisha kuwa tangu mwishoni mwa Agosti ugonjwa huu ulipotokea, kumekuwa na zaidi ya maambukizi 7000 sasa ikiwa ni pamoja na vifo 286. Dalili ni pamoja na homa na maumivu ya tumbo, kutapika na upungufu wa damu
Daktari Jean Pierre Basele anahisi kwamba ni janga jipya, kwa sasa sampuli zimefikishwa mji mkuu Kinshasa kwenye taasisi ya serkali inaoyochunguza sampuli tangu tarehe saba mwezi huu , na sasa wanaendelea kusubiri matokeo.
" Tulianza na visa zaidi ya elfu tano lakini kwa sasa tumekuwa na visa zaidi ya elfu saba tangu tarehe nane ya mwezi huu na watoto mia mbili na thamanini na sita wameshafariki.
Takwimu ni hizo hizo tu kwasasa kwabababu serkali ya jimbo ilitoa pesa na tumeeanza kutoa matibabu kwa watoto, kwa sasa tumengudua kama ni malaria lakini tukilinganisha na miaka iliyopita, kesi zinaongezeka kwa mara tano kwa hiyo tunaona ya kwamba limekuwa janga linigine jipya" Alisema Dkt. Basele.
Kituo cha afya cha Mukedi ambako kesi ya kwanza iliripotiwa tangu tarehe 15 Agosti , wakati maafisa wa afya walipokuwa katika mgomo na hivyo ulichelewesha viongozi wa ngazi ya juu kufatilia haraka ,na kwa sasa karibu watoto mia tatu wamepoteza maisha kwa kipindi cha miezi mitatu na takribani watoto 7000 wameugua.
Shirika la raia jimboni kwilu linalaumu serkali ya Congo kuchelewesha jibu lake kila mara kukiwa mlipuko wa janga .
Kwa mujibu wa placide Mukwa kiongozi wa shirika la raia jilmboni kwilu, haiwezi heleweka kuona zaidi ya watoto mia mbili wamefariki kwa kipindi cha miezi mitatu katika jimbo hilo ambalo linapakana na mji mkuu kinshasa na ni siku moja tu kwa njia ya gari ndo maafisa wa afya wanaweza kufika huko na kupata suluhisho .
Shirika la raia linataka idara ya serikali inayochunguza sampuli kuharakisha utafiti ili wafahamu haraka ugonjwa gani huo unaosababishavifo vya watoto.
DR Congo yaondoa marufuku ya wimbo wa kumkosoa rais

Chanzo cha picha, AFP
Maafisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameondoa marufuku ya wimbo unaomkosoa Rais Félix Tshisekedi.
Marufuku hiyo ilitangazwa Jumanne na tume ya udhibiti na kisha kuondolewa Jumatano baada ya waziri wa sheria kuingilia kati.
Kundi linalounga mkono muziki huo, MPR, pia lilisema limeomba marufuku hiyo kuondolewa.
Marufuku hiyo ilikuwa imeonekana kuwa ya kidikteta na ilikosolewa sana.
Vyombo vya habari sasa vimeruhusiwa kupiga wimbo Nini Tosali Te (Nini Hatukufanya katika lugha ya Kilingala). Wimbo huo unalinganisha kile ambacho Bw Tshisekedi aliahidi alipokuwa kwenye upinzani na kile ambacho amefanikiwa kufikia sasa akiwa rais.
"Ulituahidi furaha baada ya [marehemu rais] Mobutu kuondoka. Mobutu alienda lakini hatukupata chochote. Ulisema ungerekebisha mambo ikiwa [rais wa zamani] Kabila atajiuzulu. Kabila aliondoka lakini bado ni ngumu," AFP. shirika la habari linanukuu maneno hayo yakisema.
Wimbo mwingine mmoja katika Kifaransa, Barua kwa Ya Tshitshi, jina la utani la marehemu babake Bw Tshisekedi, Etienne, bado umepigwa marufuku.
Mwimbaji, Bob Elvis, anasema: "Tangu uondoke, mwanao Felix amekuwa rais... Tumebadilisha utawala bila kubadilisha mfumo," AFP inaripoti.
Msemaji wa serikali Patrick Muyaya alitweet kwamba marufuku hiyo haikutoka kwa serikali.
“Mwananchi yeyote ana uhuru wa kutoa maoni yake, mradi yanazingatia sheria,” alisema.
Idadi ya kutazamwa kwa nyimbo hizo mbili imeongezeka kwenye YouTube tangu kupigwa marufuku, kulingana na tovuti ya habari ya Actualite Congo.
Rais wa Msumbiji amtimua kazi Waziri wake wa Ulinzi

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amemfuta kazi waziri wa ulinzi Jaime Augusto Neto.
Hatua hii inakuja siku moja tu baada ya rais kumfukuza kazi waziri wa mambo ya ndani, Amade Miquidade.
Rais hajaeleza ni kwanini amewafuta kazi viongozi wakuu wa ulinzi na usalama wa nchi.
Inaaminika kuwa uamuzi huo unahusiana na kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara, mauaji, ugaidi na ufisadi, pamoja na kuongezeka kwa idadi ya ajali za barabarani.
Baadhi ya kesi hizo zimehusisha askari wa ulinzi na usalama.
Waangalizi wa mambo wamemtaka Rais Nyusi kueleza maamuzi yake ili kuepuka uvumi, hofu na fujo.
Wanasema si jambo la kawaida kuwatimua viongozi wawili wakuu wa usalama kwa siku chache na kwamba lazima kuwe na sababu.
Afrika Kusini kumsafirisha waziri wa zamani wa Fedha Msumbiji kwenda Marekani..kunani?

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Manuel Chang Mahakama ya Afrika Kusini imeamuru kwamba aliyekuwa waziri wa fedha Manuel Chang anapaswa kupelekwa nchini Marekani ambapo anasakwa kwa makosa ya uhalifu kuhusiana na kashfa kubwa ya ufisadi.
Uamuzi wa mahakama hiyo unafutilia mbali uamuzi wa waziri wa haki nchini Afrika Kusini Ronald Lamola mwezi Agosti kumhamisha Chang katika nchi yake.
Jaji wa mahakama kuu Margaret Victor alisema mahakama haikupata uamuzi huo kuwa unaokubalika.
Makundi ya wanaharakati yalipinga kumhamisha Chang kuelekea Msumbiji akihofia kwamba asingekabiliwa na mashtaka.
Waziri huyo wa zamani amekuwa kizuizini nchini Afrika kusini tangu 2018kutokana na agizo la kumkamata kwa madai ya kutaka kufanya ulaghai na utakatishaji wa fedha.
Kashfa hiyo inahusisha zaidi $2.7bn (£2bn) za deni la serikali lisilojulikana ambalo serikali iliomba ili kujenga kiwanda cha samaki , kununua wavu wa kuvulia samaki na mabotoiya kijeshi ili kuweka usalama , lakini kiwango kikubwa cha fedha hizo zilidaiwa kugawanyiwa maafisa wafisadi.
Chang, 66alikana kukubali $7m kama hongo. Alikamatwa kufuatia ombi la Marekaniambapo wawekezaji waliathiriwa na kashfa hiyo.
Wanandoa waliosambaza picha bandia za utupu za rais wa Zimbabwe waachiliwa

Chanzo cha picha, bbc
Maelezo ya picha, Rais Mnangagwa Wanandoa wa Zimbabwe wameachiliwa huru kutoka kizuizini baada ya hakimu kufutilia mbali kesi dhidi yao kwa madai ya kusambaza picha bandia za utupuza rais wa taifa hilokatika mtandao wa WhatsApp, amesema wakili wao.
Sarudzayi Ambiri Jani, 39, na Remember Ncube, 35, walihukumiwa kifungo Juni 2020 kwa madai ya kuhujumuna kumtusi rais lakini hakufunguliwa mashtaka.
Picha hizo bandia zilionekana kumuonesha rais Emmerson Mnangagwaakiwa utupu , huku akiwa amezibwa na kitambaa kidogo cha bendera ya Zanu-PFna barakoa ambayo ilikuwa imeficha sehemu zake za siri.
Hakimu Takudzwa Gwazemba, aliwaachilia huru wawili hao kutoka kizuizini kwasababu upande wa mashtaka ulikuwa umeshindwa kuwafungulia mashtaka mwaka mmoja baada ya kukamatwa.
Natumai hujambo . Ni siku nyengine ambapo tutakupasha moja kwa moja kuhusu matukio tofauti duniani
