Je Tanzania iko tayari kwa matumizi ya sarafu ya kidijitali?
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa nchi hiyo kujiandaa kutumia ya sarafu za mauzo ya mtandaoni, maarufu Bitcoin.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Hofu yakumba kijiji cha Afrika Kusini kinachodaiwa kuwa na almasi
Kundi kubwa la watu limekusanyika katika kijiji kimoja mkoani KwaZulu-Natal ambako kumetokea uvumi wa kupatikana kwa madini ya almasi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini Afrika Kusini
Video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha watu wakichimba ardhi kutafuta mawe hiyo ya thamani .
Mamlaka ya mkoa pia imeweka kwenye Twitter kanda ya video ikielezea wasiwasi wake kuhusu "watu wanakimbilia almasi".
iliongeza kuwa "imepokea kwa wasiwasi, ripoti za shughuli za uchimbaji haramu zinazofanyika KwaHlathi nje kidogo ya mji wa Ladysmith".
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mamlaka za mitaa bado hazijathibitisha ikiwa mawe hayo ni almasi halisi.
Idara ya kitaifa ya madini na nishati inasemekana imeahidi kutuma timu yake - pamoja na vitengo vya utekelezaji na uzingatiaji, pamoja na wanasayansi wa jiolojia - kukagua eneo hilo.
Utawala wa KwaZulu-Natal pia umesema katika taarifa ya vyombo vya habari kwamba unahofia msongamano wa watu unaweza kuchangia ukiukwaji wa kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Covid-19.
Kaunda anaomba maombi baada ya kulazwa hospitalini

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanzilishi wa taifa la Zambia, Kenneth Kaunda amelazwa hospitali baada ya ''kutojihisi vyema'', taarifa kutoka ofisi yake inasema.
Kiongozi huyo aliye na umri wa miaka 97- ni mmoja wa wapiganiaji uhuru wa Afrika miaka ya 1950.
Alikuwa rais wa kwanza wa Zambia mwaka 1964.
Taarifa inasema Dr Kaunda "anawaomba Wazambia wote na jamii ya kimataifa kumuombea wakati madaktari wake wanapofanya kila juhudi kahakikisha amepona".
Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu ugonjwa wake.
Dkt Kaunda, ambaye aliondoka madarakani mwaka 1991,amekuwa hospitali mara kwa mara.

Habari za hivi punde, Mfanyabiashara maarufu wa Kenya Chris Kirubi afariki dunia

Chanzo cha picha, Capital FM
Mtaalamu mashuhuri wa viwanda na mmoja wa wafanyabiashara tajiri zaidi Afrika, Dkt Chris Kirubi amefariki dunia, familia yake imethibitisha.
Dkt Chris Kirubi ambaye pia ni Mwenyekiti wa makampuni kadhaa ikiwemo ya habari ya Capital Group Limited, alikuwa akiugua saratani tangu mwaka 2016.
Kirubi aliorodheshwa na jarida la Forbes kuwa Mkenya wa pili kwa utajiri mwaka 2011 katika orodha iliyojumuisha familia ya kiongozi mwanzilishi wa nchi hiyo, Marehemu Rais Jomo Kenyatta.
Alifanikiwa pia kushika nafasi ya 40 ya tajiri zaidi barani Afrika baada ya katika nafasi ya 31, mali yake ikiwa na thamani ya dola milioni 300.
Bw. Kirubi atakumbukwa kwa kuwahimiza vijana kujiamini wanaweza bila kujali walikotoka akiongeza kwamba yeye pia alinzia chini na kufikia upeo wa maisha yake, baada ya kufiliwa na wazazi wake akiwa na umri mdogo.
“Haijalishi ulikotoka. Hata kama unaishi kwenye mabanda. Hatma ya maisha yako iko mikononi mwako,” alisema.
Kirubi pia amekuwa akitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwahamasisha vijana kujiepusha na watu ambao huenda wakawa kikwazo katika ndoto ya ufanisi maishani mwao.
Kiongozi wa 'familia kubwa zaidi duniani' afariki nchini India

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanamume wa miaka 76- anayeamiiwa kuwa kiongozi wa familia kubwa zaidi duniani amefariki katika jimbo la Mizoram, nchini India.
Ziona Chana, mkuu wa dhehebu la kidini ambalo linaunga mkono ndoa ya wake wengi, alifariki Jumapili, na kuwaacha wake 38, watoto 89 na wajukuu 36.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Waziri Mkuu Kiongozi wa jimbo la Mizoram, Zoramthanga,ambaye alitoa salamu zake za rambi rambi katika mtandao wa Twitter "kwa masikitiko makubwa ".
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Chana aliripotiwa kuugua ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu
Madaktari waliiambia shirika la habari la PTI kwamba hali ya Chana ilikuwa mbaya zaidi nyumbani kwake katika kijiji cha, Baktawng Tlangnuam. Alilazwa hospitali Jumapili jioni ambako alithibitishwa kufariki alipofikishwa.
Ni vigumu kubainisha ikiwa kweli Chana alikuwa kiongozi wa familia kubwa zaidi duniani kwa kuwa kuna wengine ambao wamedai taji hilo.
Pia ni vigumu kukadiria ukubwa wa familia ya Chana. Ripoti moja ilidai alikuwa na wake 39, watoto 94, wajukuu 22 na kitukuu mmoja, ambao kwa jumla ni watu 181.
Wakati ripoti kadhaa za habari nchini humo zimemtaja kuwa anashikilia "rekodi ya ulimwengu" kwa familia kubwa kama hiyo, haijulikani ni rekodi gani ya ulimwengu.
Imeripotiwa pia kuwa familia hiyo imeangaziwa mara mbili kwenye kipindi maarufu cha Ripley's Amini au la.
Wafuasi wa Bobi Wine waliachiliwa baada ya miezi sita

Chanzo cha picha, AFP
Mahakama ya kijeshi ya Nnchini Uganda imewachia kwa dhamana wafuasi 18 wa manasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, ambao wakamatwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mnamo Desemba 2020.
Wafuasi hao ni hao ni pamoja na aliyekuwa mlinzi mkuu wa Bobi Wine Ssebufu Edward maarufu Eddy Mutwe, mutunzi mwenzie Bobi Wine Ali Bukeni maarufu Nubian Li.
Walikuwa sehemu ya kundi la watu 49 walioshtakiwa kwa silaha kinyume cha sheria.
18 kati yao waliachiliwa huru mwishoni mwa mwezi Mei na wengine 13 walikuwa wamepewa dhamana mweizi Februari mwaka huu.

Chanzo cha picha, Reuters
Walikamatwa katika kisiwa cha Kalangala, wakati wa mkutano ambapo Bobi Wine pia alishikwa na kusafirishwa kwa nguvu nyumbani kwake Kampala kwa helikopta ya jeshi.
Katika mashariti ya dhamana waliopewa hawaruhiwi kutoka nje ya wilaya ya Kampala na Wakiso na wametakiwa kulipa milioni 20 na kuripoti mara mbili kwa mwezi.
Wakati wa msimu wa uchaguzi na miezi kadhaa baada ya ya uchaguzi wa Januari, Uganda ilishuhudia wimbi la watu kukamatwa na madai ya utekaji ya kile kinachoaminiwa kuwa mamia ya wafuasi wa upinzani.
Taarifa iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Wazir wa Mambo ya ndani wakati huo Jenerali Jeje Odongo mwezi Aprili ilionesha kuwa vikosi vya usalama wakati mmoja vilikuwa vikiwazuilia watu 1000.
Familia katika mji mkuu Kampala na maeneo mengine ya nchi zinaendelea kuomba serikali kuwaachia wapendwa wao ambao wanasema walikamatwa na maafisa wa usalama na bado hawajulikani waliko.
Ramaphosa asisitiza juu ya haja ya kuondolewa kwa hati miliki ya chanjo

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rais wa Afrika Kusini alialikwa katika mkutano wa G7 Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza haja ya kuondolewa kwa hati miliki ya chanjo ili kuiwezesha Afrika kujitengenezea chanjo ya Covid-19.
Rais aliiambia BBC kwamba hatma ya bara hilo sasa iko "mikononi mwake" baada ya mataifa mengi kuripoti ongezeko la maambukizi ya virusi.
Ni asilimia mbili pekee ya watu katika bara hilo wamechanjwa kufikia sasa huku baadhi ya nchi zikikabiliwa na uhaba wa chanjo.
Rais huyo wa Afrika Kusini ambaye alikuwa mgeni katika kongamano la G7 liliomalizika nchini Uingereza hivi punde, amesema Bara la Afrika linahitaji kujitengenezea chanjo zitakazotumiwa na zaidi ya watu bilioni 1,2.
"Tumetoa pendekezo la kuondolewa kwa hati miliki zinazohusiana na biashara. Hatua au mchakato, ambao tunayohitaji sasa ili kujitengenezea chanjo zetu," alisema.
Rais Ramaphosa alisema Afrika Kusini "inakabiliwa na hali tete" huku visa vya maambukizi vikiongezeka kila uchao.
Amesema bara hilo limeachwa nyuma katika chanjo.
"Tuliachwa nyuma kwa sababu walinunua chanjo zote kwa kuwa wana fedha na wanamiliki kampuni za utengenezaji chanjo na sisi hatuna, hiyo ndio sababu tumeachwa nyuma,"alisema.
Urembo wao uliwavutia wengi,kumbe walidaiwa kuwa majasusi wa Urusi

Chanzo cha picha, FACEBOOK/ MARIA BUTINA
Tabasamu zao zilikuwa za kuvutia ,urembo wao ulikuwa kama chambo na misheni zao zilikuwa za siri kubwa. Soma zaidi
Majeshi yaanza kutengeza gesi ya Oksijeni Uganda

Chanzo cha picha, Reuters
Wanajeshi nchini Uganda wameanza kutengeza gesi ya Oksijeni kwa ajili ya tiba baada ya hitaji la bidhaa hiyo ''kuongezeka mara dufu" hospitalini kutokana na wingu jipya la maambikizi ya Covid-19.
Tvuti ya gazeti la New Vision linaloendeshwa na serikali imesema, kupitia kitengo chake cha biashara,Shirika la Kitaifa la Biashara (NEC), linazalisha oksijeni katika viwanda vya Luweero, katikati mwa Uganda.
Hospitali kadhaa nchini Uganda zimeripoti kukabiliwa na uhaba wa oksijeni wakati taifa hilo la Afrika Mashariki linapokabiliwa na wimbi la pili la maambukizi ya corona.
Kufikia sasa Uganda imethibitisha kuwa na wagonjwa 60,250 wa corona na vifo 423 vinavyohusiana na ugonjwa huo.
Wiki iliyopita Shirika la ndege la Rwanda(RwandaAir) lilisitisha kwa muda safari zake nchini humo kufuatia ongezeko la maaambukizi ya Covid -19.
- Mbinu ya kuwalaza wagonjwa wa corona kifudifudi inavyookoa maisha yao
Rais Samia ataka Tanzania kujiandaa kwa matumizi wa sarafu ya kidijitali

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa nchi hiyo kujiandaa kutumia ya sarafu za mauzo ya mtandaoni, maarufu Bitcoin.
Samia aliiambia Benki Kuu ya Tanzania,siku ya Jumapili kuwa macho wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la matumizi ya sarafu hiyo kote duniani.
"Najua nchi nyingi duniani hazijaanza kutumia sarafu za mauzo ya mtandaoni. Hata hivyo, natoa wito kwa Benki ya Kuu ya Tanzania kuaanza kufuatilia yanayojiri na kujiandaa.
"Hatutaki kupatikana ghafla au kufahamu baadae kwamba raia wako mbele yetu na wameaanza kutumia sarafu za kidijitali," alisema.
El Salvador wiki iliyopita ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuorodhesha rasmi sarafu ya kidijitali, Bitcoin, kuwa sarafu halali.
- Je wakati umefika kwa serikali za Afrika kuruhusu biashara ya sarafu za mauzo ya mtandaoni?
- Tanzania yazindua mtambo mkubwa zaidi Afrika Mashariki wa kusafisha dhahabu
Mkuu wa Twitter aweka bendera ya Nigeria mtandaoni- Kunani

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkuu wa Twitter Jack Dorsey ameweka ujumbe wenye picha ya bendera ya Nigeria mtandaoni katika hatua ambayo vyombo vya habari nchini humo vinaashiria ni kuunga mkono maandamano ya Jumamosi dhidi ya uongozi mbaya na kulalamikia kufingiwa kwa Twitter.
Ujumbe wa Bw. Dorsey umewavutia Wanageria wengi wanaotumia mtandao wa VPN kufikia programu hiyo tumishi.
Twitter inajadiliana na serikali ya baada ya kupigwa marufuku nchini humo tarehe 5 mwezi Juni.
Marufuku hiyo ilifuatia hatua ya mtandao huo kufuta ujumbe wa Rais Mohammadu Buhari lakini ofisi yake imesema hatua hiyo haihusiani kivyovyote na suala hilo.
Raia wa Nigeria siku ya Jumamosi waliandamana kulalamikia uongozi mbaya, ukosefu wa demokrasia na kupigwa marufuku kwa Twitter.
Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanji na kuwakamata baadhi yao,kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
Maandamano ya Jumamosi ni ya kwanza tangu maandamano ya #EndSARS ya kupinga ukatili wa polisi yaliyofanywa kwa wiki kadhaa.
Soma zaidi:
Viongozi wa G7 waahidi chanjo bilioni moja za corona kwa mataifa masikini

Chanzo cha picha, PA Media
Viongozi wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi na kiviwanda duniani wameahidi kutoa dozi bilioni moja za chanjo ya Covid- 19 kwa mataifa maskini kama "hatua kubwa kuelekea upatikanaji wa chanjo kwa watu wote duniani", amesema Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.
Wakati wa kumalizika kwa kongamano la G7 mjini Cornwall, Bw. Johnson alisema mataifa yanapinga "mbinu za kitaifa".
Lakini akaongeza kuwa chanjo ya ulimwengu itaonyesha faida za maadili ya kidemokrasia ya G7.
Pia kulitolewa ahadi ya kuwaondolea mchango wa kushughulikia mabdailiko ya tabia nchi
Baada ya mkutano wa kwanza wa viongozi wa ulimwengu ndani ya miaka miwili , Bw. Johnsona alisema "Ulimwengu ulikuwa unatutegemea sisi kukataa baadhi ya njia za ubinafsi, za kitaifa ambazo ziliharibu mwitikio wa kwanza wa ulimwengu kwa janga hiyo na kutumia juhudi zote za kidiplomasia, kiuchumi na kisayansi kutokomeza Covid -19".
Alisema viongozi wa G7 waliahidi kusambaza chanjo hizo kwa nchi masikini moja kwa moja au kupitia mpango wa Shirika la Afya Ulimwenguni la Covax - zikiwemo dozi milioni 100 kutoka Uingereza.
Maelezo zaidi:
Rais wa Zambia awahakikishia wananchi kuwa 'hana neno' baada ya kuzimia

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Zambia Edgar Lungu amewahakikishia wananchi kwamba hana neno baada ya kuzimia akihudhuria mkutano wa hadhara.
Alikuwa akiongoza siku ya ulinzi hapo jana (Jumapili) mara "ghafla akashikwa na kisunzi"mjini, Lusaka.
Katibu wa baraza la mawaziri Simon Miti alitoa taarifa akisema rais ''ni mzima na anaendelea na shughuli zake za kazi".
Dkt Miti anasema Rais Lungu alipata nafuu mara moja baada ya tukio hilo.
Rais alikabiliwa na hali kama hiyo ya kiafya mwaka 2015 na wakati huo ofisi yake ilisema kwamba ilitokana tatizo katika umio wake.
Rais Lungu anagombea tena uongozi wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaoandaliwa tarehe 12 mwezi Agosti.
Karibi katika matangazo mubashara leo Jumatatu 14.06.2021
