Zuma akanusha mashtaka ya ufisadi dhidi yake
Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
'Nikiwa Binti wa miaka 9 nilikua mraibu wa ngono'

Chanzo cha picha, EULENE MURHANDO
Eulene Murhando anajionea fahari ufanisi alioupata lakini rohoni mwake ana kumbukumbu za madhila aliyoyapitia utotoni ambayo karibu yasambaratishe maisha yake. Soma zaidi
Rais na Waziri Mkuu wa Mali wanaozuiliwa 'wajiuzulu'
Rais wa mpito wa Mali na Mali Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane wamejiuzulu rasmi, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Bwana Ndaw na Bwan Ouane wamekuwa wakizuiliwa tangu Jumatatu jioni katika kambi ya kijeshi nje ya mji mkuu, Bamako.
Afisa aliyeongoza mapinduzi ya mwaka jana aliyekuwa makamu wa wa rais wa serikali ya mpito, Col Assimi Goïta, amewalaumu kwa kuzembea katika majukumu yao na kujaribu kuhujumu mchakato wa mpito ya nchi hiyo.
Ripoti za kujiuzulu kwao zinajiri wakati wapatanishi wa Afrika Magharibi wamewasili nchi humo kujadili kupanga kuachiliwa kwao kutoka kambi ya kijeshi.
- Mali :Assimi Goïta afanya Mapinduzi ya pili ya kijeshi chini ya mwaka mmoja
De Gea ndiye mlinda lango bora wa Man Utd kushiriki fainali ya leo - Schmeichel

Chanzo cha picha, Getty Images
Aiyekuwa mlinda lango wa Manchester United Peter Schmeichel aliulizwa nani anastahili kuanza katika mchuano wa fainali ya leo ya kombe la ligi ya Uropa kati ya manchester United na Villareal kati ya David de Gea na Dean Henderson.
"Bila shaka yoyote nitaanza na David de Gea," amesema kupitia BBC Radio 5 Live. "Tunapozungumzia timu hii kwa misingi ya soka ya Ulaya, imekumbana na panda shuka zake.
"Hatuwezi kusahau ukweli wa kwamba Manchester United ilianza msimu huu katika Ligi ya Mabingwa, kisha kila kitu kikaonekana kwenda mrama, kwahiyo, hakuna uhakika wa kuwa salama kucheza ugenini, Uaya.
"David de Gea amekuwa katika klabu hiyo kwa miaka 10 na anasemekana kuwa mchezeji mzuri katika kipindi chote hicho. Alionesha kama anashuka kidogo takriban mwaka mmoja uliopita lakini nafkiri ameonesha kuwa yeye ndio mlinda lango bora Manchester United.
"Mchezo uliochezwa Roma wiki tatu zilizopita (katika mechi ya nusu fainali) huenda ingekuwa moja ya nyakati za aibu sana kuwahi kutokea kwa klabu hiyo. Kama hangecheza alivyocheza, timu hiyo ingeondolewa (baada ya kupata ushindi wa mabao 6 kwa 2). Nakumbuka fika alivyookoa mara nne."
- Tetesi za soka Ulaya Jumatano 26.05.2021: Zaha, Pochettino, Martinez, Neves, Coutinho, Willian
Muokaji wa Kenya kumfidia mteja kwa 'slesi za zenye mashimo'

Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni Mini Bakeries Limited nchini Kenya, linalooka mikate ya Supa Loaf, limejitolea kumfidia mteja aliyelalamika katika mtandao wa Twitter kuhusu "slesi zenyze tundu" katika mkate alionunua.
Mteja huyo, ambaye alidai kula mkate wa Supa Loaf maisha yake yote, alilalamika akisema "kuwa na mkate ulio na shimo katika slesi ya kwanza hadi ya mwisho" haikuwa ya haki.
Kampuni imemuomba msamaha mteja kwa "tukio hilo baya", ijapokuwa haijabainika jinsi itakavyomfidia.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Siku ya Jumatatu, Mamlaka ya kudhibiti mashindano ya kibiashara nchi Kenya imeiagiza kampuni hiyo kutoa taarifa ya kina kuhusu bidhaa zao, ikiwemo uzani na viungo vinavyotumiwa.
Hii ni baada ya mjadala kuibuka kwamba waokaji wanauza mikate midogo kuliko ilivyoidhinishwa viwandani.
Fahamu programu inayokuwezesha kudhibiti maisha ya mtu mwingine

Chanzo cha picha, NEWNEW
Utajihisi vipi ikiwa utalipa pesa kuweza kudhibiti maisha ya mtu mwingine kwa mambo mbalimbali binafsi yanayomhusu? Fahamu programu itakayokuwezesha kufanya hivyo.Soma zaidi
Habari za hivi punde, Zuma akanusha mashtaka ya ufisadi dhidi yake

Chanzo cha picha, EPA
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekana mashtaka ya ufisadi mwanzoni mwa kesi yake katika mahakama ya Pietermaritzburg.
Akionekana mdhaifu na kukiongea kwa utulivu, Jacob Zuma alisema NAPINGA makosa yote 18 ya ulaghai, ufisadi, ulaghai, ukwepaji wa kodi na utakatishaji fedha haramu.
Mashtaka hayo yanahusiana na matukio ya zaidi ya miongo miwili - katika siku za mwanzo za demokrasia ya Afrika Kusini - pamoja na mpango mkubwa wa silaha wenye utata.
Bwana Zuma na washirika wake wanasisitiza kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa.
Umati wa watu umekusanyika nje ya ukumbi wa mahakama huko Pietermaritzburg kuashiria kuwa Bwana Zuma bado ana umaarufumiongoni mwa wafuasi wake.
Lakini sasa kuna ushahidi mkubwa wa ufisadi uliofanikiwa katika kipindi cha uongozi wa madarakani, na Waafrika Kusini wengi wanataka kuona haki ikitendeka.
Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.
Waafrika Kusini wanaamini kesi hiyo inaweza kuashiria mabadiliko ya nchi hiyo.
Baadhi ya mashujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini waliohai wamemshtumu Bw. Zuma– kumlinganisha na jambazi na kuonya itachukua muda mrefu kurekebisha uharibifu alioufanya dhidi ya taasisi changa za nchi.
- Aliyekuwa Rais Afrika Kusini Jacob Zuma anakabiliwa na 'kosa la kuidharau mahakamani '
Wafuasi 17 wa Bobi Wine waachiliwa huru Uganda

Chanzo cha picha, Reuters
Mahakama ya kijeshi mjini Kampala imewaachilia kwa dhamana wanachama 17 wa chama cha upinzani cha National Unity Platform waliokuwa wakizuiliwa.
Kuachiwa kwao kunakuja miezi mitano tangu walipokamatwa mwezi Desemba mwaka jana wakiwa katika mkutano wa kampeni ya mgombea wao wa urais Robert Kyagulanyi, ambaye pia anajulikana kama Bobi Wine katika wilaya ya kisiwani ya Kalangala.
Wanachama hao 17 wanajumuisha maafisa wa mawasiliano wa Bobi Wine pamoja na walinzi na maafisa wa itifaki.
Walikuwa miongoni mwa watu 49 waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka katika mahakama kuu ya kijeshi ya Makindye baada ya kupatikana na silaha kinyume cha sheria.
Walioachiliwa wamepewa masharti makali ya dhamana.
Mwenyekiti wa Mahakama, Andrew Gutti, aliwazuilia kusafiri nje ya mji mkuu, Kampala, na Wakiso, wilaya iliyokaribu.
Mamia wanakimbia makazi yao baada ya tetemeko la volkano kutokea Rwanda

Maelezo ya picha, Watu walionekana katika vituo vya usafiri wakijaribu kuondoka mji huo Mamia ya watu wanasadikiwa kutoroka makwao siku ya Jumanne katika mji wa Gisenyi Magharibi mwa Rwanda kufuatia mitetemeko ya ardhi inayoshuhudiwa kwa siku ya nne baada ya mlipuko wa volkano nchi jirani ya DR Congo.
Kifaa cha kufuatilia matetemeko ya ardhi nchini Rwanda kimeripoti matetemeko ya ardhi yaliyofikia kiwango cha 5.3 na 5.1 katika vipimo vya richa Jumanne na Jumatano asubuhi.

Mamlaka nchini Rwanda imetoa wito wa utulivu na kusema kuwa imechukua hatua ya kuwasaidia watu waliyo katika hali ya hatari, baada ya nyumba kadhaa kuharibiwa.
Shule, benki, soko na maduka yamefungwa, huku watu wakilala nje usiku wa Jumanne kwa kuhofia nyumba zao kuporomoka na kuwaangukia.
Baadhi ya watu walionekana Jumatano asubuhi katika kituo kikuu cha usafiri wakijaribu kuondoka Gisenyi kuelekea maeneo ya mashariki.

Maelezo ya picha, Nyumba kadhaa ziliporomoka Hospitali katika mji huo zilihamisha baadhi ya huduma na wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika maeneo yam engine ya magharibi na kaskazini mwa Rwanda.
Bi Mwajuma Gakuru ameomba srikali imsaidie baada ya nyumba zake kuharibiwa katika mtetemeko wa ardhi wa Jumanne
“Hali ni mbaya sana, tuna hofu tangu (mlipuko wa volcano) Jumamosi,anhalia nyumba zangu, zote,tunaomba serikali itusaidie .” – alisema.
Kwa nini John Cena ameiomba radhi China?

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Muigizaji huyo wa filamu ya Fast and Furious 9 pia ameweka video mtandaoni kuomba msamaha Kichina Nyota wa WWE John Cena ameomba radhi China kwa kutambua Taiwan kama nchi.
Muigizaji huyo na mwanamieleka wa zamani wa WWE alitaja Taiwan kuwa nchi katika video ya biashara ya filamu ya hivi punde ya Fast and Furious.
Hatua hiyo iliikasirisha China ambayo inachukulia Taiwan inayojitawala kuwa chini ya himaya yake.
Bwana Cena ameweka video nyingike katika mitandao ya kijamii akizungumza Kichina kuomba radhi kwa "kosa" hilo.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Utata ulianza wakati Bwana Cena aliposema Taiwan itakuwa "nchi" ya kwanza kuweza kutazama Fast and Furious 9, katika mahojiano na kituo cha utangazaji cha Taiwan TVBS (kwa Kichina).
Jumanne, Bw Cena alichapisha video kwenye wavuti ya Wachina ya Weibo, akiomba msamaha kwa "kosa" hilo.
Kenya kupata chango ya Corona kutoka Sudan Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Sudan Kusini itasalia na dozi 52,000 ambazo zinatarajia kutumiwa kabla ya tarehe 18 mwezi Julai Kenya itapokea dozi 72,000 cha chanjo ya Covid-19 kutoka kituo cha Covax wiki hii.
Chanjo hizo zilisambazwa tena kutoka Sudan Kusini baada ya maafisa wa afya wa nchi hiyo kusema hawawezi kuzitumia kabla ya muda wake wa matumizi kumalizika.
Sudan Kusini ilipokea dozi 132,000 za chanjo ya Astra Zeneca kupitia mpango wa Covax mwishoni mwa mwezi Machi.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mayen Machout, aliwaambia waandishi wa habari kwamba hawana uwezo wa kutumia chanjo hizo zote kwasababu bunge ilichukua muda kuidhinisha matumizi yake.
“Pia tuligundua kuwa baadhi ya wahudumu wa afya hawakutaka kuchanjwa na muda mwingi ulitumiwa kuwaonesha watu jinsi ya kudunga chanjo ,” Dkt Machout alisema.
Sudan Kusini itasalia na dozi 52,000 ambazo zinatarajiwa kutumiwa kabla ya tarehe 18 mwezi Julai,ambao ndio muda wake wa mwisho wa matumizi, kulingana na Shirika la habari la AFP.
Mwezi Aprili, Sudan kusini ilisema ina mpango wa kutupa dozi 60,000 za chanjo ambazo muda wake wa matumizi umemalizika walizopokea kupitia msaada wa Muungano wa Afrika.
- Ukweli kuhusu hali ya mtu baada ya kupata chanjo ya Covid-19
- Je aina mpya za corona ndio sababu ya ongozeko kubwa la maambukizi India?
Kesi ya rushwa dhidi Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Chanzo cha picha, Reuters
Kesi ya ufisadi dhidi ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma inatarajiwa kuanza leo, baada ya kuahirishwa mara kadhaa.
Kiongozi huyo ambaye wakati mmoja aliwahi kusherehekewa kwa mapambanodhidi ya ubaguzi wa rangi anatarajiwa kukana mashtaka ya udanganyifu na ulaghai katika kesi ambayo ilianza na mkataba wa silaha miaka ya 1990.
Alidai kuwa mwathiriwa wa hujuma za kisiasa- na kwamba mahakama nchini humo zinashirikiana na mahasimu wake wa kisiasa.
Bwana Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.
Waafrika Kusini wanaamini kesi hiyo inaweza kuashiria mabadiliko ya nchi hiyo.
Baadhi ya mashujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini waliohai wamemshtumu Bw. Zuma– kumlinganisha na jambazi na kuonya itachukua muda mrefu kurekebisha uharibifu alioufanya dhidi ya taasisi changa za nchi.
- Aliyekuwa Rais Afrika Kusini Jacob Zuma anakabiliwa na 'kosa la kuidharau mahakamani '
Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatano 26.05.2021
