Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Weah ampongeza mwanawe kwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa

"Mimi mwenyewe kama mshindi wa taji la Ligue 1, nafahamu fika kwamba unahitaji kujitolea na kufanya kazi kwa bidii kila wiki ili kupata ushindi ,” Rais Wear alisema katika ujumbe uliowekwa katika tovuti yake rasmi ya urais.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  2. 'Mipasuko yaonekana ardhini Goma'

    Mipasuko miwili mikubwa imeonekana ardhini mjini Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, siku kadhaa baada ya Mlima Nyiragongo ulio karibu kulipuka, Shirrika la habari la AFP limeripoti.

    Mtiririko wa lava uliharibu mamia ya nyumba na zaidi ya watu 30 sasa wanasadikiwa kufariki baada ya mlipuko huo.

    Goma na maeneo yaliyo karibu imekuwa ikishuhudia msururu wa mitetemeko ya ardhi ntangu siku ya Jumamosi mlipuko ulipotokea.

    AFP inasema mmoja wa wanahabari wake ameona mipasuko miwili mikubwa, baadhi zikiwa na upana wa karibu senti mita 50cm katika maeneo mengine.

    Wakazi wa Goma wanahofia huenda kukatokea milipuko zaidi.

  3. Mkenya ashinda tuzo ya WHO kwa kutoa huduma ya uzalishaji wakati wa corona

    Daktari wa Kenya Jemimah Kariuki ameshinda tuzo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutokana na mchango wake wa "kuendeleza afya ya kimataifa".

    Mwaka jana, alisaidia kubuniwa kwa huduma inayofahamika kama Wheels for Life ambayo ilitoa usafiri wa bure kwa wanawake wajawazito ili wawezi kufika hospitali wakati wa marufuku ya kutotoka nje ili kudhibiti maambukizi ya corona.

    Wakati huo, polisi walikuwa wakiendesha msako mkali dhidi ya wale wanaokiuka amri ya kutotoka nje.

    Hali hiyo iliwafanya wanawake wengi kuhofia kutafuta huduma za matibabu

    Kupitia mtandao wake wa Twitte, Dkt Kariuki aliishukuru WHO kwa kumpatia tuzo ya Mkurugenzi Mkuu wa Afya Duniani na kuwapongeza wafanyakazi wenzake.

    "Kwa vijana katika jamii hii in ishara kwamba tunawezat," aliongeza.

  4. Facebook yazindua huduma ya uchangiaji damu nchini Tanzania

    Mtandao wa kijamii wa Facebook kwa ushirikianao na Huduma ya Kitaifa ya uchangiaji wa Damu nchini Tanzania (NBTS), imezindua huduma ya uchangiaji damu.

    Kulingana na Gazeti la The Citizen, mpango huo utasaidia kuinganisha NBTS na vituo saba vya uchangiaji damu nchini Tanzania.

    Katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo siku ya Jumanne, na meneja wa mawasiliano wa kanda ya Afrika Mashariki Janet Kemboi mpango huo utawawezesha watu kuwashirikisha marafiki na jamaa zao kujisajili ili wapate taarifa kuhusu utoaji damu.

    Tangu ilipozinduliwa mwaka 2004, NBTS imeondokana na mfumo wa kutegemea utoaji damu kupitia familia na kugeukia mfumo ambao unahamasisha watu kutoa damu kwa hiari.

    Soma zaidi:

    • Utoaji Damu: Ukweli kuhusu nani anaweza kuchangia damu
  5. Weah ampongeza mwanawe kwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa

    Rais wa Liberia mwanasoka wa zamani wa kimataifa George Weah amempongeza mtoto wake wa kiume, Timothy Weah, baada ya klabu yake ya Lille kushinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa.

    "Mimi mwenyewe kama mshindi wa taji la Ligue 1, nafahamu fika kwamba unahitaji kujitolea na kufanya kazi kwa bidii kila wiki ili kupata ushindi ,” Rais Wear alisema katika ujumbe uliowekwa katika tovuti yake rasmi ya urais.

    “Licha ya kuumia mara kadhaa na kucheza mechi 28 , hiki ni kitu ambacho kimekuwa ndoto ya Tim.

    “Tunashukuru kwamba akiwa mshambulizi wa kikosi chake , alichangia kwa kiwango kikubwa ufanisi wa Lille kuwa mabigwa kwa mara nyingine,” Bw. Weah aliongeza.

    Rais Weah alichezea klabu kadhaa za Ulaya, Ikiwemo Paris Sainte Germaine, Monaco, AC Milan, Chelsea na Manchester City kabla ya kustaa mwaka 2004 kwuenda kujitosa katika siasa za kitaifa.

    Mwaka 1995 alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa na hatimaye kuchaguliwa kuwa rais wa nchi yake mwaka 2017.

    Pia unaweza kusoma:

    • Tetesi za soka Ulaya Jumanne 25.05.2021: Sancho, Bale, Hazard, Alli, Lingard, Ramsey
  6. Siku ya Afrika yaadhimishwa leo

    Watu barani Afrika wanasherehekea Siku ya Afrika.

    Sherehe hizo zinazoadhimishwa kila mwaka ni ukumbusho wa siku ambapo Shirika la Umoja wa Afrika (OAU),ambalo sasa ni Muungano wa Afrika ulianzishwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, mwaka 1963.

    Nchi Zimbabwe, Rais Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuzindua sanamu ya Nehanda Charwe, maarufu Mbuya Nehanda, ambaye aliongoza mapinduzi ya miaka ya 1800.

    Muungano wa Afrika umekuwa ukuwa ukiweka mtandaoni dondoo za kuvutia kuhusu nchi 55 wanachama wake.

    Nchini Cameroon, Muungano huo uliangazia juhudi za mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo ambaye ameboresha huduma za afya nchini humo.

    Katika ujumbe wake, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza haja ya nchi za Afrika kudhibiti uhuru wao.

    "Kama mataifa ya Afrika, tunataka kujisaidia na wala sio kuambiwa ni kitu gani kizuri kwetu. Kanuni ya 'hakuna chochote kinachotuhusu kitakachojadiliwa bila sisi' inapaswa kutumika, "aliandika.

  7. Congo volcano: Mamia ya watoto waliopotea waokolewa

    Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef, linasema limewaokoa watoto 530 waliopotea baada ya kutenganishwa na wazazi wao walipokuwa wakitoroka mlipuko wa Volkano usiku wa JumamosiMashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Karibu nyumba 500 ziliharibiwa baada ya Mlima Nyiragongo, ambao uko sehemu ya Kaskazini mwa mji wa Goma, kulipuka.

    "Tulifanikiwa kuwapata karibu watoto 530 ambao walitenganishwa na wazazi wao na kufikia sasa tumewakutanisha 360 na wazazi wao," Afisa wa nyanjani wa Unicef mjini Goma Jean Metenier aliiambia BBC.

    Amesema kulikuwa na hali ya wasiwasi mlipuko ulipotokea usiku wa Jumamosi na karibu watu 25,000 walilazimika kuondoka maeneo yaliyoathirika zaidi.

    • Mlipuko wa Volkano Goma: ' Mume wangu alikuwa mgonjwa,sikuweza kumuokoa akaochomwa na lava'
    • Volkano: Milipuko hii ilisababisha maafa na uharibifu ambao haujawahi kutokea
  8. Bunge la Uganda lapata Spika mpya

    Jacob Oulanyah, Mbunge wa Kaunti ya Omoro Kaskazini mwa Uganda, ameteuliwa kuwa Spika wa Bunge la 11. Alishinda uchaguzi kwa jumla ya kura 310.

    Bw. Oulanyah anachukua nafasi ya Rebecca Kadaga, aliyekuwa Spika wa kwanza mwanamke nchini humo, ambaye alishikilia wadhifa huo kwa miaka 10. Pia alikuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 30.

    Kinyang'anyiro cha kutafuta Spika kilisababisha mvutano ndani ya chama tawala cha NRM, huku wakosoaji wa Kadaga wakisema ameshikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu.

    Wikendi iliyopita, chama hicho kilimuidhinisha Oulanyah, ambaye alikuwa naibu wa Kadaga kuwa mgombea wake katika kinyang'anyiro hicho. Kadaga pia alishiriki uchaguzi huo kwa kuzingatia uwezo wake binafsi lakini hakufanikiwa.

    Kufuatia uchaguzi wa mwezi Januari, Uganda sasa ina bunge kubwa zaidi la wajumbe 529.

    Wabunge pia watamchagua naibu wa Spika katika kikao chao cha kwanza ambacho kilifanyika katika Uwanja wa Uhuru wa Kololo, ili kudhibiti maambukizi ya corona.

    Soma zaidi:

    • Msichana aliyechekwa kwa kunuka shombo sasa ndiye mbunge mdogo zaidi Uganda
  9. Jinsi kuwabusu kuku kunavyoweza kueneza mlipuko wa bakteria

    Kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) kimewataka watu waache kuwabusu kuku hai huku kukiwa na mlipuko wa bakteria aina ya salmonella.Soma zaidi

  10. Umoja wa Mataifa wataka kuachiwa mara moja kwa Rais wa Mali Bah Ndaw

    Ujumbe amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali umeagiza kuachiwa huru mara moja kwa Rais wa Mali Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane, baada ya taarifa kuibuka kwamba wanazuiliwa na wanajeshi.

    Katika ujumbe wa Twitter ulioandikwa kwa Kifaransa, Minusma pia imetoa wito wa utulivu katika taifa hilo masikini la Afrika Magharibi.

    Kauli hiyo imetokana na ripoti kwamba Rais wa mpito Ndaw na Bw. Ouane walipelekwa na wanajeshi hadi kambi ya kijeshi ya Kati karibu na mji mkuu, Bamako.

    Hali ambayo ilizua wasi wasi wa kutokea kwa mapinduzi ya pili ndani ya mwaka mmoja nchini humo.

    Waziri wa Ulinzi Souleymane Doucouré pia ameripotiwa kuzuiliwa.

    Soma zaidi:

    • Mapinduzi ya kijeshi Mali: Je ni kina nani waliopanga na kutekeleza?
    • Mali: Kwa nini mapinduzi yanashangiliwa nyumbani, majirani wakilalamika

    Jumatatu jioni, Bw. Ouane aliliambia shirika la habari AFP kwa njia ya simu kwamba wanajeshi "walikuja kumchukua". Shirika hilo la habari baadaye ilisema mawasiliano ya simu baadaye yalikatizwa.

    Ripoti ya kuzuiliwa kwa viongozi hao ilikujua saa kadhaa baada ya serikali kufanya mabadiliko ambayo yalipelekea kuondolewa kwa maafisa wawili wa ngazi ya juu jeshini waliohusika katika mapinduzi ya mwaka jana.

    Kwa mara nyingine tena Mali inakabiliwa na hali ya msukosuko miezi tisatu baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa madarakani Rais Ibrahim Boubakar Keïta.

    Anasema kwamba baadhi ya raia wengi Mali waliunga mkono kuondolewa kwa Bw. Keita- lakini ghadhabu zilipanda tena kutokana na ongezeko la ushawishi wa jeshi katika serikali ya mpito na mwendo wa kinyonga wa mageuzi yaliyoahidiwa.

    Mapinduzi ya mwaka 2012 yalifanya wanamgambo wa Kiislam kuteka maeneo ya kaskazini mwa Mali.

    Vikosi vya Ufaransa vilisaidia kukomboa maeneo hayo lakini mashambulio yaliendelea.

  11. Chifu aamuru mwili wa Mugabe kufukuliwa na kuzikwa upya

    Kiongozi wa kitamaduni nchini Zimbabwe ameaamuru kwamba mabaki ya rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe yafukuliwe na kuzikwa katika makaburi ya kitaifa.

    Mugabe alifariki mwaka 2019 na alizikwa nyumbani kwake Kutama kulingana na ombi lake na wala sio katika makaburi ya mashujaa wa kitaifa katika mji mkuu, Harare, kama alivyotarajia mrithi wake Rais Emmerson Mnangagwa na wengine.

    Familia yake imesema Mugabe alikuwa ameelezea hofu yake kwamba mahasimu wake wa kisiasa waliomuondoa madarakani mwaka 2017 huenda wakatumia mabaki yake kufanya kafara ikiwa atazikwa katika makaburi ya kitaifa.

    Siku ya Jumatatu, chifu wa kitamaduni katika wilaya ya Zvimba, magharibi mwa mji mkuu wa Harare, alisema kwamba amepokea malalamishi kutoka kwa jamaa wa ukoo wa Mugabe kuhusu mahali alipozikwa.

    Aliamua kuwa Grace Mugabe alikuwa na makosa kwa kukiuka muongozo wa kimila kwa kumzika mume wake nyumbani kwake.

    Bi Mugabe hakufika mbele ya kikao hicho, lakini chifu alimpiga faini ya kulipa ng’ombe watano na mbuzi mmoja.

    "Yeye [chifu] hana mamlaka dhidi ya Kutama. Na hata kama chifu alifanya uamuzi sahihi tungelikata rufaa mahakamani," Leo Mugabe, msemaji wa familia, aliliambia shirika la habari la Reuters.

    • Je Robert Mugabe ni nani?
  12. Hujambo na karibu katika matangazo haya mubashara leo Jumanne 25.05.2021.