Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mbwa wa Joe Biden wafurushwa White House
Mbwa wanaomilikiwa na Rais wa Marekani Joe Biden na mke wake Jill Biden wameondolewa Ikulu ya White House baada ya mmoja wao, kwa jina Major, kuripotiwa kumuuma ajenti wa usalama.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Mwambusi arejeshwa Yanga
Klabu ya Yanga imemrejesha kikosini aliyekuwa kocha msaidizi wa Timu hiyo Juma Mwambusi, zikiwa ni siku chache toka kumtimua kocha wake Cedric Kaze. Mwambusi amepewa jukumu la kuwa kocha mkuu wa muda huku timu ikiendelea na mchakato wa kumsaka kocha mpya.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Mshindo Msolla amesema kuwa ‘‘tunatengemea mwalimu Mwambusi ataichukua timu wakati tunatafuta kocha mkuu hana ugeni na timu tulikuwa nae kwenye michuano ya kombe la mapinduzi kwa hiyo kurudi kwake sio jambo geni.’’
Mwenyekiti huyo wa Yanga amesema pia utaratibu wa kumpata kocha mkuu mpya kamati ya ufundi yabtimu hiyo inapokea wasifu wa makocha na kamati hiyo itaamua ni kocha yupi anafaa kuwanoa vijana wa Jangwani.
Oprah Winfrey: Maoni ya rangi ya ngozi "sio ya Malkia wala ya Mwanamfalme"
Oprah Winfrey amesema Mwanamfalme Harry alifafanua kwamba Malkia na mume wake Mwanamfalme Philip Mtawala wa Edinburgh hawakuhoji rangi ya ngozi ya mtoto atakapozaliwa.
Siku ya Jumatatu Winfrey, aliambia kituo cha habari cha CBS kwamba Mwanamfalme "hakutaja waliohusika katika mazungumzo hayo".
Taarifa kwamba baadhi ya wanafamilia walihoji "rangi ya ngozi" ya Archie itakavyokuwa ilifichuliwa katika mahojiano ya televisheni iliyopeperushwa nchini Marekani.
Mwanamfalme Harry Mtawala wa Sussex alielezea jinsi kauli hiyo ilivyomuathiri.
Soma zaidi:
- Meghan na Harry: Ubaguzi ndio sababu kubwa kwanini tuliondoka Uingereza
- Mahojiano ya Meghan na Harry: Mazungumzo ya dharura ya Ufalme yafanyika juu ya madai ya ubaguzi
Wakazi wa Cabo Delgado walalamikia ukosefu wa usalama
Wakazi wa mkoa wa Cabo Delgado nchini Msumbiji, wamelalamikia vikosi vya usalama kutowapa ulinzi wa kutosha dhidi ya mashambulio kutoka kwa wanamgambo wa Kiislamu.
Karibu jamii 10 zimeathiriwa ndani ya wiki mbili zilizopita, huku baadhi ya vijiji vikishambuliwa mara kadhaa.
Wanasema majeshi ya Msumbiji yamekataa kuwasaidia kwasababu hawajaidhinishwa na makamanda wao.
Mkuu wa majeshi amesema wakazi wa mji wa bandari wa Mocimboa da Praia, ambao ulitekwa na wanamgambo mwaka jana, watarejea makwao hivi karibuni.
Mamia ya watu wameuawa, maelfu ya wengine kutoroka makwao katika kipindi cha miaka mitatu iliopita kufutia ghasia zilizotokea kaskazini mwa Msumbiji.
Soma zaidi:
- Msumbiji: Je, Cabo Delgado ni kituo cha wapiganaji wa Islamic State?
- Msumbiji kuchunguza video ya kutisha kuhusu mauaji
Mbwa wa Joe Biden wafukuzwa White House
Mbwa wanaomilikiwa na Rais wa Marekani Joe Biden na mke wake Jill Biden wameondolewa Ikulu ya White House baada ya mmoja wao, kwa jina Major, kuripotiwa kumuuma ajenti wa usalama.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, mbwa hao aina ya 'German shepherd' wamepelekwa nyumbani kwa Biden huko Wilmington, Delaware.
Hii ni kutokana na ukali wa Major dhidi ya wafanyakazi wa White House.
Bw. Biden na familia yake walimuasili Major mwaka 2018. Alikuwa mbwa wa kwanza kutoka makao ya wanyama kuishi katika Ikulu ya Marekani.
Mbwa wao, Champ, ana miaka 13.
Tazama mtoto wa miaka sita mwenye kipaji cha hesabu Tanzania
Charles Mmbeba ambaye hajui kusoma wala kuandika ni mwanafunzi wa darasa la awali kwenye shule ya msingi Nyingwa iliyoko wilayani Morogoro mashariki mwa Tanzania.
DRC:Marekani yamwekea tena vikwazo tajiri wa Israel
Marekani imebadili uamuzi wa kulegeza kwa muda, vikwazo dhidi ya bilionea wa Israel Dan Gertler, anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi unaohusisaha biashara ya madini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hatua hiyo ya hivi punde inabatilisha uamuzi uliotolewa siku za mwisho za utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Mwaka 2017 na 2018, hazina ya Marekani iliweka vikwazo dhidi ya Bw. Gertler – ambayo ilimzuia kufanya biashara na raia wa nchi hiyo na taasisi zake, hatua ambayo ilimzuia kupata huduma za benki za kimataifa.
Ilimtuhumu kwa ufisadi na ukiukaji wa maadili katika sekta ya madini na kutumia ushirikiano wake na rais wa zamani wa DR Congo,Joseph Kabila kupata mikataba ya kibiashara.
Bw. Gertler amekana kufanya makosa yoyote.
Utawala wa Trump ulikua umemuondolea vikwazo Bw. Gertler kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Januari 31, mwka 2022, kuendelea kufanya biashara na kampuni za Marekani.
Soma zaidi:
Simba wamshambulia na kumuua afisa wa wanyamapori Afrika Kusini
Mtu mmoja amefariki baada ya kushambuliwa na simba wawili katika hifadhi ya wanyama nchini Afrika Kusini, mamlaka zimesema siku ya Jumatatu.
Malibongwe Mfila, 27, ambaye alifanya kazi ya kufuatilia mienendo ya wanyama katika mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Marakel,amekuwa akiwatafuta wanyama katika mbuga hiyo siku ya Jumamosi aliposhambuliwa na simba hao.
Polisi wanasema alikuwa akiendesha gari kuwatafuta wanyama kama vile simba na tembo ili kutoa ushauri kwa wanaowaelekeza watalii mbugani.
Aliamua kuacha gari na kuendelea kuwatafuta wanyama kwa miguu "mara ghafla akashambuliwa na simba wawili hadi akafariki," polisi waliongeza.
Simba hao pia waliuawa kwa kupigwa risasi.
Mwaka jana mtunzaji mashuhuri wa Afrika Kusini Mathewson Magharibu, alifariki baada ya kushambuliwa na simba alipokuwa akiwapeleka matembezi wageni katika hifadhi ya wanyama ya Limpopo.
Mmarekani aliyevamia bunge ashtakiwa baada ya kufukuzwa Kenya
Mwanamume anayehusishwa na maandamano ya ghasia dhidi ya Bunge la Marekani amefikishwa katika mahakama mjini New York siku ya Jumatatu baada ya kufurushwa kutoka Kenya wikendi, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari.
Isaac Sturgeon alikamatwa na maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F. Kennedy huko New York.
Amekuwa akiishi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki tangu Januari 24, kulingana na nyaraka za mahakamani.
Alikuwa anapanga kurudi Marekani mwezi Aprili.
Isaac Sturgeon anatuhumiwa kuvamia bunge la Marekani mwezi Januari.
Idadi ya vifo katika mlipuko Equatorial Guinea yaongezeka hadi 98
Idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko mkubwa nchini Equatorial Guinea siku ya Jumapili imeongezeka hadi 98, maafisa wanasema
Mlipuko huo ulitokea katika kambi ya jeshi mjini Bata.
Maafisa wanasema mlipuko huo ulitokana na silaha ambazo zilihifadhiwa vibaya ambayo ilichomeka baada ya moto uliowashwa na wakulima katika shamba lililokuwa karibu.
Idadi ya waliofariki iliongezeka baada ya wadumu wa kujitolea kuchukua karibi siku nzima kutafuta miili katika vifusi. Awali ilikadiriwa ni watu 31 pekee ndio waliofariki kutokana na mkasa huo.
Watoto wadogo watatu walipatikana wakiwa hai na kupelekwa hospitali.
Karibu mijengo yote na nyumba za makazi katika mji huo ''ziliharibiwa vibaya'' na mlipuko huo, Rais Teodoro Obiang Nguema alisema.
Katika taarifa, Rais Obiang Nguema alisema mlipuko huo ulisababishwa na "uzembe" uliohusishwa na hifadhi ya baruti kali katika kambi ya kijeshi ya Nkoantoma.
Mambo matano muhimu kuhusu EquatorialGuinea:
- Ni nchi pekee barani Afrika inayozungumza Kihispania na ilipata uhuru wake kutoka kwa Uhispania 1968
- Imegawanywa katika sehemu ya bara na kisiwani, uliopo mji mkuu wa Malabo
- Rais Obiang Nguema, amekuwa madarakani tangu mwaka 1979, na amelaumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.
- Maafisa wa nchi za Ulaya na mashirika yasiokuwa ya kiserikali yamemlaumu rais na familia yake kwa kujihusisha na ufisadi.
- Licha ya kuwa na utajiri wa mafuta na gesi asilimia 76, watu milioni 1.5 wanaishi katika hali ya umasikini, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia.
Karibu katika matangazo mubashara leo Jumanne 09.03.2021