'Vuguvugu pingamizi' la Raila sio halali asema waziri
Waziri wa usalama na masuala ya ndani,Fred Matiang'i ameiita vuguvugu pingamizi dhidi ya serikali,NRM kuwa 'kikundi cha wahalifu' gazeti binafsi la Nation limesema
'Matiang'i atangaza NRM kuwa kikundi cha uhalifu akinukuu kipengele cha 22 cha sheria ya uhalifu uliopangwa ya 2010' limesema gazeti hilo katika akaunti yake ya Twitter
Wakati huo huo Raila ametoa chapisho la 'kiapo' alilokisoma mapema leo. Nakala ya chapisho hilo imetiwa saini na Raila Odinga pamoja na wakili wake