Kuapishwa kwa Raila Odinga Kenya

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Bwana Raila Odinga amejiapisha kuwa rais wa wananchi, huku serikali ikifungia baadhi ya vituo vya habari vilivyokuwa vinapeperusha matangazo moja kwa moja.

Moja kwa moja

  1. 'Vuguvugu pingamizi' la Raila sio halali asema waziri

    Waziri wa usalama na masuala ya ndani,Fred Matiang'i ameiita vuguvugu pingamizi dhidi ya serikali,NRM kuwa 'kikundi cha wahalifu' gazeti binafsi la Nation limesema

    'Matiang'i atangaza NRM kuwa kikundi cha uhalifu akinukuu kipengele cha 22 cha sheria ya uhalifu uliopangwa ya 2010' limesema gazeti hilo katika akaunti yake ya Twitter

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Chapisho la 'Kiapo'

    Chanzo cha picha, Raila Odinga/Twitter

    Maelezo ya picha, Chapisho la 'Kiapo'

    Wakati huo huo Raila ametoa chapisho la 'kiapo' alilokisoma mapema leo. Nakala ya chapisho hilo imetiwa saini na Raila Odinga pamoja na wakili wake

  2. Wadhifa wa Odinga Twitter wabadilishwa

    Wadhifa wa Odinga ya badilishwa kuwa "Rais wa Kenya" katika ukurasa wake wa Twitter.

    'Hii ni ukurasa rasmi wa mheshimiwa Raila Amolo Odinga, Rais wa Jamhuri wa Kenya' imesema.

    Akaunti ya Twitter ya Raila Odinga

    Chanzo cha picha, Twitter

    Maelezo ya picha, Akaunti ya Twitter ya Raila Odinga
  3. Odinga: "Nawashukuru Wananchi wa Kenya"

    Bw Odinga kupitia mtandao wa jamii wa Twitter amewashukuru Wakenya kwa 'kumpatia mamlaka na kumuani'

    Amesema 'mlijitokeza kutoka kila kona ya wa taifa kushuhudia kuapishwa kwangu.Ni vizuri kuwaona mkijitokeza kwa mamilioni'

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Odinga: 'Tumetimiza ahadi yetu'

    Maneno ya Raila alipojiapisha katika uwanja wa Uhuru Park

    Chanzo cha picha, Raila Odinga/Twitter

    Maelezo ya picha, Maneno ya Raila alipojiapisha katika uwanja wa Uhuru Park
  5. Upinzani washerehekea kuapishwa kwa Odinga

    Shangwe na nderemo zinaendelea katika maeneo ya Kisii na Homa Bay, magharibi mwa Kenya ambayo ni maeneo ya ngome za upinzani.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2

    Mwisho wa X ujumbe, 2

  6. Raila aapishwa bila wenzake

    Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameapishwa kuwa rais wa wananchi.

    Kiapo hicho alilishwa na mbunge wa Ruaraka TJ Kajwang.

    Hatahivyo wakuu wa chama hicho akiwemo Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula hawakuwepo wakati wa kiapo hicho kilichochukuliwa katika eneo la Uhuru Park

    Raila Odinga na naibu wake Kalonzo Musyoka katika picha ya awali

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Raila Odinga na naibu wake Kalonzo Musyoka katika picha ya awali
  7. Raila aondoka uwanja wa Uhuru Park

    Punde tu alipofika na 'kula kiapo' Raila Odinga ameondoka.

    Wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu na ghamu, bila kutegemea kwamba atachukua muda mfupi hivyo.

    Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ' si mapinduzi ya serikali'

  8. Odinga akula kiapo uwanja wa Uhuru Park

    Raila Odinga amefika katika pamoja na viongozi kadha wakuu wa NASA na kujiapisha akishika Biblia.

    Amewaambia kuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.

    Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika wuanja huo.

    Bw Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.

    "Hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya"

    "Maelekezo mengine mtayapata baadae"

    Raila 'akula kiapo'

    Chanzo cha picha, KTN Youtube

    Maelezo ya picha, Raila 'akula kiapo'
  9. Habari za hivi punde, Odinga aingia uwanjani na kujiapisha kuwa rais wa wananchi

    Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameingia Uhuru Park na moja kwa moja akainua Biblia na kula kiapo kama kiongozi wa wananchi wa Kenya.

  10. Wengi wajitokeza kushuhudia Odinga 'akila kiapo'

    Baada ya polisi kuondoka uwanja wa Uhuru Park, wafuasi wa upinzani walianza kuingia kwa wingi na kwa sasa maelfu wamo ndani.

    Hizi hapa ni baadhi ya picha za hali ilivyo sasa:

    Umati
    Umati
    Wahudumu wa bodaboda wanaonekana wakiwa wameegesha pikipiki zao nje ya uwanja
    Maelezo ya picha, Wahudumu wa bodaboda wanaonekana wakiwa wameegesha pikipiki zao nje ya uwanja
    Waziri wa zamani Prof Sam Ongeri (pili kulia) ni miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu waliofika uwanjani
    Maelezo ya picha, Waziri wa zamani Prof Sam Ongeri (pili kulia) ni miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu waliofika uwanjani
  11. Odinga bado anasubiriwa Uhuru Park

    Afisa mkuu mtendaji wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) Norman Magaya alikuwa amesema Bw Odinga, na viongozi wengine wa muungano huo wangewasili uwanjani katika muda wa dakika 40 hivi.

    Sasa hivi ni saa moja inaelekea kupita tangu wakati huo:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  12. Odinga: Tunachokifanya si mapinduzi ya serikali

    Odinga

    Bw Raila Odinga amezungumza na kituo cha habari cha KTN kwa njia ya simu ambapo amesisitiza kwamba Rais Uhuru Kenyatta hakuchaguliwa kwa njia halali.

    Alipoulizwa anni atamwapisha, amesema: "Ngoja uone” na akasisitiza kwamba wanachokifanya leo kina msingi wake katika sheria na si mapinduzi.

    “Hatutambui uchaguzi wa Oktoba 26 (uchaguzi wa marudio ambao Odinga alisusia), zaidi ya asilimia 86 ya Wakenya hawakushiriki. Tuna serikali ambayo si halali ambao inajidai kuwa mamlakani,” amesema.

    Kuhusu taarifa kwamba amepokonywa walinzi, amesema: "Walinzi wangu waliondolewa muda mrefu sana uliopita. Najihisi kuwa hatarini ndio lakini watu raia ndio usalama wangu.”

    Bw Odinga ameitaka serikali kutotumia nguvu kuusambaratisha mkutano wa leo.

    "Wafuasi wangu wamo safarini kuelekea Canaan. Safari yetu ni halisi na haiwezi kuzuiwa.

  13. Odinga: Kufungwa kwa vyombo vya habari inasikitisha

    Raila Odinga alisema wataendelea na sherehe ya kuapishwa

    Chanzo cha picha, KTN YOUTUBE

    Maelezo ya picha, Raila Odinga alisema wataendelea na sherehe ya kuapishwa

    Raila Odinga azungumza na vyombo vya habari dakika chache kabla ya kuelekea ‘kuapishwa’.

    Akizngumza kwa njia ya simu na kituo cha habari cha KTN, Odinga amesema kuwa hawakutarajia kufungwa kwa vyombo vya habari.

    Ni hali ya ‘kusikitisha’ na ‘inaonesha kuwa tumefika kiwango cha Uganda.'

    Alipoulizwa nani haswa atamuapisha, Odinga alijibu ‘ngoja uone.’

    Alielezea kuwa shughuli yao ni halali na haikiuki katiba. Pia amesema haamini kwamba wanachokifanya si mapinduzi ya serikali.

  14. Gavana wa Mombasa aelekea Uhuru Park

    Gavana wa Mombasa Hassan Joho, mmoja wa viongozi wa chama cha ODM chake Bw Odinga, ni miongoni mwa viongozi ambao wamefunga safari kuelekea uwanja wa Uhuru Park.

    Kupitia Twitter, amesema ameandamana na viongozi wengine wa kaunti hiyo ya pwani.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  15. Polisi watumia gesi ya kutoa machozi Nairobi

    Polisi wameripotiwa kutumia geis ya kutoa machozi dhidi ya wafuasi wa upinzani waliokuwa wakielekea katika uwanja wa Uhuru Park, kupitia barabara ya Uhuru Highway.

  16. Maandalizi kwenye jukwaa yaanza Uhuru Park

    Maandalizi kwenye jukwaa kuu uwanja wa Uhuru Park yameanza, na viti vimeanza kupangwa.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  17. Kwa Picha: Wafuasi wa upinzani na mbwembwe zao

    Wafuasi wa upinzani wanaendelea kuingia uwanja wa Uhuru Park, baadhi wakiwa wamevalia mavazi yenye ujumbe. Wengine wamevalia kuonyesha uzalendo na wengine utiifu wao kwa Bw Odinga.

    Tazama hali ilivyo kupitia picha hizi za waandishi wetu David Wafula na Peter Njoroge.

    Kujivunia
    Maelezo ya picha, 'Najivunia kuwa Mkenya', ndivyo vazi la mwanamke huyu lisemavyo.
    Machozi
    Maelezo ya picha, Huyu amefungia bomu la kutoa machozi kwenye fulana yake

    Fomu 34A na 34B za matokeo vituoni na katika ngazi ya maeneo bunge zilikuwa na utata wakati wa uchaguzi. Mwanamume huyu akaamua kujipamba na 34A na 34B. Na ana ujumbe pia wa Canan Direct - kuashiria matumaini ya kwenda nchi ya ahadi.

    Fomu 34A
    Gor Mahia
    Maelezo ya picha, Kiongozi anahitaji ulinzi kupitia jeshi. Kenya kuna Majeshi ya Ulinzi ya Kenya (KDF) lakini huyu ni wa K'Ogalo Defence Forces (KDF). Anaashiria kwamba pia ni shabiki wa klabu ya Gor Mahia ambayo hufahamika kama K'Ogalo
    Nasa
  18. Vituo vya habari vyafungiwa matangazo Kenya

    Baadhi ya vituo vya redio na televisheni vya Royal Media Services (RMS), vikiwemo runinga ya Citizen TV, vimefungiwa matangazo pamoja na kituo cha televisheni cha NTV kinachomilikiwa na kampuni ya Nation Media Group (NMG) katika baadhi ya maeneo.

    Vituo hivyo vimekuwa vikipeperusha matangazo kuhusu sherehe iliyopangiwa kufanyika leo ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga.

    Serikali ilikuwa imetahadharisha vituo vya habari Kenya dhidi ya kupeperusha moja kwa moja hafla hiyo.

    Mmoja wa wahariri wakuu wa Citizen Peter Opondo ameambia BBC kwamba maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) kwamba polisi wakiandamana na polisi walivamia vituo vya kupeperushia matangazo na kuzima matangazo.

    Citizen TV ndicho kituo cha runinga kinachoongoza Kenya. Matangazo ya kituo cha NTV yanapatikana pekee kupitia ving'amuzi vya kulipia.

    Kituo kingine kikubwa KTN bado kinarusha matangazo.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  19. Wafuasi wa upinzani waliozuiliwa Voi waachiliwa

    Wafuasi wa upinzani waliokuwa wanasafiri kuelekea Nairobi ambao walizuiliwa awali mjini Voi wameachiliwa na kuruhusiwa kuendelea na safari.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  20. Hali ilivyo uwanjani Uhuru Park

    Mwandishi wetu David Wafula yupo uwanja wa Uhuru Park ambapo upinzani umepanga kumuapisha Raila Odinga kuwa kiongozi wa Kenya baadaye leo.

    Tazama hali ilivyo: