Jake Paul amchapa kirahisi Mike Tyson katika pambano la uzito wa juu

Mike Tyson alipiga ngumi 18 pekee katika shindano hilo la dakika 16, ikilinganishwa na 78 kutoka kwa Jake Paul.

Muhtasari

  • Kimbunga cha sita ndani ya mwezi mmoja chakumba Ufilipino
  • Katika Picha: Kuanguka kwa jengo Kariakor
  • Zelensky asema vita 'vitamalizika mapema' Trump akiwa rais
  • Mwanaume aliyemuua mwanafunzi anayeshiriki mapenzi ya jinsi moja afungwa maisha
  • Tanzania: Jengo languka eneo la kibiashara Kariakoo
  • Walioteuliwa mawaziri la Trump wanakabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu
  • Taylor azomea katika ushindi wa pointi finyu dhidi ya Serrano
  • Paul amshinda Tyson kwa urahisi katika pambano la uzani wa juu

Moja kwa moja

Ambia Hirsi & Munira Hussein

  1. Kimbunga cha sita ndani ya mwezi mmoja chakumba Ufilipino

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kimbunga kikubwa ambacho kinaweza kusababisha maafa kimetua Ufilipino - kimbunga cha sita kukumba nchi hiyo ndani ya mwezi mmoja.

    Man-Yi, anayojulikana kama Pepito, kilitua saa tatu na dakika arubaini saa za ndani (13:40 GMT) kwa kasi ya juu ya upepo ya kilomita 195 kwa saa kwenye ufuo wa kisiwa cha Catanduanes mashariki, mamlaka ya utabiri ya hali ya hewa alisema.

    Imeonya kuhusu "kuongezeka kwa dhoruba ya kutishia maisha", mvua kubwa na upepo mkali, na maelfu ya watu wamehamishwa kabla ya kutua kwa kimbunga hicho.

    Takriban watu 160 wanaaminika kufariki kutokana na dhoruba tano za awali.

  2. Katika Picha: Kuanguka kwa jengo Kariakoo

    xx

    Watu watano wamefariki dunia, na zaidi ya 40 kujeruhiwa katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam, nchini Tanzania.

    Shughuli ya uokoaji inaendelea huku wananchi wakishirikiana na vyombo vya dola ikiwemo jeshi la Zimamoto.

    xx
    xx
    xx
  3. Raia wa Gabon wanapiga kura maoni kuhusu marekebisho ya katiba

    xx

    Chanzo cha picha, REX/SHUTTERSTOCK

    Raia wa Gabon wanapiga kura ya maoni ya kuidhinisha katiba mpya ambayo katika hatua ambayo inaonekana kuwa muhimu ya kurejesha maisha ya utawala wa kiraia katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

    Upigaji kura ulianza mwendo wa saa moja asubuhi kwa saa za ndani katika vituo 2800 vya kupigia kura ili kupigia kura ya ndiyo au hapana rasimu ya katiba mpya.

    Kura hiyo ya maoni inaonekana kuwa hatua muhimu zaidi katika mchakato ulioanzishwa baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Agosti 2023.

    Rais wa mpito Brice Oligui Nguema alichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka jana, na kumuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Ali Bongo ambaye alikuwa ameshinda uchaguzi wa marudio.

    Wanajeshi walivunja taasisi na kuunda bunge la mpito.

    Uchaguzi umepangwa kufanyika Agosti 2025, na Jenerali Nguema anaweza kugombea, kulingana na baadhi ya wachambuzi wa kisiasa.

    Katiba mpya ikipitishwa itampa mamlaka ya kushindana.

    Wanaounga mkono katiba inayopendekezwa ya wanasema rasimu ya hiyo ya sheria inawakilisha kujiondoa kwenye utawala wa miaka 55 wa familia ya Bongo.

    Lakini wakosoaji wanasema inaweza kumpatia rais madaraka makubwa zaidi, na wanahofia hatua hiyo inaweza kumuingiza madarakani mtawala mpya.

    Chini ya rasimu ya sheria iliyopendekezwa, marais wangechaguliwa moja kwa moja na wananchi kuhudumu mihula miwili ya miaka saba badala ya miaka mitano kama ilivyo katika katiba ya sasa.

    Soma pia:

  4. Zelensky asema vita 'vitamalizika mapema' Trump akiwa rais

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

    Chanzo cha picha, Getty

    Maelezo ya picha, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema ana uhakika kwamba vita na Urusi "vitamalizwa mapema" mara tu Donald Trump atakapokuwa rasmi rais wa Marekani.

    Zelensky alisema amekuwa "mazungumzo mazuri" na Trump kwa njia ya simu baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa Marekani.

    Hakusema kama Trump alitoa tamko lolote kuhusu uwezekano wa kufanya mazungumzo na Urusi, lakini alisema hakusikia chochote kutoka kwake ambacho kilikuwa kinyume na msimamo wa Ukraine.

    Trump amekuwa akisema mara kwa mara kipaumbele chake ni kumaliza vita na kuacha kile anachosema ni kutumia vibaya rasilimali za Marekani, kupitia msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

    “Bila shaka vita hivyo vitamalizika mapema kwa sera za utawala mpya katika Ikulu ya White House. Huu ni mtazamo wao, ahadi yao kwa raia wao,” Zelensky alisema katika mahojiano na chombo cha habari cha Ukraine.

    Aliongeza kuwa Ukraine "lazima tufanye kila linalowezekana kumaliza vita hivi mwaka ujao, kwa njia ya kidiplomasia".

    Hali kwenye uwanja wa vita ni ngumu, na vikosi vya Urusi vinasonga mbele, Zelensky alisema.

    Pia unaweza kusoma:

  5. Mwanaume aliyemuua mwanafunzi, mpenzi ya jinsi moja afungwa maisha

    Samuel Woodward

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Samuel Woodward

    Mwanaume wa California aliyepatikana na hatia ya kumuua, mwanafunzi wa Kiyahudi wa chuo kikuu nchini Marekani katika uhalifu wa chuki amehukumiwa kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa kuachiliwa huru.

    Samuel Woodward, 27, alishitakiwa mwezi Julai kwa kifo cha 2018 cha Blaze Bernstein, 19, ambaye Woodward alimchoma kisu zaidi ya mara 28 usoni na shingoni kabla ya kuuzika mwili wake.

    Baada ya uchunguzi wa wiki nzima, polisi walipata mwili wa Bernstein katika bustani ya Lake Forest, takriban kilomita 70 kusini-mashariki mwa Los Angeles.

    Wakati wa kesi hiyo, waendesha mashtaka walisema Woodward alikuwa akishirikiana na kundi la Wanazi mamboleo wenye msimamo mkali, Kitengo cha Atomwaffen, na walimshtaki kwa kuwanyanyasa mtandaoni wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsi.

    Usikilizaji wa hukumu ulicheleweshwa kwa saa kadhaa, kwa sababu Woodward alikataa kutoka kwenye seli yake.

    Soma pia:

  6. Tanzania: Watu watano wafariki baada ya jengo kuporomoka Kariakoo

    XX

    Watu watano wamefariki dunia, na zaidi ya 40 kujeruhiwa katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam, nchini Tanzania.

    Shughuli ya uokoaji inaendelea huku wananchi wakishirikiana na vyombo vya dola ikiwemo jeshi la Zimamoto.

    Kuna hofu huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka

    Kwa mujibu wa mashuhuda walionukuliwa na Gazeti la Mwanachi ghorofa hilo lilianguka ghafla majira ya saa tatu asubuhi wakati mafundi wa ujenzi walipokuwa wakiendelea na shughuli ya kuongeza maduka.

    ''Tunawasihi wananchi kutulia kwani tupo imara na tunaendelea na jitihada za uokoaji kwa kushirikiana na vyombo vingine,'' alisema Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Naibu Kamishna Puyo Nzalayaimisi.

    Wahanga hao wamepelekwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili iliyopo jirani na eneo la Kariakoo.

    Prof. Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema: ''Majeruhi wote wamepata huduma na tumewaruhusu, kwa sasa tuna majeruhi saba tu.”

    Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa walioathirika na mkasa huo.

    xx

    Chanzo cha picha, Calvin Nkya

    xx

    Chanzo cha picha, Calvin Nkya

  7. Walioteuliwa mawaziri na Trump wanakabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu

    Trump

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais Mteule wa Marekani Donald Trump

    Baadhi ya wateule wa baraza la mawaziri la Rais mteule wa Marekani Donald Trump wanakabiliwa na uchunguzi mkali, ikiwa ni pamoja na madai ya utovu wa nidhamu.

    Pete Hegseth aliyeteuliwa kuwa waziri wa ulinzi anakanusha madai ya unyanyasaji wa kijinsia na huku mwanasheria mkuu mtarajiwa Matt Gaetz akikabiliwa na uchunguzi wa maadili.

    Robert F Kennedy Jr, aliyeteuliwa na Trump kuwa waziri wa afya anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusiana na msimamo wake juu ya chanjo.

    Trump atahitaji Baraza la Seneti la Marekani kuwaidhinisha baraza lake la mawaziri atakapoingia madarakani mwezi Januari mwakani.

    Baraza hilo litadhibitiwa na Warepublican wenzake, wateule wake katika baraza la mawaziri watakabiliwa na maswali magumu wakati wa vikao vya pande mbili.

    Maelezo zaidi:

  8. Taylor azomea katika ushindi wa pointi finyu dhidi ya Serrano

    Katie Taylor (kulia) alishinda kwa uamuzi wa pamoja licha ya shindano la karibu sana

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Katie Taylor (kulia) alishinda kwa uamuzi wa pamoja licha ya pambano kali

    Bondia Katie Taylor wa Ireland alizomewa alipofanikiwa kuhifadhi taji lake la uzani wa light-welter kwa kushinda pointi tata dhidi ya Amanda Serrano katika Uwanja wa AT&T mjini Texas.

    Wawili hao walitifikia kiwango kingine cha hali ya juu katika mechi yao ya marudiano, huku Serrano akijibu bila kuchoka na ngumi za Taylor.

    Taylor alitumia kichwa chake mara kwa mara kujikinga, hatua ambayo ilimtatiza vibaya Serrano katika raundi ya nne matokeo athari hizo yakijitokeza baadaye kwenye pambano huku damu ikimwagika usoni mwa bondia huyo wa Puerto Rico.

    Serrano mwenye umri wa miaka 38 alipewa pointi moja kwa kupigwa kichwa katika mechi ya nane, jambo ambalo liliwashawishi waliohudhuria kuwa Serrano alikuwa amefanya vyema kulipiza kisasi kwa kupoteza pointi karibu 2022.

  9. Jake Paul amchapa kirahisi Mike Tyson katika pambano la uzito wa juu

    Tyson na Paul

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanamasumbwi Jake Paul aliacha doa la kudumu kwenye urithi wa ndondi wa bingwa mara mbili wa uzito wa juu Mike Tyson kwa kushinda kupitia uamuzi wa pamoja mbele ya mashabiki 70,000 Texas - na kufuatiliwa na mamilioni ya watu waliotazama pambano hilo kupitia Netflix.

    Jake Paul na Mike Tyson walikwenda raundi zote nane, huku Paul akiibuka mshindi kupitia uamuzi wa pamoja.

    Mara tu baada ya pambano hilo, Paul alikuwa mnyenyekevu kuhusu ushindi wake, akisema, "Kwanza kabisa, Mike Tyson ... ni heshima kubwa. Mike, yeye ni mkongwe, nimetiwa moyo naye, na tusingekuwa hapa leo bila yeye.”

    Tyson alizungumza juu ya uchezaji wake, akisema, "Sikutaka kuthibitisha chochote kwa yeyote ila nina furaha."

    Pia alitoa kongole kwa Paul kama mwanariadha, akisema, "Yeye ni mpiganaji mzuri sana."

    Mike Tyson sasa ameshindwa mara saba kwenye rekodi yake ya kitaaluma.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 58, anayeshindana kwa mara ya 59, amepoteza mapambano yake matatu ya mwisho, ingawa mara ya mwisho alipanda ulingoni katika nafasi ya kitaaluma kabla ya usiku wa leo ilikuwa mwaka 2005.

    Kwa upande wa Paul huu ni ushindi wa 11 Kati ya mashindano 12 aliyowahi kufanya.

    Soma pia:

  10. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja.