Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Trump: Tutafanya uamuzi haraka kuhusu kuishambulia Yemen

Trump ametoa kauli hii baada ya shambulizi kubwa kufanyika Jumamosi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa King Khalid, mjini Riyadh na kuua watu wasiopungua 12 na kujeruhi wengine 309.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Yusuph Mazimu

  1. Tetesi za soka Ulaya: Liverpool yamtaka Kounde, Chelsea yamfuatilia Camara

    Liverpool inatajwa kuwa na nia ya kumsajili beki wa Barcelona na timu ya taifa ya Ufaransa, Jules Kounde, huku klabu hiyo ya Hispania ikiripotiwa kuwa tayari kupokea ofa ya pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo. (Fichajes - kwa Kihispania)

    Chelsea bado inamtaka kiungo wa Monaco na timu ya taifa ya Senegal, Lamine Camara, mwenye umri wa miaka 22, baada ya kushindwa kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi. Hata hivyo, Chelsea haiko tayari kulipa euro milioni 70 (pauni milioni 59) zinazotakiwa na Monaco kwa ajili ya mchezaji huyo. (Goal)

    Liverpool pia inatajwa kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil, William Gomes, mwenye umri wa miaka 20, anayekipiga Porto. Klabu hiyo ya Ureno imeongeza kipengele cha kuvunja mkataba wa mchezaji huyo hadi euro milioni 100 (pauni milioni 85), huku Liverpool ikionyesha nia ya kumsajili. (A Bola - kwa Kireno)

    AC Milan bado inamfuatilia kiungo wa Bournemouth, Alex Scott, mwenye umri wa miaka 23, licha ya thamani yake kuongezeka. Scott, ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya England, anaendelea kuvutia klabu hiyo ya Italia. (Tuttomercatoweb - kwa Kiitaliano)

    Bayern Munich imefanya mazungumzo mapya kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Manchester United, JJ Gabriel, mwenye umri wa miaka 16, lakini bado haijatoa ofa. Hata hivyo, Barcelona na Real Madrid zinaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili kijana huyo, ambaye anadaiwa kuvutiwa zaidi na uwezekano wa kuhamia Hispania. (Sky Sports Germany)

    Manchester City ilifanya mawasiliano na Borussia Dortmund katika dirisha la majira ya kiangazi kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Marekani, Mathis Albert, mwenye umri wa miaka 17. (Goal)

  2. Trump: Tutafanya uamuzi haraka kuhusu kuishambulia Yemen

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema anafikiria uwezekano wa nchi yake kujiunga na Saudi Arabia katika mashambulizi dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen, baada ya shambulizi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa King Khalid, mjini Riyadh, kuua watu wasiopungua 12 na kujeruhi wengine 309.

    Trump amesema Marekani itafanya uamuzi huo haraka, akieleza kuwa utawala wake ulikuwa umepata taarifa kuhusu shambulizi hilo muda mfupi kabla ya kutoa kauli hiyo. Miongoni mwa waliouawa ni raia mmoja wa Marekani.

    Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Saudi Arabia imesema waliouawa pia ni pamoja na raia wanne wa Saudi Arabia, Wabangladeshi wawili na raia mmoja mmoja wa Misri, Jordan, Syria, Palestina na Sudan. Baadhi ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imelaani shambulizi hilo, ikiwatuhumu waasi wa Houthi kuishambulia Saudi Arabia. Hata hivyo, waasi hao hawajathibitisha kuhusika na shambulizi la Jumamosi, licha ya kudai kuhusika na mashambulizi mengine ya awali dhidi ya uwanja huo.

    Shambulizi hilo limefanyika wakati mapigano kati ya waasi wa Houthi na vikosi vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia nchini Yemen yakizidi kushika kasi. Mamlaka za Saudi Arabia zimesimamisha shughuli za uwanja huo wa ndege, huku mamia ya safari za ndege zikifutwa au kuelekezwa kwenye viwanja vingine.