Idadi ya waliouawa vitani Gaza huenda ikawa kubwa zaidi, watafiti wasema
Idadi ya watu waliouawa katika vita vya Gaza, huenda ikawa kubwa zaidi. Haya ni kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizoripotiwa na wizara ya afya inayosimamiwa na kundi la Hamas.
Takwimu hizo zimechapishwa katika jarida la masuala ya matibabu la Lancet. Tathmini hiyo iliyoongozwa na wataalamu kutoka Uingereza, imeangazia miezi tisa ya kwanza ya vita hivyo, ambavyo vilianza punde tu baada ya kundi la Hamas kushambulia Israel mnamo Oktoba 7 2023.
Watafiti walitumia data kutoka kwa wizara ya afya ya Palestina, kwa pamoja na kutoka kwa Tathmini nyingine iliyochapishwa katika mitandao iliyoangazia taarifa za jamaa za waliofariki, na vile vile matangazo ya vifo. Ilikadiria kwamba hadi tarehe 30 Juni 2024- Wapalestina 64,260 walifariki baada ya kupata majeraha mabaya, kumaanisha kwamba viwango vya kuripoti vifo rasi vilikuwa hcini na asilimia 41.
Ubalozi wa Israel nchini Uingereza, umesema kwamba ‘taarifa zozote zinazotokea ndani ya Gaza haziwezi kuaminiwa,’ na kuwasilishwa na Hamas. Umoja wa mataifa umetumia taakwimu za wizara hiy na kuzitaja kama halisi na sawa.
Takwimu za wizara hiyo hazitofautishi kati ya wapiganaji na raia, ila ripoti ya hivi karibuni ya umoja wa mataifa imesema kwamba idadi kubwa ya vifo vilivyothibitshwa ni vya waathiriwa wa kike na watoto. Israel imesema kwamba takwimu za Hamas haziwezi kuaminika.
Mwezi agosti, jeshi la Israel lilisema kwamba lilikuwa limewamaliza magaidi 17,000, japo haijabainika wazi jinsi idadi hii ilivyofikiwa.
Jeshi hilo la IDF linasisitiza kwamba linawalenga wapiganaji pekee na linajaribu kupunguza idadi ya raia wanaouawa katika mashambulizi yake.
Watafiti kutoka Chuo cha London school of Hygiene and Tropical Mdicine waliangalia ni watu wangapi walijitokeza zaid ya mara moja walipokuwa wakihesasbu idadi ya waliofariki vitani.
Viwango vya kupishana katika takwimu hizo vinaashiria kwamba idadi ya waliofariki moja kwa moja kutokana na majeraha mabaya katika vita hivyo huenda ikawa kubwa zaidi ya takwimu zilizotolewa na hospitali;takwimu ambazo zilichapishwa na wizara ya afya.
Wizara ya afya ya Gaza, hutoa taarifa mpya ya jumla ya waliofariki katika vita hivyo, kila siku. Hujumlisha takwimu hizo za vifo kutoka kwa hospitali mbalimbali na vile vile taarifa za vifo zinazotolewa na familia na vile vile taarifa kutoka kwa vyombo vya habari vinavyoaminika.
Ripoti ya Lancet, inakadiria kwamba idadi ya jumla ya wlaiofariki huenda ikawa kati ya watu 55,298 na 78,528 ikilinganishwa na 37,877 iliyochapishwa na wizara ya afya.
Takwimu za ripoti hii zinaonyesha kwamba idadi hii ni kubwa zaidi, au huenda ikwa ya chini kulingana na taarifa za kina za Tathmini. Taarifa hiyo pia inasema kwamba asilimia 59 ya wlaiouawa , ni wanawake na watoto na watu wazee.
Vita vya gaza vimechochewa na shambulizi la Hamas nchini Israel ambapo watu 1200 waliuawa na wengine 251 kutekwa nyara na kuzuiliwa Gaza.
Israel ilinzisha operesheni kali ya kivita kujibu hatua hiyo ya Hamas. WIzara ya afya, imesema kwamba watu 46,006 wengi wao wakiwa raia wameuawa katika shambulizi hilo la Israel.
Unaweza kusoma;