Taliban wadhibiti uwanja wa ndege muda mfupi baada ya Marekani kuondoka
Picha mpya zimeibuka za Taliban wakiingia kwenye uwanja wa ndege wa Kabul, baada tu ya ndege ya Marekani kuondoka.
Moja kwa moja
Lizzy Masinga
Tanzania yapunguza rasmi viwango vya tozo za miamala ya simu baada ya kupigiwa kelele

Chanzo cha picha, Google
Maelezo ya picha, Waziri wa fedha Tanzania, Mwigulu Nchemba Serikali ya Tanzania imepunguza tozo za miamala ya simu kwa asilimia 30, kufuatia kilio cha wananchi juu ya kiwango kikubwa cha tozo hizo.
Pamoja na punguzo hilo la tozo ya miamala ya simu, serikali hiyo pia imepunguza kwa asilimia 10 viwango vya tozo wanazotoza makampuni ya simu katika miamala ya kutuma na kutoa fedha kati ya mtandao mmoja na mwingine.
Taarifa iliyotolewa leo na wizara ya fedha na mipango ya nchi hiyo, inasema waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba amekwisha tia saini marekebisho ya kanuni za tozo za mialamala ya kieletroniki za kutuma na kutoa fedha za mwaka 2021 kwa ajili ya kupunguza viwango vya tozo hizo.
'Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi kwa tangazo la serikali Septemba Mosi, 2021', ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Julai 19, 2021 Rais wa Tanzania, Samia Suluhu alitoa maelekezo kwa wasaidizi wake kupitia upya viwango vya tozo hizo na kutoa unafuu kwa wananchi waliokuwa wanapigia kelele tozo hizo wakitaka zipunguzwe ama ziondolewe kabisa.
Kwa mujibu wa taarifa iliytolewa na serikali, tangu kuanza kukwata kwa tozo hizo mpya mwezi uliopita jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 48.4 zimepatikana na kuelekezwa katika kujenga vituo vya afya 150 na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 560 nchi nzima.
‘Tuko hapa kuwahudumia watu’ – msemaji wa Taliban

Chanzo cha picha, Reuters
Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid ametoa wito wa umoja wa kitaifa baada ya majeshi ya Marekani hatimaye kuondoka nchini Afghanistan baada ya miaka 20.
Ametoa wito kwa Waafghanistan "kuweka kando tofauti zao na kuja pamoja", akisema jamii ya kimataifa haitasaidia nchi hiyo ikiwa watu wake hawataungana.
Ameongeza kuwa serikali ijayo itawawakilisha watu wote wa Afghanistan.
Pia aligusia suala la uchumi wa nchi hio na kuomba nchi zingine kuwekeza nchini Afghanistan.
Aliisema kuwa Taliban inatafuta "uhusiano mzuri" na jamii ya kimataifa na kwamba itatafuta njia "mwafaka" kutatua suala lolote.
Kenya inashika nafasi ya nne kwa idadi ya tembo ulimwenguni

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Ni Zimbabwe, Botswana na Tanzania pekee zilizo na tembo zaidi Kenya ni ya nne duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya tembo, kulingana na matokeo ya awali ya senya ya wanyamapori iliyofanywa hivi karibuni.
Nchi hiyo ina jumla ya tembo 36,280 aina ya - ongezeko la zaidi ya tembo karibu 2,700 kutoka walipohesabiwa mwaka 2017.
Ni Zimbabwe, Botswana na Tanzania zina tembo wengi zaidi.
Kwa miaka kadhaa wanyamapori wa Kenya wamepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na uwindaji haramu na muingiliano wa watu na wanyama hali ambayo imechangia kupotea kwa makazi ya wanyama hao na njia wanazotumia wakati wa kuhama.
Lakini Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini Kenya (KWS) linasema sensa, iliyofanywa kati ya mwezi Mei na Julai, ilionesha kupungua kwa idadi ya tembo, vifaru na spishi zingine za wanyama wanaokabiliwa na tishio la kuangamia.
Nchi hiyo ina vifaru 1,739, miongoni mwao vifaru weupe wa kaskazini duniani, vifaru weusi 897 na vifaru 840 weupe wa kusini.
Idadi ya vifaru weusi wanaokabiliwa na tisho la kuangamia imeongezeka kwa 200 tangu walipohesabiwa miaka minne iliyopita.
- Utafiti: Mitetemeko ya Tembo inavyoweza kuashiria walipo
- Tembo aliyeanguka kisimani alivyookolewa
Zaidi ya shule 7,000 zilizoharibiwa katika vita vya Tigray- Waziri

Chanzo cha picha, AFP
Vita katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia imelazimisha zaidi ya wanafunzi milioni 1.42 kutoka shule na kuharibu zaidi ya shule 7,000, waziri wa elimu wa nchi hiyo anasema.
Getahun Mekuria alisema maeneo jirani ya Amhara na Afar pia yameathiriwa kwani mapigano yalikuwa yameenea katika maeneo hayo:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Tayari mamia ya shule katika majimbo ya Amhara na Afar ilikuwa imeharibiwa katika mapigano ya mwezi uliopita, alisema.
Sehumu kubwa ya miundo mbinu katiika eneo hilo imeharibiwa katka vita hivyo vy amiezi 10.
Maelfu ya watu wameuawa, mamilioni ya wengine kufurushwa makwao huku maelfu wengine wakihitaji misaada ya kibinadamu.
Mlipuko wa kipindupindu waua makumi ya watu Niger
Mlipuko wa ugonjwa wa kuhara na kutapika yaani kipindupindu umesababisha vifo vya watu 83 people nchi Niger, ambako mamlaka zimerekodi zadi ya visa 2,300 tangu Machi 13.
Sita kati ya maeneo manane nchini Niger yameathiriwa na mlipuko huo, umeongezeka zaidi kutomana na mafuriko.
Janga la kipindupindu lilitangazwa rasmi Agosti 9 na Waziri wa Afya Idi Illiassou Mainassara.
Balozi wa Kenya ashtumiwa kwa uwindaji haramu wa wanyamapori nchini Namibia
Balozi wa Kenya nchini Namibia ameshambuliwa mtandaoni baada ya picha inayomuonesha akiwa karibu na swara aliyeuawa akiwa na bunduki mkononi kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Benjamin Langat, ambaye hajatoa tamko lolote kuhusu picha hiyo , ametuhumiwa na baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Twitter kwa kukiuka kujitolea kwa Kenya kwa uhifadhi wa wanyamapori licha ya kupata ruhusa ya kuwinda nchini Namibia::
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Wengi walitoa maoni juu ya kejeli ya picha hiyo kwenye chapisho la Ikulu kuhusu rais akipongeza mashirika ya wanyama pori ya Kenya kwa juhudi zao za kupambana na uwindaji haramu- mtumiaji mmoja wa twitter alitoa wito wa balozi huyo kurejeshwa nyumba:
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Kenya ili piga marufuku uwindaji haramu mwaka 1977 ili kuhifadhi wanyamapori wake.
Namibia inaruhusu uwindaji wanyamapori na kutumia fedha hizo kuhifadhi wanyama wanaokabiliwa na tisho la kuangamia.
Hatima ya Kesi ya Mbowe ya Ufisadi kujulikana kesho

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi nchini Tanzania itatoa uamuzi wake kesho Septemba Mosi, 2021 kama inaweza kuendelea na kesi ya kiongozi wa Upinzani nchini humo ama la.
Hatua hiyo imekuja kufuatia hoja za pingamizi zilizowasilishwa mahakamani hapo na Mbowe pamoja na watuhumiwa wenzake, wanaodai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo.
Mbowe na wenzake wameiambia mahakama hiyo kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni Divisheni Maalum.
Maelezo ya video, Freeman Mbowe:Mahakama itaamua kesho iwapo kesi yake ya ufisadi itaendelea au la Hata hivyo Serikali imepinga hoja hizo ikisema sheria zilifanyiwa marekebisho ikiwemo namba 3 ya Mwaka 2016 ambapo makosa yaliyoko kwenye Sheria ya Ugaidi yaliwekwa kwenye Sheria ya Uhujumu Uchumi.
Kwa hoja hii upande wa serikali unaona Mahakama hiyo ya ufisadi ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka hayo yanayomkabili Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo (CHADEMA).
Jaji wa Mahakama hiyo Elinazer Luvanda amehairisha kesi hiyo hadi kesho kwa uamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande zote.
Ronaldo: 'Nimerudi kwa ajili yako Sir Alex Ferguson'

Chanzo cha picha, Getty Images
Cristiano Ronaldo ametambulishwa rasmi leo na kusema "amerudi nyumbani" kwenye klabu yake ya Manchester United na akisema amerejea nyumbani kwa bosi wake wa zamani Sir Alex Ferguson.
United imelipa dau la £12.85m kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Juventus, muongo mmoja baada ya kuondoka klabu hiyo kujiunga na Real Madrid.
Amesaini mkataba wa miaka miwili, huku akiwa na nafasi ya kuongeza mwaka mwingine mmoja.
"kila mtu ananijua, wanajua mapenzi yangu yasiyokwisha kwa Manchester United," aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram.
"Ni kama ndoto vile, baada ya mara kadhaa kucheza dhidi ya Manchester United, tena kama mpinzani, lakini bado naona mapenzi na heshima kutoka kwa mashabiki jukwaani.
Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ‘Ballon d'or anasema: "Nipo apa, imrejea nyumbani! Tupambane kwa mara nyingne! - Sir Alex, hii ni kwa ajili yako…"
Ruka Instagram ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
Sir Alex Ferguson alikuwa meneja wa United wakati Ronaldo anacheza Old Trafford, na kufunga mabao 118 katika mechi 292 kabla ya kutimkia Real Madrid mwaka 2009.
Inaaaminika alizungumza na Ferguson kabala ya kuamua kutua United.
Meneja mpya wa mashetani hao wekundu Ole Gunnar Solskjaer alisema: "Unakosa maneno unapomuelezea Cristiano. Sio mchezaji mzuri na wa ajabu, lakini pia ni mtu mzuri.
Ronaldo anaweza kuwepo kwenye mchezo wa United dhidi ya Newcastle United Septemba 11, utakua mchezo wa kwanza kuchezwa na klabu hiyo baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
Jerry Silaa atiwa hatiani na kamati ya maadili ya Bunge

Chanzo cha picha, Silaa
Taarifa ya Kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge imetolewa kuhusu tuhuma za kuvunja haki za bunge na kusema uongo zinazomkabili mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa.
Jerry Silaa alinukuliwa akizungumza na wananchi katika jimbo la Ukonga, kuwa mishahara ya ubunge haikatwi kodi.
Kauli zake zilikuwa na maneno yafuatayo, alinukuu mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka
'' Mimi nimeanza ubunge juzi,mwaka jana, mwezi wa 11, kwahiyo nimekuta hayo yanayosemwa na mengine yameshapistishwa tayari bungeni na katika hili mimi niungane na mheshimiwa wa kinondoni kwamba vikiliwa vya mwali na vya kungwi viliwe.''
''Ni wakati mwafaka kwa sisi wabunge ili tupate moral integrity, ili tupate kusimama mbele za watu kuwaambia walipe kodi sisi tuanze kulipa kodi kwenye mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa na wengine wanalipa wengine hawalipi. ukishakuwa hulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe'' Alinukuliwa Silaa.
Jerry Silaa alikiri mbele ya kamati kuwa kauli hizo ni kweli alizitoa yeye alipokuwa akihutubia wananchi wa jimbo la Ukonga
''Kutokana na kukiri kwake na ushahidi wa video kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, kamati imejiridhisha kuwa Jerry Silaa alitoa kauli zinazolalamikiwa''. Alisema Mwenyekiti wa kamati
Silaa alikiri kuwa kauli zake zimeleta tafrani kwenye jamii.
Kamati imejiridhisha kuwa Jerry Silaa alikuwa na nia ovu ya kudharau na kudhalilisha bunge pamoja na kuchonganisha wabunge, serikali, uongozi wa bunge na wananchi kwa kusema uongo.
''Kamati ilimtia hatiani Jerry Silaa kwa kusema uongo, hatua hiyo ni baada ya kuzingatia ushahidi uliokuwepo mbele ya kamati pamoja na sheria zinazosimamia mishahara ya wabunge, kamati iliona jambo hilo ni dharau kwa bunge, spika na shughuli za bunge.'' Alisema Bw. Mwakasaka.
Kutokana na hatua ya Jerry Silaa ya kutosahihisha kauli yake aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara licha ya kutakiwa na Spika kuomba radhi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Jerry Silaa alielezwa kuwa alikaidi maelekezo ya Spika.
''Katika suala hili kamati imejiridhisha kuwa kitendo hicho ni utovu wa nidhamu uliokithiri''.
Mapendekezo ya kamati
Kamati imependekeza Jerry Silaa asihudhurie mikutano ya bunge miwili mfululizo
Aondolewe kwenye uwakilishi wa nafasi ya bunge katika bunge la Afrika PAP
Kesi ya R. Kelly: Mwathiriwa wa kiume atoa ushahidi wa unyanyasaji wa kingono

Chanzo cha picha, Reuters
Kesi ya msanii R. Kelly kuhusu unyanyasaji wa kingono imeingi asiku ya nane Jumatatu , huku mlalamishi wa kiume akitoa Ushahidi kwamba nyota huyo wa muziki alimuahidi umaarufu akikubali kufanya ngono naye.
Mwanamume huyo aliyetoa Ushahidi kwa kutumia jina la kisiri la Louis, alisema alikuwa na miaka 17 wakati Bwana Kelly alipomuuliza "yuko tayari kufanya nini kwa ajili ya muziki".
Kisha akelezea jinsi mwanamuziki huyo alivyotambaakuelekea kwake akifanya onyesho la kimapenzi , ijapokuwa "sikutaka kujihusisha na hayo".
Bwana Kelly, 54, amekanusha mashtaka yote dhidi yake.
Hii ni pamoja na hshtaka moja la udanganyifu - ambayo inamuonyesha kama mkuu wa biashara ya jinai ambayo lengo lake lilikuwa "kuwateka wanawake wadogo na vijana" kwa madhumuni ya ngono - na makosa manane ya kukiuka sheria ya biashara ya ngono inayojulikana kama Sheria ya Mann.
Mwimbaji huyo ambaye jina lake kamili ni Robert Kelly, hajashtakiwa kwa ubakaji na kushambulia, lakini waendesha mashtaka wanaruhusiwa kutoa ushahidi wa uhalifu wowote unaohusiana na mashtaka ya ujambazi, bila kujali ni lini ulitokea.
Aliiambia mahakama kuwa Bw. Kelly alimpatia namba ya simu na kumkaribisha nyumbani kwake, akisema angeweza kutumbuiza katika studio ya kurekodina kupokea vidokezo kadhaa kwenye biasharaya muziki.
Siku ya Jumatatu, majaji walisikia ushahidi wa waathiriwa wawili, wote wanasema walikuwa watoto wakati walipokutana na na Bw.Kelly.
Louis alisema alikutana mara ya kwanza na Bw. Kelly mwaka 2006, akiwa na miaka 17-akifanya kazi nyakati za usiku katika McDonald's mjini Chicago.
Kamati ya maadili ya Bunge yamtia hatiani Gwajima

Kamati ya Haki, maadili na madaraka ya bunge ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemkuta na hatia Mchungaji na Mbunge wa jimbo la Kawe Josephat Gwajima ya kutoa taarifa za uongo kuhusu chanjo za corona.
Mwenyekiti wa Kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge, Emmanuel Mwakasaka amesema kauli zilizotolewa na Gwajima zimedhalilisha nafasi ya mbunge, zinashusha heshima ya bunge, wabunge na viongozi, zinachonganisha mhimili wa bunge dhidi ya muhimili wa serikali, serikali na wananchi na bunge na wananchi.
''Kauli za Josephat Gwajima zinagonganisha, zinachonganisha na kufarakanisha serikali na wananchi kwa kuwaaminisha kuwa serikali inawalazimisha wananchi kuchanjwa wakati jambo hilo ni la hiyari.''
''Kwa kauli kwamba anayekubali chanjo amepokea pesa kutoka nje ya nchi na kampuni zinazotengeneza chanjo ni jambo linalotafsiriwa kuwa rushwa, kauli hizi zinaathiri mahusiano kati ya nchi yetu na nchi nyingine, jambo hili ni dosari kwa kiongozi anayetumia nafasi ya mbunge''. alisema Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Mwenyekiti Mwakasasa amesema Mch.Gwajima hajutii kauli zake na kwamba ataendelea kutoa kauli na kusisitiza kuwa huo ndio msimamo wake, imani yake na majibu yake yalikuwa yamejikita katika kueleza kuwa kamati haina mamlaka ya kuhoji mahubiri yake ya kanisani.
Hivyo, Kamati imependekeza Gwajima apewe adhabu kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge.
Serikali ifuatilie matamshi na matendo yake kwani kuna uwezekano wa jinai ndani yake.
Pia apelekwe kwenye Chama chake kwa hatua za kinidhamu kwa taratibu za Chama.
Afrika Kusini yabaini aina mpya ya virusi vya Corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Watafiti wanachunguza aina mpya ya virusi vya corona nchini Afrika Kusini. Virusi hivyo aina ya C.1.2, ambavyo huzaana mara mbili zaidi lakini havijatajwa kuwa vyenye kutia wasiwasi.
Matukio ya virusi hivyo yamerekodiwa katika kila mkoa nchini Afrika Kusini pamoja na mataifa saba ya Afrika, bara Asia, Ulaya na maeneo ya Oceania.
Wanasayansi wanatathmini jinsi aina hiyo ya virusi inavyokabiliana na viini vinavyopigana na corona. Pia wanachunguza jinsi vinavyozaana na maambukizi yake.
Maria van Kerkhove, afisa wa kiufundi anayeongoza uchunguzi huo kwa niaba ya shirika la la Afya duniani WHO amesema kwamba virusi hivyo havionekani vikiongezeka.
Amesema kwamba aina hiyo ya virusi ndio inayoendelea kuwaathiri wengi na kwamba WHO itaufahamisha umma iwapo kutakuwa na mabadiliko yoyote.
Afrika kusini ni taifa ambalo limeathiriwa vibaya na aina zote mbili za maradhi ya corona ikiwemo yale ya virusi vya Delta na Beta ambayo yanasambazwa kwa urahisi zaidi.
Taifa hilo limesajili maambukizi 2,770,575 ya virusi vya corona ikiwemo vifo 81,830.
Marekani yaharibu ndege na vifaa vyake vya kijeshi walivyoviacha Afghanistan
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Jeshi la Marekani lilihakikisha linalemaza ndege zao na magari ya silaha waliyoyaacha kwenye uwanja wa ndege mjini Kabul kabla ya kuondoka usiku wa Jumatatu. Maafisa wameeleza.
Kamanda wa majeshi ya Marekani Jeneralo Kenneth McKenzie amesema vikosi ''vililemaza'' ndege zake 73, na magari 70 ya silaha na magari mengine ya kijeshi ili Taliban wasiweze kuyatumia.
''Ndege hizo hazitaweza kuruka tena.....Hakuna mtu yeyote atakayeweza kuyaendesha,'' alisema.
Video iliyotumwa na mwandishi wa habari wa Los Angeles imes ilionesha Taliban wakiingia kwenye uwanja wa ndege eneo ambalo ndege za Marekani zimeegeshwa wakionekana kukagua vifaa hivyo.
Pia Marekani imelemaza mfumo wa roketi wa teknolojia ya juu-ulioachwa uwanja wa ndege. Mfumo wa C-RAM ulifanya kazi Jumatatu kudhibiti shambulio la roketi la wanamgambo wa IS lililolenga uwanja wa ndege.
Kama tulivyoripoti awali, wapiganaji wa Taliban katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita wameonekana wakiwa na vifaa vya kijeshi vya Marekani na vyombo vya moto. Vifaa hivyo vilikuwa vimegawiwa kwa jeshi la Afghanistan, lakini baada ya jeshi la Afghanistan kuweka silaha chini, vifaa hivyo viliingia mikononi mwa Taliban.
Taliban wawazuia Wamarekani wanaoingia uwanja wa ndege-Ripoti

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati Ndege ya Marekani inaondoka Afghanistan bado kulikuwa na raia wa Marekani na Waafghani waliokuwa wakitarajia kuondoka, wakijaribu kuingia kwenye uwanja wa ndege, maafisa wameeleza.
Katika mkutano wa waandishi wa habari awali, Jeneali McKenzie, Mkuu wa vikosi vya Marekani alithibitisha kuwa kuna Wamarekani 100-250 ambao wameshindwa kufika uwanja wa ndege au wameshindwa kuingia kwenye ndege.
Mwanajeshi wa zamani wa Marekani ambaye amesema kuwa alikuwa akisaidia kuratibu shughuli za uokoaji akiwa katika makazi yake Connectcut amesema Taliban waliwazuia wengi kupita. Alikuwa akiwasiliana na wengi, aliandika katika ukurasa wa twitter.
''Taliban walikuwa hawawezekani kuratibu nao mpaka mwiho. Walikataa kutoa ushirikiano nje ya milango ya kuingilia,'' alisema.
BBC haijathibitisha madai haya.
Alex Plitsas, Mwanajeshi wa zamani amesema bado anawasiliana na Wamarekani wanaotaka kuondoka Afghanistan, lakini baadhi hawajajisajili kwenye mamlaka za Marekani ''Hatuwezi kuwaokoa watu ambao hatujui kama wako huko,'' alisema.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mfululizo wa matukio wakati wa mzozo wa miaka 20 nchini Afghanistan

Chanzo cha picha, Reuters
Huku vikosi vya Marekani vikiwa vimeondoka nchini Afghanistan, vita vya muda mrefu vimefikia tamati.
Ufuatao ni mfululizo wa matukio makubwa wakati wa mzozo wa miaka 20.
Oktoba 7 , 2001: Majeshi ya muungano yakiongozwa na Marekani yalishambulia kwa mabomu ngome za Taliban na al-Qaeda nchini Afghanistan. Miji iliyolengwa ni Kabul, Kandahar na Jalalabad. Taliban, ambao walichukua madaraka na kufuatiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe wakikataa kukabidhi mamlaka kwa kiongozi wa al-Qaeda, Osama Bin Laden.
Novemba 13, 2001:Muungano wa Kaskazini, kundi linalopinga waasi wa Taliban, lililoungwa mkono na vikosi vya muungano viliuchukua mji wa Kabul.
·
Februari 7, 2009: Rais wa Marekani Barrack Obama aliidhinisha kuongezwa kwa idadi ya wanajeshi nchini Afghanistan, idadi iliyofikia wanajeshi takribani 140,000.
Desemba 28, 2014: Nato yatamatisha operesheni zake nchini Afghanistan.Marekani yaondoa maelfu ya wanajeshi wake. Wengi waliosalia walibaki walikuwa kwa kazi za mafunzo na kusaidia vikosi vya Afghanistan.
Februari 29, 2020: Marekani na Talibani wasaini‘’mkataba wa amani’’ mjini Doha, Qatar. Marekani na washirika wa Nato wakubali kuondoa vikosi vyote ndani ya miezi 14.
Aprili 13, mwaka 2021: Rais wa Marekani Joe Biden atangaza kwamba vikosi vyote vya Marekani vitaondoka Afghanistan ifikapo tarehe 11 mwezi Septemba mwaka huo.
Agosti 16 mwaka 2021: Katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja,Taliban yadhibiti miji nchi nzima, ikiwemo Kabul. Vikosi vya usalama vya Afghanistan vyapoteza nguvu yake mbele ya Taliban.
Agosti 31,2012: Marekani yatamatisha rasmi uwepo wake Afghanistan.
Taliban wadhibiti uwanja wa ndege muda mfupi baada ya Marekani kuondoka

Chanzo cha picha, EPA
Picha mpya zimeibuka za Taliban wakiingia kwenye uwanja wa ndege wa Kabul, baada tu ya ndege ya Marekani kuondoka.
Mwandishi wa gazeti la Los Angeles Times Nabih Bulos, aliwafuatilia wapiganaji wa Taliban walipokuwa wakilitazama eneo ambalo kulikuwa na ndege iliyoachwa na vikosi vya Marekani
‘’Tuko hapa na Taliban wakati wakiingia uwanjani ikiwa ni dakika chache zimepita tangu sehemu ya eneo hili la uwanja wa ndege lilipokuwa likidhibitiwa na Marekani.Sasa wamechukua udhibiti,’’ alisema mbele ya kamera.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Video nyingine zinaonesha wapiganaji wa Taliban wakifyatua risasi angani ikiwa ishara ya kushangilia, walishangilia na kupiga picha, na kuzunguka katika eneo lote la uwanja.
Habari! karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja

