Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Besigye

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Dkt Besigye amekamatwa akielekea makao makuu ya Tume ya Uchaguzi

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi.

Watu walioshuhudia wanasema amekamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake.

Amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani tangu Ijumaa wakati polisi walimtuhumu kupanga kujitangazia matokeo.

  • <link type="page"><caption> Mtazamo wa Kizza Besigye kuhusu uchaguzi</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/medianuai/2016/02/160219_besigye_interview" platform="highweb"/></link>
  • <link type="page"><caption> Museveni: Uchaguzi wa Uganda ulikuwa shwari</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/02/160222_museveni_rxn_uganda2016" platform="highweb"/></link>
Besigye
Maelezo ya picha, Besigye alizuiliwa na polisi mara tatu wiki iliyopita

Wakili wake amethibitisha habari za kukamatwa kwake.

Awali kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais.

Polisi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Polisi walivamia afisi za chama cha FDC Ijumaa wiki iliyopita

Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi wiki iliyopita.