Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Paka amrukia imamu anayeongoza sala wakati wa ibada ya Ramadhan Algeria
Tangazo la moja kwa moja lilinasa wakati paka alipomrukia imamu, ambaye alikuwa akiongoza sala ya usiku ya Ramadhani huko Bordj Bou Arreridj, Algeria.
Imam Walid Mehsas alikuwa akiswali Tarawehe, swala ya usiku inayotokea kila jioni katika mwezi wa Ramadhani, ndipo paka huyo alipomrukia na kupanda juu ya mabega yake.