Omanyala: Mkenya anayetaka kuvunja rekodi ya dunia ya Usain Bolt

Mbali na kushikilia rekodi ya Afrika ya mbio za mita 100, Mwanariadha Ferdinand Omanyala pia amekuwa himizo kwa wimbi jipya la wanariadha wanaotaka kushiriki mbio fupi- jambo ambalo limepewa jina la ‘Omanyala-mania’ katika nchi yake ya Kenya.

Sasa kwenye mashindano ya riadha ya Afrika yatakayofanyika nchini Mauritius, Omanyala analenga ushindi wa dhahabu tatu kwenye mbio za mita 100, 200 na zile za kupokezana vijiti za mita 100 kwa wanariadhatu wanne. Lakini ndoto yake haikomei hapo-: Anataka kubadilisha dhana kuwa mbio fupi sio sifa ya wakenya na anasema yeye ndiye atakayevunja rekodi ya dunia ya mita 100 inayoshikiliwa na Mjamaica Usain Bolt. Haya ni mahojiano yake na BBC.