'Niliuona mwili wa mwanangu kwenye Facebook': Kuteswa na kuuawa na wanajeshi wa Myanmar

Joseph anaomboleza kifo cha mwanawe.

Baada ya wanajeshi wa Myanmar kuingia kijijini kwake, alikimbilia msituni lakini Pali Nang mwenye umri wa miaka 13 hakufanikiwa.

Joseph aliona picha ya maiti ya mwanawe kwenye mtandao wa Facebook ambapo ilionyesha dalili za kuteswa.

Yeye ni mmoja wa takriban wakimbizi 40,000 wa Myanmar ambao wamevuka mpaka na kuingia India.