Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Bingwa wa kujenga misuli mwenye mkono mmoja anayetoa ujumbe wa matumaini
Kim Na-yoon alipoteza mkono wake katika ajali ya pikipiki.
Alihisi ndoto yake ya kuwa katika ulimwengu wa uwanamitindo umegonga mwamba lakini hakupoteza matumaini maishani.
Alipokuwa akifanya mazoezi ya urekebishaji, alijipa changamoto ya kuwa mtaalamu wa kujenga misuli.
Hivi karibuni aliibuka wa kwanza katika mashindano ya kujenga misuli, kuwashinda wanariadha wasio na ulemavu. Sasa anawasilisha ujumbe wake wa matumani kwa wengine.