Wiki ya Afrika kwa picha: 11 - 17 Septemba 2020

Mkusanyiko wa picha bora za wiki kutoka maeneo tofauti barani Afrika:

Wawakilishi wa Ecowas na CNSP katika meza ya mazungumzo mjini Accra, Ghana.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Viongozi wa Muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibu Ecowas wakiongoza mazungumzo ya kukwamua mzozo wa kisiasa na wanajeshi wa Mali siku ya Jumanne, katika juhudi za kubuni serikali ya mpito ya kiraia kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliyopita.
Picha ya mafuriko Sudan iliyopigwa kutoka kwa ndege ya shirika la lisilo la kiserikali la Bahrain Royal (RCO).

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mafuriko makubwa yanaonekana kuathiri maeneo mengi ya mji mkuu wa Sudan Khatoum katik apicha iliyopigwa kutoka angani siku ya Jumatatu.
Wanafunzi wa shule wakipiga foleni.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mwanafunzi anayeonekana kuwa na usingizi anapiga miyayo siku ya Jumanne wakati Tunisia ilipofungua shule kwa mara ya kwanza tangu ilipoondoa amri ya kutotoka nje iliyowekwa kukabiliana na janga la virusi vya corona mwezi Machi.
Wanawake watatu wanaonekana wakiruka viunzi katika mbio za mita 3000.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku ya Jumapili wanariadha wa Kenya Hyvin Kiyeng, Mercy Chepkurui na Beatrice Chepkoech -walishindana katika mbio za Istaf nchini Ujerumani.
Canoeists paddle together in the twilight.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wanume watatu wakijivinjari majini kwa kutumia mitumbwi mapema asubuhi ya jumanne katika bwawa la Emmarencia mjini Johannesburg, Afrika Kusini...
Siku kadhaa zilizopita mkazi wa Soweto, alionekana akitoka saluni...

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Siku kadhaa zilizopita mkazi wa Soweto, alionekana akitoka saluni...
Mteja akiondoka saluni baada ya kutengezwa nywele zake .

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wengine walionekana hapa nje, pia siku ya Ijumaa.
Henri Konan Bédié stands on a podium waving at crowds in Yammousoukro.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Siku ya Jumatatu maelfu ya wafuasi wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Henri Konan Bédié walihudhuria mkutano wa kisiasa katika mji mkuu wa nchi hiyo. Kiongozi huyo anawania tena kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujao. Hasimu wake wa kisiasa wa muda mrefu Alassane Ouattara ana gombea muhula wa tatu madarakani kufuatia kifo cha ghafla cha mshirika wake wa karibu ambaye alitarajiwa kuwa mrithi wake Amadou Gon Coulibaly.
Watoto na watu wazima wakisubiri kuuaga mwili wa George Bizos.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Na hapa Wafrika Kusini wanasubiri kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanaharakati aliyepambana na ubaguzi wa rangi George Bizos. Wakili huyo wa haki za binadamu, alimwakilisha Nelson Mandela katika kesi ya Rivonia , alifariki wiki iliyopita akiwa na miaka 92.

Picha zote zina haki miliki kutoka kwa Reuters, EPA na AFP.