Virusi vya corona: Makamu wa rais wa Sudan Kusini Wani Igga atangaza kuwa na virusi

Makamu wa rais wa Sudan Kusini Dkt James Wani Iga amesema amebaini kuwa ana corona baada ya kufanyiwa vipimo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Makamu wa rais wa Sudan Kusini Dkt James Wani Iga amesema amebaini kuwa ana corona baada ya kufanyiwa vipimo
Muda wa kusoma: Dakika 2

Makamu wa rais wa Sudan Kusini Dkt James Wani Iga amesema kuwa amepatwa na virusi vya corona.

Akitangaza taarifa hiyo kupitia shirika la habari la taifa la Sudan Kusini amesema: ''Sampuli zangu zilichukuliwa siku chache zilizopatikana na leo nimepatikana na ccorona...kwahiyo ninawaomba raia wote wa Sudan Kusini kwenda kupimwa , hii ni muhimu ili tupunguze kusambaa kwa virusi kwa watu wengi'', amesema .

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Taarifa ya kupatwa kwa maambukizi ya virusi vya corona kwa Dkt James Wani Iga , inakuja baada ya viongozi wengine wakuu wa nchi hiyo kutangaza kupatwa na Covid-19 mkiwemo makamu rais wa nchi hiyo Riek Machar na mkewe pia waambukizwa virusi vya corona mwezi huu.

Miongoni mwao ni Dkt. Machar alisema kwamba yeye na mke wake ambaye pia ni waziri wa ulinzi, walipata maambukizi baada ya kutangamana na jopo la ngazi ya juu la kukabiliana na virusi hivyo nchini humo.

Wakati huo Bwana Machar amesema kwamba hana dalili zozote na hali yake ya afya iko sawa lakini atajiweka karantini kwa siku 14.

Riek Machar na mkewe waambukizwa virusi vya corona

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Riek Machar na mkewe waambukizwa virusi vya corona

Mwalitangaza kwamba virusi hivyo vimefikia kwenye kambi ya waliotoroka makazi yao ambao wamekuwa wakiitaka Umoja wa Mataifa iwalinde katika mji mkuu wa Juba tangu 2013.

Nchi hiyo bado inakabiliana na baa la njaa hata baada ya Machar na Rais Salva Kiir — waliokuwa mahasimu kuunda serikali ya umoja wa taifa Februari.

Viongozi hao wawili bado hawajakubaliana masuala ya msingi kama udhibiti wa majimbo.

Kuchukuliwa kwa sampuli za vipimo cya corona

Chanzo cha picha, Getty Images

Wengine waliothibitishwa kuambukizwa ni walinzi kadhaa na wafanyakazi.

Mawaziri 10 tayari wameambukizwa virusi vya corona nchini Sudan Kusini, kulingana na taarifa iliyotolewa mwezi huu na msemaji wa serikali katika mahojiano na BBC.

Waziri wa Habari wa Sudani Kusini Michael Makuei aliiambia BBC kuwa mawaziri wote hao walikuwa ni wajumbe wa kamati ya juu ya serikali ya kupambana na corona nchini humo.

Katika mawaziri waliopo kwenye kamati hiyo, ni Waziri wa Afya pekee ambaye hakukutwa na maambukizi.

Iliripotiwa kuwa mawaziri hao waliambukizwa Covid-19 baada ya kukutana na aliyekuwa mjumbe wa kamati hiyo ambaye alikuwa na virusi vya corona.

Mawaziri wote 10 walijitenga kwa sasa na serikali imesema kuwa wote wanaendelea vizuri kiafya.

Waziri wa habari Michael Makuei alitangaza awali kuwa mawaziri 10 wa Sudan Kusini walipatwa na corona na kujiweka karantini

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Waziri wa habari Michael Makuei alitangaza awali kuwa mawaziri 10 wa Sudan Kusini walipatwa na corona na kujiweka karantini

Walinzi wa viongozi kadhaa nchini humo pia walikutwa na virusi na na kuwekwa karantini.

Mpaka sasa zaidi ya watu 300 wamethibitishwa kupata corona Sudani Kusini, huku watu wane wakipona na sita kufariki.

Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya hatari ya kuporomoka kabisa kwa mfumo wa afya wa nchi hiyo ambao una uwezo mdogo kutokana na mgororo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambao umeathiri ustawi wa maendeleo.

Kwa sasa rais Kiir wameweka tofauti zao za kisiasakando na kutengeneza serikali ya umoja wa kitaifa, japo hawajaweza kukubaliana katika baadhi ya mambo ya msingi kama udhibiti wa majimbo.

Wakati corona ikiendelea kuleta wasiwasi, nchi hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa chakula kwa sasa.

Coronavirus
Banner