Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Newcastle inamfukuzia Ugarte Man Utd

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle United inataka kuimarisha safu yake kati msimu huu na wanapania kumsajili kiungo wa Manchester United Manuel Ugarte, 25,(Football Insider)
Tottenham Hotspur na West Ham United zina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Marc Casado, 22. (Tuttomercato - kwa Kiitaliano).
Liverpool na Chelsea wako tayari kupigana vikumbo kwa mshambuliaji wa Bournemouth Eli Junior Kroupi, 19, huku Cherries wakiwa tayari kukubali ofa ya pauni milioni 60. (Caught Offside)
Coventry City inataka uhamisho wa mkopo wa mlinda lango wa Brighton Carl Rushworth, 24, kuwa wa kudumu msimu wa joto lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Leeds United. (Team Talk)
Mshambuliaji wa Leeds United Joel Piroe, 26, huenda akaondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto kwa sababu ya kukosa muda wa kucheza, Rangers ikitarajiwa kuwa makao yake mapya. (Football Insider)
Manchester United inajiandaa kumsajili winga wa Leicester City, Jeremy Monga, 16, huku Manchester City na Arsenal pia wakimtaka kinda huyo. (
Fulham wanachunguza dili la kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Malik Tillman, 23, huku wakijiandaa kwa maisha bila Harry Wilson ambaye mkataba wake unaisha msimu wa joto. (Team Talk)











