Jinsi wadudu walivyochukua nafasi ya mlo wa nyama DR Congo

Duniani kuna watu bilioni wanaokula wadudu, hili linafanyika sana barani Afrika kuliko sehemu nyingine yoyote duniani.

Kuna zaidi ya wadudu aina 500 Afrika wakiwemo nzige, senene, kumbikumbi, konokono na mende.

Nchini DRC, mlo wa wadudu ni jambo la kawaida, na chakula kinachopendwa sana .

Wadudu hawa huvunwa misituni na kuuzwa katika masoko mbalimbali.

Mwandishi wa BBC Joyce Etutu ametuandalia taarifa ifuatayo.