Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ugonjwa usio wa kawaida kwa jina shetani nchini Kenya
Karibu watu 300 wanaishi kwenye mapango ndani ya msitu wa Utut eneo la bonde la Ufa nchini Kenya.
Watu hawa wamezoea maisha ya kukutana na nyati, nyoka na wanyama wengine hatari wakiwa kwenye shughuli zao za kila siku.
Na pia wanapokuwa wagonjwa, kimbilio lao ni dawa za asili kutoka kwa majani ya miti inayopatikana kwenye msitu huo.
Hata hivyo wengi wao wamekuwa wakiugua ugonjwa wa ngozi usiokuwa wa kawaida unaofahamika kama Curtaneous Leishmaniasis ambao kwao wao huona kama ni shetani au laana
Mwandishi wetu Mercy Juma ametembelea eneo hilo na kutuandalia taarifa ifuatayo