Wanga wanaohangaisha wanakijiji kwa mazingaombwe usiku kucha Kenya

Maelezo ya video, Wanga wanaohangaisha wanakijiji Kenya

Kwa vizazi vingi tu, wakaazi wa maeneo ya vijijini wamelalamika kuhusu wanga wanaowahangaisha usiku kucha. Inasemekana ni wanakijiji waliopagawa na mapepo yanayowashurutisha kuwahangaisha na kuwaongopesha majirani zao usiku.

Lakini hakuna anayafahamu ni akina nani na lengo lao ni lipi.

Kwa niaba ya BBC Africa Eye, mwandishi Tom Odula amechungunza mazingaombwe hayo, na kuangazia ukweli katika kinachoaminika kuhusu wanga hao na kutoa picha ambazo hazijawahi kuonekana za wanga wakiwa kazini.