Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tanzania: Mwili wa Reginald Abraham Mengi wawasili Dar es salaam
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi umewasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere Dar es salaam kutoka Dubai ambapo alifikwa na umauti Jumatano iliyopita.
Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo amesema mwili wa mfanyabiashara huyo maarufu nchini Tanzania utahifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo baada ya kuwasili.