Ni ipi nguvu ya upinzani katika mataifa ya Afrika?

Maelezo ya video, Ni ipi nguvu ya upinzani katika mataifa ya Afrika?

Nchini Kenya, kusalimiana kwa mkono kati ya rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake Raila Odinga kunaoenekana ni kana kwamba kumeivua nguvu ya upinzani nchini.

Nchini Uganda na Tanzania, kukamatwa, kukandamizwa, na kuidhinishwa sheria zinazoonekana kwenda kinyume na demokrasi kadhalika kunaonekana kuyumbisha ushawishi wa upinzani katika masuala ya umma.

Kuongezeka kwa visa vya wapinzani kujivua uanachama na kuhamia katika chama tawala Tanzania CCM kunaonekana kuipunguza nguvu ya upinzani nchini. Basi tunauliza jukumu na uwezo wa upinzani katika mataifa ya Afrika mashariki ni ipi?

Koigi Wamwere ni mwanasiasa Kenya, mwanaharakati wa haki za binaadamu, mwandishi habari na vitabu.

Alipata umaarufu na alifungwa kwa kupinga utawala wa marais Jomo Kenyatta na Daniel Arap Moi Kenya. Alichaguliwa bungeni baada ya kutoka kizuizini. Anatathmini hapa