Watoto wanaougua 'microcephaly' pwani ya Kenya watelekezwa

Maelezo ya video, Watoto wanaougua 'microcephaly' pwani ya Kenya watelekezwa

Baadhi ya familia katika kaunti ya Kilifi nchini Kenya wamekuwa wakijifungua watoto wenye hali isio ya kawaida.

Hali hiyo inayojulikana kama microcephaly husababisha ubongo wa mtoto usikuwe kama unavyohitajika kawaida na hivyobasi kusababisha hali ya mtoto kuwa na kichwa kidogo ikilinganishwa na watoto wengine umri wao.

Jamii imekuwa ikiwatelekeza watoto wenye hali hiyo na wamekuwa wakiwachukuliwa kama laana na wanaosababisha majanga kama alivyogundua mpiga picha wetu Anthony Irungu.