Kwa Picha: Tofauti bayana ya maisha ya maskini na matajiri yalivyo

Picha za kupigwa kutoka angani kwa kutumia ndege ndogo zisizo na rubani maarufu kama drone zimefichua tofauti kubwa iliyopo baina ya matajiri na maskini ambao ni majirani katika miji mingi duniani.

Mpiga picha Johnny Miller amefichua tofauti kubwa ya makazi na maisha kati ya maskini na mabwanyenye katika miji iliyo Afrika Kusini, Mexico na India.

Picha hizi zingepigwa Dar es Salaam, Mombasa, Nairobi na Mwanza au Dodoma taswira ingekuwa tofauti?

Santa Fe, Mexico City.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Santa Fe, Mexico City.

Picha hizo ni sehemu ya mradi wa Bw Miller wa Taswira Zisizo Sawa ambao aliuanzisha Aprili 2016 kuwahamasisha watu kutokubali tena ukosefu wa usawa katika jamii.

Mpiga picha huyo mwenye makao yake Afrika Kusini anasema: "Punde tu unapotua Cape Town, unazingirwa na vibanda na makazi duni.

"Vyumba vya maskini huuzingira uwanja wa ndege, ambavyo inakulazimu kupitia katikati ya vyumba hivyo kwa dakika kumi hivi ukitumia gari kabla ya kufika maeneo wanamoishi watu matajiri na watu wengine wenye mapato ya wastani, maeneo wanamoishi watu waliobahatika (mimi nikiwemo)."

Vukuzenzele, Sweet Home, Cape Town.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Vukuzenzele, Sweet Home, Cape Town.

Bw Miller anaendelea: "Hii ndiyo hali halisi ya mambo yalivyo Cape Town, Afrika Kusini, na katika maeneo mengi duniani, lakini ni hali ambayo hainipendezi kamwe.

"Kwa kumnukuu Barack Obama, ninaamini kwamba ukosefu wa usawa na changamoto ambayo kizazi za sasa kinafaa kukabiliana nayo."

Santa Fe, Mexico City.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Santa Fe, Mexico City.
Grey line
Casey Park, Johannesburg.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Casey Park, Johannesburg.

Picha za kupigwa kutoka juu angani, zinaonesha vitu vinavyowatenganisha maskini na matajiri.

Wakati mwingine ni barabara, kwingine ukuta au uzio na kwingine ni chemchemi au mto au bahari. Upande mmoja kuna majengo duni na upande ule mwingine majengo ya kifahari.

Mumbai.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Mumbai.
Grey line
Mumbai.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Mumbai.
Grey line
Papwa Sewgolum Golf Course, Durban.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Uwanja wa Golf wa Papwa Sewgolum, Durban.
Grey line
Ixtapaluca, Mexico City.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Ixtapaluca, Mexico City.
Grey line
Tembisa, Johannesburg.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Tembisa, Johannesburg.

Ili kupata maeneo mazuri ya kupigia picha zake, Bw Miller hufanya utafiti sana.

Hutumia picha za awali, takwimu kutoka kwa sensa, taarifa katika vyombo vya habari na pia kuzungumza na watu.

"Ninapotambua maeneo ninayotaka kupiga picha zangu, huwa naangalia muonekano wake utakuwaje kwa kutumia huduma ya ramani ya Google Earth, na kujaribu kuandaa njia ambayo droni yangu itapitia. Hii ni pamoja na kuzingatia msukumo wa hewa angani, sheria, usalama, muda ambao betri inaweza kudumu ikiwa na chaji, hali ya hewa, ni wakati gani ufaao, na mambo mengine mengi."

Lake Michelle, Masiphumelele, Cape Town.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Lake Michelle, Masiphumelele, Cape Town.
Grey line
Otto's Bluff, Pietermaritzburg.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Otto's Bluff, Pietermaritzburg.
Grey line
Kya Sands, Bloubosrand.

Chanzo cha picha, Johnny Miller / mediadrumimages.com

Maelezo ya picha, Kya Sands, Bloubosrand.

Unaweza kusoma pia:

Picha zote na Johnny Miller.