Mafuriko yatatiza uchukuzi maeneo mengi Kenya

Moja za barabara zilizofurika jijini Nairobi
Maelezo ya picha, Moja za barabara zilizokumbwa na mafuriko jijini Nairobi
Muda wa kusoma: Dakika 2

Baadhi ya maeneo nchini Kenya yameathirika vibaya baada ya mafuriko ya ghalfa kukata mawasliano ya barabara.

Ripoti kutoka maeneo mbalimbali nchini humo zinaeleza kuwa nguvu ya maji ilikuwa kubwa hivyo baadhi ya watu na magari kusukumwa.

Shirika la Msalaba Mwekundu imeripoti kuwa watu watano waliokuwa kwenye lori walisukumwa na maji eneo la Kitui kilomita 180 Mashariki mwa Nairobi.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Shirika la Msalaba Mwekundu kwenye ukurasa wake wa Twitter imesema baadhi ya barabara nchini humo zimeharibiwa ikiwemo barabara ya Kajiado-Namanga kusini mwa Kenya, na kufanya eneo hilo kushindwa kupitika.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Maelfu ya wakazi wa Nairobi wamekwama na kushindwa kuendelea na shughuli zao kwa sababu ya mvua hizo.

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa kanda yote ya Afrika Mashariki imesababisha mafuriko makubwa ambayo miundo mbinu ya barabara za miji ya Nairobi haziwezi kumudu.

Mitaro ya maji yameshindwa kukabili mvua
Maelezo ya picha, Mitaro ya maji yameshindwa kukabili mvua

Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Nairobi yalikwama mengine huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita.

Magari yyakihangaika kupita kwenye barabara jijini Nairobi
Maelezo ya picha, Magari yakihangaika kupita kwenye barabara jijini Nairobi

Kawaida msimu wa mvua nchini Kenya huwa kati ya mwezi Machi na Mei, lakini wadadisi wanasema kuwa safari hii mvua imenyesha kwa wingi zaidi.

presentational grey line

Mbinu za kubaki mkavu wakati wa mvua:

Ukimbie au utembee?

Mwanafizikia aliwasilisha mawazo mapya kuhusu ni namna gani ya kuendelea kuwa mkavu wakati wa kutembea kwenye mvua.

Ukikimbia, unaepuka kuloa kwa muda mfupi, hata hivyo utaendelea kuangukiwa na matone zaidi. Je kasi kiasi gani inahitajika?

Franco Bocci, akiongea na jarida la masuala ya Fizikia la Ulaya,anasema kwa pamoja uelekeo wa upepo na kimo cha mtu vinaweza kuwa na majibu.

Mara nyingi, jibu la ujumla ni kukimbia haraka iwezekanavyo: lakini jibu hili linabadilika kutokana na upepo na wembamba.

Mwaka 1987, mtafiti mwingine mwenye asili ya Italia alitetea kwenye jarida kuwa kubadili mbinu hakuthibitishi utofauti huo.

Mwaka 2011, mtaalam wa kutengeneza nguo alitumia jarida hilohilo akisema kuwa kasi inahitajika, kutegemea na uelekeo wa upepo.

Kitu kinachofanya swali hili kuwa gumu ni pamoja na umbo la mwanadamu.

Profesa Bocci alibaini kuwa jibu la suala hili linategemea urefu, upana, uwiano pia uelekeo wa upepo na ukubwa wa matone ya mvua