Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tume: Uchaguzi DR Congo utafanyika 2018
Taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zinasema kuwa tume huru ya Uchaguzi nchini humo, imetangaza kuwa uchaguzi mkuu sasa utaandaliwa Novemba mwaka wa 2018 na wala sio mwaka huu kama ilivyotarajiwa.
Viongozi kadha wa upinzani walioshiriki katika mazungumzo ya amani ya kitaifa wameafikiana na uamuzi huo, lakini kuna wale wanaoupinga wakisema ni njama ya Rais Joseph kabila kusalia madarakani.
Mwandishi wa BBC Mbelechi Msoshi anaripoti.