Kwa Picha: Vinyago vya utupu vya Trump

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha kutoka Marekani, ambapo vinyago vya utupu vya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump viliwavutia sana wapita njia.

Watu wakipiga selfie na vinyago vya Donald Trump New York 18 Agosti 2016

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vinyago vya utupu vya Donald Trump viliwekwa maeneo mengi ya miji ya New York, Los Angeles, Seattle, San Francisco na Cleveland nchini Marekani mnamo Alhamisi na kuwavutia sana watu.
Wafanyakazi wa New York City Parks wakikagua kinyago cha Trump eneo la Union Square

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vinyago hivyo vinavyomuonesha Trump akiwa na sura ya ukali viliwekwa chini ya mradi wa INDECLINE, na viliundwa na msanii kutoka Cleveland.
Watu wakitazama kinyago cha Trump mjini San Francisco

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, "Ni kupitia vinyago hivi ambapo tunaonesha umma sura na sifa halisi ya mmoja wa wanasiasa wabaya na wanaochukiwa zaidi Marekani," INDECLINE walisema kupitia taarifa.
Mwanamke akipiga busu kinyago cha Donald Trump mjini San Francisco

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wapita njia wengi walivutiwa na kufurahishwa na vinyago hivyo, baadhi wakiamua hata kuvibusu...
Mwanamume apigwa picha karibu na kinyago cha Donald Trump mjini Los Angeles

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, ...wengine walijaribu kuiga.
Mwanamke apigwa picha karibu na kinyago cha Donald Trump jijini San Francisco

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kwa jumla, mradi huo ulionekana kuwasisimua sana Wamarekani.
Wafanyakazi wa New York City Parks wakiondoa kinyago cha Donald Trump

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Lakini wafanyakazi wa bustani na maeneo ya umma New York waliondoa vinyago hivyo. "NYC Parks inapinga vikali kuwekwa kwa vinyago visivyoidhinishwa katika bustani za jiji, bila kujali ukubwa wake," alisema msemaji wa Sam Biederman.
Mabaki ya kinyago cha Donald Trump mjini New York

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Maafisa wa kampeni wa Donald Trump kufikia sasa hawajazungumzia vinyago hivyo.