Ujumbe wa kwanza wa twitter wa Jack Dorsey wauzwa $2.9m

Ujumbe wa kwanza wa muazilishi wa mtandao wa Twitter Jack Dorsey umeuzwa kwa dola milioni 2.9 kwa mfanyabiashara wa Malaysia.Ujumbe huo ulichapishwa tarehe 21 mwezi wa Machi mwaka 2006 uliosema 'naanzisha twitter yangu'. Bwana Dorsey amesema pesa hizo atazitoa kwa ufadhili.