Mwanamziki Nicki Minaj alazimika kumlipa Tracy Chapman $450,000

Rapa Nicki Minaj atamlipa mwimbaji Tracy Chapman $ 450,000 ili kumaliza mzozo wa haki miliki baada ya kuchukua sampuli ya wimbo wake wa Baby Can I Hold You. Chapman alimshtaki Minaj mwaka wa 2018, akisema alikuwa ametumia sehemu za wimbo wake na ingawa wimbo wa Nicki Minaj haukuwahi zinduliwa, sehemu kidogo ya wimbo huo ulivuja mitandaoni.